KAMUSI ELEKEZI YA ULEMAVU

Størrelse: px
Begynne med side:

Download "KAMUSI ELEKEZI YA ULEMAVU"

Transkript

1 KAMUSI ELEKEZI YA ULEMAVU Toleo la Kwanza Inclusive Development Promoters & Consultants (IDPC) Dar es Salaam-Tanzania i

2 Hakimiliki IDPC, 2016 Haki zote zinamilikiwa na Inclusive Development Promoters & Consultants (IDPC) S.L.P , Dar es Salaam-Tanzania, Barua pepe: ISBN Toleo la Kwanza 2016 Chapisho hili haliuzwi Tabaruku Kamusi hii imeandaliwa mahususi kwa watu wote wenye ulemavu duniani. Usanifu na Uchapaji Nesmap Printing Technology S.L.P ; Dar es Salaam (T) Baruapepe ii

3 Dibaji J apo inakadiriwa kuwa takribani watu bilioni moja 1 duniani ni wenye ulemavu, idadi ya watu wenye ulemavu nchini haikuweza kuwa bayana kwa kipindi kirefu kutokana na sababu mbalimbali zikichangiwa na elimu ndogo kwa wahojiwa ambao walitakiwa waeleze ukweli wa hali ya ulemavu kwa wanafamilia/wanakaya. Kadiri siku zilivyokwenda, hali hii ilibadilika ambapo Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, na hasa utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) ndio matukio ya awali yaliyochachawiza zaidi matakwa ya kitakwimu nchini kuhusu kundi hili. Kwa umuhimu wake na kwa kuzingatia sera za Taifa za Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 2004, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilibeba dhamana kwa kuendesha utafiti mahususi wa Watu wenye Ulemavu mwaka 2008 na kubaini kuwa, kundi la watu wenye ulemavu ni asilimia 7.8 ya idadi ya Watanzania wote. Aidha, matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, yamebainisha kuwa kundi hili ni asilimia 9.3 ya Watanzania wote nchini. Ni wazi kuwa ulemavu uliotambuliwa zaidi kwenye utafiti wa mwaka 2008 na 2012 ni ule wa kuonekana. Imedhihirika kuwa bado kuna idadi kubwa ya Watanzania wenye ulemavu wa kutoonekana bayana, mathalani, matatizo ya afya akili, uzee, magonjwa ya kudumu kama vile kifafa, magonjwa ya kusendeka, n.k. ambao bado hawajatambuliwa wakati hali zao zinaangukia kwenye kundi hili. Takwimu hizi zimethibitisha pasi na shaka kuwepo kwa kundi hili kama sehemu stahilifu na ya kudumu katika jamii ya Kitanzania. Kwa uelewa huu, jitihada za ujumuishaji wa kundi lenyewe zimeshika kasi kuliko muda mwingine wowote. Pamoja na umuhimu wa takwimu za Watu wenye Ulemavu, ni vema kila ngazi ya utungaji sera na utoaji uamuzi ikazingatia nasaha ya kwamba: idadi kamwe haiwezi kuathiri madai ya haki ya ujumuishaji. Kundi hili liwe ni asilimia mbili au kumi na hata zaidi, bado ukweli ni kuwa linakabiliwa na matatizo ya kipekee tofauti na raia wengine; na daima matatizo haya ni matokeo ya kutengwa na mtazamo hasi wa jamii dhidi yake. Suala la msingi hapa ni lile la haki za binadamu ambalo tafsiri yake ni ya kiulimwengu. Katu malengo mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa hayawezi kufikiwa iwapo hapatakuwapo na mipango madhubuti ya ujumuishaji wa kundi hili kwenye michakato ya kimaendeleo 2. 1 World Report on Disability (2011) 2 EC, Study of Disability in EC Development Cooperation (2010) pg 27 iii

4 Ofisi ya Taifa ya Takwimu imepokea fursa hii nyingine iliyotunukiwa na kuwa sehemu ya kujielimisha zaidi kuhusu jamii nzima ya watu wenye ulemavu. Fursa hii imetolewa na Waandishi wa Kamusi Elekezi ya Ulemavu kwa kuiomba Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwaandikia dibaji ya toleo la Kwanza la Chapisho hili. Kuijumuisha Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kuandika Dibaji ni kutoa uelewa na kupanua wigo mpana kwa Watakwimu ambao utasaidia wakati wa kuandaa utafiti kuhusu watu wenye ulemavu, namna ya kufanya uchambuzi na kusambaza takwimu zenyewe katika kupanga mipango ya maendeleo kwa jamii. Kwanza, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inaunga mkono jitihada zilizofanywa na Asasi ya Uenezi na Ushauri kuhusu Maendeleo Jumuishi (Inclusive Development Promoters & Consultants). Juhudi hizi zinaipatia jamii na hasa watunga sera, wapanga mipango ya maendeleo na watoa uamuzi marejeo mahususi kuhusu kundi hili yenye fasiri inayobeba mtazamo wa wahusika wenyewe. Pili, matokeo ya jitihada hizi ni ushahidi kwamba, kundi hili linao uwezo wa kufikiri, kubuni na kutenda sawa na Watanzania wengine bila kujali maumbile, hadhi ya kiuchumi na kijamii. Sambamba na hilo, chapisho hili litakuwa msaada mkubwa kwetu tulio na wajibu wa kutekeleza kikamilifu Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (2006) ulioridhiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sanjari na utekelezaji wa Agenda ya Malengo ya Maendeleo Endelevu itakayoishia mwaka Dhana kuu zote zimetafsiriwa na Kamusi hii kwa mapana. Aidha, mnyumbulisho wa aina za ulemavu na mahitaji yake umetolewa kwa kina. Zana imepatikana, hivyo ni vyema ikatumika kikamilifu ili kuwezesha matumizi halisi ya lugha inayotakiwa kwa kundi hili la walio na ulemavu nchini na duniani kote. Ni matumaini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwa Kamusi hii itaendelea kuboreshwa zaidi, hivyo maoni na ushauri uwasilishwe IDPC. Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu iv

5 Shukrani Kamusi hii ni zao la tafakuri na jitihada kubwa za asasi ya IDPC katika kujaribu kutafsiri kwa vitendo matazamio na dhima yake kuhusu dhana ya maendeleo jumuishi hususani kwa watu wenye ulemavu. Kama usemavyo msemo wa Kiswahili, Mpango si matumizi. Msemo huu unahadharisha kwamba, kuwa na wazo fulani pekee hakuwezi kutoa matokeo yanayotumainiwa endapo hazitakuwepo jitihada za wazo lenyewe kufanyiwa kazi kivitendo. Pia, ili kutenda, sharti pawepo na rasilimali zinazohitajiwa na mwenye wazo ama kwa kuzimiliki au kuchangiwa na wengine. Halikadhalika, ili kuweza kuchangiwa, msingi wake ni mhusika kuwa na uhusiano mzuri kwenye jamii na jumuiya inayomzunguka. Katika hatua za awali, IDPC ilikuwa na wazo la nini kifanyike bila kumiliki nyenzo au rasilimali za kutekelezea wazo lenyewe isipokuwa uhusiano mwema na watu. Kutokana na msingi wa uhusiano huu mzuri, nakisi ya rasilimali ilichangwa, na wazo likatafsiriwa kivitendo na matokeo yake ni kuchapishwa kwa Kamusi Elekezi ya Ulemavu. Kutokana na ukweli huu, IDPC inawiwa sana na mtu mmojammoja; makundi na taasisi mbalimbali. Japo kiutaratibu itaonekana kuwa asasi hii (IDPC) ndiye mmiliki wa Kamusi, lakini kiuhalisia ni kwamba, tunda hili linamilikiwa na wengi ambao bila mchango wao wa hali na mali, tunda lenyewe lisingepatikana. Kutokana na wingi wa wachangiaji, haitakuwa rahisi kuwaorodhesha wote kwa majina. Hapa tunatoa shukurani za dhati na za jumla kwa kila mmoja aliyechangia kwa namna yoyote ile katika kufanikisha uandishi wa Kamusi hii. Wachangiaji wote katika ujumla wao tunawashukuru sana kwa uzito sawa. Hata hivyo, wapo wachangiaji wachache, binafsi na taasisi ambazo lazima zitajwe kwa majina. Tuanze kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko wa Maendeleo wa Watu wenye Ulemavu wa nchini Ufini (Abilis Development Aid for People with Disabilities). Bila mchango wa Asasi hii wa kifedha, ushirikihali na ushajiishaji, mradi huu ungeishia kwenye hatua ya dhana tu. Pia hatuna budi kuwataja Bwana Batista Mgumba na Godfrey Emmanuel kwa kuudhamini mradi huu kwa mujibu wa masharti ya Mfuko wa Maendeleo wa Watu Wenye Ulemavu wa Ufini. Wadhamini hawa walifanya hivyo kwa imani tu kwani wazo lenyewe lilikuwa bado kwenye maandishi tu. Mbali na udhamini, watu hawa walijitolea kuufuatilia utekelezaji wa mradi huu kwa hatua zote ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wake unafanyika kwa kadiri ya makubaliano. Mabibi Frida Silumbe na Nuru Awadhi walijipambanua kuwa wajumbe wa kamati ya mradi v

6 iliyohusika na usimamiaji wa mradi wenyewe siku hadi siku. Wazee waliobobea katika nyuga za lugha adhimu ya Kiswahili na uandishi, yaani, Amir Sudi Andanenga na John Mbonde, ndio hasa waliojenga msingi wa kazi nzima kwa kubaini visawe na vitomeo vya lugha lengwa vyenye kushabihiana na vidahizo vya lugha chanzi. Kadhalika, kila ilipolazimu, walibuni istilahi mwafaka na kuhariri kazi ya uandishi kwa kila hatua. Mabingwa wa lugha ya Kiswahili: Mwalimu Elizabeth Mahenge na Bwana Mayolwa John Nzala, walikubali kushirikiana na IDPC kwenye mradi tangu hatua za awali na kuendelea nao muda wote wakishauri jinsi ya kuufanikisha. Pia tunawashukuru wajumbe wa Kamati ya Ushauri na kikosi cha wataalamu, ambao taaluma zao zinawahusianisha sana na masuala ya ulemavu (matabibu, walimu, wataalamu, wanasayansi ya jamii, wanaharakati n.k.) waliojitolea muda wao kuupitia muswada kwenye hatua zake za awali na kuuboresha kwa kiasi kikubwa. Shukurani pia zinaelekezwa kwa Taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi zilizokubali machapisho yao kutumika katika kurutubisha uandishi wa Kamusi hii kwa kuyanukuu au/na kuyanakili kila ilipotakiwa. Taasisi hizi ni pamoja na Jumuiya ya Ulaya, Ecumenical Disability Advocates Network, Wachapishaji wa vitabu vya Hesperian ; Sekretariati ya Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (Ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu-Umoja wa Mataifa); Chama cha Watu wenye Ulemavu Singapo (Disabled People Association - Singapore); Ofisi ya Tanzania ya Huduma za Msaada wa Kimataifa (International Aid Services (IAS)); Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Chuo Kikuu cha Dar e s Salaam) na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA). Ni wazi kuwa, bila kukubaliwa kutumia stadi za taasisi hizi, uandaaji wa Kamusi hii usingewezekana kukamilika katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja na wala chapisho hili lisingekuwa na ubora lilionao. Pia BAKITA limeenda mbele zaidi kwa kuhariri muswada na kuipatia ithibati Kamusi hii. Pia kwa dhati kabisa tunakiri kuwa baadhi ya vielelezo vya kukolezea ufahamu katika Kamusi hii vimenakiliwa kutoka Mfuko wa Abilis (nchini Ufini), Wachapishaji wa Hesperian (wa nchini Marekani) na kwenye agobui kikoa public domain web sites. Kwa hiyo, tunachukua fursa hii kutambua na kuheshimu hisani ya wote waliosawiri vielelezo hivi na kuvipakia kwenye agobui vi

7 tajwa. Hapa tunaorodhesha vielelezo hivyo kimojakimoja kutoka agobui kikoa ambavyo ni: abakusi, njia fikivu, msalani fikivu, stadi za kila siku, kicharazio mbadala, liftitanga, tanzi la mkono, athetosisi, ubambahimo, kizuzizi, bakora, ubongo mkuu, wayopindu, kombeo amirishi, pagaro, wenzokongojea, kionyi bainifu, ubongo mkuu, matende, vifunza mitembeo, mbwa mwongozaji, kingogemeo, aina za shimesikio, hidrosifelasi, ngirimaji, hiparopia, mkingamo ufikivu, isojinsi, kiegemeo dekezi, pagaro kiuno, mikrosefali, ufikivu wa maegesho, tezi dume, roleta, mfumo wa upumuaji, kitobozi, supinesheni, mchoro mpapaso, vibamba mpapaso, kitumi cha mawasiliano kwa viziwi, mpapaso ufahamu, trakeostomi, kitufe onyeshi, video kalimani lugha ishara, kiunzi egemeo, kitimwendo, vinyanyua vitimwendo, ngazimbetuko ya kitimwendo. Anwani kamili za tovuti zilizotumika zimeorodheshwa mwishoni mwa chapisho hili. Tunapenda pia kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa IDPC, ndugu Rutachwamagyo Kaganzi ambaye alibeba mradi huu mabegani kwake tangu likiwa wazo hadi kufikia hatua ya mwisho ya kuwa na Kamusi Elekezi ya Ulemavu mikononi. Mchango wake haumithiliki katika kazi hii kwani ilifanyika katika mazingira magumu ya kutokuwapo kwa rasilimali stahilifu za kutosha. Ni moyo wa kujitolea na ubunifu wake ndivyo vilivyouvusha mradi huu kwenye milima na mabonde. Mchapishaji wa kazi hii naye anapewa shukurani za pekee kwa ushirikihali wake na jitihada za kuhakikisha kuwa kazi inakamilika katika muda uliopangwa. Rutachwamagyo Kaganzi Mkurugenzi Mtendaji IDPC Januari 2016 vii

8 Mwongozo wa Kutumia Kamusi Elekezi ya Ulemavu Kamusi hii ni elezi kwa mantiki kwamba inaelezea hisia za watu wenye ulemavu. Imetoa taarifa juu ya ulemavu wa aina mbalimbali ili jamii iweze kujitanabaisha na masuala anuwai yanayohusu ulemavu na athari zake (Mwansoko na wenzake 2013 uk. 11). Hii ni Kamusi amili kwani inachochea hisia za wanajamii kuwa chanya kuhusu ulemavu. Aidha, ina vionjo vya kiinsaiklopia kwa vile maelezo na ufafanuzi wake huzama ndani zaidi kuhusu dhana kadha wa kadha zilizomo humu kwa lengo la kutoa maarifa ya kisayansi, kiuchumi, kitaaluma, n.k., na hivyo kuifanya kuwa chombo pekee na marejeo muhimu katika uga huu wa ulemavu (ibid). Kamusi Elekezi ya Ulemavu ina lugha mbili: Kiingereza (lugha chanzi) na Kiswahili (lugha lengwa). Kwa kiwango kikubwa, Kamusi hii inazingatia matumizi ya adabu lugha na akhlaki za ulemavu kutokana na ukweli kuwa, suala zima la ubaguzi kwa misingi ya ulemavu limejikita kwenye hisia kuhusu hali hiyo na wahusika wake. Mtu au jumuia hudhihirisha hisia walizonazo kuhusu ulemavu kwa njia ya lugha inayoamuliwa kutumika kuielezea hali au mhusika mwenye kilema. Kwa mantiki hiyo, lugha inayotumiwa huwa ndio msingi wa kujenga mila na utamaduni mahalia. Ndiyo maana katika Kamusi hii, istilahi, msamiati au maelezo yenye kukirihisha kwa mtu mwenye ulemavu yamewekewa alama ya vinyota viwili mbele yake kama utambulisho maalumu kuwa, hayapaswi kutumika (kwa mfano, mguurungu**). Kwa kulizingatia hili, Kamusi hii imeandaliwa kwa jicho la ulemavu, na hivyo, kukidhi matakwa ya walengwa kuhusu kasoro za adabu lugha, maana ashirifu na mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu. Aidha, ndani ya Kamusi hii kuna vidahizo na visawe vilivyoibuliwa na kubuniwa na taasisi za taaluma maalumu k.v. BAKITA, TATAKI n.k., ambavyo viliingizwa kwa makubaliano yaliyofanyika baina ya IDPC na mamlaka hizo ili kukidhi taratibu na kanuni za haki miliki. Nukuu za aina hiyo zimewekewa tarakimu za Kirumi mwishoni mwa kila nukuu na kuandikwa jina la mamlaka inayohusika kurasa za mwisho wa Kamusi hii (mathalani, BAKITA, Kamusi Kuu ya Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa; Dar es Salaamu (2013), uk. 8). Uundaji wa Kamusi hii ulihusisha: (i) Uainishaji wa vidahizo (dhana, semi, istilahi) kutoka lugha chanzi (Kiingereza); viii

9 (ii) Utafutaji na uainishaji wa visawe na vitomeo vya lugha lengwa (Kiswahili); (iii) Uundaji wa istilahi mpya za Kiswahili ilipobidi kufanya hivyo au kutumia msamiati wa lugha za Kibantu unaofanana na dhana inayofafanuliwa (mathalani, visawe vya nsiso, kimina na ntenga kutoka lugha za Kihaya na Kingoni); (iv) Kufasiri, kutafsiri au/na kuandaa visawe au vitomeo vya lugha lengwa. Kutokana na ukweli kuwa uandaaji wa Kamusi hii umeongozwa na dhana na istilahi za Kiingereza, pia mpangilio wake wa herufi za alfabeti umefuatisha lugha chanzi (Kiingereza). Matumizi ya Alama, Ishara, Lebo na Tarakimu Alama na ishara zilizotumika katika Kamusi hii ni pamoja na zifuatazo: a) Alama za kiisimu (mabano) mnukuo (Nukta katishi..) b) Lebo Nyota ** c) Namba na Tarakimu Kiarabu (1, 2, 3 ) Kirumi (i, ii, iii.) Urejeleo Kidahizo Katika Kamusi hii, maneno angalia (ang.) na tazama (taz.) yametumika kumrejesha msomaji kwenye neno la msingi linalobainisha fasili sahihi ya mrejeo wa neno husika. Halikadhalika, kutokana na Kamusi hii kuwa ni ya lugha mbili yaani Kiingereza na Kiswahili, urejeleo umeelekezwa katika lugha ya Kiingereza ili kumrahisishia msomaji kulipata kidahizo kinachohusika. Vidahizo Kadiri ya mtiririko wa maelezo na mpangilio wake katika Kamusi hii, kidahizo kimeandikwa mkono wa kushoto kwa lugha ya Kiingereza na kwa herufi zilizokolezwa. Kila kidahizo kimeandikwa kwa herufi ndogo na katika umbo la umoja isipokuwa kwa baadhi ya vidahizo ambavyo ni majina k.m. Braille, ugonjwa wa Parkinson, n.k. Visawe ix

10 Visawe (vikiwa katika hati mlazo) na fafanuzi zake (zikiwa katika hati ya kawaida), vimeandikwa mkono wa kulia wa kila kidahizo husika. Baadhi ya visawe vimetoholewa hususani kutoka vidahizo vya kitabibu au taaluma maalumu. Baada ya kutoholewa, vimetolewa maelezo ya ufasaha na yenye kueleweka kwa urahisi. Msamiati wenye utata Kilema: na ulemavu ni istilahi changamani hasa katika lugha lengwa ya Kiswahili. Katika tafsiri na matumizi ya kawaida, neno kilema kumaanisha hitilafu kwenye kiungo au viungo vya mtu na vilevile kutambulisha mhusika wa hali hiyo. Ndani ya Kamusi hii, istilahi hii imetumika kwa maana ile ya kwanza ya kutambulisha kasoro ya kiungo. Istilahi ulemavu inatumika, kama hali ya kuwa na kiungo cha mwili chenye hitilafu. Kamusi hii inatumia na kufafanua istilahi ulemavu kwa mapana zaidi kwa kuzingatia muktadha wa Kimataifa ambapo hali ya kuwa na kilema, ikiangaliwa kwa pamoja na shughuli inayotakiwa kufanyika na mazingira itakapofanyikia, ndivyo katika ujumla wake huzalisha ulemavu. Hata hivyo, kutokana na mazoea, istilahi hii ulemavu inatumika zaidi kuliko kilema. Kwa maana hiyo, nyakati nyingine istilahi hizi mbili zimetuka kwa kubadilishana. Maneno alama na ishara mara nyingi huchanganywa. Lakini kwa kadiri ya Kamusi hii, neno ishara limetumika katika kutoa mawasiliano ya moja kwa moja. Mathalani, lugha ishara k.v. kuweka kidole shahada kwenye mdomo kumaanisha katazo la kelele. Pia lugha ishara ya viziwi kwa kiasi kikubwa imeundwa kwa ishara za matendo na maumbo mbalimbali. Lakini baadhi ya makabila huchanja nyuso, migongo, kujichora miili n.k. ikiwa ni alama ya ukoo au tukio fulani. Neno mguso na mpapaso nayo hutumika visivyo. Kamusi hii imechukulia neno mguso kuwa ni kitendo cha vitu viwili au zaidi kugusana, ambapo kitendo hicho kinaweza kuwa ni cha nasibu na agh. bila kutoa taswira au ujumbe wowote. Kwa upande mwingine, mpapaso, ni tendo la kudhamiria ambapo mhusika huwa anapapasa kitu kingine akiwa anakusudia kujenga taswira na kupata ujumbe k.m. kupapasa vidutu vya nuktanundu ili kujua kilichoandikwa au kupapasa kitu ili kujua umbo lake lilivyo, n.k. Njia hii ya kimawasiliano hutumiwa na watu wenye matatizo ya uoni. Kwa upande mwingine, neno msaada katika Kamusi hii limetumika kurahisisha lugha japo linabeba maana ashirifu ya mwega na amara. Wakati x

11 msaada huwa na vionjo vya kihisani, mwega humaanisha uhimili wa kitu au jambo fulani. Neno ugweuti na uti wa ubongo yana maana ileile; Maneno mikingamo, vikwazo, vizuizi yana maana ileile; Jamii ni mjumuisho wa watu wote wanaoishi ndani ya mfumo mpana wa kiutawala k.m. nchi ila ndani yake zipo jumuiya mbalimbali kutokana na makabila, imani, mirengo ya kiitikadi, aina ya shughuli za maisha, n.k.; Mwenye upofu na asiyeona yametumika kumaanisha hali ileile; Mwalimu mtaalamu linajielekeza kwa mwalimu aliyefuzu mafunzo ya ziada kuhusu mahitaji maalumu ya ujifunzaji. Aidha, inaitwa Kamusi Elekezi ya Ulemavu kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo: Matarajio kuwa baada ya kuchapishwa kwake, inawezekana zikaandaliwa kamusi nyingine kadha wa kadha zenye kujikita katika eneo moja la aina ya ulemavu k.m. Kamusi ya Nuktanundu kwa wasioona n.k. Ni ya aina yake katika historia ya harakati za watu wenye ulemavu katika milenia hii barani Afrika, kiasi cha kuleta changamoto za kiutandawazi katika dunia nzima. Ingawa ni ndogo kwa umbo, lakini imesheheni hekima na busara maridhawa; Imebuniwa na kuandaliwa na watu wenye ulemavu wenyewe kwa hisani kubwa kutoka taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi; Kamusi hii ni elekezi kwa mantiki kwamba imesheheni picha, michoro na vielelezo ili kurahisisha uelewa wa dhana inayofafanuliwa; Kwa kuthubutu kuandaa na kuchapisha Kamusi hii na kuisambaza bila kutoza malipo, ni mchango wa watu wenye ulemavu kwa Taifa la Tanzania, nchi nyingine na taasisi zote zinazotumia lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki na Kati, na duniani kote ukiwa ni ushahidi wa kudhihirisha ukweli kwamba, watu wenye ulemavu wana fursa pana ya kuchangia maendeleo katika nyanja mbalimbali. xi

12 Vifupisho Agh Agh. Ang. Angalia BAKITA Baraza la Kiswahili la Taifa db desibeli (kizio cha kupimia kiwango cha sauti, lakini pia hutumika sana kwenye masuala ya elektroni, ishara na mawasiliano) EJ Elimu Jumuishi IAS International Aid Services IDPC Inclusive Development Promoters & Consultants k.m. kwa mfano k.v kama vile MMU Mvurugiko Mfumo Usikivu n.k. na kadhalika SC Simu inayochapa maandishi T6, T7, T 8 Eneo la uti wa ngongo lililojeruhiwa (throracic vertebrae) Taz. Tazama TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Uk Ukurasa xii

13 Utangulizi Wanaharakati wa masuala ya ulemavu huamini kuwa, lugha ni hatua ya mwanzo kabisa kuelekea kwenye urekebishaji wa udhalimu na ubaguzi. Jitihada za kuleta usasa kuhusu ulemavu ni kwa wahusika kujihimu kwa kujielekeza kwenye kuiwezesha jamii kusikia na kujifunza matumizi ya lugha sadifu kuhusu kundi hili la watu wenye ulemavu. Mahitaji haya yanatokana na kuamini kuwa, lugha husawiri na kuakisi hali halisi ndani ya jamii. Uwepo wa lugha za kibaguzi na za kidhalilishaji ni ashirio na shamirisho la mwendelezo wa tofauti za uluwa wa kijamii kwa kutabakisha makundi. Katika hali hii, makundi ya pembezoni kama vile watu wenye ulemavu, wanawake, watu kutoka makundi mbalimbali yenye uanuwai kiusuli na kimakabila huendelea kudunishwa na kutengwa. Mamlaka mbalimbali za Kiserikali, waandishi, walimu, wanahabari, wasanii na kadhalika, wana jukumu muhimu kabisa katika kukuza na kuendeleza lugha sadifu juu ya ulemavu. Inakubalika miongoni mwa wanaisimu kuwa lugha haikiti wala kutuama daima, bali hubadilika kila mara kuendana na mabadiliko mengine ya kimitazamo na kidesturi ndani ya jamii inayohusika. Kwa kuzingatia ukweli huu, IDPC na washirika wake, wameandaa Kamusi Elekezi ya Ulemavu ili iwe marejeo na wenzo wa kuenezea istilahi, misemo, na misamiati sadifu kuhusu ulemavu. Kamusi hii ni mahususi kwa masuala ya ulemavu. Tofauti na Kamusi nyingine zinazogusiagusia masuala ya ulemavu hapa na pale, hii imeandaliwa na kusanifiwa na wahusika wenyewe na kwa ajili ya masuala yao. Kamusi hii imeitwa Kamusi Elekezi ya Ulemavu kutokana na ukweli kuwa inakidhi yafuatayo: kupunguza misigano na upotoshaji juu ya istilahi na msamiati kuhusu ulemavu, na hivyo, kuiondoa jamii kwenye mtanziko; kuwawezesha wadau kujielimisha zaidi juu ya ulemavu hususani kuhusiana na Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu; kuwezesha unyambulishaji na utambuzi wa makundi madogomadogo ya ulemavu ili yaonekane na mahitaji yake yazingatiwe badala ya mtindo wa sasa wa kuchukulia aina za ulemavu kwa ujumla (mathalani, wenye ulemavu wa akili; viziwi, n.k.). Pia Kamusi hii inarahisisha ufanyaji marejeo kwa semi, istilahi, na msamiati mingi ya kitaalamu kwani badala ya kutakiwa kupitia rundo la kamusi kusaka kisawe au kitomeo, inatumika kamusi moja ya uga huu. Umuhimu mwingine wa Kamusi hii ni kuwa imeandaliwa kwa jicho la ulemavu, na hivyo kurekebisha kasoro nyingi za xiii

14 adabu lugha, maana ashirifu na mitazamo mingine yenye ukakasi na mitazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu. Yaani, kuridhika na kufafanua jambo bila kujali hisia za wanaoelezewa. Kwa maana hiyo, Kamusi hii ni: i) elezi: inaelezea hisia za watu wenye ulemavu; ii) arifu: inatoa taarifa juu ya ulemavu kwa jamii kuu; iii) amili: inachochea hisia za wanajamii kuwa chanya mintarafu ulemavu (Mwansoko na wenzake, uk. 11 na 12). Ni wazi kuwa kwa umuhimu huo, Kamusi hii ni wenzo mahususi siyo tu kwa watu wenye ulemavu peke yao, bali kwa makundi mbalimbali yenye wajibu wa kulinda, kutenda haki kwa watu wenye ulemavu mintarafu Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu. Kwa maana hiyo, Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Serikali (Wizara na Wakala),Taasisi za Elimu ya Juu, Wasomi na Wanataaluma wanaojikita kwenye nyuga kama vile Sayansijamii, Saikolojia, Sakaitria, Utabibu, Ualimu, harakati za masuala ya kijinsia, n.k. ni miongoni mwa wanufaika wakuu wa zana hii. Licha ya kukidhi masuala ya ulemavu, inahusisha pia nyanja mtambuka kwa mtiririko endelevu. Zana kama hii ni muhimu mno kwa sasa ambapo serikali inaendelea kukifanya Kiswahili kuwa Lugha ya kufundishia kwa ngazi zote za elimu ambapo suala la ujumuishaji linapewa kipaumbele na uzito mkubwa. Umuhimu wa Kamusi hii kuwa na vionjo vya kiinsaiklopidia ni kwa kuzingatia msisitizo wa wanazuoni kwamba: Kuna umuhimu mkubwa kuzifanya kamusi zetu za lugha za Kiafrika kuwa kamusi za karne ya 21 kwa kuzipanua maeneo yao ili zikusanye dhana za kisasa. Kamusi karibu zote muhimu za kisasa zinaanza kujitoa kwenye ukamusi na kuingia kwenye lakabu ya insaiklopidia. Kamusi za kisasa zinakusanya sio maana pekee, bali maarifa pia. Maarifa haya ni ya kisayansi, kiuchumi, kihandisi na kadhalika. Unapozichunguza kwa makini kamusi za kisasa, katika utangulizi zinajiita encyclopaedic dictionaries kwa maana ya kuwa ni chombo cha marejeo reference pia. Hii ni hatua kubwa ambayo kamusi sanifu ya Kiswahili ni lazima ipige. Ili kuwa na manufaa yoyote katika viwango vya juu vya elimu, lazima ipanue upeo wake wa idadi ya maneno, ijapokuwa jambo hilo linahitaji fedha za kutosha. Lazima wahusishwe wataalamu wa sayansi, kompyuta, siasa na xiv

15 kadhalika katika kuiendeleza kamusi hiyo. Ule wakati wa kuwa na wazee pekee kama wahifadhi wa maneno unakwenda ukififia. 3 Kutokana na nasaha hizo hapa juu, uandaji wa kamusi hii umeshirikisha wabobevu katika uga wa ulemavu ndiyo maana imeingiza sura na vionjo vya insaiklopidia kwa kudadavua vidahizo ili mtumiaji apate maarifa yanayohusu eneo hilo. Kwa upande mwingine, hiyo ni changamoto sanjari na jitihada za kujitegemea, kwani imezoeleka kwamba watu wenye ulemavu, daima huomba kusaidiwa. Kwa maneno mengine, ni dhahiri kwamba kila mtu mwenye ulemavu yampasa kwa kadiri inavyowezekana, kufanya kazi kwa kushirikiana na jumuiya inayomzunguka ili kupata riziki yake ya kila siku na kuwa rasilimali kwa wengine. Aidha, ni kuwa mstari wa mbele katika kutoa msaada kwa binadamu wote wanaokabiliwa na kero mbalimbali katika maisha. Kwa mantiki hiyo, watu wenye ulemavu hawatarajiwi kujibweteka. Kamusi hii ni ya lugha mbili; yaani Kiingereza (lugha chanzi) na Kiswahili (lugha lengwa). Kadhalika, hii ni Kamusi maalumu; yaani, fafanuzi, yenye tafsiri huru na ya kiufundi kwa viwango mbalimbali. Kwa kiasi kikubwa, dhana zilizochukuliwa ni zile zinazokubalika katika uga wa ulemavu kote ulimwenguni kwa kuzingatia utamaduni ulioibuliwa wakati wa mvuvumko na hasa kipindi cha kuandaa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu. Halikadhalika, angalizo limetolewa kuhusu dhana na istilahi za kale zenye maana ashirifu hasi. Zaidi ya hapo, dhana za masuala ya kijinsia na nyingine zinazoibuka wakati huu, zimejumuishwa kwenye Kamusi hii. Kwa maana hii, wasomaji na watumiaji makini wa zana hii watafumbuka zaidi na kuhusianisha yale yanayojitokeza kwenye jamii yetu hivi sasa na silika, hulka maumbile na mienendo ya wanadamu. Japo kimsingi fasiri ya Kamusi lengwa ni ya kiufundi, hata hivyo, mbinu mchanganyiko zimetumika katika uandaaji wake: mawasiliano huru yenye kulenga hisia za msomaji, urahisi wa kueleweka, utamadunishaji; uundaji wa istilahi mpya kila ilipobidi na kuwezekana pia mbinu ya neno kwa neno kwa kiwango fulani; tafsiri sisisi kwa kuzingatia maana za msingi bila kujali muktadha. 3 H.J.M. Mwansoko na A.R. Chuwa, Tahakiki ya Uchapishaji Kamusi,Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, 1995 uk 45. xv

16 Changamoto za kufasiri kutoka lugha chanzi ni pamoja na: tofauti ya utamaduni (mila na desturi) wa lugha chanzi kuwa tofauti na lugha lengwa. Mfano, kwenye msamiati unaohusu ujinsia, teknolojia ya kimawasiliano, huduma za jamii, n.k; kamusi za marejeo kutozingatia adabu lugha na maadili ya ulemavu. Mfano, majina kama vile kikono, kiguru, mwendawazimu, kibete, n.k.; kukosekana kwa visawe kwenye lugha lengwa pale teknolojia pevu inapohusika; tafsiri ya kiufundi (mf. utabibu) kuwa na utohozi mwingi kiasi cha kupoteza ladha kwenye lugha lengwa (mfano. inflamesheni, uneresisi, n.k); ikolojia kusababisha baadhi ya istilahi za lugha chanzi kutoshabihiana na zile za lugha lengwa iwe kwa kuandikwa kuendana na matamshi au tahajia ya lugha chanzi mfano trancheobronchitis (trankobronkitisi); ugunduzi wa teknolojia saidizi na huduma kutoendana na ule wa mazingira lengwa; kukosekana kwa visawe mwafaka vyenye kubeba maana ileile katika lugha chanzi na lengwa, mathalani: gesture, signal, cue, clue (Kiswahili-yote ni alama au ishara), morals, ideals, values (Kiswahili yote maadili) n.k. Hata hivyo, waandaaji wa Kamusi hii wamepata ujasiri wa kusonga mbele kwa kuthubutu kuichapisha na kuisambaza kwa kuzingatia ukweli uliokwisha bainishwa na Mwansoko na wenzake kwa nukuu ifuatayo:..ni muhali kwa tafsiri kuwa sawa kabisa na matini chanzi kutokana na tofauti za kiisimu, kiutamaduni, kihistoria na kimazingira baina ya lugha ambayo hufanya iwe vigumu kufasiri mawazo ya lugha moja katika lugha nyingine bila kupoteza, kupotosha au kubadili maana kwa viwango fulani. Hii imepelekea tafsiri karibu zote kuwa na mipogoko au upungufu fulani. Na ndiyo maana Wataliano wakawa na msemo usemao traduttore traditore, yaani mfasiri ni mhaini (Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia na Mbinu uk 48). Ni vema ikaeleweka kuwa mpaka sasa miongoni mwa wanaharakati wa masuala ya ulemavu, bado kuna mabishano juu ya istilahi za kuchukuliwa kuwa chukizo. Muktadha wa suala hili huhitilafiana kutokana na maeneo kijiografia, utamaduni, zama, desturi za kitaaluma, mitazamo binafsi, n.k. Istilahi nyingi ambazo baadhi ya wahusika huzichukulia kuwa chukizo, kwa wengine huziangalia kwa namna chanya. Hata pale ambapo baadhi ya watu huchukizwa na misemo, msamiati au istilahi fulani, wenzao wanaweza kuchukizwa na tasifida mbadala kama vile wenye uwezo tofauti, wenye mahitaji maalumu badala ya ulemavu au kilema. Wakati baadhi ya watu huamini kuwa sharti xvi

17 kuepuka matumizi ya misemo inayoweza kuwachukiza wenzao, wengine humlaumu mwongeaji kwa tafsiri potovu ya istilahi zilizotumiwa bila kuwa na dhamira ya kumuudhi yeyote. Katika kukabiliana na changamoto za kimuktadha, waandishi wa Kamusi hii wamejitahidi kufafanua na kupambanua jinsi baadhi ya istilahi zinavyogusa hisia za kimageuzi kuhusu ulemavu katika anga za kimataifa. Pamoja na uzingativu huu, jitihada zimefanyika za kuweka uwiano ili kukwepa kigezo cha hisia kutopotosha lugha lengwa, na kutopunguza kiwango cha uelewa mpana wa hitilafu za kimaumbile na kisaikolojia zilizo miongoni mwa binadamu. Katika baadhi ya misemo, mpangilio wa sarufi kimatumizi ndio huamua kama ni chukizo au la. Mathalani, matumizi ya a, the na ic katika lugha ya Kiingereza, huchangia sana katika kuamua maana ashirifu. Msimamo wa watu kwanza hupendelea mathalani, watu wenye ulemavu badala ya yule kilema au mtu mwenye uziwi badala ya mtu kiziwi. Yote kwa yote, msisitizo kwenye matumizi ya istilahi na misemo, sharti uwekwe kwenye adabu lugha kwa maana ya kujali hisia za msikilizaji au mtajwa. Kwa kuendana na hisia za walio wengi, chapisho hili limejitahidi kuonyesha dhahiri na kutolea maelezo istilahi na misemo inayochukuliwa na wengi kwenye uga wa ulemavu kuwa ni chukizo na kuyawekea alama ** kama utambulisho maalumu. Hata hivyo, kwenye maeneo machche, mitajo yenye kubishaniwa imebakizwa kwa lengo la kuepuka upotoshaji au kuficha aina nyingine za ulemavu. Kwa wanaharakati wenye ulemavu walio makini, wataichukulia Kamusi hii kama zana yenye kuchapuza kasi ya kudai mabadiliko. Hii inatokana na imani ya muda mrefu ya kwamba lugha hubeba dhamira. Yaani, jinsi mawazo ya mtu yalivyo kuhusu jambo fulani, hudhihirishwa na lugha anayoitumia. Kimwandamano, hali hii hujitafsiri kwenye matendo, kisha hujenga mtazamo, tabia, mila, na utamaduni. Tofauti kati ya mhusika kujibatiza mwenyewe na kubandikwa jina na wengine, ni kuwa katika hali ya kwanza (ya kujibatiza mwenyewe), agh. mhusika huegemea kwenye kudhibitisha uwezo na matamanio yake. Lakini kwenye hali ya pili (ya kupachikwa jina na watu wengine), dhamira huwa ni utani (lakabu) au/na kuakisi ghadhabu za wanajamii dhidi ya hali ya mhusika. Majina kama hayo hubeba maana ashirifu hasi ya kejeli na utwezaji kwa kujiegemeza kwenye kile kinachochukuliwa kuwa hitilafu, kutoweza na chukizo. Katika historia ya ulemavu duniani, upachikaji huu wa majina ndilo lilikuwa chimbuko la falsafa ya udhibitihali (eugenics). Hii ni sayansi ya uchunguzi kwa dhamira ya kuboresha uzao hususani wa binadamu; xvii

18 yaani, kuruhusu tu watu waliochaguliwa kimakini ndio pekee wazaliane. Falsafa hii haivumilii kasoro zozote za kimaumbile, milango ya fahamu, na mivurugiko ya akili. Kwa maana hiyo, falsafa hii imekuwa ikichochea moyo wa harakati miongoni mwa watu wenye ulemavu kwa wao wenyewe kujitazama upya na kubaini kuwa madhila yao kwa kiasi kikubwa, hayatokani na vilema walivyonavyo, bali mitazamo ya wanajamii wasio na kasoro bayana. Kwa maana hiyo, chaguo la mkabala wa kupambana na falsafa za udhibitihali na upachikaji majina ni mchakato wezeshi na ndio uliochochea madai ya kuwa na Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu. Kutokana na ukweli huu, umuhimu wa kuwa na Kamusi ya Ulemavu haubishaniwi. Kwa kuwa Kamusi hii ni toleo la kwanza kabisa katika uga wa ulemavu, ni wazi utafiti zaidi kwenye uga huu bado unahitajika sana; halafu kuandaa na kuchapisha matoleo mapya ili kupunguza nakisi iliyopo ya ufahamu wa suala zima la ulemavu hususani katika lugha ya Kiswahili na utamaduni wa Kiafrika. xviii

19 Aa abacus: abakusi: kibao maalumu chenye shanga kinachotumiwa kuwasaidia wanafunzi (wasioona na wengineo) kuhesabia. abandon: telekeza: acha bila uangalizi, kujiachia, kutojali kabisa, kutekwa na hisia za kutenda bila makini au kujali kitakachotokea. abandonment: utelekezaji: hali ambapo mzazi mmoja au wote wawili huondoka na kumwacha mtu mwenye ulemavu bila uangalizi wowote. Hali hii kwa kawaida huwapata watoto wanaozaliwa na vilema. abasiophilia: abasiofilia: mawazo nafsi ya kuvutiwa kingono na watu wenye ulemavu wa ujongeaji, hususani wale wenye kutumia nyenzo za kujimudu kama vile bangiligango za miguu, vitimwendo, n.k. Hii ni hali ya kisaikolojia inayoweza kuchochea ukatili wa kingono kwa maana ya vitendo vya kubaka na ulaghai dhidi ya watu wenye ulemavu wa viungo. abdomen: fumbatio: 1. sehemu ya mwili vilipo tumbo, ini, utumbo, via 1 vya uzazi. 2. sehemu ya mwili ambayo ina uwazi ndani iliyo kati ya kiwambo na fupanyonga. i ability: uwezo: hali ya mtu kuwa na nguvu ya kiutendaji kwa maana ya kung amua, kuamua, kutumikisha akili na maungo katika kutekeleza jambo linalokusudiwa. Agh. mtu mwenye ulemavu hudhaniwa kuwa hana uwezo kwa kuangalia maumbile yake bila kujali ubunifu, vipaji na vipawa. able-bodied: -enye kujimudu kimwili au kiakili:** hali ya kuwa na uwezo wa kimwili na kiakili inayowezesha kutimiza jambo fulani. Wakati mwingine usemi huu hutumika visivyo kama kinyume cha mlemavu. Halikadhalika virai kama vile mtu mwenye ulemavu kinyume chake siyo sawa na mtu mwenye kujiweza. Kinyume kinachopendekezwa kwa mlemavu ni asiye na ulemavu au mtu bila ulemavu. abnormal: uatilifu: -enye ulemavu au kasoro ya kiungo cha mwili, kisaikolojia au afya ya akili. Mazoea ya kupambanua watu kwa msemo wa mtu wa kawaida na mtu asiye wa kawaida ni potofu, kwa muktadha wa uanuwai, kwani ukawaida ni dhahania ambayo hutegemeana na hali. Mathalani, mtu mwenye ulemavu tangu kuzaliwa kwake hivyo alivyo ndio ukawaida wake. Kwa maana hiyo, ni makosa kumchukulia kama

20 asiye wa kawaida akilinganishwa na mtu mwingine asiyekuwa na hali kama yake. abnormal bleeding: hedhi atilifu: damu ya mwezi (kwa mwanamke wa umri kati ya miaka tisa na 50) ambayo inaweza kutoka nyingi au kidogo kuliko kawaida. Pia kuzidisha au kupungua kwa siku za hedhi bila sababu dhahiri nayo huchukuliwa kuwa ni uatilifu. abrogate: futa: 1. tangua, batilisha, vunja, tengua 2. tangua amri au sheria iliyotolewa na mamlaka ya chini, 3. acha, komesha. ii abstract intelligence and reasoning: taamali dhahania: 1. uwezo wa kiakili wa kuelewa uhusiano na kutoa mwitiko, na siyo tu kwa vitu vyenye kushikika ila hata vile visivyoshikika kama vile dhana, mawazo, taswira, ishara, n.k. Kujisadikisha ni mchakato wa kuchagua au kutenga jambo fulani kutokana na vile vinavyoshikika; mathalani mabata wote ni ndege, ila siyo ndege wote ni mabata. 2. wazo au hali ya kusadikika, alama au kitu ambacho kinaweza kuchaguliwa kutokana na sifa maalumu za kimazingira. 3. jambo au kitu cha kuwazika na kisichoweza kushikika na kueleweka kwa urahisi abuse: nyanyasa: tumia vibaya haki mamlaka, au wadhifa, kumuonea au kumdhalilisha mtu au kumlazimisha kutenda jambo bila hiari na agh. kinyume cha maadili. 2 Kwa ujumla matendo yafuatayo yanaangukia kwenye kipengele hiki: dhulumu, shambulia kwa matusi, maneno machafu au makali, onea; tabia mbaya; potoa, danganya; najisi; baka, dhalilisha. iii Mtu mwenye ulemavu ni mwathirika mkuu wa hali hii ikiwa ni pamoja na kupachikwa majina bainishi yenye kudunisha. abuse of rights: ukiukwaji wa haki: 1. hali katika sheria za kimataifa inayotokea wakati nchi moja inapojipa haki kiholela na kwa udhalimu katika hali inayotesa au kuumiza nchi nyingine iv ; 2. hali ya mtu kumkataza mtu mwingine kufanya jambo ambalo ni stahiki yake. abusive and insulting language: matusi na lugha safihi: kauli yenye kutumia maneno yanayomshushia hadhi na heshima au kumuudhi mtu mwingine. Hali hii ni ya kawaida kumtokea mtu mwenye ulemavu pale jumuia inapotumia misemo na lugha visivyojali hadhi na hisia zake katika kumtambulisha. academic achievement: mafanikio kitaaluma: 1. kiwango cha ustadi katika masomo ya kitaaluma 2. kwa mtu mwenye ulemavu wa akili humaanisha kiwango cha uelewa wa ujuzi wa kufanya shughuli za kila siku maishani. academic content and assessment: maudhui ya kitaaluma na upimaji:

21 dhana ambazo hutumika zaidi katika kuamua mustakabali wa mtu mwenye ulemavu kielimu. accede: kubali: jiunga, ungana na/au ridhia, pata cheo au wadhifa. v acceptability: ukubalifu: hali ambayo huamua kiwango cha mtu kuchangamana na wanajumuiya na wanajamii wenzake. Hali hii ndicho kikwazo cha msingi ambacho humkwaza mtu mwenye ulemavu kwa kutokubalika kama alivyo ikiwa ni sehemu ya uanuwai wa kimaumbile. access: fikia au patikana: 1. ufaaji wa jengo au miundombinu mingineyo kwa jinsi matumizi ya watu wote wakiwemo wenye ulemavu yanavyozingatiwa. Katika maana pana, ufikiaji pia hujumuisha kufanya mitindo ya maandishi na taarifa kufikiwa na mtu mwenye ulemavu wa uoni au utambuzi; kutengeneza kamsa (ving ora) vinavyofikiwa na kiziwi au mtu mwenye usikivu hafifu na kuzifanya huduma kama vile elimu na usafirishaji kufikika kwa mtu mwenye ulemavu. 2. kisheria humaanisha ruhusa, njia, uwezo wa kufikia sefu; uwezo wa kuwasiliana; kujamiiana (mke na mume); kuongezeka, kulimbikiza. 3. namna huduma za kiafya na nyinginezo za umma zinavyoweza kupatikana kiurahisi kwa mtu mwenye ulemavu access aisle: ushoroba fikivu: nafasi katikati ya vitu (kama vile 3 maegesho, safu za viti kwenye majengo ya umma, (mfano nyumba za ibada, kumbi au chanja kwenye maduka makubwa au madawati darasani), kwa ajili ya ama kupitia au kufikia na kutumia vifaa au huduma. Ushoroba au uchochoro wa aina hii hutakiwa kuwa na uwazi unaostahili ili kuwezesha matumizi ya vitu na huduma stahili kufikiwa na mtumiaji ikiwa ni pamoja na yule mwenye kutumia kitimwendo. access audit: hakiki ufikivu: ukaguzi wa kina unaofanywa na mtaalamu wa kujitegemea kwenye jengo au miundombinu mingine ili kubaini ubora wake kwa matumizi ya mtu mwenye ulemavu. access device: zana fikivu: kifaa mahususi au methodolojia ambacho humwezesha mtu asiyeona au mwenye uoni hafifu kupata maarifa na kutumia taarifa na fursa zinazopatikana kiurahisi kwa watu wengine. Mathalani: a) matumizi ya nuktanundu au maandishi yaliyokuzwa kwa kusoma na kuandika, b) vifaa vya nyumbani vilivyowekewa alama mahususi, c) saa za mkononi na za mezani au ukutani zinazotoa sauti ili kuashiria wakati au kutoa taarifa kama vile adhana. accessibility: ufikivu au patikanaji: kiwango ambacho jengo au miundombinu mingine, huduma zote za kijamii inavyojali ufikiwaji (hususani) na mtu mwenye

22 ulemavu. Nchini Tanzania suala hili kimsingi linaamuliwa na sheria namba 9 (2010) ya watu wenye ulemavu na kanuni zake. accessible assistance: usaidizi patikanivu: utayari wa mtu kumsaidia mtu mwenye kuhitaji msaada kutokana na hali yake ya ulemavu; mfano, usindikizwaji kufika sehemu anakohitaji kwenda. accessible formats: miundo fikivu au patikanivu: vitu ambavyo humwezesha mtu mwenye ulemavu kufanya shughuli mbalimbali ambazo ni pamoja na: maandishi ya nuktanundu, maandishi yaliyokuzwa, vielelezosauti, matini ya kielektroni, vielelezompapaso na vitu vyote vya aina hiyo kwa ajili ya mawasiliano. accessible print (18 Pt. Or Larger) maandishi fikivu au yaliyokuzwa: maandishi yaliyoandikwa kwa herufi zenye ukubwa wa fonti18 au zaidi zinazosomeka kiurahisi na watu wenye uoni hafifu. accessible route: njia fikivu: sehemu ya kupitia bila vikwazo kuelekea kwenye vitu, vifaa na maeneo ndani au nje ya jengo. Njia za ndani za kufikia zinaweza kujumuisha ushoroba, ghorofa, ngazimbetuko, vipandishi (mfano lifti), maeneo yaliyo wazi pale palipo na vifaa vya kudumu. Njia za ufikiaji nje ya jengo zinaweza kuhusisha maegesho, kingo za barabara, vivuko milia vya barabara, ngazimbetuko na vipandishi. accessible toilet: msalani fikivu: msalani wa umma: sehemu za mwaliwato na vyumba vya kubadilishia nguo vyenye kutumiwa na umma vinatakiwa kuwa na sehemu ya ziada ambayo ni huria (yaani, isiyo na jinsi maalumu) inayofikiwa bila kuingiliana na sehemu za jinsi ya kike wala ya kiume. Sehemu hii ni kwa matumizi ya mtumia kitimwendo au jinsifiche ili inapobidi kumwezesha kuingia maeneo hayo akiandamana na msaidizi hata wa jinsi tofauti bila kuvunja desturi na maadili (ang. intersex). vipimo Mpangilio wa chumba uwe ukubwa wa walau mita 3x4 ili kuruhusu mizunguko ya kitimwendo au hata mtu wasiyeona. 4

23 Mambo muhimu ya kuzingatiwa ni pamoja na: mlango kufunguliwa kwa nje au wa kuteleza sambamba na ukuta ukiwa na sehemu ya kufungulia kwa dharura kutokea nje; sehemu ya kuwashia taa kutozidi kimo cha milimita 1200 juu ya sakafu; eneo la wazi la milimita 800 kufikia bakuli la choo ili kuruhusu kitimwendo; choo imara cha kukalia kisichozidi urefu wa milimita 500 kutoka sakafuni kikiwa imesimikwa mathubuti na kuwa na fitogemeo za chuma au plastiki ngumu pembezoni zilizosimikwa milimita 800 toka sakafuni; beseni la kunawia mikono lililosimikwa kimo cha milimita 830 toka sakafuni likiwa na bilula ya maji baridi iliyo jirani zaidi kiasi cha kufikiwa kwa mkono kutokea kwenye bakuli la choo na uwazi wa milimita 630 chini yake kwa ajili ya nafasi ya magoti (kwa mtumia kitimwendo) wakati wa kunawa. Kioo cha kujitazamia wakati wa kunawa mikono kilichosimikwa kwenye kimo cha milimita 830 kutoka sakafuni. Bakuli la kuhifadhia sabuni na vifaa vya kujikaushia mikono vilivyotundikwa karibu kiasi cha kufikiwa kutokea kwenye bakuli la choo au kwenye kitimwendo. chumba manyunyu na bafu Kwenye nyumba za kibiashara na kuishi (ikiwa ni pamoja na mabweni) vyumba vya kuogea (hamamu) vinatakiwa kuwa ndani ya chumba cha kulala mtumia kitimwendo na wengineo wenye vilema vya ujongeaji ili aweze kujikausha na kuvaa wakiwa kitandani na kwa faragha. Sehemu za hamamu sharti zizingatie pamoja na mengine vipimo sawa na vile vya kwenye msalani. Mteremko wa sakafu uwe 1:80 kuelekea eneo la kutolea maji machafu. Kuwepo na bilula moja ya kurekebishia joto la maji kabla na wakati wa kuoga; Iiwepo bafu kwa ajili ya yule asiyeweza kuoga akiwa amesimama. accessible tourism: utalii fikivu: mchakato wa kumsaidia mtu mwenye mahitaji mahususi kutambua vitu au kutenda bila utegemezi na kwa usawa na heshima ili kufurahia siku za mapumziko na wasaa wa kuburudika bila kukwazika wala kutatizika. accessible web design: usanifu wa wavuti fikivu: uundaji wa kurasa za kimtandao kufuatana na kanuni husika za dunia kwa ajili ya wote; hii ni pamoja na kupunguza vizuizi kwa mrambazaji mwenye ulemavu. 5

24 accessible: -a kufikika: 1. enye kuruhusu vifaa kutumiwa na mtu mwenye ulemavu bila shida. 2. -enye kuwasilishwa katika hali ambayo mtu mwenye ulemavu anaweza kujumuishwa kwa kuhitaji au kutohitaji usaidizi. 3. -enye kufikiwa katika hali ambapo teknolojia ya kompyuta inatumiwa na wote ama kwa usaidizi au bila usaidizi. Kutokana na matakwa ya Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu, suala zima la ufikikaji ni la faradhi. accession: kujiunga: kuingia katika mkataba wa kimataifa baada ya kupitishwa na nchi wanachama wa mkataba unaohusika. accident: ajali: tukio lisilotarajiwa ambalo husababisha madhara. accommodate: afiki: kubadilika kimwenendo, kimfumo au kimtazamo kwa lengo la kuleta makubaliano au kumaliza tofauti. accommodation: uafikishaji: 1. kufanya mabadiliko ya mwenendo, mazingira, muundo au mtazamo ili kuleta makubliano au kumaliza tofauti zilizopo. 2. urekebishaji: kufanya mabadilisho ya lazima na yanayofaa, kutokana na mahitaji mahususi ya mtu mwenye ulemavu, ili kuhakikisha kuwa ananufaika au kutumia haki zote za binadamu na uhuru wa msingi kwa kiwango sawa na wengine. 3. malazi: nyumba au vyumba vilivyo tayari kukaliwa au kupangishwa, 4. fadhila, hisani, maafikiano, uridhiano. accreditation: utambuzi rasmi: 1. idhini rasmi ya kutambuliwa kuwa balozi, asasi, mfanyakazi wa nchi au chombo husika. vi 2. kutambuliwa hasa kwenye shughuli za kiitifaki mathalani, kuteuliwa rasmi kuwa mwakilishi wa nchi au serikali kwenye shughuli za kibalozi ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mikutano ya Umoja wa Mataifa. acculturation: utamadunishaji: ufungamanishaji wa watu na fikira, mila na desturi ngeni. achievement: mafanikio: utimizwaji wa malengo au mikakati. achievement discrepancy: tofauti kimafanikio: hali ya kuhitilafiana baina ya utendaji halisi wa mtoto na vipimo vya uwezo alionao. Msamiati huu hutumika zaidi kwenye ulemavu wa ujifunzaji na kiujumla hurejea kwenye kiwango cha chini cha ufanisi kitaaluma kuliko ilivyotarajiwa. acouaesthesia: akoestezia: 1. usikivu wa sauti vii 2. hali yenye kuhusika na mtu kupoteza fahamu ya usikivu kwa kiwango kikubwa. acoupedic method: stadi matamshi: mbinu ya kumfundisha mtoto mwenye uziwi namna ya kuongea na kutumia usikivu alionao. Inasisitizwa kuwa mafunzo ya kusikia yaanzishwe mapema na 6

25 yatumike peke yake badala ya kuyaunganisha na yale ya kuona. acoustic aid: kisaidizi cha kusikia: kitu au mbinu yoyote ya kumrahisishia mtu kusikia sauti (mf. shimesikio). acoustic: -a kusikika: -enye kuhusiana na sauti. acrotomophilia: akrotomofilia: hali ya mtu na kuwa na hisia za kuvutiwa mno kingono na mtu aliyekatika viungo. Hali hii inaweza kuchochea unyanyasaji kingono. acromania: akromania: hali ya mtu kuchanganyikiwa akili ambayo huambatana na kutotulia na kwa kawaida huitwa uendawazimu**. viii Tafsiri hii ni yenye kukiuka kanuni ya adabu lugha na akhlaki za ulemavu. Kiujumla tafsiri hii ni yenye mrengo wa kitabibu na kihisani ambayo haijali hisia za mtajwa. active learning: ujifunzaji amilifu: upatikanaji wa elimu ya somo kivitendo ambao ni mtindo unaopendekezwa kutumika katika mazingira ya ujumuishaji kielimu ili kumnufaisha zaidi mwanafunzi mwenye ulemavu hususani wa akili. activities of daily living: stadi za kila siku: shughuli za mtu kwa siku ikiwa ni pamoja na: kumudu kujivalisha nguo, kujitandikia kitanda, kujiosha mwili, kujinyoa, kujichana nywele, kujilisha, kujitengenezea kinywaji na shughuli zote za aina hiyo ambazo humwezesha mtu mwenye ulemavu kutenda kwa kiwango cha juu kabisa cha uwezo wake ndani ya familia na jamii. activity: shughuli: katika uga wa ulemavu, shughuli hujumuisha pia viwango vya uwezo wa kiutendaji wa maungo ya mwili na milango ya fahamu (yaani kutumia nguvu na akili ili kujitegemea au kwa kiwango fulani kutimiza stadi za kila siku). activity based: -a kujikita kwenye vitendo (angalia ujifunzaji amilifu). acute: kali: -enye kutokea ghafla na maumivu makali yanayoweza kudumu kwa kipindi kifupi. (linganisha na usugu mathalani, ugonjwa sugu au msendeko). ad hoc: -a shughuli mahsusi: jambo au kikao kinachohitaji utekelezaji wa haraka kinachofanyika kwa sababu maalumu. Pia a dharura. ix ad hoc committee: kamati mahsusi: kamati ya muda inayoitishwa kujadili jambo moja mahsusi au lisilopaswa kufuata utaratibu uliozoeleka. x 7

26 adapt: rekebisha: 1. badili, tengeneza; tohoa (ili kufaa matumizi fulani) xi. 2. kitendo cha kurekebisha ili kukidhi manufaa fulani. xii Katika hali ya usanifishaji bidhaa, mazingirajenzi na huduma usiozingatia uanuwai wa watumiaji, hulazimisha urekebishaji ili kukidhi mahitaji. adaptability: urekebishikaji: uwezekano wa miundombinu na huduma za kijamii kufanyiwa marekebisho ili kuweza kukidhi mahitaji ya mtu mwenye ulemavu wa aina na viwango tofautitofauti, mathalani, meza za jikoni, beseni za ukutani za kunawia mikono au kuoshea vyombo, (fitogemeo) kuwa na vimo anavyoweza kuvifikia mtumia kitimwendo, mwenye kimo kifupi, n.k. adaptation: urekebishaji: 1. mchakato wa kubadilisha ili kuendana na mazingira au mahitaji mapya 2. ubadilishaji wa vifungu fulani vya sheria ili kuifanya sheria hiyo iweze kutekelezeka kulingana na mazingira halisi. adaptive: rekebifu: uwezekano wa kukibalisha kitu kutoka hali yake ya awali na kukifanya kiendane na mahitaji mapya yaliyo mahususi kwa mtu, kikundi, mazingira, n.k. adaptive behaviour: mwenendo rekebishi: 1. jumla ya stadi za kidhana, kijamii, na kivitendo ambazo mtu hujifunza na kuzitenda katika maisha yake ya kila siku. 2. uwezekano wa kubadili tabia au mwenendo pale inapobidi ili kuendana au kukabiliana na hali fulani mpya. adaptive equipment: kifaa rekebifu: zana iliyobuniwa au kuongezwa kwenye kifaa kingine ili kuboresha utendaji kazi kwa kutilia maanani uwezo wa kimaumbile, matumizi ya nishati, uchangamshaji au uburudishaji, rasilimali, muda na nafasi vinavyohitajika kwenye utumiaji. adaptive learning environments programme (ALEP): Programu ya Mazingira Rekebifu ya Ujifunzaji: programu kwa ajili ya mwanafunzi mwenye mvurugiko wa ujifunzaji ambayo imeandaliwa katika msingi wa dhana iliyofanyiwa marekebisho ili ifae kulingana na muktadha wa mhusika. 8

27 adaptive physical education: Elimu Maungo Rekebifu: elimu ya kuzoeza viungo ambayo imerekebishwa ili kukidhi mahitaji ya kipekee ya mtu mwenye ulemavu na vijana. adaptive fit: urekebifu sawazishi: hali ya kubadilisha kitu au jambo kwa minajili ya kuleta ulinganifu na hali ya kitu kingine. adaptive technology: teknolojia rekebifu: kitu chochote au mfumo uliobuniwa mahususi kwa ajili ya kuongeza, kuimarisha uwezo wa mtu mwenye ulemavu; agh. hurejelea ufikiaji na upatikanaji wa teknolojia ya kielektroni na habari. Kimsisitizo, teknolojia rekebifu hujumuisha vitu vyote vilivyosanifiwa makusudi kwa ajili ya mtu mwenye ulemavu na ni nadra kutumiwa na mtu asiyekuwa na ulemavu (taz. alternative input device ). addiction: uraibu: kujishughulisha kabisa na kitu ambacho mtu hujenga tabia inayomshurutisha kukiegemea. Kitu hicho kinaweza kuwa kemikali, mtu mwingine au shughuli (k.m. kuangalia televisheni, au kazi, matumizi ya mihadarati). Kuacha mazoea yale au kujihini kunaweza kusababisha dalili za kujitenga. adjust: rekebisha: sawa na boresha adoption: kuasili: 1. uhalalishaji wa mtoto usiyemzaa kutoka tumboni mwako awe wako kwa mujibu wa sheria za nchi husika au mahali pa asili ya mtoto. 2. kukubali azimio au wazo, 3. kuchukua au kutwaa na kutumia. xiii 4. pokea na ridhika na uamuzi uliofikiwa na ama mahakama au mkutano, pitisha hoja/kumbukumbu/ajenda. xiv adrenalin: adrenalini: 1. kichocheo chenye uwezo wa kusisimua mfumo wa neva. Huongeza msukumo wa damu, mapigo ya moyo na mabadiliko mengine ya kimwili yanayohitajika ili kuitikia hisia k.m. za kupigana au kukimbia. 2. mojawapo ya homoni zinazotolewa na tezi ya adrenali. xv adventitious deaf-blindness: uziwipofu nasibu: hali yoyote ya kupoteza hisia za vionjo au fahamu za kuona na kusikia baada ya kuzaliwa kutokana na 9

28 ama maradhi, maambukizo, ajali au mikasa mingineyo. adventitious impairment: kilema nasibu: hali ya kupatwa na kilema baadaye maishani ambacho hakikudhihirika wakati mhusika alipozaliwa na hivyo kutohusishwa sana na kuwa hali ya kurithi bali vichocheo vya nje (kwenye mazingira). advocacy: utetezi (pia uraghbishaji au uchechemuaji): 1. mchakato wa kutoa kauli dhabiti, kuandika kuhusu kuunga mkono au/na kutenda kwa niaba ya mtu au kundi ambapo mtetezi mwenyewe huwa hana maslahi ya moja kwa moja na matokeo ya anachokitenda; mathalani, mtu mzima kutetea haki za watoto, mwanamume kujihusisha na haki za wanawake, mtu asiye na ulemavu kutetea haki za mwenye ulemavu, utetezi wa haki za wanyama, n.k. 2. uraghbishaji ni msukumo wa ndani ya mtu wa kumchechemua mwingine ama aendeleze au aachane na jambo fulani kwa manufaa ya jamii au katika kuendeleza imani na maadili fulani (ilhamu, au kichocheo cha ndani ya nafsi ili kujitolea kufanya jambo); mathalani, kushawishi mtu aachane na matumizi au biashara ya mihadarati, kutunza mazingira, kudumisha desturi ya kujiwekea akiba, kujiunga na aina mbalimbali za ushirika na mifuko ya hifadhi ya 10 jamii, n.k. 3. mchakato wa kuunga mkono na kuwezesha mtu kujiunga na wenzie ili kwa pamoja waweze kuelezea maoni yao, kutafuta na kupata habari na huduma, kujua aina za chaguo zilizopo ili kufanya uamuzi na kuzipigania haki zao. advocate: mwanaharakati: mtu yeyote anayesema au kutenda kwa ajili yake mwenyewe, kwa niaba ya mtu mwingine au ilhamu. 2. kuhusiana na mipangilio ya makazi, ni mtu au taasisi itakayokuwa rafiki na kuangalia maslahi ya mtu mwenye ulemavu. Katika hali fulani ambapo mtu mwenye ulemavu anamudu kusimamia mambo yake mengi, wakili kutoka asasi ya hisani (ya msaada wa kisheria) anaweza kufaa zaidi kuliko mwangalizi mlezi kisheria. 3. mtu ambaye anaweza kuwa au kutokuwa na ulemavu ambaye anamsemea au kuingilia kati au kutetea mtu mwenye ulemavu. affect: afekti: mhemko wenye kuelezwa au kujidhihirisha hima. Hali ya kuhisi hugeuka afekti pale inapoonekana; mathalani, kujidhalilisha na kubadili sauti kwa jumla. Afekti inatofautishwa na sununu (hali ya uchangamfu au masononeko) ambayo humaanisha mhemuko unaoendelea kusambaa. Afekti ilivyo kwa sununu ni sawa na inavyokuwa kwenye hali ya hewa na tabia ya nchi. Mifano ya kawaida

29 ya afekti ni nishai (uforia), hasira, na huzuni. affirmative action: sera ikibali: 1. hatua nzuri ya makusudi inayochukuliwa kwa lengo la kuondoa ukandamizwaji. 2. hatua mahsusi inayochukuliwa kwa ajili ya kupunguza hali inayotokana na ukandamizaji uliofanyika siku za nyuma au inayotokana na ukiukwaji wa sheria. affirm: kiri: tamka kwa dhati kukubaliana na kauli ambayo mtu aliwahi kuitamka awali. afterbirth: kondo la nyuma: utando maalumu ulio katika tumbo la uzazi mahali ambapo mtoto huhifadhiwa akiogelea kwenye giligili na kupokea chakula kupitiia kiungamwana kinachoshikamana na ukuta wa uterasi. Utando huu hupasuka na kumwaga giligili muda mfupi kabla ya mtoto kuzaliwa na wenyewe husukumwa nje mara baada ya mtoto kuzaliwa. aggression: ushari: tabia ya kumkerehesha mtu ambayo inadhihirishwa ama kwa vitendo au matamshi. Haya ni mashambulizi ya dhahiri au kificho. Kwa mfano, matumizi ya utani, kutesa, kutenga, kunyonya, kukasirikia, uhasama, kulipiza kisasi kama njia ya kudhihirisha hisia za kero au maudhi dhidi ya mtu mwenye ulemavu n.k. aggressive and coercive behaviour: tabia ya ushari na ushurutishaji: hali 11 ya mtu kuwa na silika ya kumuudhi mwenzake kwa kumlazimisha kufanya jambo pasipo hiari. aggressive behavior: tabia ya mtu kuwa mgomvi. albino: albino: kiumbe ambacho kimekosa rangi yake asilia kama vile ya ngozi au ya manyoya kutokana na hitilafu ya vinasaba. (ang. melanini). Miongoni mwa binadamu wenye ngozi nyeusi, ualbino hujipambanua zaidi na hivyo kumfanya mhusika aonekane mastaajabu. Kutokana na dhana hiii, mhusika amekuwa akipachikwa majina yenye kutweza kama vile zeruzeru**, mlemavu wa ngozi**, mzungupori**, mtu aliyebadilishwa na shetani**, n.k. albinism: ualbino. Utohozi wa albinizimu kumaanisha mtu mwenye hali hiyo siyo sahihi. alfatory nerve: nevanusishi: mshipa wa fahamu unaosafirisha harufu kutoka puani na kuipeleka katika ubongo. allergy: mzio: 1. tatizo kama vile mwasho, kupiga chafya, mabaka ya ngozi, ukurutu na wakati mwingine ugumu wa kupumua au mshtuko ambavyo huwaathitri baadhi ya watu pale ambapo kitu fulani hupulizwa, huliwa, huingizwa mwilini au huguswa. 2. hali ya mwili ya kutendana kupita kiasi dhidi ya dutu fulani punde dutu hiyo inapoingia mwilini k.v. kupumua kwa shida, uvimbe wa

30 ngozi, kuwashwa, kuharisha, n.k. xvi allergic reaction: mjibizomzio: mwitikio usiohiari wa mwili baada ya kupokea vitu visivyotakiwa. allergic shock: mshtukomzio: kiwango cha juu cha mjibizo unaotokana na mzio. alternative input device: kitumi mbadala: kitu kingine kinachomwezesha mtu kutumia kompyuta yake kwa njia nyingine zaidi ya kicharazio cha kawaida k.m kicharazio mbadala. alternative keyboard: kicharazio mbadala: kifaa chenye ama umbo dogo au kubwa kuliko vicharazio vya kawaida na hata mpangilio mbadala ili kuruhusu kutumia mkono mmoja. Vitumi vingine vya aina hii ni pamoja na: kitumi oneshi cha kielektroni; usukani fimbochombeza: -mfumo pumua; skrini mpapaso; kitufe sogezi; kirungu na fimbo mpapaso. alternative formats: miundo mbadala: njia mbalimbali za kuwasilishia ujumbe kiasi kwamba wanajamii wengi waupate na kuuelewa vilivyo. Miundo hii ni pamoja na: vitabu, majarida, magazeti sikika, na matini ya kompyuta sikika. 12 Alzheimer s disease: ugonjwa wa Alzema: ugonjwa usio na tiba wa usawijikaji mfululizo wa ubongo unaoweza kuhusisha dalili mchanganyiko zikiwemo za deliriamu, kuchanganyikiwa na kuvurugika kwa tabia. Ugonjwa huu hauhusiani na mchakato wa kawaida wa kuzeeka. amblyopia: ambliopia: 1. uoni hafifu au upofu kabisa wa jicho wenye kusababishwa na hali inayoathiri ukuaji wa kawaida wa uoni. Hali hizi ni pamoja na makengeza ambapo macho ama hukingama kuelekea ndani (esoforia), kuelekea nje (eksoforia) au anisometropia ambapo kunakuwepo na tofauti kubwa kwenye makosa ya uchepukaji kati ya macho mawili ya uoni karibu na uoni mbali au uastigimati. Visababishi vya nadra vya ambliopia hujumuisha tosisi mojawapo ya mboni za jicho, ugonjwa wa konea (kwa kuzuia mwanga kupenya kwenye jicho), kuzaliwa na mtoto wa jicho, na mtoto mchanga kuumia jicho. 2. kutoona vyema ambako hakutokani na lesheni bayana katika jicho. xvii ambliopia alcoholic: ambliopia ulevi: kutoona vema kutokana na ulevi. xviii amblyopia toxic: ambliopia ya sumu: hali ya kutoona vizuri kutokana na madhara katika jicho

31 yanayosababishwa na aina fulanifulani za metali k.v. plambi na thaliumu au dawa (mathalani, krolokwini) na egoti kwa matumizi ya pombe au tumbaku. xix ambulant disabled person: mtu mwenye kudemadema: 1. mtu ambaye kwa kusaidiwa na msaidizi au bila msaidizi anamudu kujikongoja kwenye sehemu ziliyosawazishwa, au kupanda ngazi zilizoboreshwa kwa kutegemea viungo bandia (mathalani, kalipa, fimbo au aina nyingine ya wenzokongojea), na uwepo wa fitogemeo. 2. mtu mwenye kudemadema humaanisha yule ambaye anapungukiwa na uwezo wa kutembea kutokana na ukomo wa maumbile (fahamu au ujongevu), uzito wa ubongo, umri, maradhi, au sababu nyingineyo ya ulemavu ambayo kwa hali yake huzua changamoto wakati wa kutumia vyombo vya usafiri kiasi cha kulazimu kupata uangalizi maalumu na kuhitaji urekebifu wa huduma zitolewazo kwa wote ili kuendana na mahitaji ya mhusika. ambulift: liftitanga: aina ya gari kama lile la kubebea mizigo ambalo limesanifiwa maalumu ili kuhakikisha viwango vya juu vya usalama na utoaji huduma bora kwa abiria aliye na ulemavu(kwenye kiwanja cha ndege), mgonjwa, mzee, anayetumia kitimwendo, kabla na 13 baada ya safari ili kupanda na kushuka kwenye ndege. Abiria mwenye ulemavu husogezwa kwenye ndege kwa kupandishwa ndani ya gari maalumu kupita mlango wa nyuma na kupandishwa kwa ngazi (zinazoshuka na kubeba abiria na kitimwendo hadi ndani ya gari). Kisha hunyanyuliwa hadi usawa wa mlango wa ndege, na hivyo kuweza kusogeza kitimwendo hadi ndani ya ndege. Ili kufika kwenye kiti chake alichopangiwa, aina nyingine ya kitimwendo (kidogo) hutumika ili kupita kiurahisi kwenye safu za viti ndani ya ndege. amnesia: amnesia: hali ya usahaulifu wa matukio ya nyuma hususani yale yaliyoambatana na aina fulani ya majeraha kwenye ubongo. xx amputee: mkatwa kiungo: mtu aliyekatwa kiungo cha mwili au zaidi hususani mkono na mguu. Istilahi za kawaida za kumtambulisha mtu mwenye hali hii ni k.v. kiguru**,

32 kikono**, kibubutu** na kibugutu** ambazo hukiuka kanuni ya adabu lugha na akhlaki za ulemavu. Kiujumla hii ni tafsiri yenye mrengo wa kitabibu na kihisani ambao hauzingatii adabu lugha na kujali hisia ya mtajwa. androphobia: androfobia: hali inayompata mtu wa jinsi ya kike ya kujenga hofu ya kudumu dhidi ya wanaume. Hofu hiyo hutokana na mwitiko uliokithiri mbao hujipangilia kuashiria hatari. Mwathirika hukataa kuachwa peke yake na mtu wa jinsi ya kiume hata kama ni rafiki au jamaa wa karibu. Hofu hii inaweza kusababisha kuota jinamizi juu ya wanaume, kuathiri kwa kiasi kikubwa ubora wa maisha pale mhusika anaposhindwa kuendesha maisha ya kawaida kwa kukataa kuwa na uhusiano na wanaume au kuhamanika kufanya kazi na wanaume. Visababishi vya hali hii ni vingi ikiwa ni pamoja na kukumbwa na kisa hasi au cha mateso k.v. kubakwa au kunyanyaswa kingono ambacho kinaweza kuhusika na hali ya ubongo kujifunza kujenga taswira za hofu ileile ya wakati wa tukio. anisometropia: anisometropia: hali inayojidhihirisha kwa uwezo wa macho yote mawili kupishana kwa ama jicho moja kuwa linaona karibu wakati jicho jingine linaona mbali au jicho moja kuwa na kiwango kikubwa cha uoni kuliko jingine. Hali 14 hii huwa tata zaidi kwa mtoto mchanga kwani inaweza kusababisha ambliopia (kilema cha uoni wa jicho moja). Pale inapotokea anisometropia kuwa ya kiwango kikubwa, ubongo hushindwa kusawazisha tofauti za sura zinazoletwa na macho yote mawili. Hivyo, huzua upendeleo wa sura zinazotoka kwenye mojawapo ya jicho. Kadiri muda unavyopita, ubongo hupoteza kabisa uwezo wa kuona sura kutoka kwenye jicho lililokandamizwa. anorexia: anoreksia: hali ya kukosa hamu ya kula. Pale hali hii inapotokana na sababu za kimaumbile, husababisha ulemavu kwa mhusika kupata uatirifu wa viungo vingine na kisha kuathirika kiutendaji. anorexia nervosa: anoreksia nevosa: ugonjwa wa kinyurotiki utokeao hasa kwa wanawake vijana ambao hugoma katakata kula na hatma yake ni ukondefu, kusita kwa hedhi na nywele kunyonyoka. xxi anoxia: anoksia: hali ya mtu kupungukiwa oksigeni kwenye damu. ante: kabla: hali fulani inayotokea kabla ya kitu kingine kufuatia. antibiotic: kiuavijasumu: 1. dawa inayotumiwa kupigana na maambukizo yanayotokana na bakteria. 2. enye kuondoa uhai. 3. kemikali inayotokana na vimelea hai

33 hasa kuvu ambayo huzuia ukuaji au huua vimelea vingine. xxii antibody: fingomwili : 1. kitu kinachozalishwa na mwili ili kukabiliana na maambukizo. 2. protini ya mwili iliyo katika seramu hupatikana kwa kurithishwa au baada ya mwili kupambana na antijeni. xxiii antirevirrals: dawa punguza makali: dawa zinazotumika kuwasaidia mtu mwenye virusi vya UKUMWI kwa kuwawezesha kuishi maisha marefu zaidi akiwa na siha njema (ila haziponyeshi UKIMWI). antisocial: ufarakani: hali ya mtu au kikundi cha watu kujitenga au kwenda kinyume na shughuli zinafonywa na kukubalika kufanywa na wanajamii. anxiety: wahaka: wasiwasi, kiherehere, machugachuga, kutojituliza ili kuikabili hali iliyopo au itakayojitokeza. apathy: kutojali: hali ya kutokuvutiwa na jambo fulani na kutofanya jitihada zozote za kubadilisha au kuboresha hali hiyo. aphagia: afagia: hali ya mtu kushindwa kumeza kitu chochote iwe ni chakula au kinywaji kutokana ama na kuumia au mfereji wa chakula kuwa na matatizo. aphasia: afasia: 1. kupoteza uwezo wote au sehemu ya uwezo wa kutamka maneno kwa ufasaha au/na kuelewa maneno yanayosemwa. xxiv 2. kupatwa na tatizo la kushindwa 15 kutumia lugha vizuri linalojidhihirisha kwa mwathirika kushindwa kutambua lugha, msamiati na alama za lugha husika wakati wa kusoma, kuandika au kuongea. Tatizo hili, agh.hutokana na ubongo kudhurika kwa namna fulanifulani, kwa mfano kupata kiharusi, majeraha ya kichwa, au maradhi yanayoshambulia ubongo. Wakati mwingine, tatizo hili huandamana na matatizo mengine kama vile mtu kushindwa kutamka neno ingawa anaweza kuwa anaielewa lugha. apotemnophilia: apotemnofilia: kupenda ngono kutokana na kukatwa kiungo. apraxia: apraksia: hali ya kinyurolojia yenye kubainishwa na kutoweka kwa uwezo wa kufanya shughuli ambazo kimaumbile mtu angeridhia na angemudu kuzifanya. Zipo aina nyingi za apraksia miongoni mwake ni pamoja na: -a shavu na mdomo: hali ya kumsababisha mtu ashindwe kufanya matendo yasiyo ya hiari yanayohusisha msogeo wa uso kama vile kukohoa, kujilamba midomo, kupiga mbinja na kukonyeza; -a msogeo wa viungo: hali ya kushindwa kwa mikono na miguu kufanya misogeo dhahiri. -a dhana: hali ya kukosa uwezo wa kutenda jambo lenye kuhusisha mifuatano ya mijongeo. Mtu mwenye hali hii anaweza kupata shida ya kuvaa, kula, na kuoga; - apraksia undaji: hali ya kushindwa

34 kunakiri, kuchora au kuunda maumbo mepesimepesi; -a msogeo wa macho: hali inayobainishwa na kushindwa au kupata ugumu wa kusogeza macho; -a maneno: hali inayohusisha ugumu wa mpangilio wa midomo wakati wa kuongea. Pia, hujulikana kama apraksia ya matamshi. arbitrary:-a holela: hali isiyo na mpangilio au utaratibu maalumu. arbitrate: suluhisha: tatua mgogoro baina ya mtu na mtu au kundi moja na jingine. architecture: usanifujenzi: ustadi wa kubuni na kuchora ramani za majengo au/na miundombinu. Fani hii ina uhusiano wa moja kwa moja na ulemavu kwa vile kiwango cha mtu mwenye ulemavu kuchangamana na jumuiya au jamii, hutegemea pia jinsi mazingirajenzi yalivyozingatia mahitaji yake wakati wa usanifu (taz. accessibility). arm sling: tanzi la mkono: kipande cha nguo au ngozi kinachofungwa shingoni ili kusaidia kushikilia mkono uliojeruhiwa, k.v. kuvunjika. 16 armpit, under arm or axilla crutch: nsiso: 1. wenzo ambao hutumika kumwezesha mtu mwenye kilema cha ujongeaji kumudu kujikongoja. Kwa hiyo hii ni aina mojawapo ya nyenzokongojea. Umbo la wenzo huu hutegemeana na aina pamoja na kiwango cha kilema alichonacho mtumiaji. Kwa mtu aliyedhoofu mguu kuanzia nyongani kushuka chini au ambaye anakosa mojawapo ya miguu yake, aga. hutumia wenzo wa kuweka kimto kwapani sambamba na mbavu na kushikilia kishikizo kilicho chini katikati ya wenzo wenyewe. Wenzo huu unaweza kutengenezwa kwa malighafi mbalimbali ikiwa ni pamoja na miti ya porini, boriti, bomba za chuma au plastiki ngumu. Aina hii ya wenzo huitwa nsiso kwapa. Hata hivyo, kumekuwepo na upotoshaji wa ubainishaji wa nyenzo mbalimbali za kujikongojea kwa maana ya vifaa vinavyobuniwa ili kumwezesha mwenye kasoro ya au kukosa mguu mmoja au yote miwili

35 kumudu kujikongoja. Kifaa cha aina hii kinaweza kikatumika chenyewe au pamoja na bangiligango au nyenzo nyingine kulingana na kiwango cha kilema cha mtumiaji. (ang mifano ya michoro). Jina la jumla la kuziita nyenzo hizi magongo ni potoshi kwani gogo linaweza kuwa aina mojawapo ya nyenzo mbalimbali au kipande kinene cha mti chenye matumizi tofauti na kujikongoja, mfamo kuchezea mpira wa kriketi. 2. fimbo ya kutembelea kufuatia kuumia au kukatwa mguu. 3. kitu kilichotengenezwa kwa ubao au chuma chenye urefu wa kutokea kwapani au kiwiko hadi ardhini ambacho ni kwa ajili ya kusaidia kutembelea kufuatia kuvunjika kwa mguu au kujeruhika kwa namna hiyo, au ulemavu. 4. kisaidizi cha kutembelea au kitu chenye sehemu ya kukamata na kuegesha mkono au kwapa cha kusaidia mtu asiyemudu kutembea mwenyewe. Halikadhalika, wenzokongojea huhamishia uzito ardhini kupitia mtaimbo lakini huwa na sehemu mbili za mguso, yaani mkono 17 kwenye kiko au kwapani. Hii huruhusu sehemu kubwa ya uzito kubebwa na nyenzokongojea kuliko ilivyo kwa bakora au henzirani. arthrodesis: uhagizi: upasuaji wa kufanya kifundo kishikane pamoja. arthrosis: athrosisi: sehemu ambayo mifupa miwili hushikamanishwa kwa lengo la kuwezesha msogeo wa sehemu za mwili. Athrosisi agh. hufanywa na tishu au gegedu na hugawanywa katika makundi kulingana na mjongeo wake, yaani vifundo egemeo, vifundo nyirika na vifundo pingili. arthritis: baridi yabisi au jongo: uvimbe, maumivu au/na mwasho kwenye mojawapo au vifundo vyote. Zipo aina nyingi za baridiyabisi. Halikadhalika hali hii inaweza kuwa ya maumivu ya taratibutartibu ama makali au sugu. Pia inaweza au/na kulemaza kwa kiwango fulani. Hata hivyo, hali ya hewa ya ubaridi au/na unyevunyevu huongeza maumivu kwa mwenye ugonjwa huu japo siyo chanzo cha hali yenyewe. arthrogryposis: mkunyatofundo wa kuzaliwa: ugonjwa wa mkunyato

36 wa fundo ambao ni matokeo ya vifundo kutojongea kwa kiwango cha kawaida hali ambayo mtoto huzaliwa nayo. arthroscopy: tibafundo: utoboaji wa tundu kwenye mfupa unaofanywa na bingwa wa upasuaji kwa lengo la kuchunguza na kutibu matatizo ya kifundo, goti, kiwiko, bega na nyonga. article: kifungu: moja ya ibara katika matini za sheria na mikataba ya kimataifa. artificial limbs: kiungo mnemba: kiungo kisichokuwa na uhai kilichofaraguliwa na kinachoweza kuwa mbadala wa mguu, mkono, jicho, titi, mfupa, koklea ya sikio, jino, fupa la wajihi, kaakaa, nyonga, goti au kifundo kinginecho. Kiungo cha aina hii kinaweza ama kumsaidia mhusika kuongeza kiwango cha uwezo kiutendaji baada ya kuondokewa au kukosa kile cha asili (hususani zama hizi ambapo teknolojia imekua sana), kuboresha mwonekano au vyote viwili. Hata hivyo, pale lengo hili la pili linapokuwa ndilo la msingi, husababisha madhara kisaikilojia kwa kumchochea mhusika asijikubali kama alivyo. assisted respiration: upumuaji mnemba: hali ya kumsaidia mtu kupumua tena kwa kumpulizia hewa mapafuni kupitia puani na mdomoni. asocial: -siyo changamka: 1. -enye kutoonyesha hisia za furaha, haya. 2. enye kuona aibu. Hii ni aina ya ulemavu wa kisaikolojia. Asperger syndrome: mlimbikodalili wa Asperger: mvurugiko wa akili anaokuwa nao mtu ukamfanya ashindwe kujenga uhusiano na kuzingatia jambo moja tu. Huu ni ulemavu wa kudumu wa aina ya usonji ambao huathiri jinsi mtu anavyoutafsiri ulimwengu, anavyochakata taarifa na anavyohusiana na watu wengine. Mtu mwenye hali hii huwa na shida katika maeneo makuu matatu ya kijamii: mawasiliano, kuchangamana na taswira. Huwa na matatizo machache ya uongeaji na agh. ni mwenye akili za wastani au hata juu ya wastani. Kwa kawaida mtu namna hii huwa hana ulemavu wa ujifunzaji unaoambatana na usonji ila huwa na ugumu mahususi wa kutosoma vizuri (disleksia), 18

37 dispraksia au kutindikiwa umakini, kutotulia na kifafa. asphyxia: mkwamopumzi: hali ya ukosefu wa hewa, kuzimia kutokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya oksijeni kwenye seli za damu mwilini k.v. mtu aliyekabwa. xxv assent: ridhia: ruhusu jambo au kitu kufanyika. assertion: usemithabiti: hali na msimamo wa kiharakati anaotakiwa kuwa nao mtu mwenye kukandamizwa ili aweze kujitetea mbele ya wanaomkandamiza ama hata watesi au hata wanyanyasaji wake. assert: tetea: dai kwa dhati kitu au jambo linaloaminika kuwa la kweli. assertive behaviour: mwenendo jinaki: hali ya kujigamba, kujisifia na kujiona. assertive skills: stadiutetezi: 1. ujuzi wa kudai stahiki. 2. uwezo wa mtu kuelezea mawazo na hisia zake. assertiveness: utetezihaki: tabia ya kujiamini; kuwa na msimamo; kujitokeza kudai na kutetea haki kwa nguvu zote. assess (ability, conduct, etc): pima (uwezo, tabia na ubora): tathmini utendaji, ubora na ukubwa wa jambo. assessment: upimaji: kutathmini utendaji, ubora na ukubwa wa shughuli iliyofanyika. Hii ni mojawapo ya kazi za kudumu za Vituo vya Rasilimali ili kubaini jinsi ya kumsaidia mtoto mwenye ulemavu. assimilation: usilimishaji: 1. hali ya mtu kujiingiza na kujishikamanisha na mfumo mpya kimatendo na kifikira; mathalani, kuweka na kuunganisha uhalisia mpya kwenye mfumo wa kifikira uliopo k.m. sera za Wafaransa na Wareno za kuwageuza wenyeji wa makoloni yao ili wafanane na mabwana zao wa kigeni. 2. ufyonzaji wa virutubisho vya chakula mwilini baada ya mchakato wa umeng enyaji. assistance animals: wanyamamwega:wanyama waliopatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya kumsaidia mtu mwenye ulemavu. (taz. Service animals). assistive listening system: mfumo saidizi wa kusikilizia: mfumo huu hupeleka sauti iliyokuzwa kupitia wenzo wa kipokea sauti kilichobaniwa masikioni (shimesikio) na vifaa vinginevyo. Hivi ni pamoja na mifumo ya miali isiyoonekana, kitanzi na urekebishaji masafa. Mifumo inayobebeka inaweza kupatikana kutoka kwa wagavi wa vifaa vya vielelezo vinavyosikika na kuonekana wanaohudumia makongamano na mikutano. assistive technology: teknolojia saidizi: ukuzaji wa kiwango cha kujitegemea kwa kumwezesha mtu 19

38 kufanya shughuli ambazo hapo kabla hakuzimudu au alizimudu kwa shida sana. Hili hufanyika kwa kuboresha au kubadilisha jinsi ya afua za kiteknolojia zinazotakiwa kufanikisha shughuli ya aina hiyo. Bidhaa za teknolojia saidizi zinaweza pia kutumiwa na watu wasiokuwa na ulemavu; mathalani, gari linalotumia teknolojia saidizi ili liendeshwe na mtu mwenye ulemavu wa kujongea, linaweza pia kuendeshwa na yule asiyekuwa na ulemavu huo kwani mara nyingi gari la kawaida huongezewa nyenzo ili aliye na ulemavu atumie mikono badala ya miguu, saa ya mtu asiyeona inaweza kutumiwa na anayeona, kompyuta yenye programu rekebifu inaweza kutumiwa pia na mtu mwenye uoni kamili (ang teknolojia rekebifu). asthenic: -embamba:- isiyokuwa nene: aina ya ulemavu wa viungo ambapo mtu huzaliwa nao na kuendelea na ukondefu maishani. astigmatism: uastigimati: hitilafu katika uchepushaji mwanga katika konea ya jicho kutokana na dosari kwenye mpindo wa konea, au mara chache kutokana na hitilafu ya lenzi au misuli ya siliari; mojawapo ya hali hizo husababisha miale ya mwanga isikutane katika retina na hivyo husababisha shida ya kuona. xxvi asylum: hifadhi: 1. ulinzi unaotolewa na serikali ya kigeni kwa mtu 20 aliyeikimbia nchi yake kwa misingi ya hofu ya kuteswa kutokana na msimamo wake au imani yake kisiasa au kuwa mwanachama wa kikundi cha dini au cha jamii fulani; pia kimbilio xxvii ; 2. hospitali au mahali pa kutunzia wagonjwa hususani wenye matatizo ya akili. ataxia: mwondoko varange: ukosefu wa ushirikiano wa misuli unaoweza kuathiri matamshi, mpepeso wa macho, uwezo wa kumeza, utembeaji, uokotaji vitu na ujongeaji wa hiari. Kuna aina tofauti za ataksia ikiwa ni pamoja na ataksia ya Friedrech na ataksia ya 6 ya ubongo nyuma. Aina ya ataksia isiyojulikana sana ni ile ya mpanuko wa mishipa midogo ya damu (telangiectasia ataxia). Neno ataksia linaweza kutumika pia kwa mapana kuashiria kutokuwepo kwa mapatano kwenye mchakato wa kisaikolojia na ataksia ya macho (agh. sehemu ya dalili ya Balinti) inayojumuisha ukosefu wa ulinganifu wa uono mzuri na misogeo ya mikono), au upumuaji wa kiataksia (mitweto isiyo sawa).

39 ataxic syndrome: mlimbikodalili wa ataksia: mwondoko varange na kutowasiliana kwa misogeo hiari ya misuli ya kiwiliwili na ile ya mikono na miguu; agh. miguu huhusika zaidi kuliko kiwiliwiwli. athetosis: athetosisi: 1. hali ya upekee usiokuwa wa kawaida ambao kwa makusudi hutokea kwenye vidole vya mikono na miguu. 2. hali yenye kubainishwa na kunyonganyonga au kupindapinda vifundo na vidole vya mikono. 3. misogeo ya taratibu na tulivu; mara nyingi ikihusisha misuli ya mikono na miguu. 4. hali siyohiari inayotokana na hitilafu ya ubongo ya kutembeza mikono hasa vidole kwa rithimu inayofanana ya supinesheni, kubainisha na kunyoosha na kisha pronesheni, kutanua na halafu kukunja xxviii athroplasty: athroplasti: 1. uundaji wa kifundo bandia. 2. uundaji wa kifundo kipya kutokana na kifundo chenye ankilosisi. xxix atrophy: msinyao: 1. mnyong onyeo au udhoofikaji unaoendelea wa misuli unaotokana na tatizo kwenye neva. 2. kupungua kwa ukubwa wa seli, 21 ogani au tishu kutokana na dosari ya kimakuzi au ya lishe. attachment disorder: mvurugiko upendo: hali ambapo mtoto mchanga na mtoto mdogo hushindwa kuwa na uhusiano mzuri na wazazi au walezi. Kumbuka kwamba mtoto ambaye dalili hazijitokezi kiasi cha kutakiwa kutibiwa, anaweza kuwa na matatizo ya uhusiano au hali ya hofu yenye kuhitaji kutibiwa. attention: usikivu: hali ya kuwa na uelekevu wa kuangalia, kusikia na kutafakari jambo. Ni aina nyingine ya ulemavu wa kisaikolojia inayomkosesha mtu mwenye hali hii na hivyo kuathiri kiwango cha ukubalifu na uchangamanaji kwenye jamii. attention deficit/hyperactivity disorder: usikivu mdogo: hali ya kukosa utulivu inayotokana na kuzidiwa na mihemko au wingi wa shughuli. attitude: mtazamo: 1. halitabia, uelekeo au namna ya mtu au kitu kilivyo. 2. maoni au hisia za mtu kuhusu kitu hususani zenye kudhihirishwa na tabia au mwenendo wake. audial-visual aids: vifaa vya kusikika na kuonekana: vifaa vyenye kuonekana na kutoa sauti kama vile televisheni, filamu, mpira wa kengele kwa wenye upofu. audio description: maelezo sauti: aina ya huduma kwa wasioona au wenye

40 uoni hafifu inayosababisha maigizo, televisheni, sanaa za maonyesho, video na filamu kueleweka zaidi. Maelezo ya vitu vinavyo onyeshwa huelezewa na mtu aliyefunzwa kutumia programu mahususi za televisheni na chombo cha kujaribishia usafirishaji wa matangazo vikiwa na kirekebisha sauti aina ya sterio. audiometry (VROCA): upimaji kiwango usikivu: mbinu ya kupima uwezo wa kusikia itumiwayo na mtaalamu wa kupima usikivu ambapo vitu vyenye kuonekana hutumika badala ya vile vya kugusa. Iwapo anayepimwa anageuzia kichwa sauti iliko, hupewa zawadi kama vile mwanasesere. Mtoto anayeshindwa katika upimaji huu, anapaswa kupelekwa kwa wataalamu kwa upimaji wa kina. audiometer: odiometa: kipimo kinachotumiwa kupima usikivu kwa ujumla, uelewa na mwitikio katika maongezi kwa lengo la kuwezesha tathmini ya jumla ya usikivu. auditory: -a kusikia: -enye kuhusiana na mlango wa fahamu wa kusikia. auditory processing disorder (APD) or Central auditory processing disorder(capd): mvurugiko wa mfumo usikivu (MMU): kasoro inayoathiri mchakato wa taarifa za sauti ndani ya ubongo. Maana yake kwa upana, huelezea namna mfumo mkuu wa fahamu unavyotumia taarifa za sauti. Hata 22 hivyo, Mfumo Mkuu wa Neva za Fahamu ni mpana ambao pia hushughuliika na mambo mengine mengi kama vile kukumbuka, kumakinika, lugha n.k. Ili kuepuka kuchanganya kati ya MMU na mivurugiko mingine inayoweza kuathiri uwezo wa mtu wa kutenda, kuelewa na kukumbuka. Ni muhimu kusisitiza kwamba, mvurugiko wa mfumo wa usikivu ni kasoro ya kiusikivu, au kutofanya kazi kwa mfumo wa usikivu katika kupokea sauti. augmentative communication: mawasiliano kuzwa: mbinu zinazotumika kujaliza au kuwa mbadala wa usemaji au maandishi kwa ajili ya wale wenye ulemavu wakati wa kuchakata au kuzingatia lugha ya matamshi au maandishi kwa kutumia mbinu zenye au zisizo na visaidizi. Aina za ulemavu zenye kuhitaji zaidi aina hii ya kimawasiliano ni pamoja na zile za matamshi na lugha (mpoozo wa ubongo, akili, usonji, selosisi, maradhi ya Parkinson, n.k). Lugha ya ishara na tahajia ya kutumia vidole, mikonyezo, picha, michoro, herufi, maneno, sehemu za mwili, miguso na mipapaso ni mifano ya mawasiliano yasiyokuwa na visaidizi wakati yale yenye visadizi huhusishwa na teknolojia; mathalani, mifumo iliyojikita kwenye kompyuta ambayo husaidia mawasiliano ya kimatamshi na ya kimaandishi pia.

41 augumentation: ukuzaji: hali ya kuongeza nguvu au uwezo wa kitu ili kukiongezea ukubwa au namna ya kutenda, n.k. aura: ora: hali inayoashiria wema au ubaya wa mtu. aural: -a kusikia: enye kuhusiana na/ au kupokelewa na sikio. auscultation: usikilizaji sauti: kitendo cha kusikiliza sauti zinazofanywa na ogani za ndani ya mgonjwa hususani moyo, mapafu na ogani zisizo za kawaida. authentic text: matini halisi: toleo la mkataba, hati au makubaliano yenye maudhui yaliyo sawa lakini katika lugha tofauti. autistic spectrum disorder (ASD): makundi usonji: dhana iliyobuniwa na mwanasakaitria Eugen Bleuler mwaka 1911 ambayo hutambua uwepo wa makundi madogomadogo ya aina ya usonji ikiwa ni pamoja na mlimbikodalili wa Asperger. autistism: usonji: 1. mvurugiko wa kipindi cha uchanga kabla ya umri wa miaka mitatu unaodhihirishwa na kujitenga, kujichangamsha binafsi, upungufu wa kiutambuzi na kasoro za lugha. 2. ulemavu unaodhihirishwa na udhaifu katika kuchangamana kijamii na kuwasiliana, kuwa na hazina ndogo ya maarifa katika ufanyaji shughuli, shauku na kulemazwa katika mienendo tofautitofauti isiyo ya kauli au matamshi. Mathalani, kukaziana 23 macho na mtu, kushindwa kuelezea masuala ya kifedha, mkao na ishara za mwili. Kutokana na kuvia kwa mishipa ya fahamu, na hivyo kutopeleka taarifa inavyotakiwa, husababisha wahusika kuwa na tabia ya upweke. 3. ulemavu wa ukuaji wenye kusababishwa na kasoro za kimaumbile kwenye ubongo hali inayojitokeza katika miaka mitatu ya kwanza baada ya kuzaliwa. Dalili zake ni pamoja na: kuvurugika kwa stadi za kimaumbile, kijamii na lugha, mwitikio usiokuwa wa kawaida dhidi ya hisia, mionjo, uhusiano na watu, vitu, matukio, viwango visivyo vya kawaida kiutendaji (juu sana au chini sana), kung ang ania kuwa mazingira na ratiba havibadiliki, ubunifu mdogo kimichezo, na misogeo yenye kujirudiarudia kama vile kutikisatikisa, kubiringisha na kugongagonga kichwa na kupindisha mikono. autoimmune disease: ugonjwa wa kinga nafsia: kundi la magonjwa ya uharibifu wa tishu yanayotokana na antibodi zinazotengenezwa na mwili dhidi ya tishu nyingine za mwili. xxx automatic dysreflexia: disrefleksia isohiari: hali ya dharura ya kitabibu yenye kutishia uhai ambayo huwaathiri walioumia ubongouti kwa kiwango cha T6 au zaidi ya hapo Japo kwa nadra, wale waliojeruhika kwa viwango vya T7 na T8

42 hukumbwa na hali hii. Kwa waathirika walio wengi, hali hii inaweza kutibiwa au kukingwa kiurahisi. Jambo la msingi ni mhusika kujua kiwango chake cha chini cha msukumo wa damu, vichocheo na dalili. Bila hatua za haraka, hali hii inaweza kusababisha kiharusi. Baadhi ya dalili za hali hii ni kupanda kwa msukumo wa damu, kichwa kugonga kwa nguvu, kuiva uso, kuvuja jasho juu ya eneo lililoumia, kuwa na kimbimbi chini ya eneo lililojeruhika, pua kutokwa na kamasi, kichefuchefu na mapigo ya moyo kushuka chini ya 60 kwa dakika. autonomy: kujitawala: hali ya kujiamulia mambo na kutenda kwa kadiri ya utashi binafsi pasipo kuingiliwa na mtu mwingine. Kwa kiwango kikubwa mtu mwenye ulemvu hukosa fursa hii kiasi cha maamuzi mengi kufanywa kwa niaba yake. avoidant: mkwepaji: mtu kuwa na tatizo la kisaikolojia kwa kushindwa kutimiza wajibu na majukumu yake bila kujali matokeo. awareness: ufahamu: hali ya mtu kuwa na uwezo wa kuelewa na kufafanua kinachosemwa. Hii ni zana muhimu kwa binadamu katika kuchangamana, kupata habari, kufanya uamuzi kwa kulinganisha na kulinganua mambo na kuwa 24 mwanajumuiya amilifu. Mtu mwenye ulemavu hukosa ufahamu wa mambo mengi katika jumuia yake kutokana na viwango vidogo vya uchangamanaji na hata habari nyingi kutolewa bila kuzingatia mahitaji ya kila mmoja katika jumuia. Rejea miundo mbadala na mawasiliano kuzwa.

43 Bb babbling: kubwabwaja: 1. hatua katika kukuza uwezo wa kuongea ambapo mtoto hucheza kwa kuiga matamshi ya sauti na kwa nasibu hutoa irabu zinazofanana na ba-ba ma-ma hali ambayo kwa kawaida huanzia kwenye umri wa miezi minne. 2. utamkaji sauti zisizo na maana au zisizoeleweka, ropoka, toa sauti mithili ya kijito. backbone: uti wa mgongo: mtungo wa mifupa unaoanzia shingoni hadi mwanzoni mwa matako (kidungumavi). Mtungo huu husimika kiwiliwili na kuhifadhi ugweuti (uti wa ubongo). back slab: ubambamwimo: kifaa cha plastiki au vipande vya miti vinavyofungiwa mkono au mguu ulioumia hasa kwa kuvunjika ili kuzuia utengukaji wa mifupa na misuli. back brace: pagaro mgango: aina ya wenzo unaotumika kuimarisha mkao wa kiwiliwili cha mtu mwenye maungo tepetevu kutokana na kupooza. barrier: mkingamo: kikwazo kinachomzuia mtu mwenye ulemavu kumudu kuishi kwa kujitegemea, kufanya kazi, kusafiri au/na kufikia na kuingia ndani ya majengo, kupata huduma, habari au taarifa na maumbo. Mathalani, asiyeona kujihatarisha kwa kulazimika kutembea kwenye njia zilizojaa vigingi, madimbwi ya maji, makorongo, n.k. barrier-free facility: huduma bila mkingamo: jengo kiunzi, au miundombinu lililobuniwa au kusanifiwa na kujengwa kiasi kwamba mtu mwenye ulemavu wa ujongeaji (mathalani, wenye kutumia kitimwendo) anamudu kuzunguka au kupita kwa uhuru na kwa muda wote kuyafikia maeneo bila kukumbana na vikwazo wala kuhitaji msaada. baseline: taarifa msingi: 1. takwimu ambazo hukusanywa ili kusaidia kujua hali ilivyo kwenye jumuiya au jamii husika ili ziwe kigezo ama 25

44 cha kuandaa afua au kupimia mabadiliko baada ya kutekeleza afua. 2. maelezo ya awali yanayojulikana na ambayo hutumika kuwa msingi wa kuamulia na kulinganisha kinachopimwa; kwa mfano shinikizo damu na jotomwili. behaviour checklists: orodhahakiki mwenendo: mfululizo wa vitu au matendo mahususi yanayomruhusu mwangalizi kuhesabu au kukagua kuwepo au kutokuwepo kwa mienendo fulanifulani kwa kumchunguza mtathminiwa. behaviour disorder (BD): mvurugiko mwenendo: dhana inayotumika kwa mtoto mwenye kuonesha mienendo inayopotoka kwa kiasi kikubwa na kwa kipindi kirefu tofauti na desturi zinazokubalika katika hali hiyo na kwa umri huo. behaviour-management: kuadabisha: kukuza, kuendeleza, kuimarisha ama kudumisha au kupunguza mienendo katika mtindo uliopangiliwa. behaviour-modification: marekebisho mwenendo: mbinu za kubadilisha tabia za binadamu kwa kujikita kwenye nadharia ya tabia za kiutendaji ambayo hujikita kwenye uchunguzi makini kabla na baada ya matukio na mwenendo husika kuhitajika na mazingira kuwepo katika hali inayofaa ili kuimarisha mwitikio unaotakiwa, na kwa hiyo 26 kuleta mabadiliko tarajiwa kimwenendo. behaviour shaping: uundaji mwenendo: dhana ya jumla inayoainisha michakato ya kubadili mwenendo wa mtu, agh. kwa kuibua mienendo mipya ambayo ilikuwa haijidhihirishi kwa kutumia mojawapo ya michakato mingi yenye kuhusika na tiba ya mienendo. behaviour, emotional and social difficulties (BESD) or emotional and behavioural disorders (EBD): matatizo ya kimwenendo, kijamii na kimihemko: dhana kasoro mbalimbali ikiwa ni pamoja na: hali ya mtoto kujitenga, kutotulia kutokana na kujishughulisha mno kila wakati, mwenye matatizo ya afya ya akili, asiyemudu kudhibiti hasira zake, na yule mkorofi au mharibifu. behaviour or conduct: mwenendo: tabia ama ya kudumu au ya muda mrefu ambayo mtu anakuwa nayo ikijidhihirisha kwa matendo yake na jinsi anavyochangamana na wengine. behavioural contract: mkataba wa kimwenendo: makubaliano ya kimaandishi au kauli baina ya pande mbili yanayoelekeza kwamba upande mmoja ukiwa na mwenendo fulani (k.m. kukamilisha kazi za nyumbani) upande mwingine (mwalimu, mzazi,) utatoa zawadi maalumu.

45 behavioural manifestations: dalili mwenendo: kipimo cha viainisho vinavyojielekeza kwenye ufafanuzi wa mwenendo. beliefs: imani: hali ya kuamini, kushawishika kuwa kitu fulani ni cha kweli, hususani upande wa kidini au kiroho, kiitikadi, n.k. Bell s palsy: kipanda uso: ugonjwa unaosababisha maumivu makali ya sehemu ya paji la uso ambao unachochewa na uharibifu au kujeruhika kwa mojawapo ya mishipa miwili ya uso inayodhibiti mpepeso na ufumbaji wa macho, lugha mwili kama vile kutabasamu na kununa, tezi za machozi, mate na mionjo ya ulimi. Hali hii inapotokea, huingilia utendaji wa mishipa ya fahamu ya uso na hivyo kusababisha muingiliano wa ujumbe unaotumwa na ubongo kwenye misuli ya uso, halafu husababisha udhaifu au mpoozo unaoshusha upande mmoja wa uso. Kipandauso ni tofauti na kiharusi cha kawaida na kwa vile mishipa ya fahamu ya uso ina shughuli nyingi changamani, uharibifu wa au kuingiliwa kwa shughuli zake kunaweza kusababisha shida nyingi. Dalili za hali hii hutofautiana kati ya mtu na mtu ila huwa ni pamoja na: mtetemo na kupooza kwa uso, kushuka kwa kigubiko cha jicho na mdomo, kukosa mionjo, kutoka machozi kwa wingi, maumivu 27 sehemu ya ufizi na nyuma ya sikio, milio ndani ya sikio, kuumwa kichwa, kuwa na hisia kali dhidi ya sauti kwa upande ulioathirika, kushindwa kutamka, kizunguzungu na kushindwa kutafuna. bestiality: uhayawani: hali ya mtu kuvutiwa kufanya ngono na wanyama kama vile mbwa, farasi, mbuzi, n.k. bias: kumili: tabia ya kupendelea upande mmoja na kuchukia upande mwingine wa watu, vitu, au mawazo. biasness: upendeleo: hali ya kumpa mtu haki asiyostahili au zaidi ya mwingine mwenye haki sawa na mwenzake; unga mkono jambo bila kujali hoja za upande mwingine. bilateral hemiplegia: hemiplejia pandembili: hali ambapo miguu na mikono iliyopooza hupata mishtuko ya misuli kwa mara moja ila upande mmoja ukiwa na mishtuko zaidi ya mwingine. Ang mshtuko kwadriplejia. bill: muswadahati, waraka: 1. maandishi yenye kuonyesha kiasi kinachodaiwa kutokana na manunuzi ya bidhaa au huduma. 2. rasimu ya mapendekezo ya sheria au sehemu ya sheria inayowasilishwa Bungeni lakini kabla ya kupitishwa na kuidhinishwa kuwa sheria. bill of rights: haki za raia: stahiki za msingi ambazo raia wa nchi wanapaswa kuzipata.

46 binding: shurutishi: hali ya mtu, asasi, taasisi, shirika au nchi kulazimika kufanya jambo kutokana na masharti yaliyowekwa agh. kwenye mikataba au shurutisho la uamuzi wa mahakama (faradhi). biopsy: biopsi: 1. kipande cha tishu au kioevu kinachochukuliwa kutoka sehemu fulani juu au ndani ya mwili na kuchunguzwa ili kuona iwapo kiko hai au kimekufa. 2. uchunguzi wa tishu iliyokatwa kutoka katika mwilli-hai kwa kutumia darubini. xxxi bipolar: hisiageugeu: mabadiliko ya ghafla ya hisia; yaani kufurahi sana wakati mmoja na kujawa huzuni punde. birth control: uzazi wa majira: uzuaji wa utungaji wa mimba au upandikizaji wa mbegu kwa kutumia mbinu za asili au kisayansi. Pia uzazi wa mpango birth defect: dosari wakati wa kuzaliwa. hali ya mtoto kuzaliwa na matatizo ya viungo vya mwili au dosari kuhusiana na viwango vya uelewa au ujifunzaji. Hata hivyo, kwa muktadha wa kijamii, misemo kama vile hali ya kuzaliwa nayo au kuwa na ulemavu tangu kuzaliwa au kuzaliwa na kilema ndiyo inayopendelewa ili kuepuka maana ashirifu zenye kudhalilisha. birth rights: haki za kuzaliwa: 1. haki za msingi mtu anazostahili kupata kwa sababu ya uraia wake wa nchi fulani. 2. stahiki, umiliki au 28 upendeleo ambao mtu anapaswa kuwa nao kisheria kutokana na kuzaliwa kwake. 3. upendeleo maalumu anaopewa kifungua mimba. xxxii birth spacing: upangiliaji uzazi: utumiaji wa mbinu za mpango wa uzazi ili kutoa nafasi kati ya kuzaliwa kwa mtoto mmoja na mwingine. bisexual: huntha: mtu mwenye via vya uzazi vya jinsi zote mbili. bisexuality: uhunta. mtu ambaye matamanio yake ya kimaumbile, mihemko ya kimahaba huwa ni kwa wanawake na wanaume. blind: -pofu**: -enye hali ya kutoona. Hata hivyo, istilahi hii hupewa maana ashirifu ya chukizo hasa pale inapotumika kama tamathali mfano kipofu kaona mwezi ukila na kipofu usimguse mkono ; n.k. Istilahi inayopendelewa ni mtu mwenye upofu. blindness: upofu: hali ya kutoweza kuona, au kuwa na ugumu wa kuona kuanzia kiwango kidogo, cha kati hadi kikubwa sana kutokana na uatilifu kwenye mlango husika wa fahamu. blood pressure: shinikizo damu: 1. msukumo wa damu kwenye mishipa na ambao husababisha madhara unapozidi kiwango cha kawaida kwa ama kuwa juu au chini sana. Hali hii huhitilafiana kwa vigezo vya umri na siha ya mtu. 2. kanieneo la damu inayozunguka katika ateri. xxxiii

47 blood transfusion: uongezaji damu mwilini: upewaji damu na mtu mwingine kwa njia ya mshipa na kwa kutumia sindano maalumu ili kuwa mbadala wa damu iliyopotezwa na mpokeaji kutokana na maradhi, ajali, uzazi kinzani, n.k. boredom: uchoshi: 1. hali ambapo mtu hana kitu cha kufanya. 2. uchovu unaotokana na mazungumzo au shughuli zisizovutia. bowlegs or rickets: matege: 1. mpindiko wa miguu kwa nje. Hii ni hali ambapo miguu hupinda karibu au chini ya magoti. 2. ulemavu wa miguu wa kupinda kwa ndani katika sehemu za magoti. xxxiv brace: bangiligango: wenzo wenye kushikilia vitu pamoja au kusaidia kuviweka kwenye mkao wake, mathalani, bangiligango ya shingo huvaliwa ili kushikilia shingo baada ya kuumia. Braille: Braille: mfumo wa kusoma na kuandika kwa kupapasa unaotumiwa na mtu asiyeona. Mfumo huu uligunduliwa na Mfaransa Luis Braille ( ) ambapo yeye mwenyewe alipatwa na upofu mwaka Braille cell: maandishi ya nuktanundu: seli hii ina doti sita zilizotuna na kupangana kimstatili; tatu kwa kwenda chini na mbili kwenda kulia zikihesabika kuanzia kwenye kona ya juu kushoto kwenda chini (doti 1, 2, 3, ) kuelekea kwenye kona ya juu kulia (4, 5, 6). Mtumiaji wa mfumo wa Breli anaweza kuunda abjadi au herufi zilizopangiliwa kwa kutumia ala mbalimbali za kuandikia nuktanundu kama vile: kibao na kalamu maalumu (kitobozi), mashine ya Perkins na mashine chapa ya nuktanundu. Braille embosser: kitunisha nuktanundu: 1. mashine inayotarakilisha maandishi yaliyotokana na kompyuta kisha kuyachakata kwenye nuktanundu. Programu za kunukuu maandishi hubadilisha tini zilizoskaniwa au zilizotokana na programu za kuchakata maneno ya kawaida kwenye nuktanundu, ambazo

48 huweza kuchapishwa kwenye kitunishi. 2. mashine ya kieletroni yenye kunukulisha maandishi toka kwenye kompyuta ya kawaida na kuwekwa kwenye nuktanundu. Braille symbol: alama ya Braile: kiashirio kinachoonesha wamba machapisho yanapatikana pia kwenye nuktanundu ikiwa ni pamoja na uwekaji alama wakati wa maonyesho, machapisho na mbao za maelekezo. brainstem: shinabongo: mhimili wa ubongo. brand name: rajamu: 1. jina la biashara linalotumiwa na kampuni kuhalalisha bidhaa inazozitengeneza. 2. alama inayoonyesha aina, mmiliki na mahali bidhaa ilipotengenezwa. bridge plates: daraja kibamba: aina ya teknolojia inayotumika kwenye vituo vya vyombo vya usafiri (treni, mabasi, ndege, n.k.) ili kufikiwa na mtumia kitimwendo. Daraja vibamba huenea kutoka kwenye chombo hadi kwenye jukwaa la kupandia ambapo sharti liinuliwe hadi usawa na sakafu ya chombo kiasi kwamba kitimwendo kisilazimike kutembelea ngazimbetuko yenye mwinuko mkali. Halikadhalika, basi lenye sakafu za chini hutumia daraja vibamba ambavyo huchomoza hadi kwenye kingo za barabara kwa madhumuni yaleyale ya kurahisisha ufikivu kwa kitimwendo. Basi lenye sakafu ya kimo kifupi linaweza kutumia ngazimbetuko amabazo agh. huwa 30 ni sehemu ya sakafu yenyewe, ila huweza kubingirika au kupinduliwa kupitia mlangoni hadi kwenye kingo za barabara. Katika hali hii, ngazimbetuko huwa ndefu vya kutosha ya kuhudumia kitimwendo. brittle bone disease: ukechu: ugonjwa wa mtu kuzaliwa na mifupa laini (yenye kuvunjika kwa urahisi). bronchial arteries: ateripafu: mshipa unaopeleka hewa kwenye mapafu ili damu ipate oksijeni. bronchus: kikoromeo: tawi la koromeo linaloelekea kwenye mapafu. bronchopulmonary dysplasia: displasia ya mapafu na bronkasi. browse: vinjari: ingia kwenye intaneti ili kutafuta habari. Kwa kawaida shughuli hii hutumia mikono. Kwa maana hiyo, ubunifu wa kiteknolojia huhitajika ili kumwezesha yule

49 asiyeweza kutumia mikono anufaike na utumiaji wa kompyuta. bulimia: bulimia: njaa kali xxxv bullying: ukandamizaji: mwenendo, kauli au maoni yasio ya haki dhidi ya mtu au kundi la watu. 31

50 Cc caliper: kalipa: kifaa kinachosaidia kuimarisha mguu dhaifu au uliojeruhiwa. Neno sawa na bangiligango. cancer: saratani: ugonjwa usiotibika kiurahisi unaosababisha seli kubadilika na kukua katika hali atilifu ikisababisha vichipukizi. Saratani inaweza kuathiri seli ya sehemu yoyote ya mwili ambacho ndiyo chembe hai ndogo kabisa mwilini. cane: bakora au henzirani: mojawapo ya aina mbalimbali za fimbo za kutembelea ambazo hutumika kwa sababu mbalimbali k.v. silaha, urembo, haiba, wenzo kwa wenye matatizo ya maungo au kiongozi kwa wasioona na walio na uoni hafifu. Pale fimbo inapotumika kama wenzokongojea, husambaza upya uzito kutoka mguu mfupi ambao huwa dhaifu au kuuma, huongeza mwega, wakati mwingine hutoa taarifa mpapaso ardhini au sakafuni na hata kuboresha usawa kimkao. Mkwaju nao pia hukidhi mahitaji hayahaya. capacity: uwezo: hali ya mtu ya kufanya uamuzi binafsi, kuhusu 32 maslahi na mustakabali wake kimaisha. capitation grant: ruzuku wiani: 1. kodi inayotozwa kwa kiwango sawa kwa kila mtu. 2. fedha zinazotolewa kwa kila mtu anayestahili chini ya masharti fulani. Ruzuku za aina hii hutolewa ili mlengwa apatiwe huduma mahususi kama vile elimu, afya, n.k. cardiac disorders: mdororomoyo. 1. ugonjwa wa moyo unaoathiri utendaji kazi wake na matokeo yake. 2. hali ya moyo kushindwa kuzungusha damu mwilini kwa ufanisi wa kutosheleza mahitaji ya mwili. cardiologist: bingwa magonjwa ya moyo: mtaalamu wa tiba aliyebobea katika kutibu matatizo ya moyo. career guidance and counselling: malezi na unasihi ajira: programu ambayo huandaliwa kwa ajili ya mtu binafsi ikiendana na teknolojia na mbinu zinazolenga kumwendeleza kwa kumjengea ufahamu, kujua jinsi ya kujipanga kishughuli, kufanya uamuzi, stadi za kuajirika, maarifa na uelewa kuhusu shughuli, elimu, soko la ajira, mielekeo na fursa. caregiver: mhudumiaji: mtu ambaye ama ana taaluma, rafiki au jamaa anayemwangalia mwenzake aliye na ulemavu. Shughuli zinazohusiana na huduma hii ni pamoja na zile za maisha ya kila siku (kula, kuvaa, usafi wa mwili, kutandika kitanda), kulea mtoto mwenye kiwango kikubwa cha ulemavu, kuongoza mtu

51 asiyeona, kumgeuza asiyemudu kujigeuza mwenyewe (mfamo kitandani), kumkumbusha na kumpatia dawa kwa wakati asiyemudu kufanya hivyo mwenyewe. Katika baadhi ya nchi huduma hizi hutolewa na wanafamilia na hivyo kuwa na taathira kiuchumi na kisaikolojia; wakati nchi nyingi zilizoendelea zimeweka utaratibu wa kuajiri na kuwalipa watoa huduma za aina hii kama sehemu ya huduma za jamii. case study: uchunguzi kifani: 1. aina ya uchunguzi unaojikita kwenye sampuli moja ya vitu vinavyofanana au eneo la kijiografia ambapo matokeo ya uchunguzi huo hutumika kutoa hitimisho la jumla kuhusu vitu vyote vya aina yake katika ujumla wake. Mathalani, kuchunguza kiwango cha uandikishwaji wa watoto wenye ulemavu shuleni kunaweza kufanyika kwenye maeneo fulani ya sampuli na kisha matokeo yake kuchukuliwa kuwa kigezo cha kuhitimisha hali ilivyo nchi nzima. 2. maelezo ya 33 kina ya maendeleo ya mtu, kundi la watu au hali inayotokana na utafiti wa kipindi fulani. caste: tabaka: 1. kundi la watu wenye hali inayotokana na mfumo wa kiuchumi ambao huwagawanya watu kutokana na kazi, njia za uzalishaji mali, vyeo, mbari, weledi, n.k. 2. hadhi, nafasi katika jamii. Tamaduni nyingi za Kiafrika ziliwatabakisha wanajamii ambapo mtu mwenye ulemavu katika takribani tamaduni zote alidunishwa na kutengwa na jamii kuu. Kutokana na mapokeo kati ya kizazi kimoja na kingine, hali hii bado inajidhihirisha katika jumuia mabimbali nchini. cataract: mtoto wa jicho: ukungu wa lensi ya jicho au wa kapsuli yake. xxxvi catheter: katheta: mpira wa kuweka katika kijia au urethra kwa ajili ya kutolea mkojo. xxxvii Kifaa hiki ni muhimu sana kwa mtu mwenye ulemavu unaotokana na kuumia uti wa ubongo ambaye agh. hupatwa na hali ya ufukunyungu. Matumi zi ya katheta huonge za kiwango cha usafi na kubores ha afya

52 kwani mikojo hutoka na kuhifadhiwa kwa njia salama. central nervous system: mfumo mkuu wa neva: muunganiko wa tishu za mishipa midogomidogo ya fahamu (neva) agh. iliyo katika ubongo na uti wa ubongo ambayo huendesha shughuli za mwili. Athari yoyote kwenye mfumo huu, husababisha ulemavu wa aina na viwango mbalimbali. center-based services: kituo maalumu cha huduma: mahali ambapo walimu wataalamu, washauri wa kitabibu na wanasihi hukusanyika na kufanya kazi pamoja kituoni katika kushauriana na mzazi mmojammoja na vikundi vidogovidogo (wazazi na walezi) kuhusu mahitaji ya mtoto wenye ulemavu na mustakabali wake kielimu, kiajira, n.k. cephalo: -a kichwa: -enye kuhusiana na kichwa. cerebellum: serebelamu: 1. sehemu ya ubongo wa mnyama; sehemu ndogo ya ubongo kwenye kitako cha fuvu nyuma ya kichwa ambayo huratibu na kudhibiti mkao na kuyumbayumba kwa mwili. 2. sehemu ya ubongo iliyo chini ya ubongo wa serebramu na juu ya ubongo wa ponsi na ubongo wa medulla oblongata, kazi yake kuu ni kupatanisha nyendo za misuli na kuthibiti balansi ya mwili. xxxviii 34 cerebral: -a ubongomkuu: -enye kuhusiana au kuathiri ubongomkuu. cerebral palsy (CP): mpoozo ubongo: 1. kundi la mivurugiko yenye kuathiri uwezo wa mtu wa kujongea na kukaa wima. Hii ni aina ya kawaida sana ya ulemavu wa ujongeaji utotoni. Neno serebro humaanisha kuhusiana na ubongo. Mtindio** humaanisha udhaifu au matatizo katika kutumia misuli (mpoozo). Hali hii husababishwa na ukuaji wa ubongo usio wa kawaida au kuharibika kwa ubongo kunakoendelea kukua kiasi cha kuathiri uwezo wa mtu kudhibiti misuli yake. 2. hali inayosababishwa

53 na kuharibika kwa ubongo, agh. hutokea kabla, wakati wa au mara baada ya kuzaliwa. Hudhihirishwa na mwenendo wa mtoto wa kuwa na matatizo ya ujongeaji na kuongea. Huko nyuma hali hii iliitwa mtindio wa akili.** cerebral spinal fluid: gilibongoti: kiwoevu cha neva kuu kilichoko ndani ya ubongo na uti wake (uti wa ubongo) ambacho hupeleka chakula katika ubongo na kwenye uti wa ubongo. cerebrum: ubongomkuu: sehemu ya mbele ya ubongo wa mnyama; juu kabisa ya sehemu ya ubongo yenye kudhibiti mienendo, haiba na uongeaji. cervix: shingouterasi: mlango wa kizazi wa mwanamke. challenging behaviour: mwenendo changamani: dhana ambayo imekuwa ikitumika kuelezea mienendo ya kiuchokozi, kujijeruhi, kuharibuharibu, au kutoshirikiana na wengine, kujigonga kichwa, kula kucha, kujipiga, kutoboa ngozi, n.k. vinavyoweza kuwa dalili zinazohusiana na mahitaji ya kimwili au kiakili. Kwa masikitiko dalili hizi pia zinaweza kumhatarisha mhusika, pale nguvu kupita kiasi zinapotumika dhidi yake, na wahudumiaji kukasirika. Matokeo yake yanaweza kuwa ni kwa mhusika kutengwa zaidi kwa kadiri familia, wahusika wengine muhimu, wahudumiaji na jamii wanapojitahidi 35 kukabiliana na mitukutiko hii changamani. character: nduni: silika au sifa maalumu ya mtu au kitu inayokipambanua na vingine. charity: hisani: moyo wa kumtendea mtu mwingine mema, fadhila, ukarimu, n.k. Huu ndio mwelekeo ambao kwao jamuiya nyingi huliona na kulihudumia kundi la watu wenye ulemavu (taz. mtindo wa kihisani). charity home: kituo cha hisani: aina ya makazi ambayo huandaliwa kwa ajili ya kumhudumia mtu mwenye ulemavu. charity model: mtindo wa kihisani: mtindo wa kiimani/kidini ambao huelekea kuwachukulia watu wenye ulemavu: kama waathirika wa vilema na kama wanufaika wa hisani, sadaka, na huduma ambazo kwazo, wanapaswa kushukuru; kama maafa na wenye kuteseka kiasi cha kutakiwa kuonewa huruma na kutunzwa. Kutokana na hali hii, mtu mwenye ulemavu: hukosa fursa ya kuwa na chaguo la jinsi gani asaidiwe na hivyo, hupatiwa huduma asizokuwa na usemi au

54 kauli juu ya maandalizi na utolewaji wake. Kwa maana hiyo, mtindo wa kihisani huwageuza watu wenye ulemavu kuwa wapokeaji tu wasioshiriki kwenye michakato inayounda mustakabali wao kimaisha. Tatizo huonekana kuwa ndani ya mhusika. Hata hivyo, mtindo huu wa kihisani hauwezi kupuuzwa moja kwa moja kwamba ni uelekeo hasi kabisa ikizingatiwa kuwa huruma na ukarimu ni hali chanya za mienendo ya binadamu na zinaweza kuelekezwa kwenye uelewa wa kina na wenye kujenga mazingira ya kujihusisha zaidi na masuala ya ulemavu. chart: chati: faili ambamo taarifa kuhusu magonjwa ya mtu na matibabu yake huhifadhiwa. charter of the United Nations: chata ya Umoja wa Mataifa: hati rasmi (ya Umoja wa Mataifa) inayoelezea makusudio, haki na kanuni za asasi. Pia mkataba, hati, ridhia. xxxix checklist: orodha hakiki: orodha ya vitu vinavyotakiwa, vitu vinavyopaswa kufanywa au kuzingatiwa na mara nyingine orodha hiyo huumika kama kumbukumbu. chemotherapy: tibakemikali: mbinu za kutibu ugonjwa kwa kutumia kemikali ambayo inaathiri vijidudu vinavyoleta ugonjwa huo au 36 vinavyoathiri uvimbe, bila kuudhuru mwili wa anayetibiwa. chest physiotherapy: tiba kifua: mbinu ya tibamaungo ya kutibu kifua kwa kutumia ajenti za asili k.m. joto, umeme, maji, mazoezi, n.k. child abuse: unyanyasaji wa mtoto: dhulumu, tumia vibaya, onea, tukana, tumia maneno makali dhidi ya motto, n.k. child guidance: unasihi kwa mtoto: utaratibu wa kuhakikisha ubora wa makuzi ya mtoto kwa kumwelekeza jinsi ya kuenenda na kumrudi kila anapopotoka. child profile: wasifu wa mtoto: utaratibu wa kuweka kumbukumbu hususani kwa mtoto mwenye mahitaji ya ziada katika kumwendeleza kielimu na kistadi. child psychiatrist: msakatriatiba mtoto: tabibu aliyebobea kwenye uga wa akili, mihemko au mivurugiko ya mienendo ya watoto na barubaru. Ana sifa za kuelekeza aina ya dawa na jinsi ya kuzitumia. child psychologist: mwanasaikolojiatiba ya mtoto: 1. mtaalamu wa afya ya akili aliyesomea saikolojia ambaye hupima, hutathimini na kumtibu mtoto mwenye mivurugiko ya mihemko. Hawezi kuamrisha dawa (angalia msakatria). 2. daktari bingwa mwenye taaluma kuhusu mienendo ya kiakili kwa watoto. child study: kumchunguza mtoto: utaratibu wa kufuatilia kwa kudadisi

55 ili kugundua uimara na udhaifu wa kila mtoto kisha kuweka utaratibu wa kumsaidia. child to child learning: ujfunzaji wa mtoto kwa mtoto: utaratibu wa mkao au mpangilio wa darasa kiasi kwamba mwanafunzi mwenye kujimudu kimasomo darasani hukalishwa na yule asiyejimudu kwa minajili ya kusaidiana kiujifunzaji. child-centred learning: ujifunzaji unaomlenga mtoto: utaratibu unaoepuka dhana ya ufundishaji wa kukaririsha unaotokana na dhana kuwa mtoto hana anachojua ila mwalimu ndiye mwenye kujua kila kitu. Mtindo unaomlenga mtoto na dhana yake ni kwamba mwalimu anachochea, kuibua na kujaziliza kile ambacho tayari mtoto ana fununu nacho. Mwalimu anajifunza kutoka kwa mtoto, na mtoto anajifunza kutoka kwa mwalimu. child in need of prolonged assistance: mtoto mhitaji mwega wa muda mrefu: 1. mtoto mwenye umri chini ya miaka mitatu ambaye 37 kutokana na ukubwa wa viwango vya ulemavu wa maungo, akili, matatizo ya kimhemko au mjumuiko wa matatizo kama haya, huhitaji huduma za kielimu, kijamii, kisaikolojia au kimatibabu zaidi ya vile ambavyo hutolewa kikawaida ili kumwezesha kufikia ukomo tarajiwa wa uwezo na ushiriki wenye manufaa kwenye jamii na kujinufaisha binafsi. 2. mtoto mwenye mahitaji maalumu ambaye huhitaji usaidizi wa ziada kwa kipindi ili ama amudu kuhudhuria masomo darasani au ayaelewe masomo anayofundishwa (mafunzo mgango) na kisha anufaike na kinachofundishwa. children of different development stages: watoto wenye kuhitilafiana kasi ya ukuaji: watoto wenye rika sawa lakini viwango tofauti vya kuelewa, kuyamudu mambo yenye kuendana na umri walio nao. cholinergic: -a kikolini, -a neva otonomiki ambazo hutoa asetilikolini zinapo-hamasishwa. xl chores: kazi ndogondogo za kila siku: shughuli za kuchosha zinazofanywa kila siku (linganisha na shughuli za maisha ya kila siku). chorea: kwarea: ugonjwa wa mfumo wa neva ambao unahusiana na uambukizo wa homa ya rumatiki; dalili zake ni hali ya kuenenda kusikohiari, kusikokusudiwa na kusikotabirika kwa misuli mwilini;

56 hutokea agh. kwa wanawake hasa katika umri mdogo. xli choreoathetosis: kwarea-athetosisi: mchanganyiko wa kwarea na athetosisi. chromosomal abnormalities: uatilifu wa chembeuzi: hali ya kuwa na kasoro au kuharibika kwa kromosomu za mtu. chromosomes: chembeuzi: kitu kama nyuzinyuzi katika kiiniseli cha kiumbe ambacho hubeba viiniurithi au vinasaba na kwa hiyo huwa na jukumu muhimu kwenye ukuaji wa tishu na sifa au tabia za kurithi. chronic: sugu: ugonjwa unaokuwepo kwa muda mrefu au unaojirudiarudia/sendeka. circulatory condition: msambao: hali ya mzunguko hususani ule wa damu mwilini. circumstantiality: mdororo kauli: dhana isiyokuwa ya moja kwa moja inayotumika katika kuelezea jambo la msingi linalozungumzwa kwa sababu zisizo za msingi. Halikadhalika, majibu au matamko yanaweza kurefushwa endapo mzungumzaji hatakatishwa ili kusema kile kilichokusudiwa. Hali kama hii hujitokeza kwa watu wenye mvurugiko wa msukumo wa haiba na wengi wenye mivurugiko ya kiakili. citizen: raia: mtu yeyote mwenye haki ya kuishi katika nchi fulani na kuwa na haki ya kupata mafao ya kijamii na kisheria ya nchi hiyo pamoja na 38 kuwa na wajibu wa kufuata masharti ya kisheria yanayohusiana nayo. xlii citizen advocacy: utetezi wa raia: uhusiano baina ya watu wawili ambao mmoja anayejitolea ana uwezo kiakili, kistadi, kitaaluma, n.k. ilihali mwingine ni mwenye ulemavu wa ukuaji na kwa hali yake anahitaji msaada wa utetezi ili kumudu kutengemaa na kuwa mwanajamii anayechangia kiustawi. Halikadhalika, hii ni mbinu ya kumsaidia mtu kukabiliana na hali zenye misukosuko, kutetea haki zake na kuwezesha mchangamano ndani ya jamii. Mbinu hii haimaanishi kuwa mbadala wa huduma za kitaaluma anazostahili mtu mwenye ulemavu wa ukuaji, ila ni kuzikamilisha kwa kuwa na uhusiano wa kusaidiana na mwanajamii. citizen advocate: mtetezi wa raia: mtu mwenye ujuzi wa sheria anayejitolea kutetea maslahi ya mwingine mwenye ulemavu au aliye na mahitaji makubwa ya kujieleza na ambaye bila msaada wa kitaalamu au uingiliaji kati maalumu, mahitaji yake hayawezi kukidhiwa. citizenship: uraia: 1. uanachama wa kisheria katika jamii inayojulikana kama nchi. 2. haki ya kisheria ya kuwa mwananchi. civil: -a raia: 1. -enye kuhusu mwananchi au makundi wanayoishi ndani ya nchi. 2. a masuala

57 yanayoihusu serikali na siyo dini au majeshi. 3. -enye kuhusisha masuala binafsi kisheria na siyo sheria za kijinai. civil rights: haki za kiraia: 1. haki ya raia kuwa huru na sawa 2. haki binafsi ya mtu katika jamii kama zilivyoainishwa kwenye Azimio la Dunia la Haki za Binadamu la 1948 ambazo zinahusiana na haki za kiraia na zile za kisiasa kwa kuahidi pamoja na mambo mengine: haki ya uamuzi binafsi; uhuru wa mamlaka ya utajiri wa asili na rasilimali; uhuru wa kutokandamizwa; haki sawa ya kuishi wanawake na wanaume; haki ya kutonyanyaswa au kufanyiwa unyama na kudhalilishwa; uhuru wa kutokuwa mtumwa; haki ya kutofungwa au kuwekwa mahabusu kinyume cha sheria; uhuru wa kutoka eneo moja na kwenda lingine ndani ya nchi; uhuru wa mawazo au dhamiri na wa dini; uhuru wa kutoa maoni; uhuru wa kukusanyika kwa amani; uhuru wa kuanzisha vyama na kushiriki katika masuala ya umma. xliii. Mamlaka nyingine zinazopanua haki hizi kujumuisha pia: haki ya kuishi, usawa mbele ya sheria, ufikivu wa vyombo vya kutoa haki, usikilizaji wa haki mashtaka mf. kuwakilishwa. Kwa mifumo na mitazamo ya kijamii iliyopo, humfanya mtu mwenye ulemavu kutonufaika na mambo haya ya msingi. 39 civil society: chama cha kiraia: chama kisicho cha kisiasa lakini pia kinachofafanua muundo, tabia, imani, utamaduni, unaohusiana na falsafa maalumu ya kisiasa. Sheria ya watu wenye ulemavu ya nchini Tanzania 2010 inaainisha asasi hizi ikujumuisha: asasi zilizojikita kwenye jumuiya, asasi zisizo za kiserikali, asasi zenye mirengo ya kidini, asasi za watu wenye ulemavu, asasi za sekta binafsi, vyama vya wafanyakazi na vya kitaaluma. classifications: uainishaji: mgawanyo wa vitu katika makundi mbalimbali kulingana na aina zake. clear floor space: ushoroba : eneo la chini lenye nafasi bila kuwa na vizuizi linalohitajika kwa ajili ya kuwekea walao kitimwendo na mtumiaji wake. cleft lip or hare lip: ukitange: 1. uwazi au pengo kwenye mdomo wa juu ambao agh. huunganika na matundu ya pua. Katika hali ambapo kuna uwazi mmoja kwenye mdomo humaanisha ukitange sahili na pale inapokuwepo michaniko miwili, hudhihirisha ukitange pacha. 2. mpasuko wa mdomo wa juu, hali ambayo mtoto anaweza kuzaliwa nayo. Wakati mwingine mtoto anaweza kuwa na mipasuko miwili kwenye mdomo huohuo mmoja. Ukosefu wa adabu lugha, umesababisha kuupachika ulemavu huu majina ya kejeli na potoshi

58 kama vile mdomo wazi** au mdomo sungura** simple cleft lip: ukitange sahili: hali ambapo kuna mpasuko mmoja kwenye mdomo. double cleft lip: ukitange pacha: hali ya kuwa na mipasuko miwili, kwenye mdomo wa juu. cleft palate: ukitange kaakaa: 1. uwazi kwenye ukuta wa juu wa kinywa unaounganika na mfereji wa pua au kaakaa gumu. 2. mpasuko wa ukuta wa juu wa kinywa hali ambayo mtoto anaweza kuzaliwa nayo. xliv clinical psychologist: mwanasaikolojia tiba: mtaalamu wa afya aliyepata mafunzo ya kufanya kipimo cha saikolojia, kutathmini na kutibu mivurugiko ya mihemko. Hata hivyo, hawezi kumwandikia mgonjwa maelekezo ya dawa. clinical reasoning: taamuli ya kitabibu: mchakato wa kufanya uamuzi kimpangilio kwa kuegemea marejeo endelevu ya wazi na kwa kutumia data za kidhanifu na zile halisia zilizokusanywa kwa kupitia michakato ya kiupimaji na kitathmini. clinical team: timu ya kitabibu: kikundi cha watu kinachohusisha mzazi, mtoto, mtaalamu wa 40 tibaviungo na tibaliwaza, fundisanifu k.v. mhandisi marekebisho au mtaalamu mwingine wenye maarifa ya ubunifu au utabibu kuhusu uwekaji au upangaji wa visaidizi, wauzaji wa jumla na rejareja wa vifaa tiba (pia hujulikana kama wachuuzi) ambao huduma zao zinaweza kuhusisha uuzaji wa visaidizi. Mchango wa mawazo kutoka kwa walimu, waamarajamii, wauguzi wa huduma za marekebisho na watu wengine vilevile unaweza kuwa na umuhimu. clinical social worker: mwamarajamii tiba: mtaalamu wa afya ya akili aliyefuzu mafunzo ya kutoa huduma kwa mtu binafsi, familia, na makundi mbalimbali. Hata hivyo, mtaalamu huyu, hawezi kutoa maelekezo au kuandaa cheti cha kupatia dawa. closed circuit television magnifier CCTV or video magnifier: kiookuza: teknolojia ya kielektroni yenye matumizi anuwai ya uoni; mathalani inaweza kuwa kamera ya usalama, televisheni yenye kioo cha kukuzia maandishi ili kumsaidia mwenye uoni hafifu kujisomea, kishikio kwa ajili ya uwekaji wa kamera pasi kushikiliwa kwa mikono, monita ya kuangalia skrini, lenzi zenye uwezo wa kukuza (mara nyingine hadi kufikia ukubwa wa 82x), na

59 namna ya utazamaji kwa kutumia mwanga, rangi, na mbinu nyingine za utofautishaji kwa ajili ya msaada wa juu wa uoni. Kwa kawaida, kuna jukwaa la kutazamia, ambalo huruhusu uwekaji rahisi wa kifaa, kitabu, au sura inayokusudiwa kukuzwa. closed captioning (CC): kidokezo fiche: alama hii huashiria chaguo la ama kuonyesha au kutokuonyesha vidokezo kwenye programu za televisheni au mikanda ya video. Aina ya televisheni zenye mifumo iliyojengewa ndani kwa ndani au visimbuzi tofauti huwa vina uwezo wa kuoyesha maelezo ya programu zenye vidokezo pale mtazamaji anapoamua kuona. Aidha video ambazo ni sehemu ya maonyesho zinaweza kuwa na maelezo ya matumizi yanayopatikana kwa kubonyeza kitufe. club foot: wayopindu (pia talipesi): 1. aina ya kilema ambapo wayo wa mtoto mchanga hugeukia ndani, agh. kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba wayo huelekea upande au hata kupinduka juu chini. Hii ni kutokana na tendoni zenye kuunganisha misuli ya mguu na wayo kuwa fupi na zilizokaza. 2. hali ya kupinda kwa kanyagio la mguu kutokana na kufupika kwa kano (tendoni) za misuli. Baadhi 41 ya Kamusi hufasili kilema hiki kama mguurungu** Hii ni tafsiri sisisi ya kidahizo cha Kiingereza. Halikadhalika, tafsiri hii inakiuka kanuni ya adabu lugha na akhlaki za ulemavu kwa kubeba maana ashirifu ya mrengo wa kitabibu na kihisani. cluster: kongano: 1. mkusanyiko wa vitu vya aina moja ambavyo vina uhusiano wa karibu. 2. hali ya kuweka vitu vinavyofananafanana kwenye makundimakundi ili kurahisisha maelezo, huduma, n.k. cochlea: koklia: kifereji kinachojizungusha mithili ya gamba la konokono ndani ya mfupa wa kichwa ambacho huhifadhi vipokeo vya sauti kutoka sehemu ya sikio la kati na kuzigeuza kuwa ishara au mawimbi ya umeme na kuyapeleka kwenye ubongo kwa ajili ya kutafsiriwa kisawiri. cochlear implant: kokliapandikizi: 1. aina ya kiungo mnemba cha tiba kinachopandikizwa sikioni ili kuhuisha usikivu. 2. upasuaji kwa ajili ya kupandikiza kifaa bandia chenye vifani bandia vya kielektroni ndani ya sikio ili kuchochea na

60 kurudisha usikivu. 3. elektrodi iliyowekwa kwenye koklia na kuambatishwa na koili ambukizi iliyopachikwa chini ya ngozi karibu na sikio. Kifaa kingine kinavaliwa mwilini ili kubadili au kugeuza mawimbi ya sauti kuwa kichangamsho (kama mawimbi ya umeme) ambacho huchochea nyuroni za mshipa wa neva. Hutoa usikivu wenye kikomo kwa wale wasioweza kunufaika na visaidizi vya kawaida vya kusikilizia. code: sheria: 1. utaratibu wa kijamii ambao hupangwa kwa mfumo maalumu. 2. msimbo mfumo wa maneno, namba au ishara inayotumiwa kutuma ujumbe wa siri au katika mawasiliano mf anuwani za posta zinazotambulisha mitaa. cognissance: utambuzi: 1. hali ya kuwa na maarifa au uwezo wa kuelewa kitu. 2. haki au mamlaka ya kushughulikia jambo kisheria. Kwa watu wenye ulemavu, kipengele hiki huzipotosha sana baadhi ya mamlaka mbalimbali hususani zile za kisheria kwa kudhani kuwa kila mwenye ulemavu anatindikiwa na hali hii. cognition: ufahamu: utambuzi, dhana, uundaji taswira, fikira au tafakuri, na uamuzi ili kuupa ulimwengu wa ndani utajiri na ubora wenye kufanana. Ulimwengu huo unapobughudhiwa huathiri ukuaji wa shauku ya kuchangamana, 42 uwezo wa kuwasiliana, kuashiria, kujifunza na kujenga hoja. cognitive and social development: ustawishaji utambuzi jamii: dhana yenye kuhusiana zaidi na mtu mwenye kilema cha utambuzi na ukuaji kiasi cha kuhitaji stadi za kuchochea uelewa wake ili ayamudu mazingira alimo. cognitive disorders: mvurugiko utambuzi: hali inayobainisha kusawajika kwa mchakato wa kukumbuka, kutafakari, kuelewa, kutatua matatizo, kutathmini na kuamua. cognitive skills: stadi utambuzi: maarifa muhimu yanayofaa kwa ajili ya matumizi bila kujali hali ya kimazingira au uwezo wa milango ya fahamu ya mhusika. cognizable: 1. -enye kuweza kushtakiwa au kufikishwa mbele ya mahakama. 2. enye uwezo wa kuchunguza jambo kisheria. colourblindness: upofurangi: kasoro ya macho kushindwa kutofautisha aina za rangi, hasa rangi nyekundu na ya kijani. communication: mawasiliano: kwa muktadha wa watu wenye ulemavu humaanisha: 1. mchakato wa kupeleka au/na kupokea taarifa katika hali ambayo pande zote mbili zinaelewana. Taarifa inaweza kutumwa au/na kupokelewa kwa njia ya ishara, maandishi, matamshi, au mpapaso.

61 2. hujumuisha lugha, onyesho la matini andikwa, nuktanundu, mawasiliano ya alama mpapaso, maandishi yaliyokuzwa, njia za mawasiliano zinazofikika na kupatikana kimaandishi, kwa sauti, lugha nyepesi, wasomaji (kwa ajili ya wasioona), mawasiliano yaliyoongezwa nguvu na njia nyingine mbadala. Njia na miundo ya mawasiliano hujumuisha upatikanaji wa habari na teknolojia ya habari. 3. kisheria humaanisha kubadili hukumu au adhabu. communication disabilities: ulemavu wa mawasiliano: aina yoyote ya ulemavu wa uoni, uziwi, ukuaji au kutokutamka ambao humpunguzia mtu uwezo wa kuwasiliana. communication disorders: mvurugiko wa mawasiliano: hali ya kutokuweza kuwasiliana katika namna inayofaa kutokana na ama uziwi, kutoweza kutamka, au kuvurugikiwa upande wa lugha. communication skills: stadi za mawasiliano: maarfa ya kuunganisha maana na madhumuni ya kile kinachosemwa na yale yanayotendwa kwa kudhamiria. community: jumuia: kundi dogo ndani ya jamii linalojipambanua kwa misingi ya mbari, itikadi, imani, eneo la kijiografia, upendeleo, aina ya shughuli, n.k. community based rehabilitation interventions: afua marekebisho za kijumuia: hatua zinazochukuliwa na wanajamii kuhusu kumwezesha mtu mwenye ulemavu kuchangamana kiurahisi na wanajamii wenzake na kisha kumudu kuchangia vipawa vyake katika ustawishaji wa jumuia na watu wake. community support system: mfumo saidizi wa jumuia: mfumo wa kuhudumia uliopangiliwa na kutolewa kumsaidia mtu mwenye mahitaji maalumu (k.v. mwenye ulemavu) kwa muda mrefu ili kuwawezesha kukidhi mahitaji yao na kukuza uwezo wao bila kutengwa na jamii pasipo na ulazima. community support: usaidizi wa jumuia: huduma zinazotolewa kwa mtu mwenye ulemavu na yeyote aliye na mahitaji maalumu, familia na jumuia za watu kama hao zinazojumuisha: i) kusaidia majirani na jamii kuwajibika zaidi kwa mahitaji ya mtu mwenye ulemavu na familia yake; ii) kujenga mitandao mahalia inayoweza kutoa miawana katika eneo hilo; iii) kuifanya jamii ifikike na kuiwezesha kutoa rasilimali na fursa zake kwa mtu mwenye ulemavu na familia yake. Miawana ya kijamii huhusisha: elimu ya kijamii, huduma za misaada, marekebisho ya 43

62 makazi na vyombo vya usafiri, msaada wakati wa kazi na usafiri. community-living activities: shughuli amara kijumuia: shughuli muhimu katika kumwezesha mtu mwenye ulemavu kuendelea kuwa na mipango ya makazi bora na miawana ndani ya jamii (ikijumuisha ile isiyokuwa ya kifedha, huduma kwa mtu, familia na jumuia). compact: maafikiano: makubaliano kati ya mataifa kadhaa kuhusu masuala fulani yanayozihusu nchi hizo. compassionate use: uraufu: hali ya utulivu ambayo mtu huhitaji hasa baada ya kupatwa na masaibu kama vile kufiwa na mtu wa karibu, kuugua, n.k. Katika mazingira ya kiajira, mwajiriwa hupewa siku kadhaa za mapumziko. compatibility: ulaiki: ulinganifu wa mambo au hali ya kitu kimoja na kingine; upatano, usawa. compensate: fidia: lipa mtu kwa ajili ya madhara aliyofanyiwa. compensatory skills: stadi tengamalishi: 1. hali ya mtu mwenye ulemavu kupata maarifa ya kujitengemalisha ambayo hupatikana kwa kumfundisha asiyeona, mwenye uoni hafifu na msaidizi wake ili amudu kuishi maisha ya kuzalisha kwa tija. Baadhi ya stadi hizo ni pamoja na: utambuzi wa maeneo wakati wa kutembea, jinsi ya kumudu shughuli za nyumbani kama vile kupika, kushona na mawasiliano kama vile maandishi 44 ya nuktanundu, maandishi yaliyokuzwa, kujua majira, n.k. 2. stadi zenye kufidia zile (stadi) zilizopotea baada ya kupata ulemavu. compensatory curriculum: mtaala fidia: mkabala wa mafunzo ambao hufundisha stadi ambazo ni za vitendo ili kumwezesha mwanafunzi kujikimu katika jamii k.v. kujitunza, stadi za kijamii na amalli, ufundi na kazi. competence: umilisi: 1. fungu au uwezo, uwajibikaji, maarifa au stadi zinazomwezesha mtu kufanya kazi inavyopaswa. 2. uwezo wa mtu kuelewa hali na kumudu kukabiliana nayo. 3. kipimo cha hali ya akili ya mlalamikiwa katika kukabiliana na shtaka la jinai wakati wa mashtaka. Vipengele vya baadhi ya sheria za nchini Tanzania, mathalani, ile ya uchaguzi, kadhalika desturi na mila, huwa na tafsiri ya kuwa mtu mwenye ulemavu hana umilisi na hivyo kumnyima haki ya kujiamulia mambo yanayomhusu binafsi au kama raia. competency to stand criminal trial: uwezekano wa kushtakiwa kwa jinai: hali ya mtu kushtakiwa pale ambapo: (1) anaelewa hali ya mashtaka yanayomkabili na matokeo yake pindi akitiwa hatiani na (2) ana urazini wa kusaidiana na wakili wake kwenye utetezi. Hii ni tofauti na matakwa (au viwango) ya mtu ya kawaida. Kwa vile hali hii

63 hutumika kama utetezi mbadala kwa mawazo yasiyokubalika zaidi yanayotolewa bila ufahamu, kushindwa kutekeleza tendo lisilothibitika (kisheria) husababisha wasiwasi. competent authority: uhalali wa kisheria: hali ya kuwa na mamlaka ya kushughulikia jambo). competent organs: -wa na mamlaka kisheria: chombo kilichokasimiwa madaraka ya na dola ili kutenda au kuamua mambo katika uga fulani. complement: jaliza: kuongezea kitu kwa kingine ili kukikamilisha, kukiboresha au kukifanya kivutie zaidi. complexity: utata: hali isiyoelezeka kiurahisi; gumu kufahamika. complementary: -enye kitu cha ziada: kitu kingine tofauti au zaidi kinachounganishwaunganishwa ili kuunda kitu kizima au kusaidiana na kile cha awali kuleta ufanisi. comprehensive: -a kina. 1. (kielimu) iliyoandaliwa kwa ajili ya wanafunzi wa aina na hali zote shuleni. 2. inayojumuisha kila kitu, takribani kila kitu, yaani taarifa, matendo, ukweli, vinavyoweza kuwa vinahitajika. compulsion: ushurutishaji: hali ya kulazimika kutenda jambo. compulsive personality disorder: mvurugiko shurutishi wa haiba: uwezo mdogo wa kuonyesha hisia za uchangamfu na upendo unaojibainisha kwa kujishughulisha na kanuni, sheria, ufanisi na mambo 45 madogomadogo; kujikusuru kufanya kazi na uzalishaji kupindukia kiasi cha kupuuzia kupumzika au/na kutokata shauri. computer accessibility or accessible computing): ufikivu wa kompyuta: hali ya kila mtu kumudu kuifikia kompyuta bila kujali aina au kiwango cha kilema chake. Kwa muktadha huu, istilahi ufikivu agh. hutumika kwa kurejelea maunzilaini. Pale ambapo maunzingumu mahususi au muunganiko wa mauzilaini na ngumu unapotumika ili kumuwezesha mtu mwenye ulemavu huitwa teknolojia saidizi. Zipo aina nyingi za vilema vyenye kuathiri uwezo wa matumizi ya kompyuta ikiwa ni pamoja na: vilema vya utambuzi, ujifunzaji, disleksia, usonji, uoni, uziwi, msogeo, mpoozo wa ubongo, n.k. concealment: kutoonekana: kuzuia kubainika au kugundulika; kujificha. concentrate: makinika: 1. hali ya mtu kuelekeza usikizi na uangalifu wake wote mahali au kwa kitu kimoja. 2. hali ya kuelekeza kitu sehemu moja. 3. kutumia muda wote kufanya jambo moja na siyo kitu kingine chochote. conceive: ikirari: kutunga wazo akilini au kulielewa jambo kwa kulitafsiri au kulichimba kwa kina zaidi kwa kuhusisha taswira thabiti. concept formation: ujenzi ikirari: uundaji wa hulka ya kutumia uzoefu

64 au tajiriba kuongoza mwenendo wa mtu katika mazingira mapya. concept paper: ikirari: 1. uhakika wa jambo lililotokea, 2. tamko la maandishi la uthibitisho. 3. ukubalifu, ungamo. 4. ushahidi, ushuhuda,. 5. hakika, neno la dhahiri. conceptual skills: stadi milisi dhana: lugha na uwezo wa kusoma,, muda na idadi ya fikira na uwezo wa kujielekeza au kujiamulia. conditioned reaction: mjibizoevu: kanuni ambayo huwa na matokeo maalumu yanayotokana na mazoea. conditioning: uzoezaji: 1. mafunzo maalumu au uzoefu alionao mnyama au binadamu unaomfanya awe na mwenendo wa namna fulani katika mazingira au hali mahususi. 2. kudhibiti hali ya joto kwa kutumia kiyoyozi conducive learning condition: hali inayofaa kiujifunzaji: kurahisisa mbinu na mazingira utoaji masomo, na uwezekanifu wa kupata maarifa. conduct disorder: mvurugiko kimaadili: hali yenye kubainishwa na mfumo usiobadilika wa mwenendo unaokiuka ama haki za wengine, kanuni au sheria zinazokubalika kijamii. Mienendo ya aina hii inaweza kujumuisha ukandamizaji dhahiri, kuvuruga, ukanaji, kutowajibika na kutotii mamlaka. confabulation: fidiamawazo: 1. utungaji wa visa au matukio katika kujibu maswali kuhusu hali au visa visivyokuwa na kumbukumbu kamili kutokana na kukosekana kwa kumbukizi. Hali ni tofauti na kudanganya kwani huwa hakuna dhamira ya kuhadaa. 2. masimulizi ya matukio bandia ambayo mgonjwa anaamini yalimkuta na ambayo si halusinensheni; masimulizi haya ya kubuni ni ya kuziba mapengo kutokana na kuwa na hali ya usahaulifu hasa kwa matukio yaliyopita hivi karibuni. xlv conforming: uendanaji: ufuataji wa sheria, kanuni, viwango vilivyokubaliwa; fanya sawa na; kuridhia kiwango kilichopo au kufikia makubaliano. congenital blindness: upofu wa kuzaliwa: hali ya mtu kupoteza uoni tangu kuzaliwa, au uchangani. Kinyume chake ni upofu wa kinasibu. congenital condition: hali rithiwa: hali ambayo mtu anazaliwa nayo kutokana na urithi au vinasaba. Hali hii inaweza kuwa kasoro za kimaumbile au tabia. congenital deaf-blindness: uziwipofu tangu kuzaliwa: hali ya upofu au uziwi ambayo mtu huwa nayo wakati wa kuzaliwa au akiwa mchanga. Visababishi vya kawaida vya hali hii ni dalili za surua isiyokali (rubella) wakati wa ujauzito 46

65 (angalia: uziwi, upofu, uziwipofu nasibu). congenital muscular dystrophy (CMD): msinyao misuli tangu kuzaliwa: kundi la misuli au mishipa iliyosinyaa ambayo huwa bayana (kwa mtoto) karibu na kuzaliwa. Kwa ujumla, msinyao wa misuli ni atiliko la kuzaliwa nalo au kupatwa na maradhi ya kusawajika ambayo kimsingi huathiri mishipa ya hiari. Msinyao wa misuli tangu kuzaliwa husababisha udhaifu wa misuli kwa ujumla na pengine ukakamavu au ulegelege wa vifundo. Kulingana na aina yake, msinyao wa misuli tangu kuzaliwa unaweza kuhusisha mpindo wa uti wa mgongo, kupumua kwa shida, ulemavu wa ujifunzaji, kasoro za macho au kifafa. Msinyao wa misuli tangu kuzaliwa, husababishwa na mabadiliko ya kinasaba yanayoathiri baadhi ya protini muhimu kwa ajili ya mifupa na mara nyingine kwa ajili ya macho na ubongo. Msinyao wa misuli tangu kuzaliwa huanzia mwanzoni (mwa ujauzito) au karibu na muda wa kuzaliwa (kwa mtoto), na maendeleo yake hutofautiana kulingana na aina yake. Aina zingine huwa ni za muda mrefu; na baadhi huchukua muda mfupi tu. congenital rubella: surua ya kuzaliwa: surua ambayo mama mjamzito huambukizwa, ikasababisha matatizo kadhaa kwa mtoto aliye tumboni ikiwa ni pamoja na mpoozo 47 wa ubongo, uziwi, upofu na matatizo mengineyo ya kinyurolojia. congenital syphilis: kaswende ya kuzaliwa: aina mojawapo ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono ambapo mama mjamzito aliye na maambukizo anaweza pia kumwambukiza mtoto aliye tumboni, na hivyo kuchochea mimba kuharibika au kuzaa mtoto mfu. connotation: uashiriaji: wazo au hisia inayotokana na tafsiri ya neno tofauti na maana yake asilia. xlvi Mathalani, neno asiyesikia, haliwezi kuwa na maana ya uziwi moja kwa moja, kutoona hakuwezi kumaanisha upofu moja kwa moja, ulemavu wa ngozi hauwezi kumaanisha ualbino moja kwa moja, ulemavu wa akili hauwezi kumaanisha moja kwa moja kutostawi au kuwa na matatizo ya afya ya akili, n.k. Kiujumla istilahi hii hujielekeza kwenye wazo au hisia inayotokana na tafsiri ya neno tofauti na maana yake asilia (usafidi au tafsida). connotative meaning: maana ashirifu: misamiati mingine kama vile kipofu, kiwete, taahira, kiziwi, n.k. inapotumiwa kumaanisha kutomudu au kutoweza. conscience: dhamiri: hali ambayo hujificha ndani ya nafsi ya mhusika na kuwa msingi wa mtu kufanya uamuzi, kuwa na tabia au imani ya aina fulani. Hata hivyo, mhusika

66 huhitaji kuwa huru ndipo aihengehenge dhamiri yake. Ufifishwaji wa dhamiri husababisha sononi kwa kukosa jambo la kulisimamia maishani. Agh., watu wenye ulemavu hukumbwa na adha hii ya kutokuwa na fursa ya kuwa na dhamiri kutokana na wanandugu au jumuia kuwaamulia kila kitu au kuwapotosha. conscious: -a ufahamu: -enye kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu jambo linalokusudiwa au linalotendwa. consciousness: utambuzi: hali ya kuchukua tahadhari au kuwa makini wakati wa kuitikia dhamiri. consent: ridhaa: hali ya utashi ambapo mtu hujiamulia jambo la kufanya au kufanyiwa. Agh. fursa ya mtu wenye ulemavu kuridhia mustakabali wake hubinywa na wenye mamlaka juu yake; mathalani, kwenye masuala ya tiba, mfumo wa maisha kwenye familia au/na ndani ya makazi, faragha, uhusiano, kuzaa na kulea, n.k. conservatorship/guardianship: uhifadhi: udhamini utolewao kwa amri ya mahakama ambao kwao mtu au taasisi huteuliwa (a) kusimamia mali au miliki za mtu aliyehukumiwa kuwa hana uwezo (sio lazima akose uwezo, maarifa, siha kiasi cha kutosha) wa kuyaangalia mambo yake; au/na (b) kuwa na wajibu wa uhifadhi na uamuzi unaofanywa kwa niaba ya mtu pale ambapo mtu yule 48 (mwenye mali) anahisi kutomudu kujitunza. Katika baadhi ya nchi, mlezi humsaidia mtu wakati mhifadhi akisaidia upande wa mali za huyo mtu. conserve: hifadhi: 1. kulinda au kuzuia kitu kisibadilishwe au kuharibiwa. 2. hali ya kubania kitu kwa kutumia kidogokidogo ili kidumu kwa muda mrefu. consortium: ubia amali: 1. hali ya kuungana au kusaidiana kufanya shughuli fulani. 2. muungano wa vyombo viwili au zaidi kwa lengo maalumu. 3. kisheria ni haki ya mwenzi kupata mafao ya uhusiano wa mume na mke kwenye ndoa. constipation: kufunga choo: hali ya kukosekana kwa haja kubwa au kukosekana kwa ukanuni wake au kupata choo kigumu na kwa shida. xlvii. Hali hii ni miongoni mwa matatizo mkubwa yanayomkumba mtu mwenye ulemavu unaotokana na kuumia kwa ugweuti. construction: ujenzi: hali inayojumuisha ujengaji, umiliki wa jengo jipya, upanuzi, ubadilishaji, kinga kwenye majengo yaliyopo, ikiwa ni pamoja na usawazishaji na uboreshaji wa eneo na ada ya ujenzi. Ujenzi ni amali ambapo programu nyingi za mafunzo hutolewa. consultant: mshauri: bingwa ambaye ni mtaalamu katika eneo fulani (mfano, ulemavu wa upofu, uziwi, n.k.) anayesaidia kundi katika kupanga mipango yake (mf. elimu

67 kwa ajili ya mtoto mwenye ulemavu). Mshauri pia huhudumia kama mfanyakazi mwega kwa mzazi na mtumishi wa shule kuhusu vifaa maalumu, mpangilio wa darasa, uendeshaji au usimamizi wa teknolojia saidizi au visaidizi vya kujazia, n.k. Mshauri hajishughulishi moja kwa moja na mtoto, au uamuzi juu ya utendaji wa mtumishi. consultation: uelekezi: 1. uwezeshaji wa wengine kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuhusu malengo ya programu. Stadi maalumu inayotumika ili kuwezesha shughuli au mipangilio kuendeshwa vizuri. 2. mchakato wa majadiliano ya pande mbili ili kufikia mwafaka wa jambo linalojadiliwa ambapo pande husika zilikuwa zikihitilafiana kimtazamo. consultative services: huduma elekezi: shughuli inayofanywa na mtaalamu ili kuinua ubora wa jambo (mf. elimu) au afua nyinginezo kwa ajili ya kundi; mathalani, la watu wenye ulemavu. contact lens: lenzi pachikwa: lenzi ya plastiki ambayo huvishwa moja kwa moja kwenye konea ya jicho ili kuboresha kiwango cha uoni. continuum of placements: huduma mwendelezo: aina za huduma zinazotakiwa kwenye shughuli kuendana na mahitaji mahususi; mathalani, kusadifu mahitaji ya mtoto mwenye ulemavu kielimu ikiwa ni pamoja na kuwa kwenye darasa la kawaida lenye mwalimu mtaalamu au asomipaka, darasa 49 maalumu, kuendesha maelekezo majumbani, na hospitalini au kwenye makazi maalumu, na maeneo ya huduma nyingine kama zile za kisheria, kiimani, kibiashara, na starehe au burudani, n.k. contracture: msinyao: 1. upungufu wa msogeo wa fundo, agh. kutokana na ufupi wa misuli. 2. mkunyatiko wa kitu kutokana na kupungua kwa joto au kujikunja n.k. 3. fupisha, kunja. 4. ambukizwa vimelea. 5. kufupika kusikohiari kwa misuli laini - yaani ufupi wa kudumu wa sehemu laini za mwili k.m. kano au ngozi; ulemavu wa kifundo kutokana na sababu kukakamaa au kufupika kwa misuli kunakosababishwa na fisiolojia au/na kutotumika, matokeo ya kupungua kwa nyendo za vifundo, mathalani, iwapo kiwiko au goti litabaki limejikunja kwa muda mrefu, itakuwa vigumu zaidi kulinyoosha. convention: mapatano au maagano: makubaliano kati ya nchi mbili au zaidi ambayo mara nyingi yanahusiana na masuala ya maslahi ya pamoja. Wakati ambao

68 aina hii ya makubaliano inatakiwa kushughulikia masuala yasiyo muhimu, lakini hushughulikia pia masuala muhimu kama vile ya makundi maalumu ndani ya jamii, mathalani, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, wakimbizi, wafanyakazi, n.k. xlviii convention on the rights of persons with disabilities (CRPD): Mkataba Wa Haki Za Watu wenye Ulemavu (MHWU): mkataba mahususi uliopitishwa na Umoja wa Mataifa (2006) ambao unazielekeza nchi wanachama mambo ama ya kutenda au kutotenda ili kumwezesha mtu mwenye ulemavu kunufaika na haki zake kama zilivyoaainishwa kwenye mkataba huo na mingineyo ya kimataifa na kikanda. conventional method: mbinu kawaida: mfumo unaotekelezwa kwa kufuata utaratibu unaodhaniwa kuwa unakubalika na jumuia kwa ujumla. conversion symptom: dalili za mabadiliko: kupoteza au kubadilika kwa utendaji kazi wa mwili ambako kunaashiria mvurugiko wa kimaumbile, lakini katika hali halisi ni kielelezo cha mkanganyiko au mahitaji ya kisaikolojia. Usumbufu haudhibitiki na hauelezeki kwa mvurugiko wowote wa kimwili (uwezekano huu unaondoshwa na uchunguzi mujarabu). convulsant: kitia kifafa: dawa au ajenti yoyote inayosababisha kifafa. xlix 50 convulsant therapy: tiba ya utukutishaji mwili: njia mojawapo ya tiba za magonjwa ya akili ya kudukiza mwili upate mtukutiko kwa kutumia umeme. l convulsion: degedege au mtukutiko mwli: 1. utikisaji wa viungo vya mwili usiohiari. 2. mshtuko wa ghafla wa sehemu au kupindisha mwili mzima. 3. mshtuko wa maungo kama kifafa, degedege au mashetani. coping skills: stadi kabilifu: mbinu au maarifa dhidi ya mhemko, sononi au msongo wa mawazo, unaosababishwa na tukio fulani k.v. kufiwa na mtu wa karibu, kuvunjika kwa ndoa, kupoteza ajira, kuzaa mtoto mwenye ulemavu, kufilisika, kupatwa na majanga kiasi cha kupoteza mali. coping strategies: mbinu kabilifu: mkakati wowote ambao mtu anautumia kupunguza hisia za kimfadhaiko; baadhi ya wanafamilia wanaweza kuchukua hatua chanya, ambapo wengine wanaweza kujaribu kubadili namna ya kufikiri. Mathalani, wazazi wa mtoto mwenye ulemavu wanapoamua kumtelekeza moja kwa moja, kumficha asionekane machoni mwa wageni au wanajumuia kwa minajili ya kujiepusha na aibu ni aina ya mkabala kabilifu ambao ni hasi. coping: ukabilianaji: 1. uwezo wa kujirekebisha na kuvumilia vichochea mfadhaiko katika maisha ya mtu, jamii na mahali pa kazi. 2.

69 mbinu anazotumia mtu kukabiliana na hali ya au msongo wa mawazo. cord: ukamba: 1. kiungo cha mwili kilicho kama mshipi au nyuzi, 2. kano au dutu yoyote kama nyuzi (angalia uti wa ubongo). li core subject: somo msingi: sehemu ya mafunzo ambayo ni muhimu na ya lazima kwa kila mwanfunzi. cork up splint: kombeoamirishi: aina ya kirekebisha kilema kitumikacho kutibia aina mbalimbali za hali; mathalani, dalili za kupinda au kuumia kwa kifundo cha mkono. corneal dystrophy: distrofia za konea: 1. ugonjwa wa kuzaliwa nao ambao huathiri macho yote na hujidhihirisha wakati wa balehe ambapo konea kwa taratibu hurundika dutu zinazofanana na hailini. lii. 2. hali za nadra za macho na nyingi ya hizi hutokea katika miongo michache maishani mwa mtu. Distrofia ya aina ya Fuch ni ya tofauti sana maana yenyewe humtokea mtu baada ya muda mrefu zaidi. Nyingi za distrofia za konea 51 hupokezana kwenye familia na pale distrofia ya konea inapogundulika kwa mmojawapo wa wanafamilia, basi wanafamilia wote wa umri wa utu uzima sharti wachunguzwe. Distrofia za konea ni hali za nadra ambapo konea hubadilika bila kuwepo kwa uvimbe wowote, ambukizi wala aina nyingine yoyote ya ugonjwa wa macho. Ung avu wa konea huathirika na uoni unaweza kuvurugika au la. corneal dystrophies familial: distrofia za konea ya familia: ugonjwa wa aina ya distrofia za konea ambao ni wa kuzaliwa nao na baadhi ya watu ndani ya familia moja huupata. corporal punishment: adhabu ya kuutesa mwili: hali ambapo mkosaji huteswa kimwili; agh. kwa kuchapwa viboko. correctional institution or approved school: taasisi adilishi: Magereza au shule yoyote ya kuadilishia aliye kwenye mgongano na sheria; mathalani, shamba la magereza, vituo vya uangalizi ambavyo hufanya marekebisho ya tabia ndani ya jamii, au taasisi yoyote ya aina hii iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzuia au kurekebisha mtenda makosa ya jinai. corset: pagaro pia banio: vazi maalumu (agh. la plastiki) linalovaliwa ili kusimika au kuzoesha unyoofu wa kiwiliwili; (mathalani, fumbatio, kifua au vyote

70 pamoja) ili viwe kwenye mkao unaotakiwa kwa minajili ya urembo au tiba. Usimikaji kwa ajili ya urembo unakusudia kupendezesha (linapokuwa limevaliwa tu) na ule wa tiba hulenga hasa kuleta matokeo ya kudumu au kuuweka mwili kwenye mkao unaotakiwa. cortex: koteksi: sehemu ya nje ya tezi, au ubongo cortical visual impairment (CVI): kilema cha uoni wa koteksi: aina ya kilema cha upofu ambacho husababishwa zaidi na matatizo ya ubongo kuliko yale ya jicho lenyewe. Visababishi hivi hupambanuliwa kwa majina, yaani kilema kinachotokana na hitilafu ya macho huitwa cha uoni wa jicho wakati kile kinachohusishwa na ubongo, huitwa cha koteksi ). Inawezekana mtu kupatwa na aina zote mbili za vilema, yaani cha koteksi na cha jicho. Kilema cha uoni aina ya koteksi wakati mwingine huitwa upofu japo mtu mwenye kilema cha aina hii hawapotezi uoni kabisa. Dhana kilema cha uoni wa kinyurolojia 52 hujumuisha aina zote mbili za upofu zilizozungumziwa awali. Ukawiaji wa kukomaa kwa uoni ni aina nyingine ya kilema cha uoni wa koteksi ila chenyewe hujirekebisha katika kipindi cha miezi michache baada ya kuzaliwa. Japo kiwango cha uoni wa mtu mwenye aina hii ya kilema (cha uoni wa koteksi) kinaweza kubadilika, ni nadra sana (kama itatokea) kurekebika kabisa. Visababishi vikuu vya kilema cha uoni wa koteksi ni pamoja na: asfiksia, hipoksia au iskemia ambazo zinaweza kutokea wakati wa michakato ya kuzaliwa, uatilifu wa ukuaji wa ubongo, kujeruhika kichwani, hidrosifarasi, kiharusi kinachohusisha ndewe ya kisogoni, na maambukizo ya mfumo wa kati wa neva k.v. meninjitisi na ensefalitisi. counseling: unasihi: utoaji elimu na ushauri kwa anayetatizwa na jambo kiasi cha yeye kushindwa kulipatia ufumbuzi. counselor: mnasihi: mtaalamu wa kutoa ushauri. covenant: mapatano: 1. ahadi ya kufanya au kutofanya jambo fulani maalumu; 2. kuingia katika mapatano rasmi (pia mkataba). 3. nadhiri ya maandishi ya siri ya kutoa malipo ya ufadhili kwa kipindi kilichopangwa. liii covenants on human rights: mapatano katika haki za binadamu:

71 mkataba au waraka wa makubaliano; mathalani kuhusu kuheshimu haki za binadamu. creative problem solving: utatuzi matatizo bunifu: 1. mchakato wa kundi kuchangamana na hatua kwa hatua kuainisha suluhisho, kutenga aula za suluhisho, kuchagua na kwa pamoja kutatua tatizo. Mfumo huu umejiegemeza kwenye dhana kwamba watu ndani ya kundi wanaweza kutoa suluhisho bora zaidi kuliko mtu yeyote peke yake. 2. utatuzi wa matatizo ya kundi kwa kutumia mbinu za kiubunifu. cretinism (hypo-thyroidism): udumazi makuzi: 1. kuchelewa katika ukuaji wa kimwili na kiakili ambao hujitokeza pale mwili wa mtoto usipozalisha homoni ya throidi au homoni iliyozalishwa na tezi pituitari zenye kudhibiti zoezi la ukuaji wa mtoto. 2. hali ya kuzaliwa na homoni ya umbilikimo**, ukosefu wa ukuaji wa kijinsia na dalili nyinginezo mwilini kutokana na ukosefu wa madini joto (iodini) mwilini liv. Baadhi ya dalili za ukreti ni: halijoto kuwa chini ya wastani, ngozi nene, kavu na yenye ubaridi, kope zilizovimba, nywele 53 nyingi, ufupi usiowiana na umri, kukosa choo kwa muda mrefu (uwezekano wa kupitisha hata majuma kadhaa, n.k. Tafsiri ya pili hapo juu pamoja na matumizi ya istilahi ukretini** ni vyenye muktadha wa kitabibu ambao haukuzingatia hisia za mtajwa. cripple: kiwete**: 1. jina analopachikwa mtu mwenye viungo vya mwili vilivyosinyaa kiasi cha kutoweza kunyanyuka au kuvinyoosha. 2. hutumika kama jina la jumla kwa watu wenye vilema vya viungo vya mwili. Maana ashirifu ya neno hili ni: mwili uliopindapinda na usiotamanika, mwenye kutambaa tu, asiyethaminika, asiyestahili kimaumbile, dhaifu, siyojimudu**, kiwete**, mwenda chopi,**, haribu, dhoofisha kabisa, hasiri** n.k. Kwa kuzingatia ukweli huu, tafsiri ya pili na maana ashirifu ya neno hili, linakuwa na mtazamo wa kitabibu na kihisani hata kidini ambapo uarifu juu ya kilema hiki hutolewa bila kujali hisia za mhusika

72 mwenyewe. Kwa hiyo, halitakiwi kutumika kwenye utaarifu wowote. Mtu mwenye aina hii ya kilema anatakiwa kutambuliwa na kutambulishwa kama mwenye kilema cha au ulemavu wa ujongevu. crisis advocacy: kukabiliana na migogoro: mbinu ya kukutana kwa hiari au uelezaji bayana wa mahitaji au matakwa yaliyotokana na hali ya hatari, migogoro au maafa unaofanywa na mtu wakati wa hali ya dharura kwa kipindi kifupi. Utetezi wa aina hii ni muhimu sana kwa mtu mwenye ulemavu kutokana na kuathirika kiurahisi nyakati za dharura. crisis intervention: ushughulikiaji wa hali ya hatari: tiba au afua ya muda kwa mtu, familia, makundi, jamii au/na asasi baada ya kuathiriwa na maafa au mabadiliko. Hasara au mabadiliko hudumaza uwezo wa mtu wa kujitatulia matatizo; kadhalika na mwenendo wa utendaji kazi wa saikolojia ya kijamii (taz. coping startegies). criteria: kigezo: taarifa zinazofafanua na kudhihirisha weledi au ubora wa jambo au kifaa kama kipimo cha kuegemea kufanyia uamuzi kwa mambo mengine ya aina yake. criterion-referenced assessment: tathmini urejeokigezo: tathmini inayorejelea upimaji wa utendaji wa mtu unapolinganishwa na 54 vigezo fulani vilivyokwisha wekwa. Katika utaratibu huu, mtu hatathminiwi kwa kulinganishwa na mtu mwingine. cross: -a mtambuko: -enye kuhusiana kila hali ndani ya jamii. cross cutting issues: masuala mtambuko: masuala ya kijamii na kiuchumi yanayoweza kuathiri masuala mengine na ustawi mzima wa binadamu. cross-disability: ulemavu mtambuko: AZAKI, tasisi za kihisani na nyinginezo zinazohudumia watu wenye ulemavu tofautitofauti; mathalani, tapo au vuguvugu la ulemavu. cultural and social bullying: mila-jamii onevu: ukatili, udhalimu, ukandamizaji wenye chimbuko katika mila au utamaduni na jamii. cultural labeling approach: mila ya upachikaji majina: mtindo wa kumpa mtu utambulisho kutokana na tabia ya kupambanua watu kwa kuelezea jinsi maumbile yao yanavyohusiana au kuwiana na viwango vilivyowekwa na mfumo fulani wa kijamii. Huu upaji majina hujielekeza kwenye kumtambulisha mtu kwa kasoro alizonazo kwenye maungo au milango ya fahamu. (angalia maneno zeruzeru, kiguru, kikono, kibiyongo, makengeza, kifutu, macho kumchuzi, n.k.). cultural pluralism: utamaduni-anuwai: hali ya vikundi vidogovidogo kuishi pamoja katika jamii kubwa kwa

73 misingi ya utamaduni huku kila kikundi kikishikilia na kuendeleza mambo yake hususani mila na desturi za kimapokeo. cultural-familial: utamaduni mbari: dhana inayotumiwa kwa mtu mwenye udumavu wa akili ambaye hali yake huhusishwa na tamaduni za kiukoo au sababu za vinasaba. cumulative: limbikivu: -enye kuongezeka idadi au athari kwa ulimbikizaji wa hatua kwa hatua. curriculum materials: vifaa mtaala: vifaa vya mafunzo, unasihi, ushauri sadifu au vyenye kutoa msaada vikijumuisha vile vinavyosaidia ujifunzaji wa teknolojia ya juu katika uga wowote wa kiufundi ili kuimarisha misingi ya taaluma kwa kumwandaa mtu kwa ajili ya ajira ya awali au kukuza uwezo wa kikazi kwa yule aliyewahi kuajiriwa au ambaye tayari ameajiriwa. Vifaa hivi ni muhimu hasa pale mlengwa anapokuwa na ulemavu. curriculum specialist: mbobezi mitaala: bingwa mwenye kutoa msaada wa huduma za ushauri elekezi kwa walimu katika maeneo ya uandaaji masomo ikiwa ni pamoja na mbinu za ufundishaji, uzingatiaji mitaala na mikakati ambatani ya utekelezaji wake hususani kwa kutilia maanani mahitaji anuwai ya kila mwanafunzi. custodial care: malezi ulinzi: matunzo ambayo kimsingi husaidia na kuendeleza afya ya mgonjwa bila 55 matibabu amilifu au yenye kutaka afua ya haraka. Mgonjwa anakuwa ama na kilema cha akili au viungo na hali yake hiyo hutarajiwa kuendelea kuwa hivyo kwa muda mrefu. cyanosis: sinosisi: hali ambapo ukosefu wa hewa ya oksijeni katika damu husababisha ngozi kuwa ya rangi nyeusi au samawati. Dd

74 dactylology: daktilolojia: mawasiliano ya kutumia ishara za vidole k.v. katika kuwasiliana na mtu kiziwi kwa kutumia alama na tahajia za vidole. daily variability: ubadilikaji wa kila mara: kama msemo unavyotumika kuhusiana na uwezo wa kusikia: kitu chochote kinachoathiri uwezo wa mtu kusikia katika siku fulanifulani kama vile mafua, maambukizo sikioni kwa visaidizi vya kusikilizia kutofanya kazi, na mabadiliko ya hali ya hewa. date rape: jimaishurutishi: pale mwanamke anaposhurutishwa kujamiiana na mchumba wake au mwanamume aliyefanya miadi naye. day blindness: upofu mchana: hali ya kutoona vema wakati wa mwanga mkali, pengine kutokana na upungufu wa koni za retina. day care: malezikutwa: hali ya mtoto kuwa chini ya uangalizi wa mtu mwingine ambaye si mzazi wake mchana kutwa kwa makubaliano kati ya mzazi au mamlaka na mlezi. deaf culture and sign language: utamaduni wa viziwi na lugha Iishara: muunganiko wa imani za kijumuia, mienendo, sanaa, desturi za kiuandishi, historia, maadili, na taasisi za pamoja ndani ya jamii zinazoathiriwa na uziwi na ambazo hutumia lugha ishara kama njia kuu ya kimawasiliano. Pale dhana hii inapotumika kwa minajili ya 56 utambulisho hususani kwa mtazamo wa kiutamaduni, agh. neno uziwi huandikwa kwa kutanguliwa na herufi U kubwa na kurejelewa kama Uziwi mkuu kwenye matamshi na ishara. Kwa upande mwingine, dhana hii inapotumika kutambulisha hali ya usikivu, huandikwa kwa herufi u ndogo. Wanajumuia ya viziwi hutokea kuuona uziwi kama tofauti za kiuzoefu miongoni mwa wanadamu kuliko kuwa na ulemavu au maradhi. Wengi wa wanajumuia hii hujivunia utambulisho wao wa Uziwi. Watu wenye uziwi kwa maana ya jumuia au utamaduni wanaweza kuonekana kuwa kundi la waliowachache na kwa maana hiyo miongoni mwa wanajumuia hii ndogo wanaweza kuhisi kutoeleweka na watu wengine wasiojua lugha ishara. Aina nyingine ya mapambano inayoikabili jumuia ya Viziwi ni ile ya taasisi za kielimu ambazo kwa kawaida huendeshwa na watu wenye usikivu wa kutosha. Hali kadhalika, wanafamilia wenye kusikia wanaweza kutakiwa kuijua lugha ishara ili kumfanya mwanafamilia kiziwi kuhisi kujumuishwa na kuungwa mkono. Tofauti na tamaduni zingine, kiziwi anaweza kujiunga na jumuia hii baadaye maishani badala ya kuzaliwa ndani yake kutokana na kukua na kukomaa kwa lugha

75 ishara; akili na mwili kwa maana ya mafunzo au uzoefu wa kutenda kazi au kutumia lugha ishara. deaf: uziwi: 1. msemo unaotumika kupambanua mtu aliyepoteza usikivu kwa zaidi ya desibeli 75 mpaka 80 ambapo uoni hutumika kama msaada wake mkuu na hawawezi kuelewa matamshi kupitia masikio hata kwa kutumia shimesikio. Hisia ya kusikia kwa kiziwi hazifanyi kazi kwa makusudio ya kawaida maishani. 2.-siokuwa na hisia ya usikivu; kiziwi: mtu ambaye hasikii. lv deaf-blindness: uziwipofu (pia hujulikana kama kupoteza hisia mara dufu): muunganiko wa vilema wa upofu na uziwi. Mtu mwenye vyote upofu na uziwi hawezi kunufaishwa na huduma ambazo zinalenga ulemavu wa upofu pekee au vilema vya uziwi tu; hivyo huduma maalumu lazima ziandaliwe kusaidia mtu mwenye uziwipofu. Hata hivyo, kwa baadhi ya wahusika wa ulemavu huu hupendelea maneno kutoona, uoni badala ya upofu au bubukipofu istilahi inayochukuliwa kubeba maana shirifu hasi. deaf-mute or deaf and dumb: uziwibubu:** 1. hali ya kutoweza kusikia wala kutamka. 2. mtu asiyeweza kusikia wala kutamka (kuwa bubu na kiziwi kwa wakati mmoja). Hata hivyo, wahusika wa ulemavu huu huchukulia 57 utambulisho huu kuwa wa muktadha wa kitabibu zaidi na wao hupendelea hali hiyo kutambuliwa kama uziwi, basi. deafness: uziwi: hali ya kukosa uwezo wa kusikia kutokana na kasoro kwenye mfumo wa kuchakata taarifa za mawimbi ya sauti. Kasoro zinaweza kutokea kwenye masikio au katika sehemu husika za ubongo. decibel (db): desibeli (db): kizio cha kupimia kiwango cha sauti, lakini pia hutumika sana kwenye masuala ya elektroni, ishara na mawasiliano. Hii ni aina ya kilogarithmu (kilogi) ya kuelezea uwiano. Uwiano unaweza kuwa wa kani, sauti, mgandamizo, volteji au mkazo au vitu vinginevyo zaidi. Hata hivyo, kwa minajili ya Kamusi hii, desibeli linatumika kumaanisha kiwango cha sauti. decongestant: kiondosha mzongopua: dawa inayotumika kukausha wingi wa kamasi unaosababishwa na maambukizo ya upumuaji. defense mechanism: mbinu kinga: hali ya asili ya mwili kujikinga dhidi ya mashambulizi ya kile kisichotakiwa kama vile bakteria, virusi au sumu visababishavyo maradhi au kifo. Pia mtu anaweza kujifunza mbinu za kujikinga dhidi ya mashambulizi ya kimwili au kisaikolojia yenye kudhuru mwili au afya ya akili. Kwa watu wenye ulemavu walio wengi, hukosa fursa ya kupata stadi za kujikinga na hivyo kubakia kuwa

76 waathirika wa mashambulizi au kujikinga kwa namna isiyofaa k.v. kutumia lugha mbaya za matusi au kuwa na ukali bila sababu. defensive behaviour: tabiakinga: mwenendo ambao unadhamiria kumlinda au kumtetea mtu au kuepuka mawazo na matokeo yasiyopendeza. defficiency disease: ugonjwatindikivu: maradhi ya upungufu unaotokana na ukosekanaji wa vitu muhimu vilivyo vya lazima mwilini k.v. ukosefu wa madini, vitamin, n.k. deformity: uatilifu kiungo: kilema au kasoro ambapo sehemu ya mwili huumbika tofauti au hushindwa kufanya kazi inayokusudiwa au hukosekana kabisa. Hata hivyo, matumizi ya istilahi hii husisitiza zaidi umbile lenye kuonekana tofauti kwa wengine au uwezo bila kujali ukweli kuwa mtu wa namna hiyo hujaliwa vipawa vingine vya kufidia kiungo chenye kasoro au kinachokosekana. deformation: uumbuaji: hali ya kusababishiwa kilema au uatilifu wa kiungo, kisaikolojia, kiakili n.k. 58 degrading treatment: kushushiwa hadhi: kumfanya mtu kujisikia kudhalilishwa, kuhisi kuaibika, kushushwa thamani, kutoheshimu maoni ya wengine. delayed language: uchelewevu wa kujua lugha: mvurugiko wa ujifunzaji lugha ambapo huwepo dalili za wazi za uzito katika kukuza msamiati na sarufi muhimu katika kuelezea na kuelewa mawazo na dhana. delayed speech: uchelewevu wa kutamka au kuongea: kushindwa kukuza uwezo wa kutamka katika umri uliotarajiwa. Kwa msisitizo zaidi, huu ni upungufu wa kuongea kwa ufasaha ambapo mtu huongea kama vile wa umri wa chini zaidi (angalia afasia). delinquency: ukosaji: kosa dogo, utukutu, uvunjaji wa sheria hususani kwa watoto wadogo au/na vijana chini ya miaka 18, uhalifu, utoro. delinquent: mtoro: 1. mtoto au kijana (kwa kawaida chini ya umri wa miaka 18) anayetiwa hatiani na mahakama kwa kuvunja sheria; 2. -enye kuonyesha dalili za kutenda kosa. 3. -enye kushindwa kutimiza wajibu. 4. mtoto mhalifu au mwenye hatia. delirium: kuchanganyikiwa: mvurugiko mkali wa akili unaokua taratibu ukibainishwa na kuchanganyikiwa na uwezekano wa kubadilika dhamiri. Hali hii hutokana na mabadiliko ya metaboli kwenye

77 ubongo yanayoweza kuhusisha kuwa au kutokuwa na njozi hata halusinesheni. Hali hii inatibika isipokuwa pale inapofuatiwa na dimenshia. Kwa kawaida mabadiliko ya kihisia hujidhihirisha kwa kuwa na wasiwasi na kufadhaika, hali ya kutotulia, kutojua mazingira na pengine kuwa na delusheni na halusinesheni za muda. delusion: delusheni: imani aliyo nayo mtu iliyojengeka kwenye misingi hitimisho mantiki makini isiyo sahihi juu ya ukweli ulio nje na kuung ang ania bila ya kujali yanayoaminiwa na watu wengine na bila kujali kutopingika kwa uthibitisho wa wazi dhidi ya anachoking ang ania. Imani inakuwa siyo ile inayokubalika kikawaida na watu wengine wenye utamaduni sawa na wake (mathalani, siyo jambo la imani ya kidini). Mila zimegawanyika kulingana na maudhui yake kama vile: delusheni ya kutawaliwa, visa visivyo vya kawaida, kujifaharisha, wivu, kukana kanuni za uadilifu au dini, kutesa, ufukara, marejeo, maungo na zile zilizopangiliwa. dement: afkani:** mtu aliye pungukiwa akili (punguani**); mtu asiye na akilli za kutosha**, butu**, mawenge**, mwathirika wa maradhi ya demenshia. Maneno haya yanayotumika kumwelezea mtu mwenye kuathiriwa na hali hii, 59 ni yenye muktadha wa kitabibu bila kujali hisia za mhusika. dementia: demenshia: 1. kuvurugika kwa utaratibu wa akili ambapo uwezo wa awali wa kiakili na kujimudu huchakaa vibaya. Usumbufu wa kumbukumbu ndiyo dalili yake kuu. Zaidi ya hapo, kuna ulemavu wa kuwaza kitaswira, kufanya uamuzi, kudhibiti shauku na mihemko au/na mabadiliko ya haiba. Demenshia inaweza kuendelea zaidi, kusimama, kurekebishika, kutegemeana na upatikanaji wa matabibu na tiba mujarabu. 2. ugonjwa wa akili ambapo mgonjwa, kwa kiasi kikubwa hupoteza uwezo wa kiubongo. lvi 3. mdororo wa kumbukumbu. deoxyribonucleic acid (DNA): Kinasaba Asidi (KA): asidi katika kiiniseli ambazo ziko katika kromosomu na ambazo huhifadhi ujumbe mbalimbali wa vinasaba. depression: mfadhaiko: 1. mvurugiko wa taratibu wa hali ya kiakili ambapo mtu huhuzunika na kujihisi kuwa hawezi kufurahia chochote kwa vile hali ni ngumu na haipendezi. Mvuruguko huu unaweza kabisa kuzama kwa kina na kung ang ania kiasi cha kufananishwa na ziwa linalolishwa na mito mingi ikiwa ni pamoja na maisha ya mateso na sononi, visa kama vile kufiwa na wapendwa, masuala ya kisaikolojia kama vile

78 kukosa matumaini ya baadaye au hali ya kuishi pweke. 2. ugonjwa wa akili wa mvurugiko wa hemko, mwathirika wa dipresheni huwa ni mwenye huzuni, utendaji kazi hushuka, na hujihisi kana kwamba hatakiwi au hapendwi. lvii derangement: kuvurugikiwa: maradhi hususani ya akili. dermatoplasty: upandikizaji ngozi: uchukuaji wa ngozi kutoka sehemu moja ya mwili na kuibandika sehemu isiyo na ngozi kutokana na ajali k.v. kuunguzwa na moto. derogation: bezo: ujengaji wa fikira mbaya kwa namna ya kuvunja au kushusha heshima au hadhi ya mtu. Hii ni hali ya kawaida kumtokea mtu mwenye ulemavu pale jumuia inapompachika majina yenye kudhihaki hali yake kimaumbile badala ya utu wake na uanuwai. derogatory: -a dharau: -enye kuaibisha, kushushia heshima au hadhi. descriptive video: video maelezosauti: huduma inayoleta utofauti kwa wale wasioona kwa kutumia vyombo vya mawasiliano fikivu kwa wote; yaani maelezo ya sauti ya elementi za vipengele muhimu vya programu. Simulizi hutokea wakati wa mapumziko ya asili katika mazungumzo ambapo mtu asiyeona au mwenye uono hafifu, huona kwa sauti na kujumuika na hadithi. Kwa maana hiyo. maonesho ya televisheni, filamu za 60 makala, vyombo jongevu vya mawasiliano, vielelezo (vya mawasiliano) kwenye wavuti au kwenye makumbusho vyote vinaweza kuelezewa. desesintisation: uzimaji mzio: usitishaji wa mzio dhidi ya dutu iliyousababisha mzio huo. design: usanifu unde: fani muhimu sana katika maisha ya mtu mwenye ulemavu kwa vile ndio msingi wa ama kumzuia au kumwezesha kuchangamana na wanajumuia au watu wengine au/na kutumia bidhaa na huduma mbalimbali. Mathalani, ufikivu wa majengo na mazingirajenzi mengine hutokana na jinsi wasanifu walivyoweza ama kuzingatia au kutozingatia mahitaji anuwai ya watumiaji; huduma za marekebisho pia hutegemea vipawa vya wasanifu ili kupata majawabu mahususi kwa hali mbalimbali. destitution: ufukara: hali ya mtu kuwa fakiri au hohehahe kwa kukosa mahitaji ya msingi maishani, yaani kipato, makazi, mavazi na chakula. Mtu mwenye ulemavu hufukarishwa kwa ama kukosa fursa za kujistawisha au huduma bora za hifadhi ya jamii. detectable warning: kionyi bainifu: kifaa chenye viwango kilichojengewa ndani kwa ndani (ardhini) au kinachopachikwa kwenye maeneo

79 ya kupitia au elementi nyinginezo kwa ajili ya kuonya mtu mwenye uoni hafifu au asiyeona kabisa juu ya hatari zilizo njiani. devaluation: ushushaji thamani: namna ambayo mtu kwa kiasi kikubwa hudhani kuwa yeye mwenyewe au mtu mwingine hana sifa nzuri. development: mabadiliko: 1. hali ya kukua, kupevuka kimwili na kiakili. 2. ustawishaji. developmental aphasia: afasia ya ukuaji: 1. mvurugiko wa lugha kwa mtoto unaosababishwa na kuharibika kwa ubongo, unaobainishwa na kilema cha kutoelewa kabisa au kwa sehemu mpangilio na matumizi ya lugha. 2. kupoteza uwezo wote au sehemu ya uwezo wa kutamka maneno kwa ufasaha au/na kuelewa maneno yanayosemwa. developmental assessment: upimaji ukuaji: kipimo cha kiwango kinacholenga kuweka kumbukumbu za matukio ya kimwenendo, kistadi au kiuwezo yanayojitokeza mfululizo kwa kipindi fulani. developmental co-ordination disorder (DCD): mvurugiko wa upatano wa 61 utaratibu wa ukuaji: kuchelewa kupata ukuaji wa stadi kamili za mjomgeo (yaani uwezo mkubwa wa misogeo ya mikono na miguu na mwili,) au msogeo wa viungo vodogovidogo (mf. vidole). developmental delay: kuchelewa kukua: hali ya ukuaji wa mtoto kuendelea kwa kasi ya kusuasua kuliko hali ilivyo kwa watoto walio wengi wa umri husika. developmental disability/disorder (DD): mvurugiko wa ukuaji: aina ya ulemavu wenye hali nyingi tofautitofauti zinazoweza kudhihirika utotoni au kabla ya umri wa miaka 22 na husababisha ukomo wa ama kimaumbile au kiakili. Hali hizi hujumuisha usonji, mpoozo wa ubongo, kifafa, vilema vya akili na matatizo mengine ya kinyurorojia. Mtu mwenye kilema cha ukuaji anaweza asijifunze haraka au kujieleza kiufasaha sawa na wenzake. Mwingine anaweza kuwa na ukomo wa uwezo wa kujihudumia mahitaji binafsi au ukomo wa ujongeaji. Pengine mhusika anaweza kukabiliwa na zaidi ya kilema kimoja. Ulemavu wa ukuaji husababishwa na vitu mbalimbali vinavyoweza kutokea kabla au baada ya kuzaliwa. Ule unaotokea kabla ya kuzaliwa ni pamoja na matatizo ya vinasaba, matunzo mabaya kabla ya kuzaliwa au wakati wa ujauzito au kijusi kukaribiana na vitu vyenye sumu,

80 mihadarati au vileo. Matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa kuzaliwa ni kama vile mtoto kukoseshwa hewa ya oksijeni au ajali baada ya kuzaliwa kama zile za kudondoka, ajali za barabarani zinazosababisha ubongo kujeruhika kadhalika na vilema vya aina hii. Ni vigumu kufafanua ukomo wa uwezo wa mtu mwenye ulemavu wa aina hii kwa vile mabingwa kwenye uga huu wanaendelea kugundua uwezo wa kipekee ndani ya kundi hili. Wakati mtu mwenye ulemavu wa ukuaji akikabiliwa na changamoto kubwa zaidi baadaye maishani, bado anaweza kuendesha maisha yenye fanaka. Anachohitaji zaidi ni kuhimizwa, kueleweka na utashi kwa wengine katika kumsaidia kupata kimajuu cha fursa za kuwa sehemu ya jamii. Ulemavu wa ukuaji na ule wa umaizi husababisha viwango vikubwa vya ukomo kwa namna nyingi za kiutendaji na pia huwa na vitu vingi vyenye kushabihiana kwa aina hizi zote mbili: hutokea kabla ya umri wa miaka 22, huwa sugu na takribani kumwathiri mtu maisha yake yote, husababisha ukomo wa viwango vikubwa katika maeneo mengi ya kimaisha k.v. kujitunza binafsi, mawasiliano, ujongeaji, ujifunzaji, kujiongoza, kuishi kwa kujitegemea na kujitosheleza. Licha ya kushabihiana huku, aina hizi mbili za ulemavu hutofautiana 62 kwa namna zifuatazo: ulemavu kiumaizi hubainishwa na sifa kuu katika hali zote mbili, yaani: utendaji wa kiumaizi; na urekebifu kimwenendo. Daima ulemavu wa umaizi hujumuisha ukomo bainifu wa umaizi au uwezo kiakili, wakati kwa upande wa ulemavu wa ukuaji, unaweza kuhusisha ama ukomo wa kiakili au kimaumbile au vyote viwili. Ukomo wa kiakili na kimaumbile unaweza usiathiri umaizi au uwezo wa kiakili, ila kusababisha kiwango kikubwa cha ukomo katika maeneo mengi ya kimaisha. Mfano, ulemavu wa ukuaji unaohusisha ukomo wa kiakili bila kuathiri uendaji wa umaizi ni usonji. Yaani, siyo kila mwenye usonji huwa na ulemavu wa umaizi, ila katika hali zote mbili, ukomo kwenye maeneo mbalimbali ya kimaisha hujidhihirisha. Ulemavu wa ukuaji wenye kuhusisha kiwango kikubwa cha kimaumbile, ni mpoozo wa ubongo. Wakati baadhi ya watu weye kasoro hii pia huwa na ulemavu wa umaizi, wengi huwa hawana hitilafu hiyo japo kasoro yao inaweza kusababisha kiwango kikubwa cha ukomo katika maeneo mengi kimaisha. developmental history: kumbukumbu ya ukuaji: rekodi za maendeleo ya ukuaji wa mtoto (tangu kuzaliwa mpaka miaka 18) zinazohusu stadi kama zile za: kukaa, kujongea, au kuongea.

81 developmental labelling approach: mtazamo wa upachikaji majina kiukuaji: mtazamo wa kupachika majina uliojikita kwenye ukengeufu wakati wa makuzi kwa kulinganishwa na kile kinachofikiriwa kuwa ukawaida. developmental milestones: dalili kiukuaji: vitu anavyovifanya mtoto mchanga wakati anapokua kama vile kukaa, kutambaa, kudemadema, kutembea, kutamka neno la kwanza, n.k. Awamu hizi za ukuaji lazima zitokee ili awamu zinazofuatia zijengeke barabara. developmental period: kipindi cha ukuaji: muda kati ya utungwaji mimba na miaka 18 ya umri ambao ukuaji wa kimwili na kiakili hutokea. Ni kipindi ambacho kwa kawaida ulemavu wa ukuaji hujitokeza. developmental sequences: mfuatano wa ukuaji: hatua inayopaswa kuwepo ili inayofuatia nayo itokee. developmental test: kipimo cha ukuaji: kigezo kinachokubalika katika ufuatiliaji wa ukuaji wa mtoto kwa kulinganishwa na ukuaji wa watoto wote wa rika lake. developmental: -a ukuaji: -enye kuhusiana na hatua au awamu za ukuaji na uendeleaji kabla ya umri wa miaka 18. deviant: kengeushi: dhana inayotumika kuelezea mwenendo hasi wa mtu anayeshindwa kuzingatia kanuni, mila na desturi za kijumuia ikiwa ni pamoja na mwenendo wa jumuia au 63 kuwa na uhusiano mzuri kati ya mtu na mtu. diabetes: diabitisi: hali ya kukojoa kwa wingi, lviii diabitese mellitus: ugonjwa wa kisukari: ugonjwa wa kukojoa kwa wingi, kuwa na kiu mara kwa mara, kukosa nguvu mwilini n.k. unaotokana na kuzidi kwa sukari mwilini. diabitis inspidus: diabitisi insipidasi: ugonjwa sugu wa kukojoa kwa wingi na kunywa maji sana utokanao na lesheni katika glandi pituitari. diagnosis: uchunguzi: hatua zinazotumiwa na watalaamu wa fani mbalimbali hususani ile ya tiba katika kubaini tatizo la mteja ili kuamua hatua za kulitatua. dialysis: dialisisi: 1. mchakato ambamo mashine hutumika kusafisha uchafu kutoka kwenye damu. Dialisisi ni muhimu pale figo zinapokuwa hazifanyi kazi ipasavyo. 2. upenyaji wa dutu iliyo katika mmumunyiko kupitia membreini nusu penyevu. lix dicephalus or conjoined twins: vichwapacha: hali ambapo viumbe huzaliwa wakiwa na vichwa viwili vilivyounganika ila mwili ni mmoja. Hawa ni pacha wanaofanana kwa kila kitu ambao huunganika wakati wa kutungwa mimba. Visa hivi hutokea kwa nadra na vikijitokeza katika nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, Afrika na Brazil. Takribani nusu ya pacha hawa huzaliwa wakiwa wafu (hususani wale wa jinsi ya

82 kiume) na theluthi yao hufa katika kipindi cha saa 24 baada ya kuzaliwa. Wengi wanaomudu kuishi ni wa jinsi ya kike. differentiate: pambanua: nadharia ambayo hasa hufundishwa katika taaluma ya elimu, ambayo ndiyo inayobeba dhana iliyoibuliwa hivi karibuni ya ujumuishaji katika elimu. Kutokana na uelewa kuwa kila mwanafunzi ni tofauti, waelimishaji hutakiwa kumtofautisha, au kumtendea tofauti mhusika ili hatimaye kila mmoja anufaike na uwepo wake darasani. differentiation: upambanuaji: 1. ubainishaji wa tofauti ya hali, ubora au ukweli baina ya mtu na mwenzake. 2. hali ya ukweli unaotofoutisha kitu kimoja na kingine. 3. mabadiliko maalumu ya kimaumbile au ya kiutendaji katika ukuaji wa mwili. differently abled: uwezo tofauti:** maneno ya kusafidi, au tasfida ili kuepusha kuibua hisia mbaya katika kuelezea dhana ambazo maneno yanayoziwakilisha humkera mtu yanaposemwa. Hata hivyo, wanaharakati wa masuala ya ulemavu hawapendelei kusafidiwa badala yake hujibatiza wenyewe, mathalani, mtu mwenye ulemavu. digestive condition: hali ya umeng enyaji wa chakula: -enye kuruhusu uvunjaji wa chakula kwa kutumia kemikali maalumu ndani ya tumbo. 64 digital divide: mgawanyiko kidijiti: dhana inayolenga mapengo yaliyopo katika upataji wa habari na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kati ya watu, makundi, nchi na maeneo. Mgawanyiko hu huwaathiri watu wenye ulemavu zaidi kuliko wenzao wasiokuwa na hali hii kwa kukabiliwa na matatizo ya asili ya ufikivu na upatikanivu; yaani kukosekana kwa mafunzo ya TEHAMA hadi mazingirajenzi, ukosefu wa teknolojia saidizi ya kompyuta na kutofikika kwa miundo ya vyombo mbalimbali vya habari. dilated student: mwanafunzi goigoi**: dhana katika uga wa elimu inayochukulia kuwa mwanafunzi aliyefundishwa kwa viwango na mazingira sawa na wenzake, anapashwa kuwa na uwezo usiopishana sana na wengine katika masomo yote. Matarajio haya yasipotimilika, mwalimu humbebesha lawama zote mwanafunzi asiyefaulu vizuri masomo yake na hata kutumia adhabu kali (viboko, kejeli, kutengwa) kama mbinu mbadala za kumweka kwenye viwango. Hali hii husababishwa na uelewa mdogo wa ulemavu wa aina ya kitatiza ukokotozi, disgrafia, disleksia na mwingineo unaokuwa kiunzi dhidi ya ujifunzaji. Pia mazingira ya nyumbani na kwenye jumuia hayapaswi kupuuzwa wakati wa tathimini ya

83 maendeleo ya mwanafunzi kimasomo. diplegia: diplejia: kupooza kwa sehemu sawia za mwili; mathalani, mikono yote miwili kwa pamoja au miguu yote miwili kwa pamoja. lx diptheria: dondakoo: 1. ugonjwa wa ghafla na wa muda mfupi uletwao na bakteria wenye dalili za homa kali. 2. utengenezwaji wa membreni bandia kooni na kuumwa sana. direct services: huduma za moja kwa moja: utoaji huduma katika utaratibu unaozingatia mahitaji binafsi yenye kuhitaji mikakati ya afua za kitaalamu ambazo zinaweza kufanywa na wataalamu wabobezi (k.v. tabibu mwamilishaji). Kwa ujumla huhitaji mawasiliano ya kila mara kati ya mtoto na tabibu. directory information: jalada taarifu: taarifa zilizomo kwenye kumbukumbu za elimu ya mwanafunzi ambazo kiujumla haziwezi kuchukuliwa kuwa na madhara au uvamizi wa faragha endapo zitawekwa wazi. Taarifa hizi ni kama jina la mwanafunzi, orodha ya simu, tarehe na mahali pa kuzaliwa, aina ya masomo anayobobea, ushiriki kwenye shughuli na michezo zinazotambulika rasmi, uzito na vimo vya wanamichezo, tarehe za mahudhurio, shahada na tuzo alizopata, na taasisi/wakala ya kielimu aliyopata kuhudhuria. 65 disability: ulemavu: 1. dhana inayobadilika na hali hii hutokea kutokana na mchangamano baina ya mtu mwenye kilema na mitizamo na vikwazo vya kimazingira, ambavyo huzuia ushiriki wake kamili na unaofaa ndani ya jamii na katika hali iliyo sawa na wengine. 2. udhaifu, upungufu, ulemavu, kilema cha kudumu; kutoweza. 3. sheria inayobatilisha nyingine iliyokuwa ikitumika kabla 4. kilema cha kudumu, upungufu**, udhaifu fulani** 5. kilema** (ang. watu wenye ulemavu). Ni jambo la msingi kuelewa kuwa mtu mwenye ulemavu hubainishwa kwa: sifa zake binafsi, haiba yake chaguo lake wala siyo aina ya kilema alichonacho, muda aliodumu na hali hiyo, kiwango cha hali yenyewe athari ya hali ya kiafya Hata hivyo, ni vema kukielewa fika kilema cha mtu ili kuweza kutoa mwega stahili kwa mhusika; na, ni muhimu zaidi kumjua kila mhusika binafsi anachokihitaji maishani na kumpa fursa ya kujichagulia aina ya mwega. Tafsiri namba 2-4 hazikubaliki miongoni mwa wanamageuzi wenye ulemavu kwani huzichukulia kuwa na muktadha wa kitabibu ambao hujikita kwenye upambanuaji wa kimaumbile kati ya

84 yaliyo na kasoro na yale ya kawaida bila kujali hisia za wahusika. Wakati 66 mwingine, tafsiri za kitabibu na kihisani hupindukia mipaka na kuwakejeli walengwa. disabled: -enye kulemazwa: dhana hii ndiyo hutumiwa na Waingereza. Mantiki yake ni kwamba mbali na kasoro au upungufu alio nao mhusika kimaumbile, yapo mambo mengi yaliyo nje ya uwezo wake yanayobinya fursa zake za kutumia kiukamilifu viungo na vipaji alivyosalia navyo katika kujistawisha na kuchangamana na jamii. Kimantiki, dhana hii haisigani na ile ya Kimarekani iliyochukuliwa kimataifa ya mtu mwenye ulemavu. Tafsiri zinazopatika katika baadhi ya Kamusi za Kiswahili (ang ulemavu 2). istilahi hii kumaanisha: ni yule kilema**; nyima**; ondolea uwezo**, hukinzana na dhana ya kimageuzi katika uga wa ulemavu. disability culture: utamaduni wa ulemavu: dhana yenye kutumika kwa mapana iliyoasisiwa mwishoni mwa miaka ya 1980 ili kupambanua tofauti ya mifumo kimaisha inayosababishwa au/na kuenezwa na ulemavu. Uwepo wa utamaduni huu huendana na jinsi jamii zinavyochukulia dhana nzima ya ulemavu. Tamaduni hizi za ulemavu, hujumuisha mitandao ya kisanii ikiwa ni pamoja na (na bila kuishia kwa) ushairi, vilabu vya muziki, uchongaji

85 wa aina mbalimbali, uigizaji, ubunifu wa misemo mipya na ishara mpya, utambulisho wezeshi wenye kuwakilishwa na maongezi au dhana zinazoakisi ubembelezi, umahabubu, ukubalifu wa uanuwai, utegemeanaji, kukubali uwepo wa makundi ambayo yanaweza kudhurika kiurahisi, moyo wa kupambana dhidi ya dhuluma, imani, maadili na maono ya pamoja ambavyo huzaa mikakati ya pamoja yenye kulenga kuishi na kustawi kwa pamoja. disability etiquettes: akhlaki za ulemavu: maadili, adabu kuhusu ulemavu. Istlahi hii hupendekeza namna nzuri ya jinsi ya kuchangamana kati ya jamii na mtu mwenye ulemavu kwa kusisitiza matumizi ya istilahi zinazofaa pale anapohusika (mtu mwenye ulemavu) kama njia ya kulinda heshima yake na kujenga tangamano lenye kufaidisha wote. disability prevention: kinga dhidi ya ulemavu: sehemu muhimu ya kinga dhidi ya ulemavu kwa muktadha wa kijamii na kimatibabu. Mtazamo huu wa kinga dhidi ya ulemavu unatokana na jinsi ulemavu ulivyofafanuliwa na MHWU. Kipengele cha kijamii huangalia kinga kwa jicho la ufahamu kuhusu kigezo cha haki za binadamu kinachotetea utamaduni wa kutobagua, unaojumuisha kila mtu. Uzuiaji wa aina ya kimatibabu hujikita kwenye kinga dhidi ya 67 kilema. Hii ni ngazi ya msingi ambayo kushughulisha suala hili kwa njia kama vile chanjo, n.k. (taz. prevention ). kueneza ufahamu, kuboresha disability proofing: uhakiki ulemavu: hatua ya msingi katika ujumuishaji inayolenga kuhakikisha kwamba mtu mwenye ulemavu anashiriki (na mahitaji yake kuzingatiwa) katika kupanga na kuendeleza miundombinu yote, sera na utekelezaji. Mikakati muhimu ni pamoja na: kukuza ufahamu juu ya harakati na matokeo; kukagua taarifa muhimu kwa kushauriana na mtu mwenye ulemavu; kuendesha shughuli za kupima matokeo. disability access symbol: kiashirio cha ufikivu (wa mtu mwenye ulemavu): alama zinazokusudia kusaidia kutangaza huduma za ufikivu kwa wateja, hadhira, watumishi na walengwa wengine katika jamii. Matangazo, majarida, mikutano na brosha za programu, fomu za uanachama, alama kwenye majengo, mipangilio ya ghorofa na ramani ni mifano ya vitu vinavyoweza kuonyesha alama hizi. Mtu mwenye ulemavu na waandaji wengine wa shughuli za umma wanahimizwa kuweka alama hizi kando ya kila taarifa kwenye machapisho na vyombo vya habari. Lugha yoyote inayoambatana na alama hizi ilenge kwenye ujumuishaji au huduma na siyo mtumiaji wa

86 alama husika. Mathalani mlango wenye ngazimbetuko unaweza kuambatana na alama ya kitimwendo. Hii ni muhimu kwa vile siyo mtu mtumia kitimwendo peke yake huhitaji ngazimbetuko, vilevile na msukuma kigari cha kubebea mtoto, mbeba mizigo, vifurushi na marobota, n.k. Lugha inayoendeleza heshima ni muhimu. Mathalani, maegesho maalumu yanaweza kutumiwa sambamba na alama ya kitimwendo kuashiria kuwa yapo kwa ajili ya mtu mwenye ulemavu. disadvantage: upungufu: hali inayomweka mtu kwenye mazingira yanayobinya fursa zake za kufaulu au kuwa na ufanisi. disadvantaged: mtule: mtu asiyekuwa na fursa wala anasa za maisha kama vile kumiliki mali, kuwa na kipato cha uhakika, 68 kupata fursa za elimu, ajira yenye uhakika, huduma za afya, n.k. ambavyo huchukuliwa kuwa muhimu maishani na hali linganifu ndani ya jamii. disaggregated data: data pambanuzi: takwimu zinazotumiwa kupambanulia taarifa za kundi la watu kwa madhumiuni ya utafiti, sensa au idadi ya watu na makazi, utoaji huduma, n.k. ambazo zinaweza kuwa za kitarakimu au taarifa zisizo za kitarakimu. Mathalani, waelimishaji, wanafunzi wenye ulemavu, na wazazi katika shule ya umma, wanaweza kuchunguzwa kuhusu mada fulani. Taarifa kutokana na uchunguzi huo zinaweza kujumlishwa pamoja kwa kuonyesha mtiririko wa fikira na hisia za makundi haya matatu-yaani, waelimishaji, wanafunzi (wenye ulemavu) na wazazi. Taarifa hii itajielekeza kwenye tarakimu na mambo yasiyokuwa ya kitarakimu yaliyokusanywa (i) kutoka vyanzo mbalimbali au/na juu ya hatua viashria au watu mbalimbali, (ii) kujumuishwa katika takwimu pambanuzi kwa kutoa muhtasari wa takwimu kwa malengo mahususi ya kutaarifu umma au kufanyia uchambuzi na (iii) kuvunjwavunjwa kwenye vipengele mbalimbali vya kitakwimu. Mathalani, taarifa kuhusu mwelekeo wa uandikishaji mwanafunzi mwenye ulemavu aliye na umri stahili wa kuwa shuleni, kwa

87 kuifupisha katika kiwango kimoja cha uandikishaji shuleni na kwenye jumuia katika kipindi maalumu. Viwango vya uandikishaji vinaweza kuchambuliwa zaidi ili mathalani, kuonyesha asilimia ya wanafunzi wa kike na kiume (wenye ulemavu) au wanafunzi wenye ulemavu na wenzao wasiokuwa na ulemavu. Kwa ujumla, takwimu huchambuliwa kwa makusudio maalumu ya kubainisha chimbuko la mwelekeo, mpangilio, utambuzi wa yale ambayo yasingebainika kwenye makundi ya takwimu mjumuiko, mathalani, tofauti za mpangilio wa uandikishwaji shuleni kwa makundi mbalimbali ya wanafunzi. Uchambuaji wa takwimu kwa mtindo huu unatakiwa pia wakati wa kuandaa taarifa zinazohusu kundi la watu wenye ulemavu lenyewe peke yake ili kila aina ya ulemavu ichambuliwe na hali zake kuwekwa bayana kwa ajili ya mlinganisho na hatua za msawazisho. disarticulation: katatindi: uachanishaji viungo kwa kuvitenganishia kwenye maungio au kifundo. disclosure: kuweka wazi: kuruhusu ufikiwaji wa au usambazaji, uhawilishaji au mawasiliano mengineyo kwa njia yoyote ikiwa ni ya kimazungumzo, kimaandishi au kieletroni au kumbukumbu za taarifa zinazobainisha haiba ya mhusika kwa mtu yeyote au upande 69 mwingine. Suala hili ni muhimu kwa mtu mwenye ulemavu hasa kuhusiana na kipengele cha faragha na adala ya mtu. discretionary: uamuzinafsia: mchakato unaofanywa kwa hiari ya mtu, na uamuzi au chaguo la mtu. discrimination on the basis of disability: ubaguzi kwa misingi ya ulemavu: kutofautishwa kokote, kutengwa au kuzuiwa kwa sababu ya ulemavu ambako kuna nia au athari ya kudhoofisha au kubatilisha utambulisho, ufaidikaji au utekelezwaji wa haki zote za kibinadamu na uhuru wa asili kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kiraia au eneo lolote lile kwa misingi ya usawa na watu wengine. Ubaguzi ni pamoja na aina zote za ubaguzi, ikijumuisha kunyimwa marekebisho muhimu anayostahili mtu mwenye ulemavu. discrimination: ubaguzi: upambanuaji usio wa haki kati ya makundi ya watu kwa dhana ya wao dhidi ya sisi. Aidha, msemo ubaguzi hutoa maana hasi zaidi pale unapotumika kuelezea jinsi binadamu wanavyotendeana. Kusema kwamba mtu fulani amebaguliwa, kimsingi humaanisha kuwa siyo tu kwamba katendewa tofauti bali pia ametendewa visivyo. Kutendewa visivyo, kunaweza kuwa dhahiri kabisa k.v. sheria kumbagua mtu mwenye ulemavu (ubaguzi wa

88 moja kwa moja) au kunaweza kutendeka kwa njia isiyokuwa ya dhahiri kama inavyotokea pale sheria inapokuwa haipendelei upande wowote lakini utekelezaji wake ukiathiri vibaya baadhi ya makundi (ubaguzi usiokuwa dhahiri). Ubaguzi wa aina ya pili unaweza kudhuru kisirisiri kwa watu kudhaniwa kuwa kukosekana kwa ubaguzi wa waziwazi kunazifanya kanuni au sheria kuwa za haki hata kama ni kandamizi. Hata hivyo, siyo kila wakati watu wanapotendewa tofauti kunaashiria tendo hasi. Ndiyo maana, katika hali nyingine, nchi zinatakiwa kufanya ubaguzi kwa misingi kwamba kanuni za kutobagua hukamilishana. Mathalani, ubaguzi wa muda mrefu na wa kihistoria dhidi ya kundi fulani umelizuia kutonufaika kwa viwango sawa na makundi au watu wengine. Ili kuubadili mwendelezo huu, nchi inatakiwa kuchukua hatua ambazo katika maneno na aina nyingine za muktadha hujulikana kama sera ikibari au ubaguzi chanya. disintegrative disability: ulemavu msambaratiko: ulemavu wa aina hii hutambulishwa kwa tabia mahususi ya usawajikaji na kurudi nyuma katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji kama vile ya kimatamshi na yasiyo ya kimatamshi (kwa kujieleza na kwa kusikia), uhusiano wa kijamii, michezo, na tabia za 70 kuiga. Kuharibika zaidi katika mitangamano na wenzake, (mtu mwenye ulemavu wa aina hii), huchelewa au hukosa hisia za kutendeana kijamii au uwezo wa kuendeleza au kuanzisha mazungumzo, kuwa na tabia za kujirudiarudia na kukariri, kuvutiwa na kitu na shughuli za kimwenendo. disorder: mvurugiko: 1. kuvurugika kwa utendaji wa kawaida wa mifumo ya kimaumbile kiakili, au kisaikolojia unaohusisha na kutokomaa na kutotosheleza mahitaji ya mwili. 2. mvurugiko wa kimwenendo ambao kwao mtu anaweza kuwa goigoi, kutofaa kijamii au kuvurugikiwa kwa kushindwa kujua. disorientation: mzubao: 1. kukosa mwelekeo na kuchanganyikiwa tarehe au muda wa siku, mahali mtu alipo au kutotambua sura. Kukosa mwelekeo ni dalili ya mvurugiko wa utaratibu wa akili kama vile deliramu na demenshia. 2. hali ya kupotelewa na uwezo wa kutambua mahali, wakati au mtu. dispersed advocacy: utetezi niaba. hali ambapo mwongozwa anahudumiwa na watu wawili au zaidi katika majukumu tofautitofauti. Mfano, panaweza kuwa pale mtu anapohudumiwa na watu wawili; yaani, -mwelekezi msemaji na mwelekezi kiongozi au mtu mzima anayefanya kazi sambamba na

89 mwelekezi mwanagenzi mwenza. Ni sawasawa na mtetezi mwenza. disphonia: disfonia: hali ya kushindwa kutoa sauti vizuri. displacement: uhamishaji: mbinu ambayo mtu hujumuisha na kupanga upya hisia kuhusu jambo au mwitiko kutoka kwenye kitu kimoja kwenda kitu kingine (kwa kawaida kile) kisichoudhi (muktadha wa kisaikolojia). dissociation: mtengano (wa fikira): hali ya kiakili ambamo mawazo na matamanio yanaachanishwa kutoka kwenye mkondo wa ufahamu au kutoka kwenye haiba ya mtu kiasi cha mawazo na matamanio kutofikiwa tena kwenye kumbukumbu au fahamu. Muathirika anakuwa na ugumu au hawezi kuona vitu au hali katika ukamilifu wake na badala yake huitikia sehemu tu ya vishawishi hivyo. distractibility: utenguaji mawazo: hali ya kila wakati kumakinikia vitu visivyokuwa na umuhimu au kuvutiwa na vishawishi nje ya jambo muhimu mtu analokabiliwa nalo. Mathalani, wakati wa kusailiwa, msailiwa kila mara kuvutiwa na kelele zinazotoka ofisi jirani, kitabu kilicho ndani ya shubaka au mlio wa kengele ya shule mtahiniwa alipo. distressed person: msononi: mtu aliyesononeshwa, au kuhuzunishwa kwa kipindi kirefu. 71 diversity: uanuwai: kutambua na kuthamini tofauti miongoni mwa watu, vitu na makundi kama dhana muhimu katika kujumuisha kila mmoja ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na mtu mwenye ulemavu. diversity of persons with disabilities: uanuwai wa watu wenye ulemavu: kutambua kuwa ulemavu ni wa aina mbalimbali. Halikadhalika, mahitaji yanayoambatana nao na uwezo wa kila mhusika hutofautiana. douche: pigabomba: kusafisha uke kwa kupiga bomba. Mbinu hii inaweza kuleta madhara kwa vile huosha na huondoa kioevu asilia chenye afya ndani ya uke. down syndrome or mongolism: mlimbikodalilidu mazi: aina ya kawaida sana ya uzito wa akili ambapo mtoto huwa mzito zaidi kuliko wenzake katika kujifunza kutumia mwili na akili zake kuwa tepetepe na dhaifu, kushindwa kulia kwa nguvu, uzito wa kujigeuza, kufumbata vitu, kukaa na kutembea. Hizi ni baadhi ya dalili za mapema za aina hii ya ulemavu au mvurugiko wa kuzaliwa nao (wa kikromosomia) ukidhihirishwa na wajihi bapa, ulemavu wa akili wa kiwango cha chini hadi cha juu na kimo kifupi. Ni hali anayokuwa nayo mtu maisha yake yote na hutokea

90 kutokana na baadhi ya seli za mtoto mchanga kuwa na kromosomu zaidi ya 21. Dalili nyingine ni pamoja na: macho kuelekea juu; wakati mwingine huwa na kengeza au kuwa na uoni hafifu, masikio huwa chini, mdomo mwembamba, hukaa umeachama, kaakaa huwa juu na jembamba, na ulimi huning inia, mikunjamano ya jicho hufunika kona za kope za macho, kope za macho huvimba na kuwa nyekundu, mboni ya jicho huwa na chembe ndogo nyeupe kama mchanga ambazo hupotea baada ya umri wa miezi 12, mikono mifupi na mipana ikiwa na vidole vifupi. Kidole kidogo kinaweza kuwa kimejikunja au chenye mkunjo mmoja; macho kumchukuzi:** ni istilahi inayotumiwa na baadhi ya watu kwa madhumuni ya kudhihaki na kumkejeli mhusika. Kwa maana hiyo, haifai kutumika katika mawasiliano ya aina yoyote. dramatise: igiza tamthilia: geuza hadithi kuwa ya kimaigizo, tia chumvi, fanyia usanii. lxi dromomania: dromomania: ugonjwa wa akili ambao husababisha msukumo usiodhibitika unaojenga utashi wa kutaka kusafiri wakati wote. Tafsiri nyingine za kuiita hali hii uendawazimu** ni kukosa adabu lugha na kutojali hisia za mtajwa. drop-foot or foot drop: wayokokotwa: ulemavu wa kunyooka kwa kanyagio. Ulemavu huu 72 husababisha ugumu wa kunyanyua sehemu ya mbele ya wayo kiasi cha kulazimika kuuvuta chini wakati wa kutembea. Wayokokotwa siyo ugonjwa bali ni matatizo fiche ya kinyurorojia, misuli na maumbile. Wakati mwingine ulemavu huu huwa hali ya muda na nyakati zingine huwa ni hali ya kudumu. Mtu mwenye hali hii huhitaji kuvaa bangiligango kwenye kifundo na wayo ili kuviweka kwenye mkao wake wa kawaida. dual enrolment: ujiandikishaji mara mbilimbili: udahili ambao mwanafunzi huhudhuria shule zote, ya kawaida na maalumu ili kupata elimu yake. Mathalani, mtoto kiziwi kuhudhuria darasa la viziwi na wakati huohuo kuwa na baadhi ya masomo katika mfumo wa darasa la kawaida akisaidiwa na mkalimani wa lugha ishara. due process: mchakato stahiki: 1. msemo wa kisheria wenye maana ya kitendo cha kulinda haki za mtu. 2. katika elimu maalumu istilahi hii humaanisha kitendo kinachochukuliwa kulinda haki za kielimu kwa mwanafunzi mwenye ulemavu (taz. haki ya kutendewa sawa kisheria). dumb: ulemavu matamshi: mtu asiyeweza kutamka wala kutoa sauti. Istilahi isiyozingatia hisia za mhusika imekuwa ikibainisha kundi hili la watu kama bubu.** Istilahi hii haiwapendezi baadhi ya

91 wanaharakati viziwi ambao hupendelea aina zote za ulemavu wa kimatamshi na usikivu zitambulishwe kama uziwi. dwarfism or short stature: -a kimo kifupi: 1. hali ya mtu kuwa mfupi kuliko kawaida kutokana na ukosefu wa madinijoto mwilini ambao huathiri ukuaji wa ncha za mifupa mirefu. 2. kibirikizi,** umbilikimo,** kibete,** kibeti,** na kisheta** ni baadhi ya istilahi za kitabibu na wanajamii ambao humtweza mhusika na hivyo hazifai kutumika katika jamii zenye kuheshimu haki za binadamu. Wahusika hupendelea kuitwa watu wenye vimo vifupi. dysarthria: disathria: 1. hali inayoathiri kwa kiasi kikubwa utamkaji wa maneno kutokana na kuathirika katika ala za sauti. 2. hali ambayo matatizo hujitokeza kwa nguvu pale ambapo misuli ambayo husaidia matamshi na kuifanya iwe vigumu kutamka maneno. Hali hii haihusiani na tatizo lolote la ufahamu na uelewa wa lugha. 3. kundi la matatizo ya kimatamshi ambapo sauti zinaweza kukokotezwa na matamshi kuwa ya taratibu au ya kulazimishwa. Mabadiliko ya uzio wa sauti, ukubwa wa sauti, mahadhi na ubora wa sauti vinaweza 73 kubainika. Matatizo kama haya husababishwa na mpoozo, udhaifu, au kutopangilika kwa misuli itumikayo kwenye matamshi. Disathria hutokea utotoni na katika utu uzima na huhusishwa na maradhi ya mishipa ya neva kama vile mpoozo wa ubongo, ugonjwa wa kutetemeka au kukakamaa, ugonjwa wa Lou ya Gehrig au hatua za kilele cha sklerosisi; unaweza pia kusababishwa na kiharusi, majeraha ya ubongo, na uvimbe. 4. hali ya kutoweza kutamka maneno sawasawa wakati wa kuongea kutokana na lesheni katika mfumo wa neva. lxii dyscalculia: kitatizaukokotozi: ugumu maalumu wa kiujifunzaji unaojidhihirisha zaidi katika eneo moja au zaidi la kuhesabu na kwa maana ya matumizi ya ishara, kupata stadi za kimahesabu hususani zile zenye kuhitaji matumizi ya kumbukumbu na uelewa wa masuala ya anga. Agh. dalili za wazi huhusiana na dhana za msingi kama vile kushindwa kujua wakati, kukokotoa bei na kujua bakaa wakati wa mauzo, kupima na kukadiria vitu kama vile halijoto na kasi ya mwendo. dysgraphia: disgrafia: 1. hali ya kuwa na mwandiko mbaya kabisa au kutomudu kufanya misogeo ya viungo inayohitajika katika kuandika. Kwa kawaida hali hii huhusishwa na kutofanya kazi kwa

92 nyurolojia. 2. athari katika uwezo wa kuandika hutokana na lesheni ya ubongo. lxiii dyslexia: disleksia: 1. hali ya kutoweza kusoma vizuri kutokana na lesheni katika mfumo wa neva. lxiv 2. ugumu mahususi wa kiujifunzaji ambao huathiri maendeleo ya kujua kusoma na stadi zinazohusu lugha. Maeneo yenye uzito ni pamoja na: kumbukumbu ya kufanyia kazi, kujipanga, kusoma kwa uelewa, hati, vituo wakati wa kusoma, umakini, kufululiza maneno na tarakimu. Wanafunzi wenye disleksia wanaweza pia kutamka vibaya maneno ya kawaida au kugeuza herufi na sauti za maneno. 3. aina ya kawaida ya ulemavu katika ujifunzaji ambapo licha ya uzoefu uliozoeleka darasani, mtu anaweza kuwa na matatizo katika kukumbuka na kutambua herufi zilizoandikwa, tarakimu na maneno, anaweza kusoma kinyumenyume na kuwa na mwandiko mbaya. Istilahi hii hutumika pale utendaji wa kinyurolojia unapokisiwa kuwa ni kisababishi cha ulemavu wa kusoma. dyspnea: dispenia: pumzi fupifupi zisizowezesha hewa ya oksijeni ya kutosha kuzunguka kwenye damu. dysmanthia: dismantia: istilahi hii humaanisha uzito wa kujifunza hususani kwa upande wa lugha. dysmelia: dismelia: istilahi ya jumla ya aina zote za tofauti za maumbile ya 74 mikono, miguu tangu kuzaliwa ambapo visababishi ni vinasaba vinavyoathiriwa na mazingira au matatizo mengine ya ukuaji wa kijusi. Hali hii hujibainisha kwa mtoto kuzaliwa na viungo vilivyoumbika tofauti. Japo hali hii hutokea kwa nadra ikihusisha viwango tofautitofauti vya usinyavu wa maungo, ila inatambulika sana. dysphagia: disfagia: ugumu au maumivu wakati wa kumeza. dysphoria: disforia: kujisikia vibaya. dysphoric mood: sununu ya kutojisikia vizuri: hali ya kutojisikia vizuri kama vile kuwa na huzuni, majonzi, wasiwasi, au hasira. dysphrasia: disfrasia: hali ya kushindwa kutamka maneno vizuri kutokana na matatizo ya akili. lxv dysplasia: displasia: mabadiliko ya ukubwa, umbile na mpangilio wa seli iliyokomaa au ukuaji usiokuwa wa kawaida wa seli, tishu na viungo. dysponen: kimuyemuye: upumuaji au upataji pumzi kwa shida. dyspraxia: dispraksia: 1. ugumu wa ujifunzaji ambao hulemaza uwezo wa kupangilia misogeo. Maeneo yenye kuonyesha ugumu ni: ukuaji kamili wa stadi za mwendo, kusimama au kukaa wima, ukuaji wa lugha, uwekaji kumbukumbu, hati, kujipanga, kumakinika, kufuatisha maneno na herufi. 2. hali ya kutoweza kutenda kilichokusudiwa. dysreflexia: tatizo la tendo siohiari: shinikizo la juu la ghafla.

93 dystrophy: distrofi: 1. kudhoofika kwa misuli hatua kwa hatua kunakotokana na matatizo ya misuli yenyewe. 2. athari yoyote ile ya ogani au tishu, hususani misuli ya mifupa inayotokana na matatizo ya lishe ya tishu hiyo. lxvi 75

94 Ee early identification (or early detection): ugunduzi wa mapema: uaguzi wa ulemavu wakati wa ujauzito au mara baada ya mtoto kuzaliwa au kwa njia ya kuchunguza kwa eksirei, kwa kutumia njia ya uchunguzi shuleni au mara tu dalili za tofauti zinapoanza kujitokeza. early intervention programmes or services: afua za mapema: 1. programu ya huduma zilizobuniwa ili kukidhi mahitaji ya ukuaji wa kila mtoto mchanga mwenye kustahili na familia husika kwa kadiri inavyoendana na ukuaji wa mtoto. Huduma kama hizo zinabuniwa ili: i) kutambua, kupima na kutibu ulemavu wa ukuaji mapema kadiri inavyowezekana ili kuzuia ulemavu usikithiri zaidi, ii) kuhakikisha kikomo juu cha ukuaji na ustawi wa mtoto na iii) kuisaidia familia ya mtoto mwenye ulemavu wa ukuaji. 2. michakato mbalimbali iliyobuniwa na kupangiliwa ili kupima na kutibu uzorotaji wa ukuaji au/na ulemavu wa mtoto pale vinapogunduliwa. early interventionist: mshughulikiaji mtoto mapema: wale wanaotoa huduma (familia, wataalamu, n.k.) za afua kwa mtoto wa umri 0-5 aliye na ulemavu. Huduma hulenga kuboresha matokeo ya ukuaji. Mtoa afua za kielimu zaidizaidi hujihusisha na utambuzi, mihemko ya kijamii na stadi za kujimudu. Yapo mabadiliko ya kujihusisha pia na stadi za 76 ujongeaji, na mahitaji ya familia. Huduma ya afua kwa mtoto ni uga wa kitaaluma wenye kujishughulisha na ukuaji wa ndani ya mtoto aliye hatarini au mwenye hali za kulemaza. early stimulation: uchangamshaji mapema: utumiaji wa mbinu mbalimbali, kumsababisha mtu hususani mtoto kuchangamka au kuwa mkakamavu. eating disorders: mvurugiko wa ulaji: hali inayojumuisha hofu isiyo ya kawaida kuhusiana na ulaji, kukondeana kutokana na: kutokula au kutocheua chakula, kusumbuliwa na taswira ya umbile, ulafi na kula vyakula visivyokuwa na virutubisho. Kuwa na njaa kali na anoreksia ni mifano ya mvurugiko wa ulaji. echolalia: mwigoradidi: 1. urudiajirudiaji wa maneno bila ya kutakiwa kufanya hivyo, kama inavyomtokea mgonjwa wa sikosisi. Aina ya afazia ambapo mgonjwa huweza kutamka maneno anayosemeshwa lakini yeye mwenyewe hawezi

95 kuyasema. lxvii 2. hatua anayoipitia mtoto wakati wa kujifunza lugha. ectrima: ektrima: taz. presure sores. education support resource and assessment centre (ESRAC): kituo cha rasilimali na huduma za upimaji maarifa: eneo ambapo mtoto hupokelewa kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi na kupimwa ili kuamua hatua sadifu za kuchukuliwa kulingana na mahitaji binafsi ya mhusika kielimu. Hatua zinaweza kujumuisha aina mbalimbali za zana na taratibu mbadala za ujifunzaji na upimaji maendeleo ya mtoto. Halikadhalika, wanajamii hunufaishwa na kituo kama hiki kwa kukutanikia na kupata huduma mbalimbali kutoka kwa familia, walimu na wadau wengine. Huduma zinazotolewa ni kama zile za maktaba, unasihi, mbinu za marekebisho na huduma kwa mtoto mwenye mahitaji maalumu ya kielimu, maonyesho na usambazaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, visaidizi kama vile shimesikio, aina mbalimbali za nyenzokongoje, n.k. educational psychologist: mwanasaikolojia wa kielimu: bingwa anayefanya upimaji wa ndani kwa mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu ya kielimu. Upimaji huhusisha mapendekezo ya kupambanua kazi za shule ili kukidhi mahitaji wa mwanafunzi. Mwanasaikolojia wa kielimu 77 anaweza pia kutoa msaada katika hali ya mwalimu na mwanafunzi au kikundi na hata kutoa ushauri kwa watumishi shuleni na wazazi. ego consciessness: nadhari : akili nzuri, busara, uangalifu. ego: igo: 1. istilahi iliyojikita kwenye nadharia ya udodosinafsi ambayo hujielekeza kwenye kipengele cha ukweli ndani ya dhamiri ya mtu. Igo husuluhisha nafsi ya mtu na uhalisia ulivyo. Igo hujengeka taratibu, kutegemeana na ukomavu wa mwili na hali ya kiuzoefu. Kazi yake kuu ni kupokea uhalisia na kuukumbatia. Shughuli nyingine za igo ni pamoja na: utambuzi ukijumuisha jinsi mtu anavyojitambua na kujifahamu, uthibiti wa misogeo, matumizi ya kanuni ya uhalisia na ile ya wasiwasi ili kujihakikishia usalama na kujilinda. 2. sehemu ya fikira ambayo hujengeka kutokanan na matukio ya ulimwengu wa nje (ya fikira) katika sehemu ya fikira iitwayo id. Igo hudhibiti idi. egocentrism: ubinafsi: hali ambayo mtu huichukulia dunia kwa jinsi anavyopenda yeye, bila kujali maoni ya wengine. ego-dystonic: mfadhaikonafsia: dalili au sifa bainishi za mtu ambazo huziona kama hazikubaliki kwake, na zisizotakiwa na hivyo kuonekana kiuzoefu kama ngeni. Mifano: wasiwasi na shuruti; ruwaza ya hisia ya mapenzi ya jinsia moja ambayo haikubaliki, kwa mtu

96 inaweza kuwa ni mfadhaiko wakati ambapo kama watu wasingefadhaishwa kwa ruwaza hiyo na kuiona kama inayokubalika, isingeweza kuwa ni mfadhaikonafsia. egoistic: -a kibinafsi: tabia ya kujiona bora na mwenye kustahilii kuliko wengine. elbow crutches: nsiso kigasha: aina ya wenzo wa kujikongojea ili kumwezesha mtumiaji mwenye kilema cha mjongeo kuwa kwenye mkao mzuri zaidi na kukipa kiwiliwili umadhubuti. Halikadhalika, humwezesha mtumiaji kutembea kwa miondoko mbalimbali kulingana na hali. Tofauti na nsiso kwapa, aina hii ya wenzo ni kwa ajili ya mtu mwenye nyonga imara ila mguu umedhoofu kuanzia pajani kushuka chini. Wenzo huu egemeo lake ni kigasha na kiganja cha mkono. elective mutism: unyamavu hiari: mvurugiko wa utotoni ambapo kijana mwenye uwezo wa kusema huamua kutoutumia. electronic device: kifaa cha kielektroni: kisaidizi kwa ajili ya matumizi ya asiyeona. Ni kifaa cha kukuza maandishi, kompyuta yenye programu za kukuzia na kuchapa maandishi yaliyokuzwa au 78 nuktanundu, kifaa cha mawasiliano ya simu n.k. (Rejea kwenye teknolojia rekebifu). electro convulsive therapy: tiba mtukutisho umeme: aina ya matibabu ya maradhi ya akili ambapo umeme hupitishwa kwenye ubongo wa mgonjwa. Pamoja na lengo zuri, hii aina mojawapo ya mateso na uvunjaji wa haki za mtu mwenye ulemavu. electronic pointing device: kitumi kioneshi cha kielektroni: kifaa kinachotumika katika kulengeshea kasa kwenye skrini ya kompyuta bila kutumia mikono. Vifaa vinavyotumika vinajumuisha kiuka sauti, miali fiche, kupepesa macho, ishara za neva au mawimbi ya ubongo. (Rejea kwenye adaptive technology ). elephantiasis: matende: uvimbe sugu, agh. wa miguu unaosababishwa na mbu wa aina ya kuleksi na huathiri lalo za ngozi na tishu. elevated mood: uchangamfu kithirifu: hali ya kuonyesha furaha kupita kiasi na siyo lazima imaanishe ugonjwa. eligibility: ustahilifu: 1. sifa au hali ya kustahili jambo kama vile kuchaguliwa au kuteuliwa, kuwa na sifa kisheria au kikawaida. 2. -enye kufaa, inayohitajika.

97 eligible expenses: gharama stahilifu: kiasi cha fedha kinachotumika katika matibabu. eligible: -a kustahili: -enye kustahili, enye sifa, iliyo na sifa kisheria. Kipengele hiki hutumika kuamua ushiriki katika masuala mbalimbali ya kiraia na kisiasa k.v. uchangiaji wa gharama za matibabu, kupata ruzuku wiani shuleni, misamaha ya kodi, n.k. embarrass: tahayarisha: chochea hofu au dunisha hali ya mtu mwenye ulemavu; mathalani, wanapotaka kupata huduma za afya ya uzazi kwa kudhaniwa kuwa hahusiki. embarrassment: tahayuri: kuona haya baada ya kufedheheshwa. embryo: kiinitete: kiumbe katika hatua za awali za ukuaji wake ndani ya tumbo la mnyama akiwemo binadamu. emergency: hali ya hatari au dharura: hali inayojitokeza kwa kusababishwa hasa na matukio ya ghafla na yenye athari kubwa kama vile maafa ya asili, (mafuriko, moto wa nyika, ukame, n.k.). Wakati mtu mwenye nguvu zake hufanya kila jitihada kuyaokoa maisha yake, yule mwenye ulemavu huwa mwathirika wa maafa hayo kwa kukosa aula ya huduma za uokozi katika jumuia anamoishi. emotion: mhemko: 1. hisia kali zinazodhihirisha furaha, huzuni, kuchanganyikiwa. 2. hisia za kimwili zinazoambatana na kuongezeka 79 kwa harakati za neva na tezi za endokrini. emotional: -a mhemko: enye hisia kali zinazodhihirisha furaha au huzuni. emotional disturbance (ED or SED): kisumbuahisia: 1. kumvurugikiwa kimhemko kunakoambatana na mabadiliko ya tabia kwa muda mrefu na kwa kiwango fulani ambayo huathiri maendeleo ya mhusika kijamii, kielimu na kitaaluma. 2. kushindwa kujifunza bila sababu dhahiri kiakili au kiafya. 3. mwanafunzi kushindwa kujenga au kudumisha mtangamano kwa kiwango cha kuridhisha kati yake na walimu na/au wanafunzi wenzake. 4. jumla ya hali ya moyo ya kutokuwa na furaha au kujawa sononi. emotional response: mwitikio mhemko: hali ya kihisia inayompata mtu baada ya kushuhudia tukio fulani au ushirikihali na mwingine anayewasiliana naye. emotional skills: stadi mhemko: ujuzi unaosadia kuboresha mihemko ya mtu. emotional well being: ustawi kimhemko: uwezo wa kudhibiti hisia binafsi hata baada ya kukutwa na jambo ama la kufurahisha au kuhuzunisha (taz coping skills ). emotional disorder (EBD): mvurugiko kimhemko: hali ya kuvurugika kimwenendo na kihisia. Mtu mwenye mvurugiko wa aina hii

98 hamudu kudhibiti vya kutosha vurugu za hisia zake, na hivyo kutoweza kuendeleza mienendo katika viwango vinavyokubalika. Mwanafunzi mwenye kuvurugukiwa kwa kiasi kidogo anaweza kusaidiwa kwa kuendelea kuwekwa kwenye darasa la kawaida akihudumiwa na mwalimu asomipaka. emotive language: lugha hemshi: matumizi ya lugha ambayo inachochea hisia za wengine kulingana na kusudio la mnenaji. empathetic: -a ushirikihali: -enye uwezo wa kuelewa hisia au uzoefu wa mtu mwingine hasahasa kutokana na kupitia kwenye hali sawa na yake hapo kabla. Mtu mwenye ulemavu anahitaji washirikihali wengi hasa katika ngazi za uamuzi ili kumjengea mazingira ya kujistawisha na kunufaika na haki zake zingine. empathise: shirikihali: elewa, hisi na guswa na hali ya mtu aliyekabiliwa na tatizo kama vile ni lako, kisha kwa pamoja naye kutafuta suluhisho au faraja. empathy: ushirikikali: 1. uwezo wa kuhisi hisia ya mwingine na kumsaidia kukabiliana vilivyo na hisia hizo. 2. huruma ya kina; mahusiano ya karibu ya mhemko baina ya watu wawili kiasi kwamba matatizo ya mmoja wao huhisiwa kana kwamba ni ya 80 mwingine. 3. uwezo wa kuelewa jinsi gani mtu mwingine anavyohisi kwa sababu ya uwezo wake wa kujilinganisha na hali au hisia alizo nazo mtu huyo. emphysema: emfisema: hali ya hewa kutuna kwenye tishu za mapafu isivyo kawaida na hivyo husababisha mkwamo pumzi. empiric: -a jarabati: -enye kujikita katika uzoefu halisi au tafiti za kisayansi kuliko nadharia pekee. employability skills: stadi ajirishi: stadi zinazohusu uchaguzi wa kazi au amali, kuipata na kuidumisha, kubadilisha kazi na kujiendeleza kwenye ajira. employment activities: shughuli za ajira: shughuli za maeneo ya aula zinazoongeza kujitegemea, uwezo zalishi, au uchangamanishaji wa mtu mwenye ulemavu wa ukuaji katika mazingira ya kikazi. empower: wezesha: -pa kumsaidia mtu (agh. mwenye ulemavu) uwezo wa kufanya jambo ambalo kutokana na maumbile yake asingeweza kulifanya. Afua na sera ikibali vinamwezesha mtu fukara kujikakamua ili kujistawisha na kuwa na hadhi ndani ya jamii. Uwezeshaji huu unaweza kuwa ni wa kimaarifa, kirasilimali na kifursa ili mhusika hasa aliye na ulemavu aweze kutumia vipaji na vipawa vyake kujinufaisha mwenyewe na jamii kwa ujumla.

99 empowerment: uwezeshaji: agh. kwa muktadha wa watu wenye ulemavu pamoja na mengine humaanisha mchangamano wa wataalamu na familia kiasi kwamba familia zinapata ufahamu wa kudhibiti maisha ya familia zao na kuchangia kuwapo kwa mabadiliko mazuri yanayotokana na ushughulikiaji mapema. enabling act: sheria wezeshi: sheria ya kuwezesha kufanyika jambo enabling: uwezeshaji: kubuni fursa na nyenzo kwa familia ili kuonyesha uwezo na umilisi walionao na katika kuongeza fursa zingine mpya ambazo ni muhimu katika kukidhi mahitaji ya watoto wao na wao wenyewe. enact: fanya kuwa sheria: tekeleza kivitendo sheria iliyopitishwa na mamlaka husika. Hatua hii ni muhimu katika ustawishaji makundi ya pembezoni kwani mara nyingi mikataba iliyoridhiwa na sheria zinazopitishwa hubakia vitabuni bila kuchochea mabadiliko chanya kwa wahusika wenye wajibu kuzembea katika hatua za utekelezaji. encephalitis: ensefalitisi: uvimbe wa ubongo. endemic: endemiki: ugonjwa mbao hupatikana mahali fulani kwa wakati wote japo kwa viwango tofauti. lxviii enema: enema: 1. kiowevu kinachotiwa kwenye njia ya haja kubwa ili kumchochea mtu atoe kinyesi au 81 kuingiza kiwango cha majimaji mwilini. 2. kiowevu kinachomiminwa ndani ya ujovu kwa ajili ya kufanikisha tiba ama uchunguzi fulani. lxix enforce: tekeleza: chukua hatua katika kuhakikisha kuwa sheria, azimio, mkataba, n.k. inatekelezwa kama inavyotakiwa. enfranchise: patia haki za kisiasa: toa nguvu za kisheria kwa raia kushiriki kwenye michakato ya kidemokrasia katika nchi husika. Hii ni hatua muhimu katika unufaikaji na haki za kirai na kisiasa (hasa kwa mtu mwenye ulemavu) kwani sheria hutoa fursa na mazingira ya wahusika kuwa na maoni au dhamiri, kujieleza, kukusanyika, kuunda asasi za kiraia na hata kisiasa, kushiriki kuchagua wawakilishi hali kadhalika na kuwania nafasi za uwakilishi. engagement: ujishughulishaji: hali ya kujiingiza katika utekelezaji wa jambo fulani. Hii ni hatua ambapo raia mmojammoja au katika makundi hutafuta na kutumia fursa za kujenga hoja na kuibua mijadala miongoni mwao na baina yao na wawakilishi au wafanyaji uamuzi kuhusu mstakabali wa makundi husika na jamii kwa ujumla. enjoyment: faidi: 1. hali ya kupata manufaa ya kitu fulani. 2. furaha. enrichment: stawisha: patia mtu fursa kwa kubadilishana uzoefu na maarifa na mwingine katika

100 mifumo rasmi na isiyo rasmi na kwa njia hiyo kutajirishana kimaarifa na kiuzoefu. entry into force: anza rasmi kutumika kisheria: mazingira na muda ambao mkataba unaweza kuanza kutumika. Kimataifa hatua hii hufikiwa hasa pale Mkataba husika unapokuwa umepitishwa na kutimizwa kwa kipengele cha idadi ya chini ya saini za wanachama wanaoukubali na kisha kuuridhia. Hatua hii hufuatiwa na ile ya kila nchi mwanachama iliyousaini Mkataba husika, kuuridhia kwa kufuata taratibu za ndani ya nchi yenyewe, na hivyo kujifunga nao kwa kutekeleza vipengele vyake. Sheria za kawaida za nchi, huanza kutumika baada ya Wizara yenye dhamana kutunga kanuni za kuwezesha utekelezaji wa sheria husika. enuresis: ufukunyungu (enuresisi): hali ya kutokwa na mkojo bila ya kukusudia, kujikojolea. lxx environment bias: mili kimazingira: mtazamo dhahania ulioegemea mazingira (utamaduni na mfumo wa kijamii). environment: mazingira: ulimwengu unaokuzunguka. environmental barrier: mkingamo wa kimazingira: aina ya kizuizi chenye kumkinza mtu mwenye ulemavu asivinjari au/na kuyafikia na kuingia kwenye majengo; mathalani, jengo lenye ngazi peke yake kama njia ya kuingilia ndani ambapo mtu mwenye kitimwendo huzuiwa kuzuru na kutumia jengo hilo. (ang. barriers ). environmental factors: kigezo cha kimazingira: hali ya kimaumbile, kijamii na kimtazamo ambamo mtu huishi na kuendesha maisha yake. Vipengele hivi vinaweza ama kuwa vizuizi au viwezeshi vya utendaji wa mtu. environmentally at risk: hatarika kimazingira: tukio la awali katika maisha ambalo linahusianishwa na kuwepo kwa wigo finyu wa kujiendeleza. (mf. elimu duni ya ulezi na matunzo ya mtoto, msaada mdogo wa kijamii, au kiwango kikubwa cha msongo wa kifamilia). epidemic: ambomlipuko: ugonjwa unaoenea kwa kasi kubwa na kuathiri idadi kubwa ya watu katika eneo fulani. epidemiology: elimumaambo: 1. uchunguzi wa kisayansi unaohusu magonjwa ya kuambukiza na vyanzo vyake. 2. tanzu ya elimu inayohusu uenezaji wa magonjwa. epilepsy: kifafa: 1. hali ya mtu kugundulika kupatwa na mfululizo wa mitukutikomwili isiyo ya hiari pamoja na kudhihirisha hali zifuatazo: kupata mfululizo wa mitukutikomiwili katika kipindi kipatacho mwaka mmoja bila sababu zilizo wazi; mtukutikomwili 82

101 mmoja usohiari baada ya ile miwili na kuwepo uwezekano wa kujirudia tena (wa asilimia 60) ikiwa na athari zilezile za kawaida katika kipindi cha miaka 10; uchunguzi wa ashirio la kifafa: kifafa hufikiriwa kuwa kimepona kwa mtu ambaye alikuwa na ashirio la kifafa kutegemeana na umri, lakini akaupita umri huo au wale ambao wameedelea kutopata mishtuko kwa kipindi cha miaka kumi na bila kutumia dawa kwa miaka mitano nyuma. 2. hali ya kimaumbile ambayo hutokea pale ambapo kuna mabadiliko mafupi na ya ghafla ya jinsi ubongo unavyofanya kazi. Wakati seli za ubongo hazifanyi kazi ipasavyo, ufahamu wa mtu, msogeo au vitendo vinaweza kubadilika kwa kipindi kifupi. Mabadiliko haya ya kimaumbile huitwa mitukutiko mwili ya kifafa. Kwa maana hiyo, kifafa wakati mwingine huitwa mivurugiko ya kimitukutiko mwili. Hata hivyo, mtu anaweza kupatwa na mitukutiko mwili bila kifafa. Mitukutiko mwili kama hiyo inaweza kutokana na ulemavu mdogomdogo au ule changamani wa kimwenendo au unaweza kukua kufikia kiwango cha jumla cha mitukutiko. 3. ugonjwa wa kurudiarudia ambapo chimbuko lake ni uchochezi wa kuzidi kiwango wa koteski ya ubongo. Shambulizi halisi la kifafa agh. huanza kwa mwathirika kujiliwa na hisia fulani ya 83 kuona, kusikia kunusa, au kuonja na ghafla kubambwa na mtukutiko wa maungo ambapo hutupa miguu na mikono huku na huko kisha kutulia na kusinzia. epilepsy Jacksoniana: kifafa aina ya Jacksoniana: aina hii ya kifafa husababishwa na hitilafu kwenye sehemu ya mota ya ubongo. Shambulio lake huanzia katika eneo la mwili ambalo sehemu hiyo ya mota inahusika. epileptic: mwathirika wa kifafa**: msamiati wenye kulenga kumtabulisha mtu mwenye kifafa kwa namna ya kutweza. epileptic psychosis: sikosisi za kifafa**: 1. kuathirika kwa akili kutokana na ugonjwa wa kifafa wa muda mrefu. 2. kuchanganyikiwa kwa kuwa na kifafa. equalisation of opportunities: usawazishaji wa fursa: 1. mchakato ambao mifumo, mazingira na shughuli mbalimbali katika jamii hupitishiana huduma kwa ajili ya watu wote hususani wale wenye ulemavu, mathalani, taarifa na nyaraka. lxxi 2. usawazishaji wa fursa za maisha ya watu katika jamii bila kujali uwezo wa mtu, hali ya kiuchumi au kijinsia. equalising difference: tofauti sawazishi: aina ya sera ikibali ambapo mtu mwenye hali fulani anaweza kupewa upendeleo maalumu au kutendewa tofauti na wenzake wasiokuwa na hali kama

102 yake ili kumfanya awe sawa nao. Mathalani, (a) mwanafunzi asiyeona kuongezewa muda wa kujibu maswali ya mtihani (b) mtu mwenye ulemavu aliye na sifa za kimachini kupewa nafasi ya ajira badala ya yule aliye na sifa za kiwango cha kimajuu lakini bila ulemavu; (c) wasafiri wenye ulemavu kulipa nusu ya nauli ya wale wasiokuwa na ulemavu. (taz. affirmativeaction ). equality: usawa: kuwa sawa, kulingana na kuwa pacha na. Hata hivyo, istilahi hii inapotumiwa kwa mtu, hailengi kumaanisha kuwa watu wote ni sawasawa au chapa ya moja kwa nyingine, kwani kiuhalisia kamwe hali haiwezi kuwa hivyo. Katika muktadha wa haki za binadamu, istilahi usawa hutumika kumaanisha kuwa usawa wa binadamu umejikita kwenye msingi kwamba: bila kujali tofauti zao, binadamu wote wana sifa zinazowapambanua ambazo hazipashwi kufanya mmojawao kuwa daraja la juu au la chini. Mikabala inayozingatiwa wakati wa kutafakari kuhusu utekelezaji wa kanuni za usawa ni pamoja na: usawa uliozoeleka au rasmi: pale ambapo sheria au/na sera huyataka makundi mbalimbali ya watu kutendewa katika hali sawa kwa kuzingatia kuwa yasibaguliwe. Hata hivyo, mkabala wa aina hii hautoshi kuhakikisha kuwa kundi la watu wenye ulemavu au kundi jingine 84 lolote la pembezoni linanufaika na usawa halisi. Mkabala huu unaweza hata kusababisha utovu wa usawa kutokana na kwamba hauzingatii hitilafu au nafuu na mahitaji mahususi ya baadhi ya makundi. usawa wa fursa: mkabala unaotambua kwamba mtu anaweza kukabiliwa na ukomo maishani mwake kutokana na mazingira na hali ilivyo nje ya uwezo wake; mathalani, rangi, jinsia, ulemavu, na hadhi ndani ya jamii. Mazingira na hali hizi peke yake au zikichangiwa na mikingamo ya kimtazamo na vinginevyo, vinaweza kumsababisha mtu mwenye ulemavu kushindwa kuishi anavyotaka au kutochangia kwenye ustawi wa jamii. Kwa maana hiyo, hakikisho la usawa wa fursa huhitaji kuchukuliwa kwa hatua mahususi za ziada ili kwenda mbele zaidi ya usawa wa kawaida na kuhakikisha kwamba mtu mwenye ulemavu ananufaika na fursa zilezile kama ilivyo kwa watu wengine. usawa kenyekenye au halisi: mkabala unaotafuta hakikisho la usawazishaji matokeo na fursa kutokana na kwamba upatikanaji kwa usawa wa fursa unaweza kuhitaji kutendewa tofauti. Mkabala huu humchukulia kila mtu kuwa na haki ya kunufaika kwa ukamilifu na haki zake bila kujali umri wake, jinsi, kabila, uluwa ndani ya jamii, asili ya mtu kijiografia au ulemavu. Mathalani, ili kuhakikisha kuwa mtu

103 mwenye ulemavu habaguliwi kwenye mchakato wa uchaguzi, nchi husika haina budi kudurusu sheria zake za uchaguzi na kutafuta mbinu za kuziba mianya kuhusu mikingamo ambayo vinginevyo hukwaza mtu stahilifu kwenye kundi hili kutoshiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi. equalisation: usawazishaji: mchakato ambapo mtu mwenye ulemavu huchukua nafasi yake katika jamii sambamba na wasio na ulemavu. Hatua hii hufikiwa kwa kupitia njia nyingi ikiwa ni pamoja na sheria, uendelezaji wa dhana ya mazingira yasiyokuwa na vizuizi, huduma za marekebisho ndani ya jamii, elimu, mafunzo na ajira. equitable: -a usawa:1.-a usawa; 2. a haki, 3. katika uga wa watu wenye ulemavu na makundi hohehahe, istilahi hii husisitiza uzingatiwaji wa mahitaji mahususi ya pande mbili. equitable distribution: ugavi linganifu: hali ambapo wagavi na wasambazaji huzingatia vizuizi vinavyoweza kumkinza mtu mwenye ulemavu kupata huduma kwa haki. equity: usawa:, utoaji haki unaozingatia siyo tu mahitaji bali pia hali zingine k.v. maumbile ili kila mmoja afaidike na huduma au fursa inayotolewa kwa kiwango sawa na wenzie (muktadha wa watu wenye ulemavu). 85 erbs paralysis: kupooza misuli bega: mpoozo wa mkono wa mtoto unaosababishwa na kujeruhiwa neva za bega wakati wa kuzaliwa. esotropia au esophoria: esoforia: makengeza yaliyoelekea ndani. estate: miliki: kisheria, neno hili humaanisha kila kitu anachokimiliki mtu ikiwa ni pamoja na rasilimali na madeni vinavyobakia wakati wa kifo chake. estrogen: estrojeni: homoni ya kike. etiquette: akhlaki: 1. adabu 2. utaratibu za kiitifaki. 3. muundo wa kanuni na mienendo ya watu katika shughuli maalumu kama zile za kitaaluma, biashara, diplomasia n.k. lxxii 4. maelekezo au kanuni rasmi za maadili ya kutumia kwa usahihi kwenye masuala yanayohusu taaluma maalumu; sherehe, dhifa za kidiplomasia; mahakama; biashara. 5. tabia ambayo jumuiya fulani ya kitaaluma au kijamii inategemea kutoka kwa wanajumuiya wake. Pia kaida (za kitaaluma na kimwenendo). 6. adabu, taratibu za kiitifaki, miiko. lxxiii eugenics: udhibitihali: 1. mbinu za kuboresha nasaba ya binadamu

104 kwa kuruhusu watu waliochaguliwa kimakini tu ndio wazaliane. Dhana hii ya uhulukishaji imeshajiisha falsafa yenye utashi wa kuboresha urithi wa sifa pambanuzi za binadamu k.v. kuumba watu wenye afya, nguvu au/na akili bora zaidi ili kuokoa rasilimali na kupunguza mateso miongoni mwa wanadamu kwa njia ya kuchagua mbegu, uchunguzi wa mimba kabla ya kuzaliwa, unasihi wa kijeneti, kudhibiti kizazi, ushahawishaji ghushi, na kurekebisha vinasaba kimaabara. 2. sayansi inayohusu njia mbalimbali ambazo zinaweza kuboresha kuzaliwa kwa mbari hasa binadamu. lxxiv 3. sayansi inayoshughulika na matumizi ya vinasaba ili kumwendeleza na kumstawisha binadamu na kukuza hali yake. Wanaharakati wa masuala ya ulemavu huichukulia falsafa hii kuwa kandamizi kwani dhamira yake ni kutoheshimu uanuwai miongoni mwa wanadamu. Hali hii inaweza kufuta kabisa uwezekano wa kundi la watu wenye ulemavu kuifaidi haki zao za kuishi. euphoria: uforia: hali ya kujisikia vizuri, nishai, hali ya kufurahia. lxxv euphoric: -enye wingi wa furaha, hali ya kufurahia. euphoric mood: mhemko furaha: hisia za raha zilizopindukia. Katika muktadha wa kiufundi, uforia humaanisha hali ya kuugua. 86 Wakati mtu mwenye hali ya kuchangamka kikawaida kuweza kuelezea kuwa mchangamfu, kufurahi sana, yule mwenye yuforiki anaweza kudai kuwa juu ya ulimwengu au kuwa mawinguni au kusema anapaa ama kurukwa na akili, kuwa na jazba. Hali hii hufuatiwa na shambulio la kisaikolojia au kifafa. eustachian tube: tyubu ya ustachia: ujia wa sikio ambao huunganisha sikio la kati na lile la ndani. euthanasia: kifohiari: kifo kitulivu ambapo kwa ridhaa ya mgonjwa au jamaa zake wa karibu, matabibu hutoa dawa au sindano ya kumtoa uhai mhusika bila maunivu au mahangaiko. Katika baadhi ya nchi, afua hii inatambuliwa kisheria kwa dhana ya kuwa mgonjwa wa muda mrefu anapumzishwa asiendelee kuumia. Hata hivyo, tapo la watu wenye ulemavu hawakubaliani na mkabala huu, kwani unafananishwa na udhibitihali ambao lengo lake ni kufuta viumbe wenye ulemavu katika uso wa dunia. euthymic mood: mchangamko: hali ya kujihisi kuchangamka katika viwango vya kawaida ikimaanisha kutokuwa na sononi au mihemko. evaluation: tathmini: 1. kielimu ni njia ya kukusanya maelezo (ikiwa ni pamoja na mitihani, uchunguzi na michango ya wazazi) kuhusu

105 mahitaji ya mwanafunzi kiujifunzaji, uimara wake na upendeleo wake. Tathimini ni mchakato wa kubaini iwapo mwanafunzi anastahili kujiunga na programu na huduma za elimu maalumu. 2. mchakato unaochukuliwa na wataalamu wa afya ya akili ambayo matokeo yake ni maoni kuhusu uwezo wa mtoto kiakili au uwezo kimihemko na inaweza kujumuisha mapendekezo kuhusu tiba au pahala stahiki au kubadilishiwa huduma. evolution: mabadiliko: 1. hali ya kimaendeleo ya mageuzi ya taratibu ya mbari au spishi. 2. ubadilikaji wa kitu kutoka kwenye hali ya kawaida kwenda kwenye hali changamani. exanimation: kuzirai: hali ya kuzimia na kupotewa na fahamu kama vile katika hali ya kupatwa na kifafa. exarticulation: uachanishaji kiungo: kuondolewa kwa kiungo cha mwili kwa kukikata katika kifundo au tindi. exceptional: -a kipekee: -enye utendaji wa kimwili, kiakili au kimwenendo unaokengeuka kupita kiasi na hivyo kulazimu huduma za ziada kukidhi mahitaji ya mhusika. excess cost: gharama ziada: ugharimiaji programu na shughuli zinazotolewa mahususi kwa mtu aliyeainishwa kuwa hohehahe au mwenye ulemavu na zisizotolewa kwa asiyekwa na ulemavu. 87 excitement: msisimko: ulemavu wa kuhisi furaha, huzuni au hofu unaompata mtu kutokana na hali ya maumbile aliyonayo. exclusion: kutenga: mchakato ambamo mtu au jumuia nzima ya watu wanazuiwa kimfumo au kukatazwa kupata kikamilifu haki, fursa na rasilimali mbalimbali ambazo kwa kawaida hutolewa kwa makundi mengine na ambazo ni za msingi kwa mchangamano wa mtu au wanakikundi hicho; mathalani, makazi, ajira, huduma za afya, shughuli za kijamii, ushiriki kwenye masuala ya kidemokrasia, na michakato mingineyo halali. Matokeo ya kutengwa huko ni mwathirika binafsi au kundi kuzuiwa kushiriki kikamilifu kwenye masuala ya kiuchumi, kijamii, maisha ya kisiasa ndani ya jamii linamoishi. executor or personal representative: kabidhi wasii: mtu au shirika ambalo hutajwa kwenye wosia ambao huwa na wajibu kisheria kutekeleza matakwa ya wosia kwa kadiri ya uwezo wao kwa mujibu wa sheria zilizopo nchini. Msimamiaji huyu anaweza kutafuta msaada wa kiutendaji kutoka kwa mwanasheria katika kukamilisha michakato ya uthibitishaji wa wosia. exemption: msamaha kisheria: kusamehewa kutotekeleza jambo ambalo agh. hupewa nguvu ya kisheria; mathalani, baadhi ya nchi, hutoa unafuu wa kodi kwa kila

106 mwenye kuajiri kundi la watu wenye ulemavu. Kwa muktadha wa watu wenye ulemavu, unafuu huu hutambuliwa kisheria au wawekezaji wa mitaji ya kiuchumi kupewa kipindi fulani cha kutoilipa serikali kama aina ya kivutio cha mitaji na teknolojia.. exhibitionism: ujianikaji uchi: 1. kujiamshia ashki kwa kuanika maeneo ya manena kwa wapitanjia. 2. ujianikaji wa utupu kwa lengo la kuamsha hisia za kimapenzi. exogenous: kilema kisicho cha kuzaliwa: maradhi au ashirio la maradhi ambapo chimbuko lake si kwa kuzaliwa nalo wala kurithi bali ni kutokana na sababu nyingine ambazo ziko nje ya kiumbe kama vile ulemavu wa kushindwa kuongea kutokana na kuumia ubongo. exorphoria: makengezanje: makengeza ya kuelekea nje. lxxvi expansive: kunjufu: -enye ari au utayari wa kuongea. explosive personality: haiba mlipuko: mparaganyiko wa udhibiti wa hisia ambapo matukio ya milipuko ya mihemko ya kutisha hutokea na kusababisha kushambuliwa kwa wengine au uharibifu wa mali bila kuwepo kwa mipiraganyiko mingine ya kifafa au ya haiba ambayo ingeweza kuhusishwa na mwenendo kama huo. exposure: mfichuo: 1. uwekaji wazi kitu ambacho kwa kawaida hufichwa k.v 88 uchi wa binadamu. 2. kuwa katika mazingira yanayohatarisha au yanayodhuru. Mfano: mfichuo wa ngozi ya mtu mwenye ualbino kwenye jua kali unavyoweza kuathiri ngozi yake au/na uwezo wake wa kuona. expressive (guide-) advocacy: mtetezi mwandani: mtu anayejitolea kukidhi mahitaji ya mwingine katika masuala ya kiuhusiano, mawasiliano, kufariji, umakini, msaada wa kiupendo na kihisia. expressive aphasia: afasia ya kujieleza: kasoro au kupungukiwa uwezo wa kujieleza kimatamshi, kimaandishi, kiishara kutokana na kujeruhiwa au kuwa na maradhi kwenye ubongokati. expressive language disability: mvurugiko elezi wa lugha: 1. ulemavu wa ujifunzaji ambapo mtu hupata ugumu wa kujieleza kimatamshi. 2. lugha ambayo agh. hutumiwa na mtoto kueleza dhana, maoni, au hisia kwa mtu mwingine kwa kuongea akitumia ishara. expressive language skills: stadi mawasiliano: ujuzi unaohitajika ili kuzalisha lugha ya kimawasiliano na watu wengine, mfano, kuongea na kuandika ni stadi za kujieleza kwa lugha. expressive language: lugha elezi: dhana, maoni na hisia n.k. extended family: familia tandavu: familia ambayo mwanafamilia yeyote

107 anawasiliana na kuchangamana na mtu wa familia yake. external factor: kisabanje: kisababu cha nje kinachoweza kufanya jambo limtokee mtu bila hiari yake wala uwezo wa kupambana kuizuia lisitokee. Mathalani, hali ya mtu mwenye ulemavu kujikuta akitengwa na jumuia. extra curriculum: nje ya mtaala: shughuli yoyote inayofanyika zaidi ya ile iliyopo kwenye mtaala. extremities: kiungo pembezoni: sehemu ya pembezoni mwa kiwiliwili. Pembezoni juu (mikono) na pembezoni chini (miguu). extrovert: msondani: mtu mchangamfu anayependa mambo mengine kuliko yake mwenyewe au/na kuwa mwepesi kuchangamana, kuchangamkia watu wengine na hata kuwashirikisha mambo yake binafsi. eye contact: mbashala: hali ya kuangaliana ana kwa ana au mtu kukaziana macho na mwenzake anayemuongelesha ambayo ni desturi ya kawaida japo siyo mara zote mzungumzaji kumkazia macho msikilizaji. Hali hubadilika kutegemeana na utamaduni wa mtu. 89

108 Ff face blindness: upofu wajihi: hali ya mtu kushindwa kuitambua sura ya mwingine ambayo alizoea kuiona (yaani hata kama ni jamaa wa karibu). facilitate: wezesha: rahisisha jinsi ya kufanya au kuelewa jambo. facility: kifaa: kitu kinachotumika kwa urahisi katika utekelezaji wa jambo. Urahisi huu wa kimatumizi unaweza kutokana na asili ya kitu (kilivyotengenezwa) au uboreshaji uliofanywa baadaye kwa kuzingatia mahitaji mahususi ya mtumiaji. Dhana hii ni pamoja na huduma ya ziada au kulenga watumiaji mahususi mathalani, kwenye michezo, burudani, maktaba, benki, maduka makubwa, n.k. Mazingatio kama haya ni muhimu kwa mtu mwenye ulemavu kwa kumtendea tofauti ili awe sawa na wengine. failure to thrive (FTT): udumavu: hali ya mtoto kutokua au kutoongezeka uzito au kimo kutokana na maradhi au kukosa lishe. familial disease: ugonjwa wa kifamilia: maradhi ya kuzaliwa nayo yanayorithiwa ndani ya familia. familial dwarfism: ufupi wa kuzaliwa: hali ya mtu kuwa na kimo kifupi kwa kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. familial: -a kurithi: -enye ugonjwa au mvurugiko unaowapata watu kadhaa wa ukoo mmoja. family centered or focus model: modeli familia: utoaji wa huduma za 90 msaada kwa mtoto mwenye mahitaji maalumu katika muktadha wa familia ili kuboresha matokeo ya ukuaji. Mfumo huu unamakinikia zaidi familia na mtoto kwa kuhimiza na kuimarisha uwezo na umilisi kwenye ngazi hii ambayo ndiyo msingi mkuu katika malezi ya mtoto. family counseling: unasihi familia: ushauri unaotolewa kwa wanafamilia ili waweze kumkubali mwanafamilia mwenye mahitaji maalumu (yanayotokana na hali yake ya ulemavu) katika majukumu ya kifamilia (taz. coping strategies ). family needs: mahitaji ya familia: vitu muhimu kwa familia katika matunzo na malezi ya mtoto mwenye ulemavu. Vitu hivi hulenga kusaidia ukuaji wa mhusika na familia ambavyo ni pamoja na rasilimali fedha, uandaaji wa bajeti, upatikanaji wa dawa, fursa ya elimu, lishe bora, matunzo, na uboreshaji wa mazingira ya familia kwa jumla. family planning: uzazi wa mpango: utaratibu wa wazazi kutumia kingamimba ili kuamua idadi ya watoto wanaowataka na wakati wa kuwapata. Kingamimba ni pamoja na matumizi ya kondomu, viwambo, kofia za shingo za uzazi, vizuizi vya kikemikali (vidonge, viuajishahawa, sindano), ufahamu wa rutuba ya uzazi, uhasishaji wanamume na ufungaji wa mirija ya ovari kwa wanawake.

109 family resources: raslimali za familia: jumla ya mali zinazomilikiwa na familia zikijumuisha fedha, vitu, maarifa, na uhusiano wa watu ndani ya jumuiya. family strengths: umadhubuti familia: vitu ambavyo familia huvitegemea katika ukuaji na ustawi wa mtoto mwenye ulemavu k.v uhusiano wa malezi, mawasiliano, imani za dini au imani binafsi, maarifa ya kulea familia, ushirikiano na jamii, n.k. family support programmes or services: huduma mwega kwa familia: misaada inayotolewa kwa familia katika kumtunza mtoto au mtu mzima mwenye ulemavu kwenye familia ili aweze kubakia nyumbani. Huduma hizi hubuniwa ili: i) kuimarisha jukumu la familia la kuwa mtunzaji mkuu, ii) kuzuia matunzo yasiyofaa nje ya familia na kudumisha umoja, na iii) kuunganisha tena familia na mwanafamilia aliyekuwa akitunzwa nje ya familia yake. Huduma hizi hujumuisha: kujihudumia kwa muda (matunzo ashekali), teknolojia saidizi, wasaidizi binafsi, mafunzo na unasihi kwa wanafamilia, matunzo kwa wazazi wazee, marekebisho ya vyombo vya usafiri na makazi, msaada wa gharama za ziada zinazohusiana na kuhudumia ulemavu. family systems: mifumo ya familia: utaratibu mahususi wa kuchangamana kijumuia ambao 91 huakisi hali za kiuchumi, ukabila na mielekeo ya watu binafsi katika maeneo yao. family therapy: tiba familia: mbinu ya kitabibu inayotumika kuboresha uhusiano na mawasiliano miongoni mwa wanafamilia wanaomhudumia mwenzao mwenye ulemavu au aliye na mahitaji maalumu. family training: mafunzo familia: maelekezo kwa wanafamilia kuhusu mahitaji muhimu ya ustawi wa mwanafamilia mwenye ulemavu. family: familia: watu wote wanaojihusisha na malezi ya muda mrefu ya mtoto au mhusika mwenye ulemavu katika familia. Hawa hujumuisha wazazi, umbu, jamaa na wengine wasio wanaukoo ndani ya kaya na wale walio na mchango wa maana katika maisha ya mhusika na familia yake. febrile seizure: tukutiko homa: ugonjwa unaosababisha homa kupanda ghafla kwa kipindi kifupi ambao sio lazima kuashiria kuwa mhusika ana kifafa. feeling book kitabumpapaso: matini yanayosomwa kwa kugusa kwa mikono (taz. Braille Cells )). feminism: uanauke: nadharia ya kutetea haki za wanawake. fetal alcohol syndrome (FAS): mlimbikodalili wa fetasi athiriko: 1. ashirio la matumizi ya vileo wakati wa ujauzito. 2. mpangilio wa kasoro za viungo na akili ambazo ni matokeo ya moja kwa moja ya

110 mama mjamzito kutumia kilevi au dawa kali za kifafa ambavyo huathiri kiumbe tumboni. Ishara za kitabibu katika hali hii hujumuisha upungufu wa ukuaji kabla na baada ya kuzaliwa, kuwa na wajihi wa kipekee na ogani kuu mwilini kutofanya kazi, matatizo kwenye mfumo mkuu wa neva, kupoteza kumbukumbu, matatizo ya mawasiliano, uoni na usikivu. 3. ujumla wa hali ambazo zinaweza kumtokea mtu ambaye mama yake alitumia kilevi wakati wa ujauzito. Athari hizi zinaweza kujumuisha zile za kimaumbile, za kimwenendo na za kiujifunzaji. Agh. mtu mwenye ashirio hili huwa na mchanganyiko wa matatizo hayo (taz. eugenics ). fetishism: wenzojimai: utumiaji vitu au sanamu kuamsha ashki. fetoscopy: fetoskopi: utaratibu wa kuchunguza mimba au mtoto ambaye hajazaliwa kwa kutumia kamera inayofanana na sindano, ambayo huzamishwa kwenye tumbo la uzazi au mji wa mimba na kuchukua picha za video ili kubaini dalili wazi za kasoro za kijusi. finger spelling: tahajia vidole: kufanya tajihia ya maneno kwa kutumia alfabeti za vidole vya mikono (ishara za mikono 26 na mkao wake ambazo huwakilisha herufi 26 za alfabeti ya kimaandishi). Ni aina ya lugha ishara ambayo kwa kawaida hutumiwa kwa uashiriaji wa mifumo ya Kiingereza na Kimarekani. 92 fits: degedege: mitukutiko ya maungo; mikazo ya nguvu na ghafla ya kundi kubwa la misuli mwilini kutokana na athari katika utendaji kazi wa ubongo. flexibility: ujikunjaji: hali ya kuweza kukunjika. flexikin: fleksini: kifaa kisaidizi katika umbo la mwanasesere kinachotengenezwa kwa mbao laini kwa ajili ya kupimia na kuhimiza maendeleo ya tibamaungo. flight of ideas: mawazo mfululizo: mtiririko wa maongezi yenye kubadilika ghafla kutoka mada moja hadi nyingine, agh. yakiegemea uhusiano unaofahamika, vivuruga vichangamshi au kuchezea maneno. Katika hali ya upevu, matamshi yanaweza kukosa mpangilio na kukosa msimamo. Mawazo mfululizo hujitokeza sana katika hali za mivurugiko mingine ya sikosisi na kwa nadra mjibizo wa sononi kali. floppy: tepetevu: -enye kuwa na misuli legelege sawa na mwanasesere aliyetengenezwa kwa matambara.

111 folic acid: asidi foli: 1. vitamini inayohitajiwa kwa ajili ya mijibizo ya enzaimu fulanifulani. Hii inaweza kusaidia kuzuia kujengeka kwa ugweuti mchomozo kwa wanawake walio katika hatari kubwa. 2. aina ya vitamini ipatikanayo katika majani inayotumika kutibu upungufu wa damu (anemia). food allergies: mzio vyakula: mjibizo ambapo dutu ngeni kama vile aina ya chakula, huchochea mfumo wa kinga. Dalili za kitabibu hujumuisha 1) upumuaji; 2) tumbo na utumbo mdogo; 3) ngozi na 4) nyurolojia. food intolerances: kutovumilia chakula: hali ambayo hutokea kwa kula vyakula ambavyo ni vigumu kumeng enywa; mathalani, vyakula vyenye kambakamba sana, mafuta mengi au vyakula ambavyo haviwezi kugeuzwa kemikali kutokana na ukosefu wa vimeng enya, mf: kutovumilia laktosi. foster care (FC): huduma malezi: uleaji wa muda katika mazingira tofauti na nyumbani kwa mhudumiwa. Huduma zinazotolewa hujumuisha zile za kielimu na kitabibu. freedom of assembly and petition: uhuru wa kukusanyika na kulalamika: hali ambayo agh. hutolewa kikatiba kwa raia ikiwaruhusu kukutanika na kutoa malalamiko. freedom of religion: uhuru wa kuabudu: haki inayomruhusu mtu kuwa na imani au/na kufuata dini au 93 dhehebu analolitaka na kutimiza matakwa yake bila kizuizi ilimradi kwa kufanya hivyo, haingilii imani, utulivu na haki za watu wengine. freedom of opinion: uhuru wa maoni binafsi: haki ya kiraia ya mtu kuwa na maoni; dhamiri au rai kifuani kwake tu bila kumshirikisha mtu mwingine. freedom of expression: haki ya kujieleza: haki ya kiraia ambayo humwezesha mtu kuwashirikisha watu wengine maoni, imani na rai alizo nazo juu ya jambo fulani ilimradi kwa kufanya hivyo asikiuke haki za watu wengine. Mfano, kueneza imani ya kidini au itikadi kwa kuwazuia watu wengine wasieneze imani zao, kuabudu kwa namna yao au kueneza itikadi zao za kisiasa n.k. freedom of the press: haki ya vyombo vya habari: haki ya kiraia ya kutafuta, kupewa, kuandika, kuchapisha na kutangaza au kusambaza habari. frequency: dafaa: utokeaji wa jambo au kitu kwa kujirudia. frotteurism: ashikiwazi: kuamsha hisia za ashiki au mtekenyo kwa kumsuguasugua na kumpapasapapasa mtu asiyeridhia tena hadharani kabisa. Aina ya unyanyasaji kingono. functioning: uamilifu: 1. ufanyaji shughuli za kila siku k.v. kuwasiliana na kuchangamana na wengine, kutunza fedha, 2. kufanya shughuli za ndani na kujiihudumia. 3. ufanyaji

112 kazi wa kawaida wa viungo au wa tishu za mwili. functional academic curriculum: mtaala amilifu wa kielimu: mtaala unaofundisha masuala ya kitaalamu (kusoma, kuhesabu, n.k.) ukiwa na maudhui ambayo kwa kiasi kikubwa yanaendana, na ni muhimu katika maisha ya mtu. functional activities: shughuli amilifu: mambo yanayofanywa kwenye matibabu yanayohusiana ama na utendaji mahususi wa viungo ambao umepotea na mhusika anajifunza upya (k.v. mtu alipoteza kiungo kujifunza jinsi ya kutembelea kisaidia ujongezi au kwa mara ya kwanza (mtu aliyepoteza uoni kujifunza mbinu kabilifu). functional age: rika amilifu: umri ambao mtu anaweza kujishughulisha na kazi mbalimbali kulinganisha na wengine wa umri sawa na wake. functional limitations of comprehension, retention and recall: ukomo amilifu wa ufahamu na kumbukumbu: upungufu wa kiutendaji katika ufahamu, na uwezo mdogo wa kumbukumbu. fundamental freedoms: uhuru wa msingi: hali ya mtu kuwa na uhuru katika kufanya mambo ya muhimu kama vile kuishi, kula, kuvaa, kuoa au kuolewa, kupendwa, n.k. 94

113 Gg gait: mwondoko: namna ambavyo mtu anatembea k.v. kuyumbayumba, kuchechemea,kuguchiaguchia, n.k. gait trainer: kifunza mtembeo: aina ya wenzo unaosaidia katika ujongeaji kwa kutoa mwega mkubwa zaidi kuliko kiunzigemeo. Kimsingi, wenzo huu hutoa mwega wenye kusaidia kubeba uzito na kuweka mikao sawa. Viambata vinavyopachikwa kwenye fremu hutoa mwega usiokuwa na uzito na kuweka mlinganisho wa mkao wima unaowezesha mazoezi ya ujongeaji kuliko viunzigemeo vya aina nyingine; na pia hutoa fursa kwa mtumiaji kusimama na kuhimili uzito katika hali salama kwenye mkao uliohimiliwa. gang rape: kupigwa mande: tukio la kuingiliwa kimwili kwa nguvu na wanaume zaidi ya mmoja. gastrostomy tube (GT): mpira lishia: mpira unaoingizwa tumboni kwa ajili ya kulishia mgonjwa aliyepoteza fahamu au asiyeweza kujilisha mwenyewe. gay: shoga: mwanamume ambaye huridhia kuingiliwa kimwili na 95 mwanamume mwenzie. Hata hivyo, istilahi hii inaweza kutumika kuwaelezea mashoga wa kike na wa kiume. Pia kundi hili hutambuliwa kwa majina mengi k.v. hanithi, msenge, basha, n.k. Kwa hivi sasa baadhi ya wanaharakati watetezi wa haki za binadamu na sheria za nchi kadhaa duniani zinalitambua rasmi kundi hili ndani ya jamii na kuhurusiwa kufunga ndoa za jinsi moja. gender identity and disability: ubainishaji jinsia na ulemavu: hali inayomsababisha mtu mwenye kilema kukabiliwa na changamoto zaidi za utambulisho kwa kuzingatia nafsi yake ilivyo, kipengele cha saikolojiajamii na maumbile. Kwa maana hiyo, mustakabali wake huamuliwa na haiba aliyonayo, jinsi na ujinsia, aina na kiwango cha kilema chake. Hii ni hali inayoweza kumfanya mhusika kukanusha, kuona aibu au kujilaumu. gender identity: ubainishaji kijinsia: mpangilio wa kisaikolojia unaojumuisha namna mtu anavyojinasibisha, jinsi yake kibailojia, uzoefu wa uhusiano na watu wengine, matokeo ya fikira za ndani kuhusu utambulisho na athari za utamaduni wa kijamii. gender perspective: mtazamojinsia: mkabala unaozingatia jinsia. gender role identity: pambanua majukumu kijinsia: hali ya ubainishaji wajibu kwa kuzingatia jinsia.

114 gender role: majukumu jinsia: namna jamii inavyofafanua maana ya kuwa mwanamke au mwanamume. gender: jinsia: 1. majukumu ya kijamii ambayo huaminika kuwahusu wanaume na wanawake katika kundi fulani la kijamii; mathalani, wanaume kama watafuta riziki na wanawake kama walezi wa watoto. Mgawanyo kama huu huasisiwa na jamii na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. 2. hali ya kuwa a kiume na a kike huelezea sifa bainifu ambazo jamii au tamaduni huzipambanua kama za kiume au za kike. Majukumu kijinsia kama mwanamume au mwanamke yanaweza kutofautiana miongoni mwa tamaduni. gene mutation: mabadilikojeni: hali ya mabadiliko yanayojitokeza katika vinasaba ambayo husababisha kiumbe kuzaliwa na maumbile atilifu. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kuhanikiza mabadiliko haya ni matumizi mabaya ya dawa, kemikali, vilevi, uchafuzi wa mazingira, n.k. genealogical: -a kinasaba: -enye uhusiano wa kizazi katika ukoo. generic: -a jumla: -enye uhusiano na kundi la vitu badala ya kimoja. genes: jeni: 1. vinasaba au sehemu za chembeuzi ambazo huamua jinsi tishu za mwili zinavyokua. Mathalani, vinasaba huamua umbile la pua na rangi ya nywele. 2. sehemu ya vinasaba ambayo hurithisha tabia na maumbile ya kiumbe. genetic counselling: unasihi vinasaba: ushauri wa kijenetiki unaohusu mchakato wa kuwataarifu wazazi kuhusu uamuzi wanaotakiwa kuufanyika kuhusu kupata watoto. Agh. mchakato huu hufanyika pale ambapo kuna sababu ya kuamini kuwa hitilafu kwenye vinasaba inaweza kutokea au tayari ipo. genetic counsellor: mnasihi vinasaba: mtaalamu ambaye huwashauri watu wanaofikiria kupata mtoto kuhusu uwezekano wa mtoto atakayezaliwa kuwa na ulemavu kutegemeana na historia ya vinasaba vya wazazi. genetic screening: uchunguzi vinasaba: upimaji unaofanyika kwa lengo la kuchunguza vinasaba vilivyorithiwa kutoka kwa wazazi ambavyo tayari vinahusishwa na maradhi au vina uelekeo huo, vinaweza kusababisa maradhi kwa vizazi vyao au huzalisha tofauti nyinginezo ambazo hazikugundulika kuhusika na maradhi. genital areas: manena: sehemu ya mwili wa binadamu iliyo kati ya tumbo na kinena. genitals or genitalia: via vya uzazi: viungo vinavyohusika na masuala yote ya uzazi. genotype: muundojeni: mpangilio wa jeni wa kiumbe, wa ama, chembeuzi au wa jeni fulani katika sehemu au ogani. lxxvii 96

115 german measles: surua: ugonjwa ambao agh. humpata mtoto unaoambukizwa na virusi ambao husababisha uvimbe wa tezi za limfu na upele au ukurutu mwekunduwaridi kwenye ngozi. gestural systems: mawasiliano ishara: namna ya kuwasiliana kwa kutumia ishara za mwili katika kueleza jambo au hisia k.v. kukunja uso, kubebedua midomo kama ishara ya dharau, na kutikisa mabega kuonyesha kukataa, n.k. gesture: ishara: vitendo vya hiari au visivyohiari vya lugha ya mwili vinavyopeleka ama ujumbe au kuukazia. Mathalani, kubeua, kukonyeza, kung onga, kusonya, kufyonza, n.k. gifted, creative, talented child: mtoto mwenye vipawa: mtoto mwenye uwezo mkubwa wa kuzaliwa nao wa kufanya jambo moja au zaidi kwa ufanisi wa kustaajabisha. Katika muktadha wa Elimu Jumuishi, watoto katika kundi hili pia huchukuliwa kuwa na mahitaji maalumu katika ujifunzaji. global developmental delay (GDD): uchelewaji katika kukua: hali ya mtoto kuchelewa kufanya au kushindwa jambo katika kipindi cha ukuaji, mfano kusogea, kutambua, kuongea, n.k. glaucoma: glaukoma: ugonjwa wa macho unaobainishwa na kuongezeka kupita kiasi kwa presha ya ndani ya jicho ambayo 97 husababisha jicho kuwa gumu, kuchimbika kwa diski ya optiki, kupungua kwa wigo na uwezo wa kuona ambako hatimaye husababisha upofu. lxxviii goal: lengo: 1. tamko la jumla kuhusu jambo ambalo mtu au kikundi cha watu kimedhamiria kulifikia au kulifanya katika kipindi fulani. 2. matokeo yanayotarajiwa katika kurekebisha hali au tabia aliyonayo mtu. goiter rovu: ugonjwa unaosababisha uvimbe kutokana na ukosefu wa madinijoto mwilini. (ang. iodine ). grabbing bars: taz. handrails gripping hooks: ndoano shikizi: kifaa maalumu kinachowekwa agh. kwenye mkono mnemba kumsaidia mhusika kujifanyia baadhi ya shughuli za kawaida na nyepesi. group pressure shinikizo kundi: hali ambapo mtu hushurutishwa na wenzake kundini kutenda jambo

116 ama kinyume na utashi wake au kwa kufuata mkumbo. guardian: mlezi: 1. mtu aliyeteuliwa na mahakama kumlea mtoto sawa na mzazi wake ila halazimiki kuishi na mtoto huyo nyumbani kwake. Katika mamlaka zilizo nyingi, mtu aliye chini ya ulezi (kutokana na maradhi ya akili) huwa chini ya udhibiti kamili wa mtu mwingine katika hadhi ya ulinzi kimwili kama vile kuridhia upasuaji, ufungaji kizazi na masuala ya mikataba ya kifedha. 2. mtu anayewakilisha mtoto au mtu yeyote asiyeruhusiwa kisheria katika kesi. guardianship: ulezi: hali ya uleaji wa mtoto na mtu ambaye hakumzaa mwenyewe agh. kwa amri ya mahakama. Sawa na ilivyo kwa mtoto, katika baadhi ya nchi sheria huruhusu mtu mwenye ulemavu k.v. wa akili kuwa chini ya uangalizi wa mtu mwingine. Pengine hutokea mwangalizi akajitwalia mamlaka ya kufanya kila aina ya uamuzi bila hata kushirikisha upande mwingine unaowakilishwa. guidance: malezi: uleaji wa mtoto kwa mujibu wa utaratibu unaokubalika kijamii. guidance counsellor: mlezi mwelekezi: mtaalamu anayefanya kazi shuleni aliyefunzwa kufanya uchambuzi, tathmini, na kushauri kuhusu taaluma na ajira. guide-advocate: mlezi mtetezi: mtu ambaye hatambuliki kisheria mwenye majukumu ya ulezi na kufanya hivyo ili kukidhi malengo. guide dog: mbwa mwongozaji: mbwa aliyepatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya kumwelekeza mtu asiyeona au kiziwi kwa ajili ya usalama kwa kutahadharisha (taz. assistance animal ). guide: mwongozaji: mtu au mnyama anayeongoza mtu asiye na uoni au usikivu. guinea pig: mjaribiwa: 1. mnyama mithili ya panya mkubwa ambaye hutumika kwenye majaribio mbalimbali ya kitabibu. 2. nungubandia au panyamajaribio au kiumbe chochote ambacho agh. hutumiwa kwa majaribio ya kisayansi. Nyakati fulani hata watu wenye ulemavu hutumika kama wajaribiwa. gym or gymnasium: jimu: chumba au ukumbi maalumu palipo na vifaa kwa ajili ya kufanyia mazoezi ya viungo. Haya huwa maeneo maalumu ndani ya jamuia siyo tu yanayotoa huduma za kufanyia mazoezi ya viungo bali pia burudani na kubarizi. Inafaa huduma hizi zinapokuwa fikivu kwa watu wote hata walio na ulemavu ili kuepuka kuwatenga. 98

117 gynaecology:ginakolojia: utanzu wa utabibu unaohusu magonjwa ya kike, hasa yanayoathiri viungo vya uzazi vya mwanamke.. lxxix gyneacologist: mginakolojia: daktari bingwa wa magonjwa ya viungo vya uzazi vya mwanamke. gynaephobia: jinofobia: hali ya mwanamume kuwa na hulka ya kuwaogopa wanawake kwa sababu za kinyurotiki. (taz. androphobia ). 99

118 Hh habilitation: uimarikaji: 1. mchakato wenye kulenga kumsaidia mtu kupata stadi fulani, uwezo na maarifa mapya. Kwa hiyo ni kutengemanisha kitu au kufanya kitu kitengamae: 2. mchakato wa kufanya mtu awe sawa kama inavyotakiwa, agh. kuhusiana na mafunzo ya stadi mpya, uwezo wa maarifa; mfano, kumfundisha kiziwi asiyeona jinsi ya kutumia msaada wa mnyama, kujua alama mpapaso au mtu asiyeona kutumia kompyuta iliyorekebishwa kwa kuwekewa maunzilaini mahususi (ang. rehabilitation ). haemophilia: hemofilia: ugonjwa wa kurithi wa kutokwa damu, ambapo damu hutoka kwa wingi kufuatia jeraha hata dogo tu. Hali hii hutokea kwa jinsi ya kiume tu japokuwa hurithiwa kwa kupitia kwa mama. lxxx hallucination: halusinesheni: maono au njozi bila kuwa na kichocheo cha nje ya kiungo cha fahamu kinachohusika. Halusienesheni ina hisia za haraka za maono halisi japo katika baadhi ya mazingira kichocheo cha halusinesheni kinaweza kudhaniwa kuwa mwilini, mathalani, halusineshaeni ya kusikia sauti inayotokea kana kwamba iko ndani ya kichwa badala ya kupitia masikioni. Halusinesheni lazima itofautishwe na ilusheni au maluweluwe ambayo kichocheo cha nje hakipokelewi au hakifasiliwi na kutoka katika michakato ya kawaida 100 ya mawazo ambayo ni uhalisia wa kipekee au maalumu. Hali ya kuwa na njozi za muda mfupi ni suala la kawaida kwa mtu asiye na ulemavu wa akili handedness: mashoto: upendeleo wa kutumia ama mkono wa kushoto kwa shughuli kama vile kuandika, kula, au kunywa. handicapped or handicapper: kilema maskini: maana ashirifu ya kisawe chenyewe ni hasi kwa kumbukizi ya zama zile ambapo watu wa aina hii huko Ulaya walioishi kwa kuomba mitaani huku wakishikilia kofia mikononi kama ishara ya uhitaji wa msaada kwa njia ya kiungwana. handrails: kingogemeo: fito nyembamba (za chuma au mbao) zilizotengenezwa kwa ajili ya kushikiliwa kwa mkono ili kujiimarisha au/na kumkinga mtu asidondoke na kujeruhiwa. Kwa kawaida hutumika wakati wa kupanda au kushuka ngazi ndefu au za ghorofa na vipandishio. Matumizi mengine ni pamoja na fito za kukamata bafuni ambazo husaidia ama kuzuia kuangushwa katika sakafu zenye utelezi au kurahisisha matumizi kwa mtu mwenye ulemavu.

119 haptic: hisiamguso: taarifa zinazopelekwa kupitia misogeo ya mwilini au/na uelekeo. Mawasiliano ya aina hii ndiyo hasa hutumiwa na wenye uziwipofu. harassment: bughudha: hali ya kumtweza mtu mwenye ulemavu ama kwa kumjengea mazingira ya kumdhalilisha au kumchokoza. Matendo yanaweza kuhusisha: maandishi au matamshi ya matusi; kuchorwa na kuandikwa kwenye kuta, ishara za viungo au sura, maigizo, utani na mizaha. hard of hearing: usikivu hafifu: 1. hali inayompata mtu ambaye kwa namna fulani alipoteza kiasi cha usikivu, ila anayeweza kuwasiliana kwa kuongea, ama kwa kusikia angalau mawasiliano ya kawaida ya simu. Wengi wa watu wenye usikivu hafifu hutumia shimesikio. 2. dhana inayotumika kumpambanua mtu ambaye ana kilema cha usikivu cha kudumu au kinachobadilikabadilika ambaye anaweza kuwasiliana kwa kuongea akiwa na au bila shimesikio.(linganisha na hare lip: mdomo sungura**taz. simple cleft lip, double cleft lips, cleft palate. health disorder: mvurugiko kiafya: hali au maradhi ambayo huathiri utendaji wa mtu ila siyo lazima yaaathiri uwezo wake wa kujongea. health nutrition: lishesiha: mlo au chakula chenye virutubisho vya kujenga afya. Lishe ya aina hii haipaswi kuwa na athari fuasi kama 101 vile utibwatibwa, kisukari n.k. ambazo ni aina za ulemavu pia. hearing impaired: mwenye kilema cha uziwi: mtu aliyepoteza kiasi cha uwezo wa kusikia ambapo huhitaji usaidizi (mathalani wa shimesikio) au urekebifu wa shughuli k.v. kielimu. Istilahi hii hujumuisha mtu mwenye usikivu hafifu na yule kiziwi kabisa (ang. deaf ). hearing impairment: kilema cha uziwi: hali ya mtu kupoteza kiasi cha uwezo wa kusikia ambapo huhitaji usaidizi wa shimesikio. Istilahi hii kwa namna fulani hukanganya miongoni mwa jamii ya viziwi ambao hupendelea msemo wa usikivu hafifu au kiziwi. Hali hii huathiri ufanisi wa mtu kielimu, kitaaluma, na/au kijamii. Upotevu wa usikivu hutabakishwa kutegemeana na kiwango cha dafaa ndani ya umbali ambao mtu kusikia. Dafaa hizi huitwa desibeli au db. Mtu hufikiriwa kuwa na usikivu wa kawaida endapo kilele cha usikivu kinapindukia mfiko wa 25 db. Uziwi huainishwa kama ifuatavyo: kidogo: ni ndani ya db 25 hadi 40 (nyakati zingine anaweza kushindwa kufuatilia maongezi vizuri hasa kama kuna kelelekelele); wastani ni ndani ya db 55 na 70 (anaweza kushindwa kufuatilia maongezi bila shimesikio); kali au juu ni ndani ya ndani ya db (ambapo huhitaji kusoma midomo au kutumia lugha ishara hata kama ana shimesikio); juu

120 kabisa ni pale db zinapopindukia 90 (ambapo hutakiwa kusoma midomo au kutumia lugha ishara). hearing aid: shimesikio: kifaa cha kielektroni ambacho hukuza mawimbi ya sauti kwa ajili ya mtu mwenye usikivu hafifu. hemiplegia: hemiplejia: kupooza upande mmoja wa mwili (mkono na mguu wa upande mmoja). hemorrhoids: bawasiri: 1. uvimbe mdogo kandokando au ndani ya njia ya haja kubwa. hepatitis: homa ya manjano: ugonjwa wa ini unaosababishwa na virusi, bakteria, pombekali, au sumu ambapo agh. huambatana na homa kali.(ang. jaundice ) heterotopic ossification ugumu wa kutofautisha vitu: hali ya mtu kushindwa kupambanua vitu. high moral standards: uadilifu wa hali ya juu: hulka na tabia ya mtu kujiepusha na matendo yanayopingana ama na sharia au taratibu za nchi na jumuia hususani kuzingatia haki na matendo mema. 102 holistic: -a utukufu: -enye hisia za kimiujiza au, uwezo wa kiungu na kiimani. home remedies: tiba asili: matibabu au dawa za asili zinazotumika bila kuchanganya na kemikali na ambazo kwa kawaida taaluma yake ni ya kurithishana. home-based services: huduma majumbani: afua zinazotolewa kwa watu ambapo mtoa huduma k.v. mwalimu, mnasihi, mshauri au tabibu humfuata mlengwa mara kwa mara nyumbani mwake au sehemu nyingine tulivu, mathalani, kituo cha malezi ya kutwa ili kutoa huduma inayotakiwa. Shughuli zote hufanyikia majumbani na wahusika binafsi wanakuwa na muda wa faragha na mwalimu au mtaalamu anayehusika. Ziara hizi huwasaidia wanafamilia kuinua kiwango cha uwezo wa kuboresha mazingira ya mwanafamilia mwenye mahitaji maalumu. Agh. hudumu hizi hutolewa ndani ya saa moja na zinaweza kufanyika mara nyingi, mathalani, kila siku au mara moja kwa mwezi kulingana na wingi wa watumishi, idadi ya familia zinazohudumiwa na umbali ambao mwezeshaji anapaswa kusafiri kuzifikia familia. homemaker: mtunza familia: mtu mzima ambaye anajitolea kutunza nyumba na familia bila malipo. homosexual age: umribasha: umri kati ya miaka 6-10 ambao mtoto

121 huvutiwa na jinsi yake. Mtoto wa kiume hupendelea kuwa na wavulana wenzake au baba yake na binti hujinasibisha na jinsi yake kwa maana ya dada au mama yake. Iwapo uangalizi makini haukuchukuliwa, mtoto huweza kuathirika na kuishia kuwa basha. hormones: homoni: 1. kemikali ambazo mwili huzitengeneza ili kuuarifu jinsi na wakati wa kukua. Estrojeni na projestojeni ndizo homoni muhimu kabisa kwa wanawake. 2. kemikali za mwili zinazotengenezwa na tezi za endokrini; ambazo hufanya kazi mbalimbali katika viungo vya mwili. lxxxi 3. kemikali iliyomo kwenye mimea na wanyama ambayo ikichukuliwa kutoka sehemu ilipotengenezwa hadi sehemu nyingine ya mwili, huleta mabadiliko makubwa sana, au marekebisho katika sehemu hiyo. human computer interaction (HCI): uathiriani wa kompyuta ana binadamu: utafiti wa kiusanifu na utumiaji teknolojia ya kompyuta ambao hujikita hasahasa kwenye mwingiliano baina ya watumiaji na kompyuta. Watafiti kwenye uga huu huchunguza njia ambayo binadamu hutendana na kompyuta na kusanifu teknolijia ambazo huwawezesha binadamu kutfanya hivyo kwenye kompyuta kwa namna vutivu zaidi. human assistance: msaada wa binadamu: kundi la wasaidizi kwa watu wenye ulemavu kulingana na 103 mahitaji yao. Mathalani, asiyeona huhitaji kusindikizwa kwenye mizunguko yake au/na kusomewa kama ni mwanafunzi au mwajiriwa ambaye bado hajaimudu teknolojia saidizi; mtu mwenye ulemavu wa mjongeo mwenye kuhitaji kusogezewa vitu au kuongezewa nguvu pale anapotumia wenzo kama kitimwendo au baiskeli visivyo vya moto; kiziwi na mwenye uziwipofu huhitaji wakalimani wa lugha ishara na mpapaso, n.k. human immunodeficiency virus (HIV): upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI): maradhi ambayo hutokana na kudhoofu kwa kingamwili baada ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI. Virusi hivi huenezwa kwa ngono zembe, ulawiti, damu (damu yenye maambukizo ya virus)i, sindano na vifaa vyenye ncha kali visivyotakaswa baada ya kutumiwa) na uambukizo wa mtoto kutoka kwa mama wakati wa ujauzito. UKIMWI huhusishwa na ulemavu kwa vigezo kuwa, katika hatua zake za kupea, (UKIMWI) huathiri kiwango cha mhusika cha utendaji kazi. Halikadhalika, mwenye kuishi na hali hii agh. hutengwa na kuchukuliwa kuwa adui wa jamii. human rights: haki za binadamu: haki za binadamu chimbuko lake ni mahitaji ya binadamu. Haki hizi huchagiza kwamba kila mtu ana stahili sawa siyo kwa kuishi tu, bali

122 kuishi kwa heshima. Haki za binadamu pia hutambua kwamba ni sharti mambo fulani ya msingi na rasilimali viwepo ili kuishi maisha yenye staha. Haki za biadamu zina sifa muhimu zinazozipambanua na dhana au kanuni nyingine: ni za kiulimwengu yaani zinamhusu kila binadamu popote alipo duniani kwa misingi ya usawa na bila ubaguzi kwa yeyote. Sharti pekee la kuzipata haki hizo ni kuwa binadamu; ni za asili - hali halisi ya mtu alivyo; haziachanishwi - yaani ni za mhusika moja kwa moja. Binadamu yeyote awaye na awavyo, hahitaji kupokea haki zake kutoka kwa watu au kwa serikali yake ama mamlaka nyingine iwayo, na wala kamwe haziwezi kupokonywa ila zinaweza kukandamizwa tu; hazigawanyiki- haziwezi kutenganishwa kati ya haki moja na nyingine; hutegemeana-haiwezekani kunufaika na haki moja bila nyingine kuwepo na huhusiana haki moja huathiriana na nyingine. human rights model: kielelezo cha haki za binadamu: mfumo unaolenga maendeleo ya jamii yenye kumakinika katika haki jumuishi na ikiheshimu uanuwai, usawa na ushiriki wa wote. Mfumo huu unatekelezeka kwa kutambua uanuwai na upekee wa mtu mwenye ulemavu na stahiki zake za kupewa fursa sawa ili kunufaika kikamilifu na vipawa vyake kiuchumi na haki zake za binadamu. hydrocephalus or big head: hidrosifelasi: 104 hali ya kuwa na maji zaidi ya wastani ndani ya ubongo kwa kushindwa kutiririka kawaida kwenye uti wa ubongo, na hivyo hujikusanya na kuweka shinikizo kwenye ubongo na mifupa ya kichwa. Hali hii isiporekebishwa mapema iwezekanavyo kwa njia ya upasuaji, husababisha upofu, udumavu wa akili, mitukutiko na mpoozo wa ubongo. Hidrosifelasi inaweza kuwa ya kurithi, kusababishwa na vipengele changamani mbalimbali vya kimazingira kama vile ugweuti mchomozo, uvujaji wa damu ndani ya ventrikali, majeraha ya kichwa, homa ya uti wa ubongo, uvimbe na nziba (kifuko cha kimembreni chenye kioevu ndani). Ni kawaida kwa mtu mwenye hidrosiferasi kupatwa na vilema vingine k.v. kile cha afya ya akili, maungo na matatizo mchanganyiko ya kiafya. Kwa mtu mwenye umri mdogo, hali hii husababisha kichwa kupanuka kuliko kawaida ila kwa mtu mzima ukubwa wa kichwa hubakia uleule wa wastani licha ya kwamba

123 anaweza kuwa na tatizo hilo. Kwa mazingatio haya, ni upotoshaji hidrosifalasi kutafsiriwa kama kichwa kikubwa. Pia kichwamaji japo ndicho kisawe sahihi, matumizi yaliyozoeleka ni tofauti kwa kubeba maana ashirifu ya kiburi. hydrocele: ngirimaji: ugonjwa unaosababishwa na mkusanyiko wa kioevu ndani ya kifuko cha pumbu na hivyo kusababisha uvimbe. Mtu anaweza kupatwa na hali hii wakati wowote maishani ila inaweza kuzuilika kwa afua zilezile za matende na kutibika kwa njia ya upasuaji. Pale hali hii isipotibiwa huwa ni kilema kwa kusababisha pamoja na mengine: mzigo ndani ya jamii, kuathirika kiuchumi na kisaikolojia, kupoteza uwezo wa kujamiiana na hivyo kuziba fursa za kuoa na kuleteleza ugumu mwingineo wa kimaumbile. Pia hujulikana kama tende la kifukokorodani. hygiene: elimusiha: maarifa na ufahamu kuhusiana na utunzaji wa afya na namna ya kuepuka maradhi. Ufahamu huu ni muhimu sana katika uga wa ulemavu. Aina na kiwango cha ulemavu, hali ya uchumi, n.k. huathiri pia kiwango 105 cha usafi binafsi, mazingira ya kuishi na usalama wa mhusika kiafya. Kupungua kwa kiwango cha usafi humaanisha kubeba uzito wa maradhi ambayo baadhi yake huzidisha kiwango cha ulemavu, kusababisha aina nyingine za vilema, mateso na hata kutishia uhai wenyewe. hyaline: hailini: dutu inayofanana na kioo kisichokuwa na mng aro. lxxxii hyperacousis: hiparakusisi: 1. hali ambayo hujitokeza kutokana na tatizo la jinsi ubongokati unaochakata usikivu na kutafsiri sauti ambapo sauti ya kawaida hutafsiriwa kama sauti kali (kelele). Hali hii inaweza kusababisha maumivu na kero. Mtu mwenye hiparakusisi hushindwa kuvumilia sauti za kila siku ambazo hata si za juu kwa watu baki; k.v. kelele za maji kutoka bombani, kupanda gari, kukanyaga majani makavu, mashine ya kuosha vyombo, feni ya jokofu, kupanguapangua makaratasi, n.k. Japo sauti zote zinaweza kuonekana kama za juu, zile zenye dafaa ya juu zinaweza kuudhi kwa hali ya kipekee. 2. hali ya kusikia zaidi kuliko kawaida. lxxxiii hyperactivity: ujishughulishaji: 1. hali ya mtu agh. mtoto kufanya

124 mambo mengi bila kutulia/mashughuli 2. kuongezeka katika utendaji, utendaji wa kupita kiwango. lxxxiv hyperlexia: hipaleksia: hali ya mtoto kupenda herufi au tarakimu kupindukia au kumudu kusoma vizuri kuliko uwezo wake kiumri. Pamoja na hayo, mtu mwenye hipaleksia anaweza kuwa na shida ya kuelewa lugha ya mazungumzo, kuchangamana, na kuchangamkiana na wengine. hyperopia, or farsightedness: hiparopia: tatizo la kutoweza kuona vitu vilivyopo karibu. Mtu mwenye tatizo hili huweza kuona vizuri kabisa vitu vilivyo mbali naye, lakini hukabiliwa na ugumu wa kutoona vile vilivyo karibu naye. Dalili za hiparopia: kuhisi maumivu ya kichwa, kupepesa macho na kusikia uchovu anapofanyia kazi vitu vilivyo karibu. Dalili hizi zinaweza hata kumtokea mtu mwenye kutumia miwani na hivyo kuhitaji kupimwa upya. Tatizo hili hutokea pale miali ya mwanga inayoingia jichoni hukutanikia nyuma ya retina badala ya kwenye retina yenyewe moja kwa moja. hypertonia: hipatonia: 1. hali ya kuongezeka kwa ukakamavu wa misuli na kupungua kwa uwezo wa misuli kujinyoosha. Hali hii inaweza kusababishwa na 106 kujeruhiwa, maradhi, au hali ambazo zinahusisha kudhurika kwa mfumo mkuu wa neva kama vile, mpoozo wa ubongo. 2. kuongezeka kupita kiasi kwa toni ya misuli. lxxxv hypochondriasis: hofu siha: hali ya wasiwasi unaompata mtu kwa kudhani ana ugonjwa fulani ilhali si mgonjwa. hypoxia: hipoksia (ang. asphyxia ). hysteria: mpagao:** hali ya kufurahi, kuogopa au kuchukia kupita kiasi kunakosababishwa na mtu kushindwa kuzima hisia zake na kuanza kulia au kucheka. Agh. huwatokea vijana wa kike na hivyo istilahi yenyewe hutumika kiudhalilishaji hasa pale mhusika mwanamke anapodai jambo kwa hisia. Pia huitwa umanyeto**.

125 Ii idea of reference: wazo rejezi: jambo la kushikiliwa sana kuliko udanganyifu, matukio ya kubuni, vitu au watu wengine walioko kwenye mazingira ya karibu ya mtu aliye na dhana maalumu na isiyo ya kawaida hususani kwake. idealization: ujikwezaji: hali ya mtu mwenyewe kujiona bora kuliko wengine. identical twins: pacha mrandano: watoto wawili au zaidi waliozaliwa kutokana na yai moja lililotungwa ndani ya mfuko wa uzazi mmoja. Pacha wa aina hii wanakuwa wa jinsi moja na agh. hufanana sana. identification: utambuzi: mchakato wa kumbaini na kumtambua mtu anayehitaji huduma maalumu. identity disorder: mvurugiko tambuzi: hali ya kujitesa au kujihuzunisha kunakosababishwa na kijana balehe kutojitambua. identity: utambulisho: hali ya kuwa na hisia binafsi zinazomfanya mtu ajitambue na hivyo kumjengea haiba. Hali hii ni kinyume cha uelewa wa mtu binafsi kung amua yeye ni nani, anapaswa kufanya nini, kwa sababu gani na katika muktadha upi. Kushamiri kwake husababisha mvurugiko wa kimwili na kiutambuzi. idiosyncrasy: upekee: 1. hali ya mwenendo wa mtu kufikiri au kujihisi kwamba ni tofauti na mtu au kundi jingine hususani katika mambo ya 107 kawaida. 2. dalili fulani ya kiakili au ya mwili ambayo ni pekee kwa mtu husika. lxxxvi 3. matokeo ya kipekee ya dawa au chakula fulani kwa mtu fulani. idiot (also see embicile): zezeta:** mtu mwenye matatizo ya akili au kiwango kidogo cha uelewa. Istilahi hii ina mtazamo wa kitabibu na kihisani hata kidini ambapo uarifu kuhusu kilema hiki hutolewa bila kujali hisia za mhusika mwenyewe. Kwa hiyo, halitakiwi kutumika kwenye utaarifu wowote uwe rasimi au usio rasimi. illogical thinking: ufikiriaji usiomantiki: hali ya kuwaza au kufikiri bila kuwa na mpangilio maalumu (kiasi cha kufikia hitimisho lisilo sahihi) unaoweza kusababishwa na mtu kuchanganyikiwa, kuwa na imani potofu au kuchoka. Hali ikizoeleka kwa kujirudiarudia husababisha matatizo ya afya ya akili. illusion: maluweluwe: hali ya kuwa na fikira zisizo sahihi kuhusu jambo fulani. Mathalani, mchakacho wa majani husikika kama sauti za binadamu; mwanamume anayejiangalia kwenye kioo na kuona sura yake imesawajika na kuumbika vibaya. imbecile (also see idiot): punguani:** mtu mwenye matatizo ya akili au kiwango kidogo cha uelewa. Maana ashirifu ya istilahi hii, inakuwa na mtazamo wa kitabibu na kihisani hata kidini ambapo uarifu juu ya kilema hiki hutolewa bila kujali hisia

126 za mhusika mwenyewe pia hufafanuliwa kwa maneno pumbavu**, bozi**, zembe.** imitate: iga: rudia kile kilichofanywa au kutamkwa na mtu mwingine. immaturity: kutopevuka: mvurugiko wa mwenendo unaohusisha kujishughulisha na jambo kwa kipindi kifupi pasipo kuwa makini, ubwete, ndoto za mchana, kuwa goigoi na mienendo mingine isiyoendana na matarajio ya ukuaji. immediate family member: mwanafamilia wa karibu: mke au mume, watoto, mama, baba au mama mkwe, kaka, dada, watoto wa kufikia au wazazi wa mtu wa kufikia. Hawa ni muhimu kuhusiana na matakwa ya huduma za matunzo ya mtu mwenye ulemavu nyumbani badala ya kumpeleka kwenye makazi maalumu. immunisations: uchanjaji: kuingiza dawa maalumu mwilini ili kumkinga mtu hasa mtoto dhidi ya maradhi ya utotoni kama vile: dondakoo, pepopunda, kifaduro, polio, tetekuwanga, matubwitubwi, surua na ugonjwa wa hemofilisi B. immunosuppressive drugs: ushinikizo kingamwili: 1. dawa zinazouzuia mwili kukataa ogani pandikizi. 2. upunguzaji wa kinga za mwili ili kuruhusu upandikizaji wa ogani unaofanyika kwa kutumia kemikali au njia za kiserojia. immunotherapy: kingatiba: matibabu yanayosaidia kuzuia ugonjwa mwilini 108 kwa njia ya kuchanjwa; mathalani, chanjo dhidi ya homa ya manjano, n.k. impact assessment: tathmini athari: upimaji wa matokeo ya utekelezaji wa jambo fulani. impairment: kilema: hali ya kiungo, sehemu yake au mlango wa fahamu kwenye mwili wa binadamu ama kukosekana, kilichopo kuwa na hitilafu au kutofanya kazi kwa kiwango kinachochukuliwa kuwa cha kawaida. Hali hii inaweza kumpata mtu kabla, wakati au baada ya kuzaliwa. Hata hivyo, ni makosa kuhusisha hitilafu hii na utendaji wa mwili mzima na pengine hadhi ya mhusika. (Linganisha na ulemavu). impartial authority: mamlaka adilifu: uamuzi usiopendelea upande wowote kati ya zile zinazokinzana. implementation and monitoring: utekelezaji na ufuatiliaji: hali ya kufanya jambo lililopangwa kwa kuzingatia mpango uliopitishwa na wahusika wote halafu, hatua kwa hatua kujiridhisha kuwa kila kitu kinazingatiwa kwa kukagua mara kwa mara ama kwa kutembelea au/na kuchambua taarifa zake. impulse control disorders: mivurugiko dhibiti msukumo: hali ya kushindwa kuhimili msukumo, shinikizo, kishawishi cha kutenda jambo lenye madhara kwa wengine. impulse: msukumo: 1. nguvu fulani ya muda mfupi. 2. hisia ya ghafla

127 kwenye mawazo inayomsukuma mtu kutenda jambo fulani. impulsivity: ukurupukiaji: utendaji au uongeaji wa haraka unaotokana na msukumo bila kutafakari kwanza matokeo au athari zake. in utero: ndani ya uterasi: dhana inayoelezea ukuaji wa mtoto kwenye mji wa mimba au kabla ya kuzaliwa kwa kujielekeza kwenye hitilafu au ajali ambazo hutokea wakati wa ukuaji wa kijusi k.v maambukizo kwenye mji wa uzazi. inaccessibility: mkingamoufikivu: hali ya kushindwa kufikia maeneo au taarifa kutokana na uwepo wa vizuizi vya kimazingira na kimtazamo. incidence: matukio: idadi ya visa vipya vya hali fulani ambayo imebainishwa kwenye kipindi maalumu k.v. majuma, miezi, mwaka, n.k. vikilinganishwa na vipindi vilivyotangulia. Mathalani, maambukizo mapya ya virusi vya UKIMWI. Pia huu ni utaratibu unaotumika sana kwenye ulinganishaji wa idadi za watu wenye ulemavu kati ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea 109 kiviwanda. Tafiti zinathibitisha kuwa visa vya kupatwa na ulemavu ni vingi katika nchi zinazoendelea kuliko zile zilizoendelea. Hata hivyo, kutokana na viwango vya ubora na upatikanaji wa huduma, idadi ya watu wenye ulemavu ni ndogo katika nchi zinazoendelea (kutokana na kiwango cha juu cha vima vya vifo) wakati idadi hiyo ni kubwa kwenye nchi zilizoendelea. inclusion: ujumuishaji: dhana ya utetezi kwamba: panahitajika mgeuzo wa kiutamaduni na mhamo wa ruwaza ambapo kila mtu (ikiwa ni pamoja na mwenye ulemavu) anahusishwa kwa hiari, kwa uwazi (na siyo kwa kuonewa huruma), katika kukabiliana na vikwazo vya aina yoyote dhidi yake pale anapohitaji kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kiutamaduni, n.k. inclusive education (IE): elimu jumuishi (EJ): mfumo wa utoaji fursa za elimu kwa pamoja ambapo watoto wote, vijana na watu wazima hujiunga, kushiriki kikamilifu na kufanikiwa katika shule za kawaida na mipango mingine ya elimu bila kujali tofauti zao kitabaka na kiuwezo, kwa kupunguza vizuizi na kuongeza rasilimali. Hata hivyo, mfumo huu huhusisha mlolongo mpana wa mikakati, kanuni na michakato inayojaribu kufikia uhalisia wa haki ya kiulimwengu ya usawa, elimu

128 husika na yenye kumfaa kila mtoto katika mazingira yenye mikingamo michache kabisa. Elimu Jumuishi imejiegemeza kwenye mfumo wa maadili na imani ambao kitovu chake ni masilahi maridhawa ya mwanafunzi yanayokuza mshikamano wa kijumuia, hisia za kuwa sehemu ya kushiriki kikamilifu katika ujifunzaji, na mchangamano chanya na wanarika na wanajumuia wengine. Inatambua kuwa ujifunzaji huendelea kwa maisha yote ikiwa ni pamoja na ujifunzaji nyumbani, kwenye familia, kwenye jumuia na katika mazingira rasmi na yasiyokwa rasmi. Inatafuta kuziwezesha jumuia, mifumo na miundo katika kila utamaduni na aina mbalimbali za muktadha kupambana dhidi ya ubaguzi, ukumbatiaji wa tofauti, na kuendeleza ushiriki kwa kuondoa vizuizi dhi ya ujufuzaji na ushiriki wa kila mtoto. Mfumo huu wa elimu ni sehemu ya mkakati mpana wa kukuza ustawi wa jamii jumuishi yenye lengo la kujenga dunia ambamo kuna amani, utulivu, utumiaji endelevu wa rasilimali, haki za kijamii na ambamo mahitaji ya msingi na haki za wote huzingatiwa. lxxxvii inclusive education system: mfumo wa elimu jumuishi: utaratibu ambao huandaliwa kwa kutazama mbele kwamba ama ndani ya jamii wamo au watakuwemo, watu wenye 110 matabaka na uwezo anuwai, na hivyo hujipanga kabla jinsi ya kukabiliana na mahitaji ya kila aliyepo na atakayekuja baadaye ili wote washiriki kwenye michakato ya kielimu bila kubaguliwa, lakini kwa kuzingatia mahitaji mahususi na hatimaye wote kunufaika. Mkabala wa sera ikibali, upambanuaji na ukondoishaji ni baadhi tu ya mikabala ya ujumuishaji. incompetency: kukosa umilisi: hali ya kutokuwa na uwezo, maarifa, siha, sifa kisheria, kiasi cha kutosha kumstahilisha mtu kuridhia jambo, kuingia mkataba au kusimamia miamala ya kibenki. incontinence: ufukunyungu: hali isiyo hiari ya kushindwa kudhibiti utokaji wa takamwili hasa haja ndogo na kubwa inayosababishwa na athari za kuumia uti wa ubongo au kuwa na ugweutimchomozo. Taz enuresis. independence: kujitegemea: kiwango ambacho mtu mwenye ulemavu hususani ule wa ukuaji anachoweza kujidhibiti na kujiamulia mustakabali wa maisha yake. independent living: kuishi kwa kujitegemea: dhana ya mtu mwenye ulemavu kuishi katika jamii kwa kujitegemea ilimradi apatiwe huduma zile zinazotolewa kwa umma pamoja na zile mahususi kulingana na aina na kiwango cha ulemavu. Hii ni kwa kuendana na imani kwamba mtu

129 mwenye ulemavu ana haki na wajibu sawa na watu wengine ndani ya jumuia. Hivyo basi, huduma zinazotolewa kwa umma sharti zimfikie na mifumo ya utegemezaji ipatikane ili kumsaidia kuishi ndani ya jumuiai na kuendesha maisha yake kwa kujitegemea (kwa kadiri inavyowezekana). individual supports measures: hatua za utoaji mwega binafsi: upatikanaji wa huduma za utengemalishaji na usaidizi mwingine ambao humwezesha mtu mwenye ulemavu kujitegemea, kuzalisha na kuchangamana kwenye jumuia. Hatua hizi hukidhi yafutavyo: i) kumwezesha mtu mwenye ulemavu kuyadhibiti mazingira yake kimaisha kwa kadiri inavyowezekana; ii) kuzuia kuwekwa kwenye taratibu nyingine za kuishi ambazo zinabana zaidi kuliko inavyolazimu; na iii) kumwezesha mtu kuishi, kujifunza, kufanya kazi na kufurahia maisha ya kijumuia. Uwezeshaji binafsi unajumuisha huduma za usaidizi binafsi, teknolojia saidizi, marekebisho ya vyombo vya usafiri na makazi, utegemezaji sehemu za kazi na kwenye usafiri. individualised educational programme (IEP): programu binafsi ya elimu: mpango ulioandaliwa kimaandishi na timu ya wataalamu k.v. walimu na 111 mabingwa wa tibamaungo, pamoja na wazazi kwa kumlenga mtoto mwenye ulemavu aliyefikia umri wa kwenda shule. Mpango huu hujikita katika tathmini ya vipengele mbalimbali kuhusu mtoto, mathalani, jinsi mtoto anavyojifunza kwa wakati huo, mahitaji ya kiujifunzaji, na huduma anazozihitaji na hudurusiwa na kuboreshwa kila mwaka. individualised family service plan (IFSP): mpango mwega kwa familia: utaratibu wa usaidizi kwa mtoto anayestahili kuupata tangu kuzaliwa hadi miaka miwili na familia yake. Utaratibu wa huduma za familia mojamoja unapaswa kuwa na: maelezo kuhusu kiwango cha ukuaji wa mtoto; uimara wake na mahitaji, uimara wa familia na mahitaji, matokeo makuu ya utaratibu, maelezo ya afua mahususi na mfumo wa utoaji wake ili kuyafikia malengo, maelezo ya mazingira asilia, jina la mratibu huduma, tarehe ya kuanzisha huduma na muda wa kukoma utoaji wake, tarehe za kutathmini mpango unaoishia na afua za mpito. industrial deafness: uziwi kazini: hali ya kupoteza uwezo wa kusikia kutokana na kuwa kwenye mazingira yenye makelele k.v. viwandani kwa muda mrefu. industrial disease: maradhi kazini: kuugua kunakosababishwa na

130 mazingira ya sehemu ya kazi k.v. kuvuta hewa yenye vumbi kila wakati, ukosefu wa usalama kiasi cha kusababisha ajali, n.k. industrial technology: tekinolojia kazini: mchakato wa mpango wa kina wa elimu wenye lengo la kuendeleza jumuia iliyo na maarifa kuhusu teknolojia, mabadiliko ya mifumo yake, mbinu, matumizi yake kazini na tasnia nyinginezo na umuhimu wake kijumuia na kiutamaduni. infant developmental stimulation: uchocheaji ukuaji wa mtoto mchanga: utaratibu wa msaada wa awali unaosisitizwa kwa mtoto mchanga kama vile vichocheo vya uoni, usikivu na viungo ili kusaidia ukuaji. Uchocheaji wa ukuaji wa mtoto mchanga husababisha mabadiliko kwenye maumbile, fikira/mawazo, au mwenendo wa mtoto mchanga unaoathiriwa kibiolojia na kimazingira (taz. early stimulation ). infant formula: maziwa ya watoto wachanga: maziwa ya yanayotengenezwa viwandani na kufungashwa kwenye makopo au mifuko kwa ajili hasa ya mtoto mdogo. Maziwa haya hutumika badala ya kunyonyeshwa titi la mama na vibadala vinginevyo vyenye lishe au manufaa ya kiafya kama yale ya asili. Kwa kutokuwa na virutubisho vya kutosha, na pengine kuwa na viambata 112 visivyofaa, maziwa haya yamekuwa chanzo cha baadhi ya maradhi na vilema kwa watoto. infantile psychosis: saikosisi ya utotoni: mvurugiko unaojitokeza kwenye umri mdogo ukijidhihirisha kwa kushindwa kuwasiliana, kutokuwa na uwezo wa kufanya mawasiliano, kujitenga na michangamano ya kijumuia, kutowiana kwa utendaji wa hisia na akili, pamoja na upishanaji kwenye ujongeaji, uoni, jumuia na mienendo rekebishi (ang. autism ). infantile spasms: degedege: mitukutiko inayowakumba mtoto mchanga mwenye umri wa miezi mitatu hadi miaka miwili inayodhihirishwa na kukakamaa kwa misuli ya mikono, miguu na kichwa. infantile: -a ukembe:- enye kuhusiana mtoto mchanga. infection: maambukizo: upataji wa vimelea vya magonjwa vinavyosababishwa na bakteria, virusi na viumbe vingine. Maambukizo huweza kuathiri sehemu ya mwili au mwili mzima. inference: hitimisho (mantiki makini): hali ya kutoa uamuzi kutokana na taarifa ulizonazo. inferiority complex: udhalili: hali ya kuwa na hisia za unyonge. inflammation: uvimbe uchungu: uvimbe wa mwili unaojibainisha kwa rangi nyekundi na kupwita.

131 information symbol: alama taarifu: bidhaa yenye thamani zaidi katika jamii ya kisasa ni habari. Kwa mtu mwenye ulemavu habari ni jambo la lazima. Mathalani, ishara inaweza kutumika kwenye mbao za maelekezo au kwenye mpangilio wa ukumbi kwa kuashiria mahali taarifa zinakopatikana au dawati la maelezo au usalama, mahali penye taarifa maalumu au matini yanayohusu masuala ya ufikivu na huduma kama vile maandishi yaliyokuzwa, maelekezo yaliyorekodiwa kwenye kaseti, au utalii wenye ukalimani wa lugha ishara. informed consent: ridhaa arifu: idhini ya kuridhia michakato ya tiba au tafiti ikiwa ni pamoja na uelewa wa: i) mchakato utakavyokuwa, ii) hatari zinazoweza kujitokeza, iii) manufaa yanayotarajiwa, iv) athari za kutoridhia, v) uwezekano wa njia mbadala, na v) uridhiwaji wa hiari. inherent dignity: hadhi sawa ya kuzaliwa: hali ambapo kila binadamu anazaliwa akiwa na hadhi sawa na wengine pasipo kujali umbilie, mbari au mazingira anamozaliwa. Hata hivyo, mifumo ya kijamii, imeupotosha ukweli huu kwa kuendekeza kuwa baadhi ya nasaba, rangi, na maumbile fulanifulani ndiyo yenye hadhi ya kuzaliwa nayo (k.m. katika koo za 113 kiflame, kitemi, watu weupe, n.k.). Wengine hadhi zao zinakuwa ni za kupigana kuzijenga. Mtu aliyezaliwa katika ukoo duni huwa na hadhi ya chini mpaka akijikusuru akajijengea umaarufu mwenyewe kwa njia ya: kulimbikiza ukwasi, ushujaa, ujanjaujanja, taaluma, n.k. inhuman: unyama: hali ya kutendewa kinyume cha ubinadamu, mathalani, kuteswa, kulishwa najisi, kubakwa hasa mbele ya kadamnasi, n.k. in-kind contributions: michangohali: makadirio ya kuridhisha ya vifaa, gharama za uendeshaji, rasilimali watu na nyenzo zilizochangiwa au kushirikiana baina ya wanufaika na mawakala kama ishara ya ushirikiano. Agh., istilahi hii hutumiwa wakati wa kuamua bajeti za ruzuku iliyoombwa kama ishara ya uchangiaji wa pande mbili. inoculation: chanjo: 1. utiaji vimelea au toksidi mwilini mwa kiumbehai kwa nia ya kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa wa vimelea hovyo. lxxxviii 2. utumiaji wa dawa maalumu ya kingamwili kwa kukinga magonjwa. 3. rutubisha (mimea) kutoa kago katika mazingira fulani na kuingiza katika mazingira mengine. inoculums: kago: sampuli kama vile ya bakteria au spora za uyoga, n.k. inayooteshwa katika chakula au mazingira maalumu. in-service training: mafunzo kazini: mafunzo ya stadi yanayotolewa kwa

132 mwalimu, mnasihi, kiongozi na msimamizi ili kumwezesha kuongeza stadi na maarifa yake kuhusiana na kazi zake ambazo ameajiriwa kuzitenda. Kwa muktadha wa ulemavu, mafunzo kazini yanaweza kulenga uwanja wa elimu ambapo mwalimu mtaalamu, mshauri, mnasihi, tabibu n.k. humfundisha kila mwalimu au/na mzazi na mlezi mbinu mahususi za kushughulika na mtoto wake mwenye ulemavu na mahitaji maalumu. Halikadhalika, mafunzo haya ni muhimu kwa mwajiri wa mtu mwenye ulemavu, mwajiriwa mwenye ulemavu, mhudumu wa mtu mwenye ulemavu ili kumudu kukabiliana na changamoto zinazotokana na ulemavu. insomnia: insomnia: hali ya kukosa usingizi au kushindwa kuendelea kusinzia ambayo inaweza kujidhihirisha kwa kukosa usingizi kabisa au kupata usingizi wa kimang amumang amu. Insomnia ya mauti ni hali ya kukaa macho walau kwa saa mbili kabla ya muda wa kawaida wa kuamka na kushindwa kupata usingizi tena. institution: taasisi: asasi au chombo kinachoendeshwa kisheria kwa ajili ya kukidhi matakwa fulani ya kiutawala au kihuduma. instructional support: usaidizi elekezi: msaada unaotolewa na mtaalamu wa tibakalima kwa mtoto, familia na/au yeyote aliye karibu na 114 mazingira ya mtoto. Tibakalima husaidia kujenga maarifa rekebishi au kimwili ambayo humsaidia mtu katika maisha na hivyo kuboresha mchangamano wake na mazingira au jumuia. Usaidizi huu hulenga kwenye ujenzi wa maarifa ya kiuamilifu yanayohusiana na mchangamano wa hisia, upangiliaji wa msogeo, maarifa mazuri ya utendaji, maarifa ya kujisaidia mwenyewe mf. kujivalisha nguo, kujilisha, n.k.; nyenzo au vifaa rekebifu, upangiliaji wa vicharazio vya kompyuta, mpangilio wa kazi za shule na shughuli zingine zinazoendana na shughuli zinazotarajiwa. instrumental (guide) advocacy: mwongozo wa usaidizi: hali ya kusaidia kutimiza mahitaji ya mtu kwa utatuzi wa matatizo ya kiutendaji, kama ilivyo kwenye kutoa ushauri wa kiutendaji na usaidizi kuhusiana na usafiri, uvaaji, upigaji kura, kununua mahitaji, makazi, kuhudhuria ibada, ustawi binafsi na usimamizi wa mali na kipato. integral part of: -enye kufungamana na: -a kuwa sehemu muhimu ya au kujumuishwa ndani ya kitu kizima. integrate: tangamana: hali ya kuchangamana au kuchanganyika pamoja. Kwa muktadha wa ulemavu, dhana hii huelezeka kiurahisi kwenye uwanja wa elimu ambapo kila mtoto mwenye umri wa

133 kwenda shule huandikishwa na kuchanganyika katika madarasa na shuleni bila kujali hali ya kila mmoja wao. integration: utangamano: hali ya kuchangamana na kuwa sehemu ya kitu, ushiriki na pia ni ukubalifu wa mtu mwenye ulemavu ndani ya jumuia kwa ujumla wake. Kwa muktadha wa watu wenye ulemavu, hii ni hatua ya kati ya kutoka kwenye ile ya kutengwa na kuelekea kwenye kujumuishwa. Hata hivyo, tofauti na ujumuishaji, hatua ya utangamano bado humlazimisha mhusika kujirekebisha mwenyewe ili kuendana na matakwa ya mfumo uliopo. Kwenye hatua ya ujumuishaji utaratibu huwa kinyume chake. intellectual disability: ulemavu akili: 1. aina ya ulemavu ambayo hubainishwa na kiwango cha juu cha ukomo wa utendaji kiakili na urekebeshaji wa mwenendo. Hii ndiyo maana aina hii ya ulemavu huhusishwa na ujifunzaji. Ulemavu wa aina hii daima hujumuisha ukomo au uwezo wa akili. Kwa upande mwingine, ulemavu wa ukuaji unaweza kuhusisha akili, ukomo wa kimaumbile au vyote viwili. Usonji ni aina ya ulemavu wa ukuaji ambapo ukomo wa kiakili na kimaumbile hauathiri uwezo wa ubongo wa kufikiri bali na kusababisha ukomo mwingine 115 katika hali mbalimbali za maisha. Wakati watu fulani wenye usonji pia huwa na ulemavu wa akili, baadhi huwa hawana, ila katika hali zote mbili, unaweza kusababisha ukomo mkubwa kwenye maeneo mengine ya maisha ya mhusika. 2. aina ya ulemavu wenye kubainishwa na kiwango kikubwa cha ukomo wa utendaji kiakili na urekebishaji kitabia ambao hugusia maeneo mengi ya maisha ya kila siku, kijamii na kiutendaji. Aina hii ya ulemavu huibuka kabla ya umri wa miaka 18. Kwa mtazamo wa kitabibu, aina hii ya ulemavu imekuwa ikiitwa taahira ya akili ** ambako ni kukosa adabu lugha na kutojali hisia za wahusika. intellectual functioning: uamilifu kiakili: uwezo wa jumla wa akili, kama vile ujifunzaji, kutafakari, ujengaji hoja, kutatua matatizo, n.k. intelligence quotient (IQ): hisa weledi (HW): alama anazozipata mtu kutokana na zoezi la upimaji wa kiwango cha akili alichonacho ili kugundua uwezo wa akili kulingana na umri alionao mtahiniwa. intelligence: umaizi: uwezo wa kuelewa, kutambua, kupambanua vitu, kuhifadhi na kuwa na kumbukumbu. intelligibility: uelewekaji: kiwango ambacho mazungumzo yanaweza kueleweka. interaction: kuchangamana: kiwango ambacho mtu au mtoto anachangamkia vitu au watu

134 waliomzunguka, na jinsi wanavyocheza na kuchangamana na vitu na watu katika mazingira yake. interdependence: utegemeano: hali ya nafsi au pande mbili kutegemeana, kiasi cha nafsi moja hujihisi kutokamilika bila nyenzake. Katika uhusiano huu huwa kuna mahitaji ya mwenza wa kumwezesha au kumnusuru au kumsaidia mwingine kila mara; na kwa namna hiyo kuendeleza mtindo huo wa maisha. interdisciplinary team: timu ya taaluma kikoa: kundi la watu wanaotoka katika taaluma zaidi ya moja lakini zenye kuingiliana na kutegemeana (taz Education Support, Resource and assessment ccentres ). intermediary assistance: usaidizi kati: msaada unaotolewa na binadamu ambapo mtu huruhusiwa kisheria na mfumo wa kimahakama kusimama na kumtetea mtu mwingine mwenye ulemavu wa akili au mkalimani wa lugha ishara kuwezesha mawasiliano pale kiziwi anapohusika. internal locus of control: kidhibiti nafsi ndani: hali ya mtu kuamini kuwa anamudu kudhibiti matukio yanayomwathiri. Kidhibiti nafsi cha mtu kinaweza kudhaniwa ama kuwa cha ndani (ambapo mtu huamini kuwa anamudu kuyadhibiti maisha yake) au nje (ambapo mtu huamini kuwa maisha yake 116 yanadhibitiwa na masuala ya kimazingira ambayo hana uwezo wa kuyamiliki), au pengine maisha kudhibitiwa kwa nasibu au kudura. Mtu mwenye kidhibiti nafsi ndani imara, huamini kuwa yanayomtokea maishani hutokana na matendo yake mwenyewe; mathalani, anapopokea matokeo ya mitihani mtu wa aina hii hujisifia au hujilaumu mwenyewe na uwezo wake. Ambapo yule mwenye kidhibiti nafsi nje madhubuti, husifia au kulaumu mambo ya nje yake kama vile walimu au mitihani. international bill of human rights: mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu: maafikiano haya yalipewa jina na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa azimio lake namba 217 A (III) sanjari na mikataba miwili iliyopitishwa na Umoja wa Mataifa. Mkataba huu hujumuisha Azimio la Haki za Binadamu (1948) na Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (1966) pamoja na Mikataba ambata ya Nyongeza na Mkataba wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (1966). interpathy: mwingiliano: hali ya kufikiri na kuhisi pamoja au, kuhusiana na watu wengine.

135 intersex: isojinsi: dhana hii hujihusisha na tofauti za kimwili kufuatana na viwango vilivyowekwa kiutamaduni vya uanaume na uanauke ikiwa ni pamoja na tofauti za kiwango cha kromosomu, gonadi na via vya uzazi. Katika muktadha wa kisasa, istilahi hii humaanisha huduma isiyojali jinsi ili kutoa uhuru zaidi wa matumizi kwa baadhi ya wanajamii, mathalani, badala ya kuwa na vyumba viwili vya msalani; kimoja cha wanaume na kingine cha wanawake, kinaongezwa cha tatu ambacho ni cha mseto kwa jinsi zote. Hali hii huwasaidia watu kama vile wenye kiwango kikubwa cha ulemavu ambao huhitaji kuingia maeneo ya faragha na wasaidizi (wanaoweza mara nyingine wasiwe wa jinsi yao). Halikadhalika kuna watu ambao maumbile ya via vyao vya uzazi ni tofauti na wanavyoonekana kijinsi. Uwepo wa huduma za aina hii huwasitiri na kuwaondolea tahayari ambazo zingeweza kutokea katika utaratibu uliozoeleka. (taz. accessible toilet ). intervention: afua: hatua zinazochukuliwa kusahihisha, kurekebisha au kuzuia na kutambua tiba zinazowezekana au matatizo ya ukuaji. 117 intramuscular injection (IM): udungaji misuli: uchomaji sindano kwenye misuli. intravenous (IV): sindanovena: 1. ni pale dawa kiowevu inapotiwa ndani ya mshipa wa vena. 2. -a ndani ya mshipa wa vena, mathalani, kudunga sindano kwenye mshipa wa vena ili kutia dawa, chakula, damu, n.k. invalid wheelchair: kiti kiwete**: dhana ya kitabibu ni kuwa kila binadamu sharti atembee kwa miguu yote miwili ndipo ayamudu mazingira yake. Kwa muktadha huo wa kitabibu, matumizi ya kitimwendo hayaonekani kufidia upungufu kwenye mota ya msogeo. Mtazamo wa ulemavu kwa muktadha wa kijamii na haki za binadamu, unapingana kabisa na ule wa kitabibu kwa kukiona kitimwendo kuwa mbadala wa miguu kiasi kwamba mtumiaji wake huyamudu maisha yake kwa kiasi cha kuridhisha ilimradi kusiwepo na vikwazo. (ang. barriers ). invalid: siojiweza:** dhana ya kikale inayodunisha mtu mwenye ulemavu kwa kuangalia kinachokosekana kwenye viungo vyake au milango yao ya fahamu bila kuzingatia kile anachomudu kukitenda. Istilahi hii inatokana na muktadha wa kitabibu ambao haujali hisia za mhusika. iodine: madinijoto: aina ya madini ambayo hutumika kuzalisha homoni ya tezishingo yenye kupatikana

136 katika vyakula. Mwili wenyewe huwa hauzalishi madinijoto ndiyo maana ni muhimu kuyapata kutokakana na vyakula. Mwili usipokuwa na madinijoto ya kutosha, hushindwa kuzalisha homoni ya thiroidi ya kutosheleza mahitaji. Upungufu huo unaweza kusababisha tezishingo, aina fulani za saratani, na udumavu wa akili kwa mtoto au kijana ambaye mama yake alikosa madini haya wakati wa ujauzito. Kwa hiyo, binadamu anahitaji madinijoto ili kusaidia katika kurekebisha metaboli ya mwili, ukuaji wa mifupa kadhalika na utendaji wa ubongo (taz. intelligence quotient ). irrevocable trust: amana isiyotengulika: kitu kilichowekwa chini ya mfuko wa udhamini, ambacho hakiwezi kuondolewa udhamini isipokuwa pale ambapo udhamini umekoma na salio kuhaulishwa au kuhamishiwa katika udhamini mwingine. Amana hii inakuwa na namba yake ya mlipa kodi kama mtu anayejitegemea. Mdhamini huandika taarifa ya kila mwaka na ana haki ya kusimamia mfuko wa fedha kwa njia za kawaida za uwekezaji, n.k. irritable mood: hali ya kukereka: hisia za fadhaa ndani ya nafsi zinazohusiana na kuwa na wepesi wa kukasirishwa. irritable: -enye kuudhika upesi: -a tatizo la kisaikolojia la kukasirishwa 118 na jambo au kitu ambalo linaweza kuathiri uhusiano na watu wengine. ischemia: iskemia: upungufu wa mtiririko wa damu yenye oksijeni kwenye ubongo au sehemu nyingine ya mwili. lxxxix itinerant teacher: mwalimu asomipaka: 1. mwalimu mwenye jukumu la kuzungukia na kuzuru idadi kadhaa ya shule ndani ya eneo fulaini la utawala na huwa na ratiba ya zamu za kumfundisha mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu ya ujifunzajii. Mwanafunzi huyu kwa kawaida huliacha darasa lake kwa muda ili kufanya kazi na mwalimu asomipaka. 2. mwalimu anayewazungukia watoto ambao hawawezi kuhudhuria shule kwa sababu yoyote ile katika mazingira ya majumbani mwao au hospitalini ili kutoa mafunzo. 3. mwalimu mtaalamu anayetembelea shule mbalimbali kusaidia watoto na walimu kuhusu ujifunzaji wa wenye mahitaji maalumu.

137 Jj jaundice: homanyongo: hali ya ngozi na macho kugeuka kuwa na rangi ya manjano ambayo inaweza kuwa dalili ya homa ya hepatitisi. jerks: mshutuko: hali ya misuli kujikunyata na kukaza kwa ghafla ikisababisha ukakamavu na kudema ovyoovyo. Hali hii hutokea pale ambapo sehemu ya mwili inajisogeza kwa kuitikia msukumo usiohiari. joystick kiegemeo dekezi: kifaa maalumu cha kieletroni kinachoendeshwa kwa mikono, miguu, kidevu, n.k. na hutumika kama mbadala wa kuendeshea kasa au kishale kwenye skrini ya kompyutana vifaa mbalimbali vya kielektroni. Pia hujulikana kama usukani fimbochombeza. 119

138 Kk keyboard filters or keyboard emulation: kisaidizi uchapaji: mfumo unaosaidia uchapaji kama vile kutabiri neno na kuongeza tahajia ambavyo hupunguza idadi ya kubofya. kinaesthesia: kinestezia: hisia ya kutambua mwendo, mahali, uzito, n.k. wa viungo vya mwili kutokana na kuhamasika kwa vipokezi vilivyo ndani ya misuli, vifundo na tendoni za viungo hivyo. xc kinaesthetic: -a kinestezia; -a hisia za misuli. kinaesiology: kinesoloji: pia hujulikana kama kinetiksi ya kuimarisha misuli ya binadamu hasa wanamichezo kutokana na utafiti wa kisayansi kuhusu utendaji kazi wa misuli ya binadamu, kiufundi na kisaikolojia. magoti kugongana wakati wa kutembea Kamusi nyingine hutambua hali hii kama mang ombwe.** kyphosis: kibiyongo:** hali ya kifua au sehemu ya juu ya mgongo kupindika. Agh. istilahi hii hutumika kama jina la mwenye hali yenyewe badala ya kutambulisha hali aliyonayo na hivyo kubeba maana ashirifu hasi; yaani, kushawishi kuwa kasoro na umbile ndio msisitizo hasa kwa wasanii na vyombo vya habari. Visawe vingine vyenye maana ashirifu hasi ni: kinundu**; kiduva**, kigongo**. kleptomia: udokozi: kasoro ya akili inayosababisha tamaa, hamu ya kuiba, ugonjwa wa udokozi. knock knees: mategendani: hali ya kupinda kwa ndani katika eneo la magoti na kusababisha 120 kyphoscoliosis or swayback: kaifoskoliosisi: mchanganyiko wa mbetuko (kifosisi) na mbonyeo wa uti. Kifosisi inaweza kusababishwa na ugonjwa unaoshambulia mifupa na misuli ya kanofupa au sababu nyinginezo zisizofahamika. Tiba yake hujumuisha tibamaungo, na uvaaji wa bangiligango mgongo, na katika hali fulani upasuaji huhitajika. Upasuaji huu unaweza kuhusisha uingizwaji wa nondo ya chuma

139 kwenye uti wa mgongo na kupangilia upya baadhi ya mifupa, na agh. hatua hii hufuatiwa na uvaaji wa kalibu na bangiligango mgongo kwa muda fulani. 121

140 Ll labeling: upachikaji majina: tabia ya kumpa mtu utambulisho kwa namna ya kumtweza au kumdhihaki. lame: kiguru:** kulemaa kiungo hasa mguu kiasi cha kusababisha mtembeo wa kuchechemea. Kwa misemo ya msimu humaanisha mtu asiyekuwa na maana au thamani, dhaifu, (taz. cripple ). language: lugha: hujumuisha matamshi au ishara na aina nyingine za mawasiliano. large-print (also large-type or largefont): maandishi makubwa: herufi za maandishi zilizokuzwa kuliko kawaida mahususi kwa mtu mwenye uoni hafifu. Herufi za kawaida huwa na kima cha pointi sita hadi kumi (wastani wa 1/16 hadi 1/8 ya inchi) na mara nyingine kubwa ya hapo. Muundo wa vitabu vya maandishi makubwa ni pointi kumi na nne hadi kumi na nane (walau 1/8 hadi ¼ ya inchi) na wakati mwingine kubwa zaidi ya hapo. Muundo wa vitabu vya maandishi makubwa pia husadifu vivyo hivyo (kawaida inchi 8 ½ x 11). Maandishi makubwa yanaweza kusaidia kama njia ya kusoma kwa mtu mwenye uoni hafifu asiyemudu kutumia maandishi ya ukubwa wa kawaida, kupata matini na machapisho mengine ya kufundishia au kujifunzia. 122 latency: halifiche: 1. hali inayoweza kuwapo lakini bila kujitokeza waziwazi; mathalani, kipindi ambacho vimelea vya maradhi vinakuwemo mwilini pasipokuwapo dalili za ugonjwa kujidhihirisha; mtoto kuwa na kipaji ambacho hakijajitokeza bayana, mwenendo usiowekwa wazi, n.k. 2. kipindi cha utulivu kati ya uhamasishi wa tishu na utendaji wake. latent: fiche: -siyokuwa bayana. learner centred: -enye kumlenga mwanafuzi: mfumo wa ufundishaji unaomlenga mwanafunzi moja kwa moja kwa kuzingatia mahitaji yake mahususi. learning difficulties: ugumu wa kujifunza: hali ya kuwa na uzito kuelewa, kukumbuka yale yanayofundishwa na kutoweza kuchambua na kutafsiri maarifa yaliyofundishwa kivitendo kwa haraka. Agh., hali hii hutokana na kuwapo kwa matatizo kwenye ubongo wa mwanafunzi (ang. learning disability ). Mtu mwenye ulemavu wa akili anaweza kukabiliwa na changamoto mahususi ambazo kwa kawaida humwandama maisha yake yote. Kutegemeana na aina na kiwango cha ulemavu, usaidizi na teknolojia za kisasa unaweza kutumika kumsaidia mtu mwenye hali hii kujifunza. learning disability: uzito wa kujifunza (pia hujulikana kama ulemavu akili):

141 upambanuaji unaohusisha maeneo mengi ya kiutendeji pale ambapo mtu huwa na ugumu wa kujifunza katika hali ya asili. Wakati ulemavu wa ujifunzaji na kasoro za ujifunzaji na ugumu wa ujifunzaji agh. huchukuliwa kuwa kitu kilekile, misemo hii hutofautiana kwa namna nyingi. i) kasoro huhusisha matatizo ya ujifunzaji katika tasnia za taaluma. Matatizo haya hata hivyo, hayatoshi kulazimu uchunguzi wa kitabibu; ii) ulemavu wa ujifunzanji kwa upande wake, ni suala la uchunguzi rasmi wa kitabibu ambapo mhusika hukidhi sifa kama zilivyobainishwa na wataalamu (wa saikolojia, mabingwa wa magonjwa ya watoto, n.k.). Tofauti ipo kwenye kiwango, mfululizo na kina cha dalili za tatizo lililotajwa. Kwa maana hiyo, vitu hivi wiwili havipaswi kuchanganywa. Pale istilahi kasoro za ujifunzaji inapotamkwa, huelezea kundi la kasoro zenye kubainishwa na kuvia kwa stadi maalumu, lugha na matamshi. Aina za kasoro za ujifunzaji ni pamoja na ugumu wa kusoma (disleksia), ugumu wa kukokotoa hesabu (kitatizakokotozi) na kushindwa kuandika (disigrafia). Baadhi ya mbinu rekebishi zinaweza kuwa rahisi wakati mwingine zinaweza kuwa tatanishi na changamani. Teknolojia za kisasa zinaweza kuhitaji ufundishaji wa mwanafunzi kuandamana na 123 usaidizi unaofaa darasani. Walimu, wazazi na shule kwa pamoja wanaweza kuandaa mpango wa upimaji unaoendana na marekebisho ya kumsaidia mwanafunzi ili amudu kujifunza kwa kujitegemea mwenyewe. Wanasaikolojia wa shule na wataalumu wengine mara nyingi husaidia katika kuandaa na kuratibu utekelezaji wa usaidizi kwa walimu na wazazi. Usaidizi wa kijamii unaweza kuboresha ujifunzaji wa mwanafunzi mwenye ulemavu. Kitu kisichofahamika ni kasoro yenye kuathiri uwezo wa ubongo wa kupokea na kuchakata taarifa. Kasoro hii inaweza kuzusha ugumu kwa mtu kujifunza kwa haraka au kwa njia ileile sawa na mtu ambaye hakuathiriwa na ulemavu wa ujifunzaji. Mtu mwenye ulemavu wa ujifunzaji huwa na tatizo la kufanya stadi mahususi au kukamilisha kazi iwapo ataachwa kugundua vitu yeye mwenyewe au kama amefunzwa katika njia ya kawaida. learning outcomes: matokeo ya ujifunzaji: athari ya upimaji ambayo hupimwa kwa kuzingatia viwango na malengo. legacy: urithi: mawazo au vitu vilivyoachwa na watangulizi katika jamii. legal advocacy: utetezi wa kisheria: hali ya kupeleka madai au malalamiko katika vyombo vya

142 kisheria ili kubainisha haki (za kisheria) za mtu mwenye ulemavu na kuhakikisha kuwa haki hizo hazikiukwi. legal capacity: uwezo kisheria: nafasi au madaraka ya mtu kisheria. legally blind: -wa na upofu kisheria: mtu anayeona kwa kiwango cha chini ya kipimo cha 20/200. Katika sheria za baadhi za nchi, hiki ndicho kiwango ambacho hutambulika kuwa cha kupoteza uoni kabisa. lens: lenzi: 1. sehemu nyeupe au angavu kwenye jicho inayolenga miali ya mwanga kwenye retina. 2. dutu inayopitisha mwanga yenye mbonyeo au mbinuko sawia katika uso mmoja au nyuso zote mbili ambayo hutumika kwa ajili ya kupitisha au kutawanyia mwanga. 3. kisahani cha tishu kilichopanuka pande zote mbili ambacho kipo nyuma ya mboni ya jicho. leper: mwenye ukoma: mtu mwenye ugonjwa unaoambukiza ambao huathiri mishipa ya fahamu za hisia mwilini na kusababisha baadhi ya viungo vyake k.v vidole, kukatika. leprosarium: kituo kwa ajili ya watu wenye ukoma: hospitali au mahali pa kutunzia wagonjwa wa ukoma. leprosy: ukoma: ugonjwa wa maambukizi ambao husababishwa na vimelea (basili) vyenye kuathiri mishipa ya neva na kusababisha 124 matatizo ya ngozi, kupoteza hisia, kupooza, na mikunyato ya ngozi na kukatika vidole vya mikono na miguu. lesion: jeraha: kidonda au madhara yoyote katika tishu hai. lesbian: msagaji: 1. mwanamke mwenye kuvutiwa kimaumbile na kimahaba, na mwanamke mwenzake. 2. mwanamke anayajiridhisha kimapenzi na mwanamke mwenziye kwa kusuguana au/na kunyonyana tupu zao. letter of intent: barua ya dhamira au azimio: mojawapo ya nyaraka muhimu sana za mpangilio wa umiliki wa mali ambapo wazazi huelezea matarajio na matamanio yao yalivyo kuhusu mustakabali wa mtoto wao kimatunzo hususani mwenye ulemavu hasa baada ya wao kuaga dunia. leukemia: lukemia: 1. hali ambamo kuna ongezeko la hitilafu la idadi ya chembe nyeupe kwenye damu. Pia hufahamika kama saratani ya damu na athari yake kuu ni kwenye ogani zinazotengeneza damu. 2. ugonjwa wa ghafla au wa taratibu wa tishu zinazotengeneza chembe nyeupe za damu ambazo ni changa katika damu; dalili zake ni kuongezeka kupita kiasi kwa chembe nyeupe za damu ambazo bado ni changa kwenye damu na katika sifongo ya mifupa, kutokwa na damu na uambukizo wa magonjwa.

143 liberty: uhuru: haki ya mtu kutumia uhuru wake; ruhusa; uhuru wa kufanya jambo. licentiate:-liopewa kibali: -enye ruhusa ya kufanya jambo au taaluma fulani. life cycle: mzunguko wa maisha: mfuatano wa kukua na mabadiliko yanayohusiana na ukuaji ambayo huathiri familia. Mabadiliko haya huzibadilisha tabia au sifa na shughuli za kifamilia na hatimaye huathiri jinsi familia zinavyochangamana. ligament: kano: 1. utepe ndani ya mwilli ambao hushikilia mifupa na vifundo pamoja. Kano huunganisha mifupa kwa mifupa wakati ukamba huunganisha mifupa na misuli. 2. tishu unganishi ambayo huunganisha mifupa au sehemu nyingine za mwili. xci limp: checheme: aina ya uatilifu wa mtembeo unayoweza kutokana na: (i) maumivu ambapo wayo hugusa ardhi kwa muda mfupi zaidi kuliko ilivyo kawaida na kama kuna maumivu ni makali mno, wayo hushindwa kabisa kukanyaga; (ii) kasoro kwenye nyonga ikihusisha udhaifu wa misuli; n.k. Agh. hali hii hutambulishwa kwa njia dhihaka k.v. chopea** au mwendochopi**; sanjari na kuiga mtembeo wa mhusika. linguistic identity (lip speech reading or visual hearing): usomaji wa matamshi au kusikia kwa kuona: mchakato wa kuelewa ujumbe wa 125 matamshi kwa njia ya kuangalia uso wa mwongeaji na mabadiliko ya midomo. Mtindo huu unaweza kutumiwa na kiziwi ambaye ana uoni mzuri; hata hivyo, ni asilimia kati ya ya lugha ya Kiswahili cha kuongea inayoweza kueleweka kwa kutumia mtindo huu peke yake. Hivyo, ipo haja ya kujalizwa na viashiria vingine kama vile matendo ya kuonyesha hisia kwa kutumia viungo vya mwili kama mikono, maelezo kwa mwonekano wa uso, ishara au vidokezo vinginevyo vya kihali. live assistance and intermediaries: usaidizi wa viumbehai: msaada, ambao mtu mwenye ulemavu huupata kutoka kwa binadamu, wanyama na/au mtu wa kati. (ang. human assistance). lobby: ushawishi: jaribio lililopangiliwa ama na kikundi cha watu au mtu ili kuwashawishi wanasiasa, watunga sera au wafanyauamuzi juu ya jambo mahususi. Pia uzengeaji. long sleived clothes: nguo za mikono mirefu: mavazi yenye mikono mirefu ambayo hutumika kama kinga kwa mtu mwenye ualbino dhidi ya miale ya jua. long pant, skirt or gown: nguo ndefu: aina ya vazi refu ambalo nimuhimu kwa mtu mwenye ualbino katika kujikinga dhidi ya miale ya moja kwa moja ya jua ambayo humsababishia saratani ya ngozi.

144 lordosis: kibina (pia lodosisi): hali ya kubonyea kwa maeneo kati ya kiuno na mifupa ya mabega kunakosababishwa na kuteguka kwa nyonga. Hali hii inapopindukia inaweza kuitwa myumbonyuma. Japo wakati mwingine lodosisi na kifosisi huchukuliwa kumaanisha kitu kilekile, lakini hayo ni matumizi mabaya ya istilahi. love: upendo: nguvu ya msukumo maishani inayosababisha muunganiko wa mtu na mtu au mtu na kitu. Hii ni hali yenye kutibu inayohitaji vipengele vya kumtathimini mwingine, urafiki na kujitoa kwa ajili ya mwenza (mwelekeo chanya). low birth weight: kuzaliwa na uzito pungufu: dhana inayotumika kwa mtoto mwenye uzito wa gramu 1,500 au chini ya hapo. Mtoto mchanga mwenye uzito pungufu ni wa aina mbili: yule aliyezaliwa akiwa na umbile dogo mno, agh. huzaliwa kabla ya kutimiza umri wa miezi tisa, na yule anayezaliwa na umri stahili ila mwenye umbo dogo sana kulingana na muda wa ujauzito. 126 Matumizi ya istilahi mtotonjiti** ina maana ashirifu hasi. low self esteem: kutojithamini: hali ya mtu kujishusha hadhi au thamani kwa ama kutojijali au kufanya matendo yasiyo-endana na desturi za eneo mahalia. low tone deafness: uziwi wa sauti za chini: hali ya kupoteza usikivu wa mawimbi ya sauti ya chini. low vision: uoni hafifu: hali ya uoni inayobainishwa kwa kipimo cha zaidi ya 20/200 lakini kisichozidi 20/70 cha uoni wa jicho. Kipimo hiki humaanisha wenye uoni, usiowezesha kusoma gazeti kwenye umbali wa kawaida wa kusomea hata kwa kutumia miwani (ya kusomea) au lensi ya kupachika. Agh., katika muktadha wa elimu, yeyote anayebainika kuwa na uoni wa vipimo hivyo, huingizwa katika mfumo wa elimu maalumu. low-vision specialist: mbobezi wa uoni hafifu: mtaalamu aliyefunzwa kuchunguza na kutoa mafunzo kuhusu kasoro za macho. low-socio-economic status: uluwa duni wa kijamii na kiuchumi: hali yenye daraja la chini kijamii na kiuchumi. lumbar: kiuno: sehemu ya chini mwa uti wa mgongo. lumbar corset: taz. corset. lumbar puncture: sindano ya mgongo: sindano inayochomwa ndani ya uti

145 wa mgongo ili kufyonza kiowevu cha uti wa ubongo au kutia dawa. lunacy: wazimu**, ukichaa**, umajinuni**: hali ya akili kuchanganyikiwa kiasi cha mtu kutenda mambo bila dhamiri au kujali matokeo. Ni ugonjwa mkubwa wa akili. Hizi istilahi huashiria hali na chimbuko kwenye asili ya kitabibu na imani za kigeni ambazo maana yake ashirifu ni hasi kiasi kwamba haifai kutumiwa na jamii iliyostaarabika. Istilahi na misimu inayoshabihiana na hii ni punguani,** uendawazimu,** mcharuko,** mwezi mchanga,** dakika tano mbele.** Tatizo la afya ya akilli au mvurugiko wa akili ndiyo misemo inayokubalika. 127

146 Mm machoistic: ajitesaye: -enye kuhusiana na kujitesa au kujidhalilisha. magical thinking: kufikiri kimiujiza: hali ya mtu kuamini kuwa mawazo, maneno au matendo yake yanaweza kusababisha au kuzuia matokeo fulani kinyume na taratibu au sheria za kawaida za kuwezesha jambo kutendeka na athari zake. Mathalani, mtu kuamini kuwa akisali sala maalumu mara tatu kila usiku mama yake atakingwa dhidi ya mauti muda wote; mama kuamini kuwa akiwa na wazo baya, mwanaye ataugua. Fikira za kimiujiza zinaweza kuwa sehemu ya fikira rejewa au zinaweza kupindukia kwenye viwango vya delusheni ambapo mhusika hung ang ania imani zake bila kujali ushahidi unaothibitisha kinyume chake. Fikira za kimiujiza hudhihirika miongoni mwa watoto, watu wa tamaduni za kale na katika mvurugiko wa haiba kisifrenia, skizofrenia, na kuwa na haiba shurutishi. mainstream programme: programu mseto: 1. programu ya mafunzo ya stadi au amali yanayoendeshwa katika mazingira mchanganyiko k.v. kuwa na wanafunzi wenye mahitaji maalumu ya viwango mbambali; na bila kuwapo kwa nyongeza ya rasilimali fedha ili kuwasaidia wale wenye viwango vya juu vya mahitaji hayo. 2. mchakato wa kuwachanganya watoto wenye 128 ulemavu kwenye mfumo wa kawaida wa elimu au programu za kijamii ili kutekeleza dhana ya mazingira yasiyokuwa na mikingamo kuelekea ujumuishaji. (taz. integration). mainstreaming concept: dhana ya ujumuishaji: mchakato wa kimfumo wa kuchangamanisha maadili, mawazo na mada kwenye nyanja kuu zote za hatua za kimaendeleo zenye malengo mahususi na ya jumla ambazo huwanufaisha raia wote. mainstreaming disability: kujumuisha ulemavu: mkakati wa kuyafanya matatizo na uzoefu wa mtu mwenye ulemavu kuwa sehemu ya usanifu, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini wa sera na programu katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi, na kijamii ili naye anufaike kwa maana ya kutoendeleza utofauti. Lengo ni kwamba katika hatua zote, programu, huduma na mazoea vinapimwa ili matokeo yathibitishe ushiriki wa mtu mwenye ulemavu badala ya kubaki akieleaelea. Hata hivyo, dhana hii haiondoshi mahitaji ya sera na programu mahususi au zile ikibali zenye kumlenga (mtu mwenye ulemavu) moja kwa moja. major life activities: shughuli kuu za maisha: utendaji kama vile kujitunza, kufanya kazi za kutumia mikono, kutembea, kuona, kusikia, kuongea, kupumua, kujifunza na kufanya kazi. (ling. activities of daily living).

147 malignant: -a uvimbe: -enye kudhuru; huashiria uvimbe au kimelea kinachoua tishu nyingine kwa kadiri kinavyokua. Agh. uvimbe huu huashiria saratani. malnutrition: utapiamlo: ugonjwa unaosababishwa na kukosa lishe bora ambao agh. humpata mtoto na mzee wasiyepata lishe bora. mandate: agizo: mamlaka ya kutoa amri hususani kwa maandishi ili jambo fulani litekelezwe. mania: mania: aina ya sikosisi ambayo huathiri mwenendo mzima wa fikira na mhemko wa mwathirika; huainishwa kwa uchangamfu wa kupita kiasi, kuongea kupita kiasi, kukosa utulivu wa mawazo (kurukia wazo hili mara lile), delusheni, halusinesheni, kwenda huku na kule n.k. xcii maniac: mwathirika wa mania: mtu mwenye mvurugiko wa mwenendo wa fikira na mhemko. Agh. istilahi hii hutumiwa na watu wasio na ulemavu kwa njia ya kukejeli bila kujali hali halisi ya mtu na yale yanayomsibu. manual communication: mawasiliano ya ishara: mawasiliano yanayotumia lugha ishara na tahajia ya kutumia mikono kama namna kuu ya kuwasiliana pamoja na/au bila ya kuongea. manual impairments: kilema cha mikono: hali ya kuwa na kasoro katika mikono. marginalisation (or social exclusion): ubaguzikijamii: ukuwekaji mtu au kitu 129 pembezoni; kutengwa kijamii. Ni hali ya mtu au kundi kutonufaika kijamii na kususwa kiasi cha kubakia pembezoni mwa michakto ya maisha ya kijumuiai. Mtu kuzuiwa kimfumo au kukatazwa kufikia haki, fursa na rasilimali mbalimbali ambazo kwa kawaida hupatikana kwa urahisi kwa kundi lingine tofauti; wakati (haki hizo) huwa za msingi katika kutangamanishwa kijamii katika kundi hilo; k.m. makazi, ajira, huduma za kiafya, ushiriki kwenye masuala ya kiuraia, kidemokrasia na michakato mingineyo. massage: chua: shikashika mwili ili kupunguza maumivu, mkazo au dalili nyinginezo. Kuchua tumbo kunaweza kusaidia mimba kujikunyata na kusimamisha kutokwa na damu kwa w ingi baada ya kujifungua au kuharibika kwa mimba. masochism: ashiki dhalilishi: 1. kuamsha ashiki kwa njia ya udhalilishaji, kufunga kamba, kupiga na kusababisha mateso. 2. kujiumiza ili kutoadhibiwa. 3. Kujidhuru ili kupata mapenzi (hasa kutoka kwa yule aliyekuwa amesababisha mchomo wa mapenzi). 4. kufurahia kitendo cha kujamiiana kwa kukubali kupigwa au kunyanyaswa, kupenda kupigwa au kunyanyaswa ili kupata mashamushamu zaidi. 5. kufurahia kujiadhibu au kuadhibiwa, kupenda kuteseka.

148 maternal infection: maambukizimimba: hali ya kuambukizwa mama mjamzito ambapo kwa kawaida huleta mashaka ya kuweza kumuambukiza mtoto aliye tumboni pia. maternal malnutrition: utapiamlo kwa mjamzito: hali ya upungufu wa virutubisho kwa mwanamke mwenye mimba. maximize: kuwa kimajuu: fikia kiwango cha juu, mathalani rasilimali, faida, n.k. means of egress: njia za kuingilia au kuondokea: eneo lolote ndani ya jengo au mazingirajenzi kuelekea maeneo mbalimbali; yaani, vyumba vinavyoingiliana, milango ya kuingilia na kutokea, ushoroba ndani ya jengo, roshani, ngazimbetuko, ngazi kawaida, maboma, kumbi au sebule, barabara, barabara kuu, vichochoro, au sehemu kama vile madaraja ambayo umma unaruhusiwa kupita bila vizuizi. Maeneo ya msaada wa vipandishi vya kuokolea yanaweza pia kujumuisha suala zima la njia za kuingilia na kuondokea. medical model: mtindo wa kitabibu: mfumo unaomuona mtu mwenye ulemavu kama mgonjwa na mwenye kuhitaji kutibiwa au kurekebishwa. Marekebisho huchukuliwa kuwa mchakato wa kuweka sawa kilema kufikia kiasi cha kuweza kuchangamana kwenye jumuia. Yanayomkuta (mhusika) baada ya marekebisho hayachukuliwi kuwa majukumu ya mabingwa wa tiba. 130 Uwezeshaji huthaminiwa tu kwenye muktadha na kiwango cha kumwezesha mtu mwenye ulemavu kufanya shughuli muhimu za kila siku zinazohusiana na kujitegemea. Wajibu mdogo tu ndio huwekwa kwenye mchango wa suala zima la mikingamo, ikiwa ni pamoja na mazingira, mifumo, na mitazamo ya wanajamii dhidi ya mwenye ulemavu. melanin: melanini: 1. rangi ya asili ya kahawia au nyeusi hasa kwenye seli za ngozi au nywele katika baadhi ya wanyama k.v. binadamu yenye kusababisha kiumbe kuonekana na rangi yake ya asili. 2. rangi nyeusi inayotokana na kemikali ya mwili ya tirosini, ambayo hupatikana katika ngozi, nywele, koraidi ya jicho na katika misuli. xciii membrane: utando: tabaka ambalo hufunika au kutanda katika sehemu ya tishu au ogani. meningitis: homa ya uti wa ubongo: ugonjwa wenye kusababishwa na makundi mbalimbali ya vimelea k.m. virusi, bakteria, kuvu na protozoa. Japo ugonjwa huu hutibika, lakini katika baadhi ya matukio husababisha ulemavu ama wa muda mrefu au hata wa kudumu k.v. kupoteza kumbukumbu, kukosa umakini, ugoigoi, uziwi, maumivu ya kichwa, uzito wa kujifunza, kifafa, mpoozo wa sehemu za mwili au ubongo, matatizo ya kimatamshi, kupoteza uwezo wa kuona, n.k.

149 menopose: ukomahedhi: kupindi ambacho mwanamke huacha kupata hedhi ambacho kwa kawaida huanzia umri wa miaka 50 na meningocele: meningoseli: aina kuendelea. nyingine ya menstruation: hedhi: damu inayomtoka ugweutimchomozo kila mwezi mwanamke aliyebalehe ambapo utando kama dalili za kukomaa kwa yai la wenye kufunika uzazi ambalo halikukutana na ugweuti huchomoza mbegu ya kiume. kupitia kwenye menstruation circle: mzungukohedhi: uwazi uliopo kipindi maalumu kutoka hedhi moja kwenye uti wa hadi inayofuatia. mgongo au mental age: umri komavu: umri ambao kichwani na kutengeneza uvimbe au mtu hukomaa kiakili. kifuko mgonngoni. Agh. uti wa mental capacity/competence: uwezo ubongo huwa hauharibiki na wala wa akili: ufahamu mzuri wa matokeo hapatokei matatizo ya muda mrefu, ya tendo. Hiki hutumika kama kigezo japo kwa nyakati kadhaa yanaweza cha kisheria kwa baadhi ya nchi kujitokeza. Aina hii ya kukiuka haki za mtu mwenye ugweutimchomozo ni ya nadra sana. matatizo ya afya ya akili kuifikia meningomyelocele: meningomiloseli: mifumo ya utoaji haki. kifuko kilichochomoza mgongoni mental construction: kujengeka kiakili: kupitia kwenye uwezo wa kuunganisha taarifa na tundu batili katika kile ambacho tayari kinafahamika. uti wa mgogo mental disability: ulemavu wa akili: 1. ambacho huwa maradhi au mvurugiko wa akili na kiwoevu, ambao unajidhihirisha sana vishipa vya damu, kisaikolojia au kimwenendo. 2. uti wa ubongo kikomo cha uwezo wa kutenda kiakili ulioharibika na shughuli za kisaikolojia katika utando. Daima viwango vya kawaida kwa huwapo na kiasi fulani cha kupooza; binadamu. Yaani, ukomo wa pia hidrosiferasi inaweza kujitokeza. ufahamu, kushika mambo na Mara nyingi ugweutimchomozo kuyakumbuka; hivyo, ni ukomo wa hutokea sehemu ya juu ya mgongo uwezo kiakili. Ukomo huu wa au kuelekea kwenye mfumbatio. kisaikolojia kama ulemavu wa akili (taz. spina bifida ). pia humaanisha, kwa namna moja 131

150 au nyingine stadi za mota kama stadi za akili kuvurugika kiutendaji, kistadi na kimwenendo. Ulemavu wa akili hujumuisha: udumavu wa akili, mvurugiko wa ujifunzaji, mvurugiko wa utaratibu wa ukuaji na uwasilianaji. mental disorder: mvurugiko wa akili: mwenendo wenye umuhimu kimatibabu, dalili za kisaikolojia au mfumo ambao humtokea mtu na ambao kwa kiasi kikubwa huhusishwa na dalili za maumivu au kilema katika eneo moja la utendaji au zaidi. Kuvurugika huku agh. huishia kwenye msuguano kati ya mtu na jamii kwa kudhihirisha ukengeufu ambao unaweza kusababisha na madhara au la. mental health (or well-being): afya ya akili: ukamilifu wa kiakili, kihisia, kimwili na kiroho. Uhusiano wa kimatunzo, makazi, mitandao ya usaidizi ndani ya jamii, ajira na wasaa wa kupumzika huchangia kwenye afya ya akili. Hata hivyo, maishani hakuna ukamilifu, hivyo afya ya akili ni pamoja na kujifunza stadi za kukabiliana na mabadiliko kimaisha kwa kadiri inavyowezekana. mental illness: maradhi ya akili: hali ya mtu kutokuwa sawa kiakili. Japo haya yanaweza kuwa maradhi ila ya viwango tofautitofauti, mnyanyapao, mitazamo hasi ya jumla husababisha ulemavu wa kisaikolojia kwa kumuua yule anayeathirika kisheria pale 132 anapobainishwa kama asiyekuwa na akili timanu, mwehu, kichaa, mwendawazimu, n.k. Maradhi ya akili ni hali yenye kushawishi jinsi mtu anavyohisi au kuenenda katika kuhusiana na wengine au/na mazingira yaliyomzunguka. Maradhi haya yasipotibiwa agh. humsababisha mhusika kushindwa kukabiliana na taratibu za kila siku na mahitaji ya maisha. Sababu zinazochangia kuwapo kwa hali hii ni pamoja na: vichocheo vya kinasaba, kibiolojia, kisaikolojia na kimazingira na dalili zake huwa ni: mfadhaiko, hisiageugeu, hofu, n.k. mental incapacity (also incompetence or deficiency): upungufu wa akili:** hali ya mtu kutokuwa na ukamilifu wa akili. Hata hivyo, misamiati kuhusu hali hii inayotumika katika nyanja za kisheria, kielimu na kitabibu hulenga kumwelezea mtu anayedhaniwa kutokuwa na akili timamu katika namna ya kukandamiza haki yake ya kujifanyia uamuzi kuhusu mstakabali wake. Agh. mtu aliyebainishwa hivyo, huwekwa chini ya uangalizi wa mtu mwingine.(taz. mental health ). mental or emotional disturbance: kuvurugikiwa kiakili au kimhemko: taz. emotioanal disorder. mentally impaired (MI): mwenye kilema cha akili: dhana inayotumika kumbainisha mtu mwenye matatizo makubwa ya kihisia au mvurugiko kisakiatria.

151 mentally retarded: mwenye udumavu akili: hali ambapo mtu hukabiliwa na ugumu katika ujifunzaji, kutindikiwa sana na kiwango cha akili au/na ulemavu wa ukuaji. Huko nyuma matabibu waliielezea hali hii kama taahira ya akili**. mental retardation (MR): taahira ya akili** 1. kiwango cha utendaji kilicho chini ya wastani wa hisaweledi sanjari na: i) upungufu wa jinsi ya kujirekebisha kuendana na maisha ya kila siku; ii) ufanisi mdogo kielimu hususani katika kujifunza stadi za kuwasiliana, kijamii, kitaaluma, kiufundi na kuishi kwa kujitegemea. 2. kuchelewa kwa ukuaji kiakili au kukua kwa taratibu mno. Mtoto hujifunza vitu taratibu zaidi kuliko wenzake wenye umri sawa. Japo hali hii haitibiki, uchocheaji humsaidia mtoto kupata uwezo zaidi na kwa kasi zaidi. Mtazamo wa kitabibu na kihisani usiozingatia hisia za mhusika huitambulisha hali yenyewe kama taahira ya akili**, msoto**, n.k. Istilahi sahihi kwa hali hii ni: udumavu wa ukuaji kiakili. mental status examination: uchunguzi uluwa wa akili: 1. mchakato wa kukadiria utendaji wa kisaikolojia na kimwenendo kwa kumwangalia mgonjwa, kudadisi jinsi anavyojitambua mwenyewe na usaili rasmi. 2. uandaaji wa mifuno ya kihaiba kuhusu vitu vinavyoweza kuelekeza visa vya historia na ukuaji wa kila hali ya kisakitria 133 inayojitokeza. 3. ukadiriaji wa uwezo na ukubalifu wa kushiriki katika matibabu mujarabu. mental status: hali ya akili: kiwango na mfumo wa utendaji wa akili ikijumuisha utendaji wa akili ya mtu, hisia, mitazamo, saikolojia na masuala ya haiba. Istilahi hii hutumika zaidi kujielekeza kwenye matokeo ya uchunguzi wa hali ya kiakili ya mgonjwa. mercy killing: uuaji kihisani: hali ambapo katika baadhi ya nchi tabibu anaruhusiwa kukatisha uhai wa mgonjwa ambaye ama amekuwa mahututi kwa muda mrefu au mwenye ulemavu mkubwa kwa kisingizio cha kumpunguzia mateso. (taz.. euthanasia). merit: ustahili: sifa inayotokana na mtu kuonyesha tabia nzuri, sifa njema, matendo mema au limbikizo la tajiriba katika fani yake. metabolic disorder: mvurugiko wa kimetaboli: 1. hali au maradhi yanayohusiana na kutofanya kazi kwenye michakato ya kikemikali na shughuli za mwili. 2. kasoro kwenye uwezo wa mwili kuchakata dutu na virutubisho katika hali na viwango vya kawaida. Kukosekana kwa tiba kwa mtu mwenye matatizo ya kimetaboliki husababisha udumavu wa akili na wakati mwingine hata kifo. Katika baadhi ya hali, lishe ndiyo tiba. Hali kama hizi hutokea kwa nadra na huhitaji kutibiwa kwenye vituo vilivyobobea kwenye

152 mivurugiko. Wakati mwingine, hujulikana kama kasoro za kuzaliwa. metabolism: umetaboli: ujumla wa mabadiliko ya kikemikali na kimaumbile katika mwili hai. xciv metastasis: metastasisi: ueneaji wa seli za saratani kutoka sehemu yenye ugonjwa hadi sehemu nyingine ya mbali mwilini kwa kupita kwenye mishipa ya damu au/na mishipa ya limfu. xcv metastatic: -a metastasisi: -enye kusambaa hujielekeza kwenye seli za uvimbe katika sehemu nyingine za mwili. micro-nutrients deficiency: tindikiwa virutubishoi: hali ya kuwa na kiwango cha chini sana cha vyanzo vya lishe bora ambayo huuathari vibaya utendaji kazi wa mwili. Kukosekana kwa baadhi ya virutubisho wakati wa ujauzito, umri wa chini ya miaka mitano, balehe, kunyonyesha, na uzee huzorotesha afya na halafu kusababisha aina fulani za ulemavu ama kwa mama au kwa mtoto aliye tumboni. midbrain: ubongokati: sehemu ya kati ya ubongo inayotokana na nyuzi za neva zinazoungana na kusikia. midget: kibete**: dogo sana (pia taz. dwarfism ). mild learning and behaviour disorders: mvurugiko mdogo wa akili na ujifunzaji: hali ya upambanuaji wa jumla wa mivurugiko inayohusishwa na 134 utendaji kitaaluma au/na uhusiano wa mtu na jamii, upungufu ambao kijumla hujidhihirisha katika mazingira ya shule na kulazimisha mtu kupewa muawala wa huduma za ziada kuliko zile ambazo hutolewa katika mfumo wa kawaida wa elimu. Hata hivyo, inadhaniwa kuwa mtoto mwenye mvurugiko wa kadiri kwa muda mwingi hubakia katika mfumo wa kawaida wa masomo. Ukubwa wa kiwango cha kutindikiwa kiutendaji kwa kundi hili huanzia ukengeufu moja hadi mbili chini ya nafsi ya mtu au/na ndani ya mtu ambaye kumbukumbu zake zinawekwa. minimize: kuwa kimachini: kinyume cha kimajuu. misandry: chukikiume: hali ya kuwa na chuki dhidi ya wanaume kunakodhihirishwa na: ubaguzi kijinsi, ubadilishaji wa jinsi za kiume, ukatili dhidi ya wanaume, kukataa tendo la unyumba. misogynist: mchukiandoa: mtu mwenye kuchukia ndoa. misogamy: misogami: hali ya kinyurotiki ambapo mtu huwa na chuki dhidi ya kitendo cha yeye mwenyewe kuoa au kuolewa. misogyn: chukikike: tabia ya kuwakwepa, kuwachukia au kutowaamini wanawake. mistreatment: utendeaji vibaya: hali ya mtu kufanyiwa jambo kinyume cha taratibu au sheria.

153 mobility: ujongevu: uwezo wa mtu wa kujisogeza kwa urahisi kutoka eneo moja hadi jingine. mobility aid: kisaidia ujongezi: kifaa ambacho hubuniwa ili kusaidia kudemadema au kuboresha utembeaji wa mtu mwenye kilema, mathalani, cha nyonga, miguu, macho, n.k. Zipo aina nyingi za visaidizi vinavyomwezesha mtu mwenye matatizo ya ujongeaji kutegemeana na aina na kiwango cha kilema alichonacho pia kiwango cha teknolojia katika eneo alipo. Vifaa hivi ni pamoja na: kitimwendo (sampuli mbalimbali), skuta, bakora, fimbo nyeupe au aina nyingine maalumu na mbwa mwongozaji. Kwa kutegemeana na mahitaji binafsi ya mtumiaji, wenzo kama huu husaidia: a) kudumisha hali ya kutembea wima ukiboresha uimara kwa kuupunguzia uzito mguu ambao ni mfupi; b) kuchapusha misogeo; c) kuashiria eneo ambalo usawa wake 135 hubadilikabadilika; d) kuongoza njia ikiwa ni pamoja na kuashiria hatari. Kutokana na umuhimu wake, kisaidizi cha aina hii hujitokeza sana kwenye nyaraka za kiserikali mathalani, kuhusiana na misamaha ya kodi na nauli kwenye vyombo vya usafiri. Ikumbukwe umuhimu wa kumwezesha mhusika kutembea au kunyanyuka kutoka alipo sawa na yule asiyetumia nyenzo, basi kisaidizi huchukuliwa kuwa sehemu ya mwili wake ndiyo maana kwa sheria za kimataifa hakipaswi kugharamiwa wakati mtumiaji wake anaposafiri nacho kwenye vyombo vya usafiri hasa wa umma. (ling. Na nsiso). mobility disability: ulemavu jongezi: hali ambapo mtu hushindwa kunyanyuka na kutembea kawaida kutokana na ama kukosekana kabisa kwa miguu yote miwili, kuwa na mguu mmoja au miguu iliyopo kuwa tepetepe au kujikunyata. Visababishi vya hali hii ni pamoja na kuzaliwa nao, maradhi, na ajali. Kutokana na mitazamo ya kihisani, kidini, kiutamaduni na kitabibu, hali

154 hii hupachikwa majina k.v. kiwete**, mwendo chopi** au chopea** ambayo kimsingi humdunisha mhusika. Kwa muktadha wa kijamii, jina ulemavu wa ujongeaji hupendelewa zaidi na wahusika. microcephaly: mikrosefali: hali ya mtu kuzaliwa na kichwa kidogo kuliko kawaida (mzingo wa kichwa ukihitilafiana mara tatu chini ya wastani kwa kuzingatia umri na jinsi). Matokeo ya hali hii ni kichwa kushindwa kukua wakati uso ukiendelea kukua kwa kiwango cha kawaida kiasi cha mtu kuishia kuwa mwenye kichwa kidogo, paji la uso lenye kuelekea nyuma, na ngozi ya kichwa iliyokunjamana. Kwa kadiri umri unavyozidi kukua, udogo wa fufu huzidi kujidhihirisha japo hata umbo zima la mwili huwa na uzito mdogo na udumavu. Pia mtu wa aina hii huchelewa kujongea na kutamka, hujishughulisha kuliko kawaida na huonyesha dalili nyingine za ulemavu wa akili, mitukutikomwili na umri wa kutarajiwa kuishi huwa mfupi. Vichocheo vya hali hii ni vinasaba, maambukizo ya virusi vya zika vinavyosambazwa na mbu na sababu nyingine za makosa ya kibinadamu. 136 modality: utaratibu: kwa muktadha wa ulemavu, istilahi hii humaanisha njia ambayo mtu hupatia taarifa na kwa jinsi hiyo kujifunza. Dhana ya mfumo hudai kuwa mtu hujifunza vizuri kupitia mfumo mmoja kuliko mwingine. Mathalani, mtoto anaweza kupata taarifa vizuri zaidi kupitia mfumo wa kuona au kutazama kuliko ule wa kusikia. model home: mastakimu mfano: kwa muktadha wa watu wenye ulemavu, nyumba ya mfano ni ile inayozingatia kanuni ya usanifu kwa ajili ya wote; yaani nyumba isiyokuwa na mikingamo ya kimazingira. Kwa mfano, uwepo wa ngazimbetuko, milango yenye upana wa kutosha, sebule iliyopangiliwa vizuri na yenye nafasi, msalani eneo la kunawia mikono au/na kuwashia taa vyote vinazingatia urahisi wa mtumiaji aliye kwenye kitimwendo au wa kimo kifupi. modelling: uoneshaji mfano: mchakato wa ufundishaji ambapo mwalimu huonyesha mwenendo unaofaa au stadi ya kujifunza kama njia ya ufundishaji. modify: rekebisha: badili kitu kwa kiasi kidogo kwa kukifanya kifae zaidi kukidhi kusudio mahususi. mongol or mongoloid: taz. dwarfism. mongolism: umongoli:** dalili za udumavu akili ambazo ni k.v. mlimbikodalili wa aina ya Langdon, na mvurugiko wa chembeuzi 21.

155 monoplegia: monoplejia: kupooza kwa kiungo kimoja, agh. mguu au mkono. monument: kumbukumbu: jengo, mnara au sanamu ya ukumbusho. 2. kazi ya mfano bora inayostahili kukumbukwa. mood swings: mabadiliko mhemko: hali ya mtu kuwa na hisia zisizotabirika; yaani kwa wakati mmoja kuwa mchangamfu na ghafla kuanza kulia au kunyamaa kimya bila sababu ya msingi. mood: sununu: hisia ya kudumu na iliyopindukia ambayo hushawishi jinsi mtu anavyoiona dunia k.v. sononi, furaha, hasira, shauku. motivated:-enye hamasa: -enye kupata msukumo wa ndani kufanya jambo hasa baada ya kutambuliwa, kuthaminiwa au kupewa motisha. Wakati mwingine, hamasa inaweza kushajiishwa na shida au chukizo dhidi ya hali fulani. Hiyo inakuwa ilhamu ya kushupalia jambo. motor development skills: stadi imarisha misogeo: ujuzi na utendaji wa mifumo inayohusiana na ukuzaji na matumizi ya misuli na sehemu za mwili kama vile mikono, miguu. Ukuzaji wa stadi za misogeo ni matakwa ya kujimudu na kutenda. motor. mota: mfumo wa utendaji kazi wa mwili unaohusiana na mwendo kama vile neva zinazotoka kwenye uti wa mgongo au ubongo 137 zikiruhusu misuli kujikunja na kunyooka. multi-disabilities: ulemavu tofautitofauti: hali ya kuwa na vilema zaidi ya kimoja kama vile kupofuka na kuwa na udumavu akili; kukosa uwezo wa kujongea na kuwa na udumavu wa akili, uziwi au upofu. Muunganiko wa vilema hivi husababisha mtanziko mkubwa wa kielimu kiasi kwamba mtoto hawezi kuhusishwa kwenye programu za elimu maalumu kwa kuzingatia aina mojawapo ya vilema alivyonavyo. multidisciplinary evaluation or assessment (MDE): tathmini kwa vigezo mbalimbali: 1. upimaji ubora na udhaifu wa mtoto kwa kutumia vigezo mbalimbali vya kitaaluma, vyanzo tofauti vya taarifa na kuhusisha wazazi wa mtoto. Kimsingi, ni upimaji wa kiwango cha wakati uliopo cha mtoto kimaumbile, kinyurolojia, kiutambuzi, kiuongeaji, lugha, ukuaji kisaikolojia na stadi za kujimudu. 2. hali ya upimaji unaofanywa na wanataaluma zaidi ya mmoja (kama vile waelimishaji, wanasaikolojia na wengineo) wanapofanya kazi kwa pamoja na kushirikishana taarifa kwenye tathimini, upimaji na uandaaji wa afua mbalimbali. multi-grade classroom: darasa mchanganyiko: chumba cha darasa chenye kuchanganya

156 watoto wa madarasa zaidi ya moja. multiple sclerosis MS/(disseminated sclerosis or encephalomyelitis disseminate): maradhi ya kukakamaa kwa tishu: ugonjwa sugu, agh. endelevu unaohusisha uharibifu kwenye ngozi za nje za neva za seli ndani ya ubongo na uti wa ubongo. Dalili zinaweza kuhusisha ganzi, ulemavu wa kutamka na kupatana kwa misuli, uono hafifu na uchovu. mumps: matubwitubwi: ugonjwa wa kuambukizwa virusi, wenye dalili za kuvimba tezi za mate za parotidi ambapo agh. hutokea utotoni. xcvi muscle dystrophy: distrofi ya misuli: hali ambapo misuli hudhoofika na kuendelea kuwa dhaifu. hali hii inaweza kushughulikiwa kiurahisi kwa kutumia miwani ili kuufanya uoni uwe angavu usio na maruweruwe. Kasoro hii hutokana na mchepusho kwenye jicho. Japo kisababishi halisi cha hali hii hakifahamiki, wataalamu wa macho wanadai kuwa ni kutokana na uchovu wa macho unaosababishwa na matumizi ya kompyuta na vitu vingine vilivyoenea vya kuangalia karibukaribu vikiambatana na sababu za kinasaba. Dalili za uoni wa karibu ni kuwa na taabu kusoma alama za barabarani na kuona vitu vilivyo mbali kwa uwazi ila ni vyepesi kuona vizuri vitu vya karibu k.m. kusoma na kutumia kompyuta. Dalili nyingine za miopia ni mkazo wa macho na maumivu ya kichwa, kusikia uchovu wakati wa kuendesha gari au kucheza michezo. muscleskeletal: misuli kiunzi mifupa: muunganiko kati ya mifupa na kano ambavyo kwa pamoja huuwezesha mwili kufanya misogeo na shughuli mbalimbali kama vile kunyanyua vitu, kutembea, kujipindapinda, n.k. myopia: miopia: 1. hali ya kuona vitu vilivyo karibu. Kwa baadhi ya watu, 138

157 Nn name calling: ang. labelling. natural environment: mazingira asilia: mazingira ambayo ni asilia kwa mtu; yaani, nyumbani, sehemu ya makazi, hospitalini, n.k. nature: hali ya asili: ulimwengu, viumbe vyote, utaratibu wa jambo la asili, kawaida ya vitu vyote. needs-based: -enye kuzingatia mahitaji: -a kuamua huduma sadifu ambazo ni muhimu kabisa kwa mahitaji ya mtu na familia yake. negativism: ukanajii: hali ya mambo ambapo mahitaji ya mtu na hasa mtoto mchanga huzidi kiwango cha utendaji wake na hivyo kusababisha hali ya kujitenga na ukimya. negativistic: mkanaji: mtu mwenye silika ya kukanusha. neonatal:-a mtoto mchanga.-enye kuhusiana na mtoto katika kipindi cha majuma ya mwanzo baada ya kuzaliwa. nerve: mshipafahamu au mshipa wa neva: kambakamba nyembamba ambamo ujumbe hupitia kuenea mwilini. Neva ni tarishi wa mwili. Baadhi ya neva humfanya mtu kuhisi vitu na humfahamisha pale kitu kinapouma. Neva nyingine huufanya mwili ujisogeze mbali na sehemu ya hatari k.m. moto, miiba, n.k. nervous condition: wasiwasi: hali ya kukosa utulivu wa moyo kutokana na jambo la kushtusha. neurological dysfunction or impairment: kilema cha nyurolojia: hali ya milango ya fahamu au mota kutoweza kutenda shughuli ipasavyo kutokana na kuharibika au upungufu kwenye mfumo wa mishipa ya neva mwilini. neuropsychologist: msaikolojia nyurolojia: mtaalamu wa saikolojia na matibabu ya akili anayeweza kupima na kumfahamisha mtu hali yake na kutoa mapendekezo ya tiba na mipango ya elimu, lakini hana mamlaka ya kuelekeza dawa za kumtibu mgonjwa (taz. occupational therapist na neurolosurgeoon ). neurosis: nyurosisi: 1. mwenendo unaohusisha kutojipangilia vizuri na hudhihirishwa kwa kuwa na wasiwasi, ushurutishaji, kujawa na hofu, woga, fazaa, jakamoyo, n.k. 2. ugonjwa wa akili wenye kubainishwa kwa dalili mbalimbali za kifikira na kimatendo kufuatia tukio kubwa au dogo. neurosurgeon or neurological surgeon: mpasuaji mfumoneva: daktari bingwa aliyefuzu upasuaji wa ubongo na mifumo ya neva. Mathalani, mpasuaji mfumoneva agh. huitwa kuingiza au kubadilisha mirija inayotumika kuondoa kiowevu 139

158 cha ziada kutoka kwenye ubongo wa mtu aliye na hidrosiferasi. neurotic disorder: mvurugiko wa nyuroni: ulemavu wa akili ambao dalili yake kuu ni usumbufu unaogunduliwa na mhusika mwenyewe kiasi cha kutoukubali wala kupoteza tabia yake ya awali. noise suppression: udhibiti kelele: uzuiaji wa sauti kwa kutumia nyenzo za kusikilizia zenye mfumo uliosanifiwa ili kuchuja sauti zisizotakiwa. Mfano, kukuza sauti yenyewe, kubana sauti, kuchakata ishara moja kwa moja, n.k. Baadhi ya aina za shimesikio huwa na programu maalumu ambapo kwa kutumia teknolojia ya kidijiti, hurekebisha mifumo ya usikivu moja kwa moja kulingana na mazingira. noise-induced deafness: uziwi unaosababishwa na kelele: kilema cha uziwi kinachoongezeka polepole kutokana na mhusika kwa muda mrefu kuwa kwenye kelele zinazozidi viwango vinavyokubalika. nominate: pendekeza: taja rasmi mtu au kitu kwa ajili ya nafasi, wajibu au tuzo muhimu. non-compliance: -siyotii: kutofuata maelekezo au sheria. (a) kuhusiana na mtoto, ni yule anayeonyesha kuwa na mwenendo wa kikorofi. (b) kuhusiana na utoaji huduma, ni wakala asiyetimiza matakwa ya kisheria au kanuni. 140 non-disabled: wasio na ulemavu: kinyume cha wenye ulemavu. non-negotiable: -siyojadilika: dhana hii husisitiza stahiki ya mtu ambako hahitaji mapatano ya kiasi gani cha kutolewa na wakati wa kukitoa; kutoa au kutotoa, bali ni kutolewa k.m. haki za binadamu ni miongoni mwa masuala yasiyotakiwa kujadiliwa. non-traditional: -siyo desturi: -enye hali isiyokuwa ya kawaida agh. kwa kundi maalumu la watu k.v. wanawake au wanaume kuwa kwenye ajira ambazo kwa desturi hufikiriwa kutokuwa sadifu kwa jinsi yao; mathalani, mwanamke mwenye ulemavu kufungishwa ndoa rasmi na kufanyiwa sherehe ya harusi. normal or normality: ukawaida: dhana ya jumla ya mienendo au uwezo unaofikiriwa kufikia viwango vya wastani vinavyokubalika na visivyo vya kipekee. normalisation principle: kanuni ya ukawaida: 1. utaratibu wa kuyafanya maisha na mazingira ya mtu kuendana na utamaduni kadiri inavyowezekana. 2. utaratibu kwamba mtoto na familia yake wanapaswa kupata huduma katika mtindo na mazingira ya kawaida kwa kadiri inavyowezekana. Kufanya hivyo husaidia mtoto na familia yake kuwa au kuendelea kuwa sehemu ya jamii yao.

159 nullify: batilisha: fanya kitu kama vile makubaliano au mkataba wa ndoa kulegeza nguvu au athari ya kisheria. nurture: mafunzo: malezi anayopaswa kupewa mtoto ambayo huamua ni kiasi gani cha uwezo kinahusiana na ushawishi wa utamadunijamii tofauti na ule wa kuzaliwa nao. nutrition assessment: upembuaji lishe: 1. ukusanyaji na upimaji wa taarifa zenye kuhusiana na virutubisho ambako hufanywa na mtaalamu wa lishe aliyesajiliwa, na anayeweza kuthibitisha kuwapo kwa tatizo la lishe au kisababishi (chake). 2. ukusanyaji na ufanyaji tathmini ya taarifa zenye kuhusiana na kiwango cha chakula alacho mtu, mtindo wake wa maisha pamoja na historia ya matibabu. Jambo hili hufanyika kwa mgonjwa ambaye amechunguzwa na daktari bingwa aliyesajiliwa na anayeweza kuthibitisha matatizo ya lishe yanayomkumba mgonjwa. nutrition package: lishekamili: mlo wenye vyakula vilivyo na virutubisho vinavyohitajika katika kulinda siha ya mwili, kujisikia vizuri na kuwa mwenye nguvu. Viinilishe hivi ni pamoja na: protini, wanga, mafuta, maji, vitamini na madini. Hivi vikichanganyika na desturi ya kufanya mazoezi ya viungo, huwa hakikisho la kudhibiti uzito, kuhifadhi afya na uimara wa mwili. Kwa yule wanayegundulika kuwa na saratani 141 ya matiti, au anayepata matibabu, kula vizuri ni muhimu zaidi. Kile kinacholiwa kinaweza kuathiri kinga ya mwili, sununu, na kiwango cha afya. Zaidi ya yote, lishe bora wakati wa ujauzito na kunyonyesha maziwa ya mama ni njia murua ya kumkinga mtoto dhidi ya aina mbalimbali za ulemavu. nutrition screening: tathmini lishe: hatua ya ukusanyaji wa taarifa za mtu kwa minajili ya kugundua kiwango chake cha lishe mwilini. Lengo ni kufahamu matatizo na kutoa ushauri wa jinsi ya kuyatatua. (taz. nutrition assessment). nutrition services: huduma lishe: hali ya kumsaidia mtoto na familia yake kwa kuhakikisha anapata kiwango cha juu cha lishe. Hii inaweza kujumuisha vijalizo vya lishe au tibalishe. nutritional supplements or therapy: tibalishe au vijalizo vya lishe: mlo unaotumika badala ya au kujaliza ule wa kawaida pale mhusika anaposhindwa kupata lishe inayotosheleza kwa njia ya kawaida. nutritionist: bingwalishe: mtaalamu wa lishe ambaye hutathmini tabia ya

160 ulaji wa mtu na uluwa wake kilishe. Bingwalishe anaweza kutoa ushauri juu ya tiba za kawaida, lishe na mbinu maalumu za kuongeza stadi za mtu za ulaji. nutrients: virutubisho: kiini kwenye chakula kinachowezesha mwili wa binadamu kukua na kupata nguvu au joto. nystagmus: nistagmasi: uchezeshaji wa jicho usiokuwa wa hiari unaofanyika harakaharaka. 142

161 Oo obesity: utipwatipwa: hali inayohusianishwa na mtu kuwa na ziada kubwa ya mafuta mwilini ambayo husababishwa na ulaji wa vyakula vyenye kalori nyingi hususani vile vyenye mafuta na sukarisukari kuzidi kiasi kinachoweza kuunguzwa kwa njia ya kuushughulisha mwili. Nguvu za ziada huhifadhiwa mwilini katika hali ya mafuta hata kusababisha mabadiliko dhahiri ya umbo la mwili, kutishia uhai kwa kuchochea matatizo makubwa ya kiafya, mathalani, kisukari, maradhi ya mishipa ya moyo, aina fulanifualni za saratani (titi au utumbo), na kiharusi. Halikadhalika, hali hii huweza kuathiri ubora wa maisha na kusababisha matatizo ya kisaikolojia kama vile mhusika kujidunisha na kuwa na mfadhaiko. Njia ya kubainishia utipwatipwa ni kwa ukokotoaji wa fahirisi ya ukubwa wa mwili (uzito), na kimo. Kwa mtu mzima mwenye kipimo cha kuanzia sentimeta 30 na kuendelea au mwanamume mwenye kufikia mzingo wa sentimeta 94 na zaidi au mwanamke anayefikia mzingo wa sentimeta 80 na zaidi huchukuliwa kuwa tipwatipwa labda kama anatoka kwenye makundi ya wanyanyua vitu vizito, wanandondi, wanamieleka, n.k. 143 Hali za kiafya kama hizi zimesababisha sheria katika baadhi ya nchi k.v. Kanada, kutoa tafsiri yenye kuzingatia suala la ubaguzi ambapo karibu kila mwenye utipwatipwa hukabiliwa nayo. Katika tafsiri hii, ulemavu hauangaliwi tena kuwa hali isiyoweza kubadilika kama ilivyochukuliwa kwenye tafsiri za awali (kwa kuzingatia ukomo wa kiutendaji wa mwili k.v. upofu au paraplejia) ila kwamba ulemavu ni zaidi ya hali za uhaitiba na unaweza kuwapo hata nje ya ukomo wa kiutendaji. objectives: malengo: hatua ndogondogo zinazochukuliwa ili kutimiza lengo kuu. (ling. na goal). obsessions: ung ang anizi: hali ya kujirudiarudia kwa fikira, wazo, taswira au shauku ambayo hutokea bila hiari, mawazo yenye kuivamia dhamiri. Hali hii hudhihirishwa na mivurugiko ya shauku na inaweza kuonekana sawia na mvurugiko wa akili. obsessive-compulsive disorder (OCD): mgubiko shurutishi: 1. hali

162 ya wasiwasi inayojitokeza yenyewe kwa kujirudiarudia au kutokana na mashinikizi ya kudumu. Hofu ni fikira, mawazo au taswira za ndani, wakati mashurutisho ni tabia za kujirudiarudia au matendo ya akili ambayo mtu hulazimaka kuyafanya. 2. kasoro ambayo hubainishwa na mawazo shinikizii yasohiari yenye kujirudiarudia na kupoteza muda, kuchochea hofu na kuingilia utendaji kwenye maisha ya kawaida. Kasoro hii hujikita kwenye ncha ya mwendelezo ambapo kila mtu hujikuta. Takribani kila mtu hukumbwa na mawazo shurutishi au/na kuonyesha mienendo shinikizi. Hata hivyo, mawazo na mienendo hii kuweza kuwa tatizo kwa mtu hutegemeana na kiwango cha kuingilia utendaji wa kawaida au athari kwenye uzuiaji wa kufurahia maisha. obstacle: kizuizi: kitu kinachokwamisha utendaji wa jambo fulani. Kitu kilivyo ndani ya nafsi ya mtu kinachomzuia kujitatulia matatizo k.m. hofu, chuki, n.k. Kizuizi cha nje huwa nje ya nafsi ya mtu (k.m. kutengwa na familia au jamii, kunyimwa fursa, n.k.) japo nacho huzuia utatuzi wa matatizo, mhusika huwa hana uwezo wa kukidhibiti (ang. barriers ). ocular muscle problem: hitilafu za mishipa ya macho: hali ya kuwa na kasoro katika mishipa ya 144 macho. Hitilafu ya kawaida zaidi ni ya aina ya makengeza (jicho moja au yote mawili kuwa nje ya mpangilio wa uelekeo); kuelekea nje, ndani, juu au chini kutegemeana na aina ya mishipa iliyoathirika. Hali inaweza kurekebishika kwa njia ya upasuaji endapo itagundulika ndani ya miezi sita baada ya kuzaliwa. Kila mwaka unaopita bila matibabu, huondosha uwezekano wa usahihi wa marekebisho na pia hupunguza uoni kwenye jicho mojawapo. occiptial lobe: ubongo nyuma: sehemu ya ubongo iliyo nyuma ya kichwa (kisogoni) ambayo ni muhimu katika kuchakata, kutafsiri na kumwezesha mtu kutambua kile kinachooneka kwa jicho. Iwapo sehemu hii ikipata hitilafu kwa kulemaa au kuumia, mhusika hawezi kutafsiri kwa usahihi alama zinazoonekana mbele yake, na hivyo kutokea mvurugiko. occupation: -a shughuli, -a kazi: tendo la kujihangaisha na kwa kutumia nguvu na maarifa ili kupata matokeo yanayokusudiwa. occupational deafness: uziwi kazini: hali ya kupoteza uwezo wa kusikia sauti inayosababishwa na kelele hususani sehemu za kazi k.v. viwandani, vituo vya kurushia matangazo ya redio na

163 televisheni, migodini, n.k. (taz. noise induced deafness ). occupational therapy: tibaliwaza (pia tibakazi tibakalimaa): taaluma ya kumsaidia mtu (wa umri wowote) mwenye hitilafu ya kiungo au mlango wa fahamu ili amudu walau kufanya shughuli muhimu za kila siku. Mathalani, mtoto mwenye ulemavu kuweza kushiriki kikamilifu katika maisha ya shule na ya kijamii; mtu aliyeumia kuweza kupata upya stadi kama vile kutembea, kuandika, n.k. Huduma hizi hutolewa kwa njia shirikishi baada ya mtaalamu, familia ya mhusika na wadau wengine kwa pamoja hutathmini na kuweka malengo binafsi ya usaidizi unaoweza kuboresha hali ya mhusika kujimudu kiutendaji kulingana na umri, mahitaji na kiwango cha hitilafu. Kwa hiyo, huduma hizi hutolewa majumbani, hospitalini, shuleni, sehemu za kazi, n.k. occupational therapist: bingwa tibaliwaza: mtaalamu anayeshughulikia tibaliwaza. oedipus complex: mapenzi ya binti kwa baba au mvulana kwa mama: hali ya upendo ambayo watoto kati ya umri wa miaka miwili hadi mitano huwa nayo kwa wazazi wao wenye jinsi tofauti (na wao). Inashauriwa kwamba, wazazi wote wanapaswa kuwapo pale alipo mtoto wa kiume au wa kike. 145 Ni kipindi cha maandalizi ya awali kwa ajili ya kuoa au kuolewa. oesophagus: umio: njia ya kupitisha chakula kutoka kinywani hadi tumboni. olfactory:-a kunusa: -enye kuhusu hisia ya harufu au kunusa. ontogenesis: ontojenesisi: ukuaji wa kiumbe au wa ogani ya kiumbe. xcvii opened captioning (OC): kidokezo wazi: alama hii huashiria kuwa vidokezo vinavyofafanua maelezo na sauti nyinginezo zilizochapishwa daima huonyeshwa kwenye mkanda, filamu au programu za televisheni. Vidokezo wazi hupendelewa na wengi akiwamo kiziwi na kila aliye na usikivu hafifu na yule ambaye lugha inayotumika ni ya pili kwake. Kwa kuongezea, mfumo huu husaidia katika kumfundisha mtu na hasa mtoto jinsi ya kusoma. Pia hufanya kupunguza sauti kupunguzwa kwa kiwango cha chini kabisa katika maeneo ya huduma k.v. makumbusho na migahawa, benki, n.k. (ling. closed caption). open classroom: darasa huria: programu na uzoefu vinavyotumika kwa ajili ya mazingira ya kufundishia kumpa mtoto fursa za kubuni shughuli zake za ujifunzaji. open school day: siku ya kutembelewa shuleni: siku ambayo shule huwakaribisha

164 wazazi na wanajumuia kuitembelea na kuona shughuli mbalimbali zinazoendeshwa pale k.v. kimafunzo, kiubunifu, kiuzalishaji au kimichezo. Siku hii ni muhimu sana kutengwa kwenye ratiba ya shule inayozingatia mfumo wa elimu jumuishi ili kuitumia kama mkakati wa kueneza ufahamu. operation: upasuaji/utoboaji: ukataji wa ngozi kwa kutumia vifaatiba maalumu unaofanywa na daktari ili kurekebisha sehemu ya ndani iliyoharibika au kubadilisha mfumo wa ufanyaji kazi mwilini. Hii ni huduma muhimu katika urekebishaji wa viungo mbalimbali. ophthalmologist: daktarimacho: tabibu anayeagua na kutibu maradhi, maambukizi, majeraha au kasoro za kuzaliwa nazo zinazoathiri uoni. Daktari huyu anaweza kuamuru dawa na kutoa matibabu kama vile kurekebisha hitilafu k.m. ambliopia, matibabu ya kutumia mwanga wa leza, upasuaji mdogo, na lenzi za marekebisho. ophthalmology: oputhalmolojia: utanzu ya uganga inayohusu macho. xcviii opportunistic infection: ugonjwa nyemelezi: maambukizo yanayosababishwa na vijidudu au bakteria ambao agh. hauwezi kumwambukiza mtu mwenye kinga 146 madhubuti, ila vinaweza kufanya hivyo pakitokea mabadiliko fulani kwenye mfumo wa kinga k.v. kuwa na virusi vya UKIMWI mwilini. oppositional defiant disorder (ODD): upinzani kaidi: hali ya kisaikolojia inayojitokeza yenyewe kama ruwaza endelevu ya utovu wa nidhamu, uhasama, uasi na kwa makusudi kabisa kuwa tabia za kimapinduzi dhidi ya watu au mifumo yenye mamlaka ambayo huenda zaidi ya mipaka ya tabia za kawaida za utotoni. Haki hii huunganishwa na mvurugiko wa kutindikiwa umakini katika kazi inayofanywa, ulemavu wa kujifunza na mvurugiko wa mawazo (wasiwasi). oppositional disorder: mvurugiko kiupinzani: hila fiche za uchokozi wa chini kwa chini unaojidhirisha kwa mitindo ya ukaidi, lakini kwa ujumla zikiwa ni tabia za kimyakimya. Mtoto mwenye mvurugiko wa aina hii, mara nyingine huwachokoza hata watu wazima au watoto wengine kwa tabia ya ukanaji, ukaidi, usutaji, ukawiaji katika kutekeleza maagizo na tabia nyinginezo. optic:-a kuona: taaluma ya nuru na vifaa vinavyohusishwa na matumizi au vipimo vya nuru. xcix optic atrophy: uoni hafifu: ugonjwa unaotokana na kudhoofu kwa nevaoptiki zinazounganisha retina na ubongo.

165 optic nerve: neva jicho: mshipa wa fahamu unayounganisha jicho kwenye kituo cha kuonea kwenye ubongo. optician: mtaalamu wa miwani: mtu aliyefuzu stadi ya kusaga, kuunda na kuunganisha lenzi na fremu za miwani kama inavyoelekezwa na bingwa wa upimaji wa kuona au daktari wa macho. optometrist: bingwa macho: daktari mbobezi wa kupima jicho lenye tatizo la uoni; kuelekeza aina ya miwani, lenzi na mazoezi ya uoni, na hunasihi na kutoa ushauri maalumu kuhusu matatizo ya uoni hafifu. Bingwa huyo siyo mganga wa kutibu maradhi mengine tofauti na jicho. oral: -enye kuhusiana na mdomo: matendo yanayotendwa kwa kutumia mdomo k.v. kutamka, kunywa, kunyonya, n.k. oral communication: mawasiliano ya mdomo: hali ya mtu (mwenye usikivu hafifu) kutumia kiwango cha usikivu kilichpo ili kupata ujumbe agh. kwa kukuza mawimbi ya sauti, kusoma matamshi na kuongea. orientation & mobility (O & M): ukabilifu na ujongeaji: hali ya mtu kupata maarifa ya kuyatambua mazingira yake hususani mwenye upofu. Maarifa haya humwezesha mhusika kukuza uwezo wa kujongea kwa uhuru na usalama kutoka sehemu moja hadi nyingine. orientation and mobility specialist: bingwa wa ukabilifu na ujongeaji: mtu aliyefuzu kufundisha dhana na mbinu za kumwezesha mtu mwenye upofu au uoni hafifu kutembeatembea. organic: -a kiumbe hai: 1.-a ogani au a dutu: -nayotokana na kiumbe. 2. a wanyama au mimea, 3. Inayoathiri muundo wa ogani. ortho: iliyofanywa sawa: asili ya neno hili ni kumaanisha kuweka sawa kile kinachoonekana kuwa tofauti. orthopedic impairment: kilema mfupa: kasoro, maradhi au majeraha kwenye mifupa, vifundo au misuli ambavyo ni hali ya mtu kuzaliwa nayo k.v. wayopindu, kukosekana kwa kiungo, au kukipata baadaye maishani (polio, kifuakikuu cha 147

166 mifupa, kukatika kiungo, mvunjiko, kuungua au ajali nyinginezo). orthopeadic boots: buti rekebisha mifupa: wenzo wa kitabibu ambao huvaliwa ili kupata nafuu kutokana na majeraha au hitilafu kwenye wayo. Zana hii hutumika sanjari na kalibu, bangiligango ya mguu, au kiungomnemba ili uweze kuhimili uzito wa mwili. orthopedics: urekebishaji vilema mifupa: 1. kinga, kuchunguza, kutibu na kurekebisha hitilafu za mfumo wa misuli kiunzi mifupa. 2. visaidizi, michakato au upasuaji unaofanyika ili kusaidia kuzuia au kurekebisha majeraha au mivurugiko ya mifupa na mifumo ya kiunzi mifupa na misuli, vifundo na ligamenti. orthopedist or orthopod: muothopedia: 1. daktari bingwa kwenye hali zinazoathiri mifumo ya mifupa na misuli. 2. dakatari mpasuaji ambaye ni mjuzi wa kurekebisha vilema hususani vya mifupa. c orthopedic lumbar corset or lumbar orthosis: pagarorekebisha kiuno: kifaa tiba kinachovaliwa kwenye kiwiliwili ili kuimarisha uti wa kiuno. Kifaa hiki hutumiwa kwenye baridi yabisi kali, kasoro za uti au kuvunjika kwa pingili za kiuno na 148 kinaweza ama kuwa na kamba za kukazia kuzunguka kiwiliwili au ulimbo kugandishiwa kwenye mwili wa mtumiaji au kukazwa na vishikizo. orthopsychiatry: tibaakili: mkabala unaojumuisha juhudi za pamoja za kisakaitria, kisaikolojia, kazi ya uamara jamii na akili na mbinu nyinginezo za kitabibu na sayansi ya jamii katika mafunzo na kutibu mienendo ya binadamu kwenye mfumo wa hospitali. Msisitizo unawekwa kwenye mbinu za kinga ili kueneza ustawi wa siha ya kihisia hususani miongoni mwa watoto. orthosis: kirekabisha kilema: kifaa kinachosaidia urekebishaji mifupa kwa ama kuimarisha, kunyoosha, kulinganisha, kuzuia, kurekebisha dosari au kuboresha utendaji kiujongeaji. (ang. braces, corset. Orthopedic lumbar corset/orthosis). orthotics: taaluma ya viungomnemba: fani ya tiba inayojihusisha na kusanifisha, kuzalisha na kutumia aina mbalimbali za visaidizi vya kurekebishia vilema. Taaluma hii hutengeneza vifaa mnemba vinavyotumika nje ya maungo ili kurekebisha tabia za mfumo na

167 utendaji wa mishipanyuroni na ule wa mifupa. Bingwa wa kurekebisha vilema, kimsingi ni mtaalamu wa tiba mwenye wajibu wa kuelekeza, kuzalisha na kusimamia virekebisha vilema na anaweza kutumika kwa: kudhibiti, kuongoza, kufubaza sehemu ya kiungo, kifundo kwa sababu maalumu; kuelekeza msogeo kwenye uelekeo maalumu; kusaidia msogeo katika ujumla wake; kupunguza kani ya kubeba uzito kwa kusudi fulani; kusaidia marekebisho ya mivunjiko baada ya kuondolewa kwa kalibu; kurekebisha umbo au/na utendaji wa mwili, kuwezesha uwezo wa kujongea na kupunguza maumivu. osteoarthritis: osteo-athritisi: 1. hali inayosababishwa na kuharibika kwa gegedu kwenye vifundo, ambapo ukingo wa utando laini unakuwa umeharibika kiasi cha kuruhusu mifupa kusagana. Hali hii hubainishwa na dalili ambazo hujitokeza polepole ikiwa ni pamoja na kukakamaa na madonda ya vifundo, kukakamaa baada ya kupumzika kunakoboresha mijongeo, kuongezeka kwa maumivu baada ya shughuli au kukaribia mwisho wa siku. 2. matatizo yanayotokana na uchakavu wa kifundo kimoja au vifundo kadhaa yanayobainishwa kwa tishu zinazozungukia kifundo kuwa nene na ukuaji wa vifupa kutoka kwenye gegedu, hali 149 ambayo husababisha vifundo kuuma, kutoweza kutumia vifundo hivyo ipasavyo na ulemavu. ci osteoporosis: osteoporosisi: 1. hali inayoathiri mifupa na kuidhoofisha kiasi cha kuvunjika kwa urahisi. 2. kusinyaa kwa mifupa ya sehemu moja au mifupa yote miwilini ambapo tishu ya mfupa hupotea, lakini bila ya kuathiri muundo wa mfupa mzima. other health impairedness: aina nyingine za kulemaa kiafya: hali ya kuwa na nguvu haba au ukakamavu kutokana na kusendeka au matatizo makali ya kiafya kama vile hali ya moyo, kifua kikuu, homabaridi yabisi, uvimbe wa tishu na/au figo, pumu, selimundu, lukemia, hemofilia, kifafa, sumu ya risasi, au kisukari, ambavyo huuathiri vibaya utendaji wa mtu k.m. mwanafunzi kielimu. Mwanafunzi mwenye usonji anapaswa kuwekwa kwenye kundi hili. otitis media: otitisi kati: hali ya kuzidi kwa uvimbe au/na maambukizo katikati ya sikio inayosababishwa na kushindwa kufyonza kiwoevu cha ziada kupitia tyubu ya ustachia. Kwa kushindwa kuigundua hali hii, kunaweza kusababisha kupoteza usikivu kwa kiasi kikubwa na hivyo kuathiri uongeaji na lugha ya mtoto.

168 otolaryngologist: bingwa sikio, pua na koo: mtaalamu wa tiba anayeshughulikia hitilafu za masikio, pua na koo na magonjwa mbalimbali ya kichwa na shingo. otologist: bingwa masikio: mtaalamu anayeshughulika na matunzo ya sikio na magonjwa yake. otology: otolojia: sayansi ya tiba inayojishughulisha na kasoro za masikio na mifumo inayohusika nayo. otoscope: otoskopu: kifaa cha kuchunguzia mfereji wa sikio la nje na kiwambo cha ngoma ya sikio. outcome: matokeo: tabia au badiliko linalotakiwa kuonekana au kuthibitika kwa namna yoyote ile baada ya utekelezaji wa mikakati iliyoandaliwa awali na rasilimali kuwekezwa. outcome-based: -enye kulenga matokeo: -enye kujielekeza kwenye chaguo la afua kutegemeana na matokeo yanayotarajiwa. output range: kiwango cha sauti: uwekaji wa kiwango cha chini na cha juu cha desibeli pale mkazo wa sauti inayoingia kwenye kipokezi hutofautiana mno. Kidhibiti cha nguvu inayotolewa hurekebishwa na mtaalamu wa vifaa vya usikivu, kiasi kwamba, sauti inayotoka nje ya kisaidizi inakuwa chini kiasi cha kutokuwa kizingiti chenye kero kwa mtumiaji. 150 overanxious disorder: wasiwasi uliokithiri: hali ya kuwa na hofu kubwa na kukereheka kwingi ambako hakuwezi kuhusianishwa na tatizo mahususi au msongo wa mawazo.

169 Pp panic attack: shambulio la kifadhaa: hali ya kukamatwa na woga au hofu kuu agh. vikihusisha hisia za maangamizi. Wakati wa shambulio huwa kuna dalilli za dispenia (pumzi fupifupi), mtwito, maumivu kifuani au kukosa amani, kupaliwa au mihemko ya chini kwa chini na woga wa kurukwa akili au kukosa udhibiti. parallel grabbing bars: fito sambamba gemeo: vipande virefu vya mti, chuma au mbao vilivyotengenezwa kwa ajili ya kufumbatiwa kwa mkono ili kujiimarisha wakati wa kujizoeza kutumia bangiligango au na kujifunza upya kujongea kufuatia kupooza kwa miguu. paralympic games: michezo ya paralimpiki: tukio kubwa la kimataifa lenye kuhusisha michezo mbalimbali ikijumuisha riadha inayochezwa na wenye vilema tofautitofauti wakiwamo wenye vilema vya nguvu za misuli (mfano paraplejia, 151 kwadriplejia, msinyao wa misuli, ashirio la baada ya mpoozo, ugweutimchomozo), wenye viwango mbalimbali vya mijongeo na kukosa viungo (mfano, kukatwa viungo au dismelia), urefu tofautitofauti wa miguu, vimo vifupi, hipatonia, ataksia, athetosisi; upofu na akili. Wanariadha wanaoshindana kwenye michezo hii wana vilema vinavyohitilafiiana na kusababisha ugumu wa kiushindani na hivyo kuhitaji mfumo upambanuaji (kuzingatia stadi, ubora wa siha, nguvu, ustahimilivu, uwezo wa kimbinu na uelekevu wa kiakili) ili kupunguza madhara ya ulemavu wakati wa mashindano. paralysis: mpoozo: hali ya udhoofu wa misuli inayoweza kuathiri msuli wowote wa mwili kutokana na virusi vya polio, mpoozo wa ubongo, kilema cha kudumu au cha muda cha utendaji wa mota. paranoia: paranoia: mchakato wa mawazo unaosadikika kushawishiwa kwa kiwango kikubwa na hofu au dukuduku kiasi cha kupindukia na hivyo kukosa mantiki na kutatizika

170 kiakili k.v mawazo ya mateso na kusumbuliwa au kufanyiwa njama, kuwasingizia na kutowaamini wengine kwa kuwadhania kuwa maadui. Paranoia imejitenga sana na fobia (woga wa kutenda kitu) ambayo pia huhusisha hofu zisizo na msingi ila zenyewe haziambatani na lawama. paranoid ideation: kuwaza kiparanoidi: hali ya kushuku au kuamini kuwa mtu anabughudhiwa, anateswa au hatendewi haki. Dhana hii wakati mwingine hutumika kama ubarishiri wa hali isiyokuwa na sifa za mvurugiko wa kidelusheni. paranoid personality disorder: mvurugiko wa haiba kiparanoia: hali ya kughubikwa kwa muda mrefu na shuku na kutowaamini wengine, kujishughulisha na kukagua mazingira ili kupata uthibitisho wa uwepo wa mitazamo ya chuki, upendeleo au kutukuza dhana binafsi. paranoid schizophrenia: skizofrenia ya kiparanoidi**: hali inayobainishwa na kudumu kwa au kujishughulisha na dilusheni za mateso au kujitukuza. Halikadhalika, panaweza kuwapo kwa dilusheni ya wivu. paraphilia: parafilia: 1. hali ya kuchagiza ashki kwa kuhusisha maongezi ya simu, maiti na sehemu za miili ya wanyama. 2. kupenda kujamiiana kwa namna isiyo ya kawaida. 152 paraplegia: paraplejia: 1. kupotea kwa udhibiti wa misogeo na hisia miguuni, katika nyonga pia sehemu za kiwiliwili zinaweza kuathirika. Halikadhalika, hali hii huambatana na kupoteza kabisa uwezo wa kudhibiti utokaji wa takamwili au kufanya hivyo kwa shida. Zaidi ya hapo, panaweza kuwapo mishtuko isohiari ya misuli, na utepetevu, mathalani wa miguu au mpoozo wa sehemu za chini ya mwili unaohusisha miguu pekee. 2. kupooza au kushindwa kusogeza misuli ya miguu yote wakati mwingine huhusisha kwa kiasi fulani maeneo mengine kunakosababishwa na maradhi au kuumia kwa uti wa ubongo. parens patriae: chombo cha kulinda haki za raia: serikali au mamlaka nyinginezo zinazochukuliwa kuwa mlinzi wa kisheria wa raia asiyeweza kujilinda mwenyewe k.v. mtoto na mtu mwenye ulemavu. Ni kanuni kwamba mamlaka za kisiasa zina wajibu wa kumlinda raia. Mathalani kwa muktadha huu, hakimu au jaji anaweza kubatilisha ulinzi au malezi ya mtoto au amri nyingine zenye kuathiri ubora wa

171 maisha ya mtoto bila kujali kile wazazi walichokubaliana. Katika muktadha wa wagonjwa wa akili, dhana hii hujielekeza kwenye nguvu za kikatiba kinchi ambapo mahakama huruhusiwa kumzuilia kifungoni mtu mwenye hali hiyo anayehitaji hduma ya matunzo na matibabu ya magonjwa aliyonayo bila ridhaa yake. parent: mzazi: baba, mama, mlezi au mtu mwenye dhima ya malezi ya mtoto ya moja kwa moja au yasiyokuwa ya moja kwa moja kwa kuteuliwa kisheria ila si nchi endapo mtoto yuko chini ya uangalizi wa nchi. parental successorship: urithishaji malezi: mpango ambapo mzazi huafikiana (rasmi) na upande mwingine ili majukumu ya malezi ya mtoto yahamishiwe kwa upande mwingine endapo mzazi mwenyewe ataaga dunia. Parkinson's disease: ntenga (ugonjwa wa Parkinson): ugonjwa unaosababisha misuli kudhoofu, kukosa nguvu na hivyo, kusababisha mikono au/na miguu kutetemeka muda mwingi. Baadaye, matatizo ya kufikiri, mwenendo na dimenshia yanaweza kujitokeza. partially sighted: taz. low vision : participation: ushiriki: hali ya mwanajumuia kupata fursa ya kujishughulisha pamoja na wenzake katika masuala ya kijumuia, kisha kunufaika na matokeo ya shughuli 153 yenyewe. Kwa muktadha wa mtu mwenye ulemavu, ushiriki wake katika masuala ya kijumuiya na kijamii hukwazwa na kuwepo kwa mikingamo hususani ile ya kimtazamo. parturient: zaa: 1. toa kiumbe kupitia njia ya uzazi baada ya kipindi cha ujauzito. 2. enye uchungu wa kuzaa. passive receivers of information: wapokea taarifa baridi: kundi la watu ambao hutumiwa, kupokea na kufanyia kazi ujumbe bila wao kuwa na fursa ya kuutolea maoni. Hali kama hii humtokea sana mtu mwenye ulemavu hasa kwenye huduma za kitabibu ambapo uamuzi hata kwa vitu ambavyo havihusiani na tiba hufanywa kwa niaba yake. Utaratibu kama huu humdhoofisha mhusika badala ya kumwimarisha. passive smoking: uvutaji baridi wa sigara: hali ambapo mtu asiye mvutaji hulazimika kuvuta moshi wa sigara au aina nyingine ya tumbaku kutoka kwa jirani mvutaji k.m. mtoto wa mzazi mvutaji

172 ambapo madhara ya moshi wa sigara humwathiri. Kama mvutaji ni mama, madhara haya yanaweza kutokea tangu mtoto akiwa tumboni. passive-aggressive personality disorder: mwenendo sharibaridi: tabia ya ubabe inayodhihirishwa kwa njia fiche kama vile kupinga, kubetua midomo, kusitasita, kuzembea kwa makusudi na utukutu. Agh. ukorofi husababishwa na kusononeshwa na kushindwa kuwa kwenye uhusiano unaoridhisha na mtu au taasisi ambayo mtu anaweza kujishughulisha nayo. pathology: patholojia: 1. taaluma ya uganga inayohusu uchunguzi wa mabadiliko ya kimuundo au kiutendaji mwilini yanayosababishwa na magonjwa. 2. mabadiliko kwa viumbehai yanayosababishwa na maradhi. patient: mgonjwa: mtu anayepata huduma ya tiba hususani kutoka hospitalini au kwa mganga mahususi. Japo kuna uhusiano wa karibu kati ya matabibu, huduma za tiba na aina mbalimbali za vilema. Kilema kilichopea na kuwa cha kudumu hakiwezi kuitwa ugonjwa bali ni hali ya kawaida ya mhusika. Kwa hiyo, ni utovu wa uelewa kwa mtu mwenye hali hii kuitwa mgonjwa. pay attention: kuwa msikivu: kuwa mwangalifu na kumakinikia yale 154 yanayoendelea katika mazingira mtu alimo. Hata hivyo, kwa baadhi ya hali za afya na magonjwa ya akili, uhalisia huwa kinyume kwa mhusika kujifanyia mambo yake bila kujali kinachoendelea kwenye mazingira alimo na hivyo kuharibu uhusiano na utekelezwaji wa mambo mengine. pedophilia: pedofilia: hali ya kuamsha ashki na kufanya ngono kwa kumtumia mtoto. peer buddies: marafiki rika: kwa muktadha wa kielimu, rafiki rika ni yule anayemsaidia mwanafunzi mwenye ulemavu kwenye shughuli au kutembeatembea katika maeneo ya shule na kwenye jumuia. Ni vema kupambanua kwamba marafiki rika hufanya shughuli pamoja na mwanafunzi huyo, badala ya kufanya shughuli kwa niaba yake (taz. child to child learning). peer tutor: mkufunzi rika: katika muktadha wa elimu jumuishi, huyu ni mwanafunzi anayemfundisha au/na kumwendeleza kistadi mwanfunzi mwenzake mwenye ulemavu. Mkufunzi rika hubeba jukumu amilifu katika kusaidia kupanua uwezo wa mwanafunzi mwenzake kwa kushiriki kwenye mchakato wa utekelezaji wa programu binafsi ya elimu; kwa hiyo hustahili kupewa hadhi ya kuwa mmoja wa wanatimu (mwenga) kulingana na kiwango cha

173 kujishughulisha na mwanafunzi mwenye ulemavu. (taz. child to child learning ). peer tutoring: ufundishwaji rika: utaratibu ambapo mtoto mwerevu darasani huhimizwa na kujengewa mazingira ya kumsaidia mwenziye mwenye uzito katika kujifunza. Utaratibu huu unashadidiwa kwenye mfumo wa elimu jumuishi ili kumpunguzia mwalimu mzigo hasa kama darasa lina idadi kubwa ya wanafunzi people first language: kumtanguliza mtu: njia ya kiungwana ya kuongea au kuandika juu ya mtu mwenye ulemavu katika hali ambayo inabainisha na kusisitiza mtu kwanza na ulemavu baadaye. Uzingatiaji wa mtu kwanza huhimiza kwamba ubainishaji wa mahitaji ya mtu, hali ya ulemavu wake, matumizi ya visaidizi maalumu, n.k. vitajwe baada ya kumtaja mtu mwenyewe kwa jina lake. Mifano: badala ya kusema mwenye mtindio wa ubongo amefungiwa kwenye kitimwendo ** sema kijana John ana kilema cha ujongeaji na hivyo anatumia kitimwendo. Msisitizo huu unalenga kumtambua mtu mwenye klema kama binadamu halisi aliye na utambulisho sawa na watu wengine. Hali ya ulemavu itajwe tu kama kuna ulazima wa kufanya hivyo na ifanyike bila udunishaji. people of diverse backgrounds and abilities: watu wenye historia na 155 uwezo anuwai: dhana inayolenga kutanabahisha kuwa kila mtu huwa na historia na uwezo tofauti. Ni dhana inayojikita kwenye kutambua uanuwai kama sifa bainifu ya wanadamu ambayo ni mhimili wa ujumuishaji wa kila mmoja katika maisha ya kila siku. child centred: lenga mtoto au mtu: enye kuzingatia mahitaji ya mtu au mtoto hususani mafunzo. person with disability: mtu mwenye ulemavu: hali ya kuwa na udhoofu wa muda mrefu wa maumbile, akili au fahamu ambao ukichangamana na vikwazo mbalimbali (mazingira, mitazamo, mifumo), vinaweza kuzuia ushiriki wake kikamilifu na kimanufaa katika jamii kwa misingi ya usawa na watu wengine.(taz. disability). perceive: kuwa na ufahamu wa moja kwa moja juu ya kitu kwa njia ya hisia au dhana ya akili. Hali hii hujumuisha tafsiri ya juujuu ya kile kinachohisiwa au kuonekana. perception: utambuzi: uwezo wa mtu kutambua na kutafsiri anachokiona, kukisikia au kukihisi au mchakato wa kutambua au kutafsiri dataghafi au vichocheo vinavyopatikana kupitia kwenye milango ya fahamu. perceptual disorders: mvurugiko utambuzi: hali ya kushindwa kutafsiri vichocheo kupitia mojawapo ya milango ya fahamu au zaidi (licha ya kuona, kusikia na

174 michakato mingine ya hisia kufanya kazi vizuri). perceptual motor: mota tambuzi: uwezo wa mtu kutafsiri vichocheo vinavyopokelewa kupitia milango ya fahamu, halafu kufanya misogeo sadifu au vitendo vya mota vikiakisi kile kinachotokea kwenye milango ya fahamu kama vile kuona, kusikia, kugusa na hisia za kinestezia. Stadi za mota tambuzi huibuka baada ya mifumo ya viingia vya fahamu kuimarishwa kwenye umri wa miaka mitano mpaka saba. perinatal: -a wakati wa kuzaliwa: -enye kuhusisha matukio ya kipindi cha au baada ya kuzaliwa kwa mtoto mchanga (majuma 28 kabla ya kuzaliwa hadi umri wa miezi 1-4). periodic paralyses: kupooza kwa vipindi: aina mbalimbali za kupooza kwa muda zinazobainishwa na kile kinachotokea kwenye viwango vya potasi katika damu (hususani serumu, au giligilii, kwenye baadhi ya sehemu ya damu. Perkins Brailler: mashine ya Braille aina ya Perkins: mashine ya kuchapia maandishi ya nuktanundu. perseveration: ustahimilivu: 1. uelekeo wa kuendelea na shughuli mara ikishaanza na kushindwa kufanya marekebisho au kuisimamisha hata kama imedhihirika kutosadifu. 2. Hali ya kujirudia mara kwa mara ya maneno, mawazo, au somo kiasi kwamba mtu akianza kuongea juu ya somo fulani, au kutumia neno fulani, basi hali hiyo hujirudiarudia. personal hearing aid: shimesikio binafsi: kifaa cha kielektroni ambacho hukuza mawimbi ya sauti kwa ajili ya mtu mwenye usikivu hafifu na hivyo kumwongezea usikivu na humilikiwa na mtu mwenyewe kwa matumizi binafsi kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu (taz. hearing aid ). personality disorders: mvurugiko haiba: 1. kasoro katika mwenendo ambapo mtu hudhihirika kuwa na shauku, aibu ya kupindukia au kuhuzunika isivyo kawaida kwa muda mwingi. 2. hali ya kutopea, kutobadilika, mipangilio isiyorekebika inayohusiana na taswira na mawazo yanayoweza kusababisha kasoro za kiutendaji au sononi. Mivurugiko ya haiba kwa ujumla hubainika kwenye umri wa balehe au mapema kabla na huendelea hata kwenye utu uzima na kuanza kufifia uzeeni. Baadhi ya mivurugiko ya kihaiba ni kama vile: ufarakani, kujiwekea mipaka, ushurutishaji, utegemezi, unafiki au uigizaji, kujijali kupindukia, ulalamishi. 3. hali ya kuwa na matatizo ya upendo na kujipanga kisaikolojia yakishadidishwa na mivurugiko fuasi ya kiusonji. 156

175 personality: haiba: 1. jinsi mtu anavyoenenda na kujichanganya kwenye mazingira mbalimbali. 2. nafsi ya mtu. pertussis: kifaduro: 1. ugonjwa mbaya wa maambukizo ya mfumo wa hewa ambao unaweza kusababisha kichomi, kuharibika kwa ubongo au kifo. 2. ugonjwa wa kikohozi cha muda mrefu unaosababishwa na bakteria wa spishi ya bodetela ambayo agh. huwapata watoto. pervasive developmental disorder (PDD): mvurugiko wa ukuaji: 1. hali ya kubadilika au kuchelewa katika kukuza mienedo na lugha. 2. dhana inayotumika kuelezea hali ya mtoto aliye tumboni ambaye hajaanza kuonjeshwa au kutumia dawa. Hali hii inaweza kusababisha mtu kuwa na utulivu wa vipindi vifupivifupi. 3. Miparaganyiko ya kimwenendo, ufinyu wa stadi za kuchakata na/au ugumu wa kuelewa maongezi. pervis: nyonga: sehemu ya mwili iliyopo kati ya kiuno na paja. phobia: fobia: hofu isiyo na msingi kiasi cha kusababisha msukumo wa shauku ya kuviepuka vitu, shughuli au hali zinazoogopwa. phonological impairment: kithembe: mvurugiko wa kawaida wa kunena; pia hujulikana kama kutotamka kiufasaha. Katika hali hii mtu hutoa sauti zisizo zenyewe, huruka au hurudiarudia baadhi ya sauti kwenye neno. Tatizo hili linaweza kuashiria udhaifu kwenye mota za nyurolojia, 157 kasoro katika ujifunzaji au ugumu wa kutambua baadhi ya sauti wakati wa kutamka. Mathalani, makosa ya kawaida ni: kutamka th badala ya s. Kasoro hizi ni sehemu tu ya mchakato wa kukua kwa mtoto na hutarajiwa katika maongezi ya kila mtoto mchanga, ila pale zinapoendelea zaidi ya umri tarajiwa, huashiria kuwapo kwa hitilafu katika ubongo. physical: -a umbile: -enye sura au muonekano wa kitu. physical ability: uwezo wa mwili na misuli: hali ambapo viungo vya mwili hufanya kazi (k.v. kutembea, kunyanyua uzito wa kawaida, kula, kuvaa, kuoga) kwa viwango vinavyochukuliwa kuwa vya kawaida bila kulazimika kutumia kisaidizi. physical accessibility: ufikivu wa maeneo: hali inayohusu namna mtu mwenye ulemavu anavyoweza kufika katika mazingira tofautitofauti ya huduma.

176 physical and mental integrity: ukamilifu kiakili na kimwili: haki ya kulindwa dhidi ya ukatili kimwili k.v. kufungiwa, kupigwa, kujeruhiwa au kuteswa, kulazimishwa kutumia aina fulani ya dawa au tiba, kunyayaswa kijinsia, kukosewa adabu, kutukanwa au kudhalilishwa kwa kupachikwa majina. physical development: ukuaji kimwili: mabadiliko ya kimaumbilie yaliyojikita kwenye biojinesisi ya sifa bainifu za mtoto ikiwa ni pamoja na uzito, mfumo na mwonekano wa mifupa na ukomavu kwenye mifumo ya mizunguko ya hewa, damu na mishipa ya neva. physical difficulty: matatizo kimwili: dhana ya jumla inayohusisha mawanda mapana ya hali ya kimaumbile kama vile jongo, usinyavu au kupooza misuli. physical disability: ulemavu kiungo: hali ya kuwa na kasoro kwenye kiungo cha mwili ama kwa kile kilichopo kutofanya kazi ipasavyo, kutokamilika au kutokuwapo kabisa. Hali hii huingilia utaratibu wa ujongeaji, mawasiliano, ujifunzaji au/na urekebifu binafsi. physical education (PE): elimu viungo: ukomazaji wa ukamilifu wa mota na stadi zake za msingi pamoja na mifumo kwa njia ya michezo binafsi au ya kikundi ikiwa ni pamoja na ile inayolenga kuta ndani ya ogani, mazoezi ya viungo 158 yaliyorekebishwa, mazoezi ya usogevu na ukuaji wa mota. physical examination: uchunguzimwili: upimaji wa afya ya viungo vya mwili. physical or mental impairment: kilema kimwili au kiakili: hali yoyote inayohusisha uharibikaji wa sura au upungufu wa kimaumbile wenye kuathiri mojawapo ya mifumo ya mwili, k.v. nyurolojia, misuli kiunzi mifupa, ogani maalumu za hisia na upumuaji. Aidha, hujumuisha ogani za utamkaji, misuli ya moyo, uzazi, umeng enyaji chakula, njia ya mkojo, mishipa ya limfu, ngozi na tezi au mvurugiko wowote kiakili, au kisaikolojia k.v. udumavu wa akili, na ulemavu mahususi wa ujifunzaji. Dhana hii hujumuisha maradhi na hali mbalimbali ikiwa ni pamoja na vilema vya: mifupa, uoni, uongeaji, kupooza kwa ubongo, kifafa, msinyao wa misuli, sklerosisi, saratani, magonjwa ya moyo, kisukari, uraibu wa mihadarati, na ulevi. Kwa maana hiyo, mtu hata kama ana kasoro bayana kwenye maungo yake, yeye hawezi kuitwa kilema bali ile sehemu yenye uatilifu; k.m. kuwa na kilema cha mguu, mkomo, macho, masikio, mwenendo, n.k. physical therapist (PT): bingwa tiba viungo: 1. mtaalamu mwenye kibali cha kusaidia kuchunguza au kupima na kutibu mtu mwenye kilema cha viungo kwa njia ya mazoezi maalumu, matumizi ya joto au baridi,

177 mawimbi ya sona, na mbinu nyinginezo. 2. msaidizi wa mafunzo na matibabu ya ulemavu wa viungo ambao hutolewa na mtaalamu aliyefuzu, chini ya maelekezo ya daktari ambayo humsaidia mtu kuboresha matumizi ya mifupa, misuli, vifundo na mishipa ya neva. Tibaviungo hujumuisha matumizi ya kuchua, mazoezi, kunyoosha, maji, mwanga, joto na aina fulanifulani za umeme ambapo vyote ni aina za kalima (kauli na vitendo) kuliko dawa. Tibamaungo husaidia kuongeza ubora wa jumla wa mtu kwa kiwango cha juu, kukuza vipokea fahamu na mota, mpangilio wa nyuromisuli, kiunzi mifupa, uamilifu wake, na hali ya moyo na mapafu. 3. mtu anayesanifu na kuendesha mafunzo ya mazoezi kwa ajili ya watu wenye vilema vya viungo, wanamichezo, n.k. Awali mabingwa hawa waliitwa baba au mama cheza **. physically challenged: -enye changamoto za kimaumbile: tasifida inayobeba dhana yenye msingi wa kutopenda kuonyesha unyanyapaa au kejeli dhidi ya mtu mwenye ulemavu. Hata hivyo, dhana hii haikukubalika sana na badala yake ile ya kutanguliza utu kwanza k.m. watu wenye ikakubalika zaidi na hata kutumika hata kwenye Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu (2006). physician: bingwa wa afya: mtaalamu mbobezi wa kukinga, na kutibu 159 magonjwa mbalimbali ya mwili yasiyo ya kiupasuaji yakiweno na ya akili. pica: pika: shauku ya kula vyakula visivyo vya kawaida au vitu vingine. Hudhihirika katika hali mbalimbali za kuugua, kuvurugika kwa mihemko na ujauzito k.m. kula udongo, vitu vichungu, n.k. pigmentation: upataji rangi: hali ya rangi ya asili ya ngozi, nywele au macho ya kiumbe. (taz. albinism ). pituitary gland: tezi pitutari: kiungo kidogo mithili ya haragwe kinachopatikana chini ya ubongo na ambacho hutengeneza au/na kuchochea aina nyingi za homoni zinazozungukia sehemu mbalimbali za mwili zikichagiza michakato tofautitofauti au kuzifanya tezi nyingine kuzalisha homoni kulingana na mfumo wa mwili. placement services: huduma ya utafutiaji nafasi sadifu: hatua za kumtafutia mtu mwenye mahitaji nafasi za elimu, ajira au mahali pa kuishi panapofaa. Kwa mtu mwenye ulemavu, aina hii ya huduma ni muhimu sana kutokana na uwezo mdogo wa kujitafutia taarifa za kutosha kujua fursa zinazojitokeza. Pia hata fursa zinapofahamika, uwezo wa kujadiliana juu ya marekebisho stahili yanayopaswa kufanywa ili kumwezesha mhusika kutumia huduma kiufanisi pia nao huwa haupo.

178 placement: weka mahali sadifu: darasa, programu au/na matibabu ambayo huchaguliwa kwa ajili ya mtu mwenye mahitaji maalumu. placenta taz. afterbirth. plant medicines: tiba ya mitishamba: maua, majani, mizizi na sehemu nyinginezo za mimea ambazo zinaweza kutumika kutibu maradhi yakiwamo yale yanayohusiana na ulemavu. play skills: stadi za michezo: maarifa ya shughuli za hiari zinazomhusisha mtu kujiburudisha akitumia stadi za viungo na saikolojia. police power: mamlaka ya polisi: katika muktadha wa magonjwa ya akili, dhana hii hujielekeza kwenye nguvu ya dola ya kikatiba inayohusu kuwafunga jela wagonjwa wa akili bila hiari yao kwa kisingizio cha kujidhuru wao wenyewe au kuwadhuru wengine. (taz. parens patriae ). polio: polio: kifupisho cha poliomelitisi ambao ni ugonjwa mkali wa kuambukizwa na virusi ambao wakati mwingine husababisha mpoozo au kuharibika kwa neva tendi kwenye ncha za mfumo wa ukamba wa ubongo wa kati, lakini ukisalimisha neva hisishi. Ugonjwa huu unaweza kuambukiza. Dalili kuu zake ni: homa na maumivu ya misuli ambapo baadaye misuli hiyo inaweza kupooza. Hata hivyo, fungomwili kwa njia ya matumizi makubwa ya chanjo kwa mtoto wa 160 chini ya umri wa miaka mitano imepunguza sana milipuko ya hali hii sehemu nyingi duniani. portfolio assessment: tathmini ya huduma: upimaji wa utoshelevu wa huduma zinazotolewa kwa mtu au kundi. portrayal: dhihirisho taswira: kuelezea mtu au kitu kwa njia ya sanaa (picha, maigizo) au maandishi. positive and constructive feedback: mwitiko chanya na saiizi: kitendo cha mtaarifiwa kutoa mwitiko kwa mtaarifu kwa njia ambayo haijengi uhasama kati ya pande mbili, bali inajiekeleza kwenye uboreshaji wa mada au maudhui na matokeo yake. positive discrimination or reverse discrimination: ubaguzi wa kimageuzi: katika muktadha wa kugawana rasilimali au ajira, ni utaratibu au sera ya kumpendelea mtu anayetokana na makundi ambayo yamekuwa yakibaguliwa kwa muda mrefu. (ang. affirmative action na equality ). positive emotional environment: mazingira ya mhemko chanya: muktadha ambapo mambo yanaendelea na wenye

179 kuyaendesha wanazingatia hisia za kila aliyepo; yaani hayamkereheshi au kuchochea mihemko ya yeyote. postlingual deafness or disorders: mvurugiko wa usikivu baada ya kujua lugha: kilema cha uziwi kinachotokea baada ya mhusika kuwa amemudu kuongea na kujua lugha. postnatal: -a baada ya kuzaliwa: -enye kufuatia kipindi baada ya mtu kuzaliwa. postpartum period: arubaini ya uzazi: kipindi cha siku 40 baada ya mtoto kuzaliwa. post-traumatic stress disorder: mvurugiko wa kisaikolojia: hali ya kuwa na maruweruwe na kusikia sauti, kuona taswira za vitu na kuziamini hasa baada ya kunusurika kwenye ajali. postural control or development: uthibiti mkao: uwezo wa kuwa na kuendelea kwenye mikao fulani ambayo ni matakwa ya msingi katika kujimudu na kutenda shughuli. Mathalani, kuweka shingo na kichwa wima na kuvibainisha vilevile kwa muda, na kupanga kiwiliwili na miguu/mikono ikisadifiana na uzito, ubadilishaji, na kuweka sawa. Haya yasipowezekana kwa hiari, visaidizi kama vile bangiligango na vibanio hutumika. poverty of content of speech: kupungua kwa maudhui hoja: 1. maongezi yanayojitosheleza kwa 161 matamshi ila yenye taarifa kidogo kutokana na kutokuwa yakini, kujirudiarudia au matumizi ya vifungu vya maneno ya kukariri au visivyoeleweka. Kama ni kwenye usaili, msaili anaweza kugundua kuwa msailiwa ameongea kwa kirefu bila kutoa taarifa za kutosha katika kujibu swali. Vinginevyo, mtu anaweza kutoa taarifa za kutosha ila akatumia maneno mengi katika kufanya hivyo, badala ya kufupisha jibu refu katika sentensi moja au mbili. 2. ubanaji wa idadi ya maneno kiasi kwamba maongezi na majibu ya hiari yanakuwa mafupi na bila kuhitaji kufafanuliwa. Pale ambapo hali ni tata sana majibu yanaweza kuwa ya mkato na baadhi ya maswali kutojibiwa. power: mamlaka: hali ya mtu, kundi au mfumo kuwa na uwezo, nguvu, akili, madaraka, jeuri au ujanja dhidi ya mtu au makundi mengine. practical demonstration: maonyesho ya vitendo: jinsi ya kutenda jambo kwa mifano dhahiri. practical skills: stadi za kiutendaji: shughuli za msingi katika maisha ya kila siku ya mtu mwenye ulemavu kama vile kujitunza kiafya, kusafiri, kujiwekea ratiba na utaratibu na kuufuata, kujiangalia kiusalama, kutunza fedha au kutumia simu. predominant disturbance: mvurugiko mkubwa: dalili au kusanyiko la dalili zenye kumsumbua mtu ambazo

180 huzitambua na kuziona kuwa ngeni kwake wakati vipimo vya uhalisia havionyeshi hitilafu kabisa. Katika hali hii, mwenendo wa mhusika haukiuki taratibu za kijamii (japo unaweza kuwa unalemaza). Mvurugiko huu unaweza kuwa unahimilika au unaojirudiarudia pale usipotibiwa na unaweza usiishie kwenye mchakatotendani wa mpito ila kuwa chanzo cha fadhaa. prejudice: taathira. hali ya mtu au kundi kuwa na hisia za mapenzi au chuki dhidi ya mtu au kundi lingine bila sababu na kwa muda wote. prelingual deafness or disorder: uziwi kabla ya matamshi: hali ya kupoteza hisia za usikivu inayojitokeza wakati wa kuzaliwa au mapema kabla ya kumudu kuongea na kuwa na lugha (agh. kabla ya umri wa miaka 2-5). Uziwi unaweza kuwa wa kuzalliwa au wa nasibu kwa kunatokea baada ya kuzaliwa ila kabla ya kutimiza umri unaotakiwa, kuvia kiukuaji na hali nyinginezo kwa mtoto mchanga aliyezaliwa mapema kuliko kawaida. Aina hii ya kilema ni kinyume cha mvurugiko wa usikivu baada ya kujua lugha. prenatal: -a kabla ya kuzaliwa: enye kuhusu kipindini cha mtoto kukua wakati wa ujauzito. presbycusis: uziwimsawajiko: hali ya kuendelea kupoteza usikivu kwa kadiri umri unavyozidi kuongezeka. pressure areas; sores or decubitus ulcer: vidonda mgandamizo: uvimbe mwekundu au baka la kuvilia kwa ngozi linakotokana na mgandamizo wa ngozi hususani maeneo yenye mifupa (magoti, nyayo, makalio). Hali hii hutokea pale mtu anapokalia au kulalia upande mmoja kwa muda mrefu bila kuwa na kitu chororo kama godoro au mto. Kwa anayetumia bangiligango, nsiso kwapa au kigasha kutokuwa na pedi za kinga dhidi ya misuguano au/na unyenyevu kutokana na jasho na kemikalli za ufukunyungu. Kwenye vilia mkandamizo, kinachoanza kama baka jekundu kinaweza kuendelea na kuwa kidonda kikubwa chenye kuzua utata kitiba. Wazazi na wasaidizi wanahitaji kuwa na utaratibu wa muda wote kuzuia hali hii ikiwa ni pamoja na kupunguza mkandamizo mathalani, kwa kubadilisha pande za kulalia au kukalia na kutumia mito inayofaa, kutumia vitu vyororo kwenye nsiso kigasha au kwapa na kwenye aina nyingine za nyenzo kongojea na visaidizi. 162

181 pressure of speech: msukumo wa maongezi: mazungumzo ambayo kiwango chake huongezeka, huchapushwa na ni magumu au hayawezekani kuingiliwa. Kwa kawaida pia hutolewa kwa sauti ya juu na yenye msisitizo. Mara kwa mara, mtu huongea bila kichocheo chochote cha kijamii na anaweza kuendelea kuongea hata kama hakuna anayemsikiliza. Shinikizo la maongezi agh. hujidhihirisha kwenye visa vya kuathiriwa kiakili, hata hivyo, vinaweza pia kujitokeza kwenye baadhi ya kasoro za kiakili, mfadhaiko mkubwa wa mwendo hiari, skizofrenia, kasoro nyinginezo za kisakotiki, na mara kadhaa hujibiza kwa sononi kali. pressure group: kundi shinikizi: watu waliojiunga pamoja na kwa pamoja wanashawishi mamlaka au wanajamii ili kutimiza lengo lao k.v. madiliko ya sharia, mila, n.k. prevalence: ushamiri: hali ya idadi ya watu katika eneo lolote wanaodhihirisha kuwa na hali au tatizo fulani lisilokuwa la kawaida katika kipindi fulani; mathalani, maambukizi ya virusi vya polio. (taz. incidence ). preventable physical and emotional health problem: tatizo la afya ya mwili na akili lianalozuilika: mvurugiko wa kimwili na kiakili inayoweza kuzuilika. prevention: kinga: shughuli ambazo hujielekeza kwenye visababishi vya 163 vilema na uzidishwaji wa ukomo wa utendaji. Shughuli za aina hiyo ni kama vile: i) zinazoondosha au kupunguza hali ambazo husababisha au huwaanika watu wenye vilema au zile zinazoongeza matukio ya watu kupata vilema. Chanjo, kampeni za kukuza ufahamu kwenye matukio na matendo mathalani, mabomu ya ardhini, usalama barabarani, ajalli za majumbani na kazini, usafi wa miili na mazingira, lishe bora au uboreshaji wa miundombinu ni miongoni mwa kinachoitwa kinga ya msingi, ii) kuongeza utambuzi wa mapema wa matatizo yaliyopo ili kuondosha mazingira yanayozalisha au kuzidisha, ukomo wa utendaji. Hizi ni afua kama vile tibaviungo ili kuzuia mikunyato, matunzo bora ya kitiba baada ya ajali, elimu kwa walioumia kuhusu jinsi ya kuendesha maisha yao ambayo huitwa kinga fuasi; na iii) kupunguza athari za ulemavu katika maisha yote ya mtu. Hii ina maana ya kupunguza athari za vilema kwa kusambaza visaidizi vya kuwezesha mwendo au ujongevu, usikivu na uoni, mfano, kalipa, vitimwendo na visaidizi kama hivyo (kwa ajili ya polio na ajali), shimesikio (kwa ajili ya uziwi), miwani kwa (kwa ajili ya upofu), kurekebisha vyombo vya usafiri, makazi au sehemu za kazi, n.k. Afua za aina hii huitwa za hatua ya tatu au ya juu.

182 primary care taker: mwangalizi mkuu: mtu ambaye dhima yake ni kutunza kitu, mtu, sehemu fulani. privilege: stahiki: haki ya kisheria ya mtu kama vile mgonjwa au mfungwa, kumzuia daktari au wakili asitoe ushahidi dhidi yake kwa kutumia taarifa alizozipata wakati akimtibu au kuhojiana naye. Hivyo, haki hii huwa na ithibati ya kisheria kama kanuni ya maadili ya usiri. privileged communication: stahiki ya mawasilano: katazo la kisheria la kutotangazwa kwa taarifa kati ya watu wenye uhusiano wa siri, au kuaminiana kutotangazwa. Katika baadhi ya nchi, uhusiano kati ya tabibu wa kisaikolojia au daktari na mgonjwa, huchukuliwa kuwa na haki ya kimawasiliano. Hata hivyo, sheria hii inakuwa kwenye mtanziko na huwa na upekee mwingi (mfano, mgonjwa anayeshitaki kwa kuegemeza mashtaka yake yote au sehemu yake kwenye vipengele vya kisakaitria, anaweza kuifuta haki hiyo). Ni vema kuelewa kuwa haki hii ni halali kwa mgonjwa na siyo tabibu, na ni mgonjwa pekee anayeweza kuiondosha labda kama taratitu za uendeshaji mashtaka zinaelekeza vinginevyo. procedural safeguards: ulinzi wa taratibu za kisheria: 1. sheria zinazolinda haki za mtoto (agh. mwenye ulemavu) na familia 164 zake. 2. matakwa ya kisheria yanayoelekeza kwamba mtoto mwenye ulemavu ahudumiwe katika mazingira yasiyokuwa na mikingamo na yanayosadifiana na mahitaji yake ya kielimu. Kwa hiyo ni muhimu kupima hali ya kutokubagua kwa kutumia vigezo mbalimbali wakati wa uwekaji mahali sadifu. proclaim: tangaza: 1. toa taarifa ya jambo au kitu kinachohusu umma au kurasimisha kitu hasa kilicho chanya. 2. onyesha dhahiri, hakikisha profession: weledi: hali ya kuwa na maarifa ya juu kuhusiana na jambo fulani. profound: -a kiwango kikubwa: -enye kiasi kikubwa cha ulemavu hasa ule wa akili, wa ujifunzaji au ule mchanganyiko, unaoweza kuwa miongoni mwa watu wenye ulemavu mkubwa katika jumuia mbalimbali. Mtu aliyeko kwenye kundi hili huwa na kiwango kikubwa cha ulemavu k.v. akili, ikimaanisha kuwa hisaweledi yake hukadiriwa kuwa chini ya 20 na kwa hiyo huwa na ukomo mkubwa wa kuelewa. Pia anaweza kuwa na kasoro mchanganyiko ikiwa ni pamoja na zile za uoni, usikivu na ujongevu, halikadhalika na changamoto nyinginezo kama vile kifafa na usonji. Kwa maana hiyo, huhitaji usaidizi kwenye ujongeaji, na mwingineo changamani wa kiafya

183 unaotekelezeka kwa kutimiza hatua mtawalia. Mtu mwenye kiwango kikubwa cha ulemavu wa akili na ule mchanganyiko, anaweza kuwa na kiasi fulani cha ugumu wa kimawasiliano na kwa hakika ukomo wa juu wa uelewa. Anaweza kujieleza kwa njia zisizo za kimatamshi, au vinginevyo kwa kutumia maneno machache na ishara. Zaidi ya hapo, anaweza kuhitaji usaidizi wa kimwenendo ambao huonekana kuwa changamoto kwa kuweza kujijeruhi. progesterone: projesteroni: 1. homoni ya kike. 2. homoni ya kopasi luteamu ya ovari ambayo huanzisha mabadiliko katika endometriumu kufuatia ovulesheni. cii progestogen: projestojeni: homoni mnemba inayotengenezwa kwenye maabara ikifanana na ile ya projestironi ambayo inapatikana katika mwili wa mwanamke. Hutumika kwenye baadhi ya njia za mpango wa uzazi zinazotumia homoni. prognosis: prognosisi: kubashiri sababu au matokeo ya hali ya ugonjwa kwa kuangalia dalili za uwezekano wa kupona; utabiri wa chanzo cha ungonjwa au matokeo ya hali bila uthibitisho wa kimaabara bali kigezo cha dalili (muktadha wa kitabibu). promotional material: kifaa cha kutangazia jambo: kifaa k.v brosha, kipeperushi, tovuti, simu n.k. 165 kinachotumika kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na jambo au bidhaa mpya. pronation: pronesheni: 1. ulaliaji tumbo, ulalaji wa kifudifudi. 2. upinduaji wa mikono kiasi kwamba kiganja cha mkono huelekezwa chini. ciii (taz. supination ). proprioceptive: nevapokezi: mishipa ya fahamu ambayo hupokea stimuli kutoka ndani ya mwili. prostate glands: tezidume: kiungo kilicho kwenye kinena chini ya kibofu cha mkojo ambacho ni sehemu ya mfumo wa uzazi kwa wanaume unaozalisha majimaji ambayo husafirisha manii yanayotengenezwa kwenye mapumbu hadi nje ya uume wakati wa kujamiiana. Kiungo hiki hukua na kupanuka taratibu katika maisha yote ya mhusika ila, kwa baadhi ya wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 45 na kuendelea, kasi ya ukuaji huongezeka kuliko kawaida na hivyo tezi hupanuka na husababisha mrija wa kupitishia mkojo kubanwa kiasi cha kuchochea adha k.v. maumivu wakati wa kukojoa, ugumu wa kuanzisha au kusimamisha zoezi la ukojoaji, mara kwa mara kusikia hisia za kutaka kukojoa, kuhisi maumivu ya tumbo la chini, maambukizo ya bakteria, uvimbe wa tezi, ugumu wa kuzaa au kujamiiana, na uharibifu kwenye figo. Agh., hali hii inaweza hata kusababisha saratani ya tezidume.

184 Kama sehemu ya tiba, matumizi ya katheta huhitajika ili kupunguza adha muda wote au kwa kipindi fulani. Kutokana na hali hii kumsababisha mhusika hushindwa kutenda kwa kiwango cha kawaida, hivyo, huangukia kwenye kundi la ulemavu hata kama bado ana umri wa kuendelea kuajirika. Kwa kuzingatia ukweli huu, katika nchi zenye utaratibu wa kutoa hifadhi kinga ya ulemavu, mtu aliyethibitika kuwa na saratani ya aina hii hustahili kunufaika na huduma ya kinga jamii ilimradi athibitishe kuwa: (i) hali hii inajirudiarudia hata baada ya kupewa matibabu; (ii) tatizo linasambaa sehemu nyingine za mwili, (iii) hali yenyewe inamsababisha asiweze kutenda shughuli alizozizoea au/na kuzisomea kutokana na kutomudu kukaa au kusimama kwa muda mrefu, n.k. prosthesis: taz. artificial limb prosthetics: prosthetikia: 1. shughuli ya utengenezaji viungo bandia vya mwili. 2. utanzu wa upasuaji unaohusu viungo bandia. protective service: huduma kinga: utaratibu ambao humsaidia mtu asiyemudu kutunza rasilimali zake au kujilinda mwenyewe dhidi ya kutelekezwa, kunyonywa, au majanga. Mifano ya huduma za aina hiyo huwa za ughani au rufaa, unasihi, kusimamia na kufuatilia mashtaka, malezi, msaada wa kifedha au kisheria na matunzo ya nyumba. protégé: mtetewa: mtu mwenye kukingwa kutokana na utetezi kufanywa kwa niaba yake. psoriasis: mbalanga: hali ya kiafya ambayo hutokea pale seli za ngozi zinapokua kwa haraka. Ishara za mfumo wa kinga husababisha utengenezwaji wa seli mpya katika muda mfupi sana. Mwili hautokomezi seli mpya za ngozi ambazo ni ziada na hivyo hurundikana juu ya ngozi na kusababisha mabaka kutokeza. Dalili zake hutofautiana kulingana na aina ya mbalanga. Licha ya kuwapo kwa aina zingine za mbalanga ile ya mabaka kwenye viwiko, magoti, chini ya mgongo, kisogoni na kwenye kucha huathiri asilimia 80 ya watu walio na tatizo hili. psych problems: matatizo ya kisaikolojia: hali ya mvurugiko unaohusisha mawazo au tabia. 166

185 psychiatry: usakaitria: ubobezi katika fani yenye kujielekeza kwenye mafunzo, uaguzi, matibabu na kuzuia mvurugiko wa akili na nafsi. Mivurugiko hii ni pamoja na aina mbalimbali za afekti, tabia, utambuzi na hitilafu endelevu. Upimaji wa hali kama hizi huanzia kwenye historia ya mhusika na uchunguzi wa hali ya kisaikolojia na kimaumbile. Upimaji huu unaweza kuhusisha taswira na nyurorojia au stadi nyinginezo za nyurorolojia ya kimaumbile. psychiatric treatment: tiba ya afyaakili: matibabu ya magonjwa ya akili. psychiatrist: sakaitria: daktari bingwa wa magonjwa ya akili au tiba za binadamu anayepima kwa kuchunguza, kuagua na kutibu mivurugiko ya akili na nafsi, saikolojia, mihemko na ukuaji au kasoro za mifumo ya kimaumbile. Sakaitria lazima ahitimu mafunzo ya ziada na ahudumu kwa kusimamia wodi ya walio na maradhi ya taaluma yake. Halikadhalika, anaweza kubobea kwenye sakaitria ya watoto au ile ya fahamu. Kwa kuwa huyu ni mganga wa tiba, wanaweza kuelekeza dawa za kupunguza dalili za mivurugiko mballimbali tofauti na yule bingwa wa kisaikolojia anavyoruhusiwa kufanya. psychoanalysis: uchunguzi nafsi: uchambuzi wa nafsi au upembuzi wa fikira. 167 psychoanalyst: mchunguzi nafsi: mtu mwenye kuchambua kuagua na kutibu mvurugiko wa kimhemko kwa mbinu maalumu ambazo hudodosa jinsi akili ya mihemko ya mgonjwa ilivyoundika. psychogenesis: saikojenesisi: ukuaji na maendeleo katika sifa mbalimbali za kiakili. psychogenic deafness: uziwi wa kimawazo: kilema cha usikivu kinachoweza kusababishwa na mihemko ya sononi kama njia isohiari ya kukwepa hali zisizovumilika. Pia hujulikana kama uziwi wa kimhemko au kimageuzi. psychological disability: ulemavu wa kisaikolojia: aina ya ulemavu wa akili ambao huathiri mipangilio ya mtu kiakili na kusababisha sononi au ulemavu ambao haukutarajiwa katika ukuaji wa kawaida. Visababishi vyake halisi havifahamiki ila hudhaniwa kuwa ni muunganiko wa hali za kiafya, na kijamii, mathalani, vinasaba, matukio ya kimazingira wakati wa ujauzito na uzazi au uvimbe kwenye ubongo, maambukizo, matumizi mabaya ya mihadarati, michakato ya kimhemko, silika ya heba, mbinu za kumudu na hali ya jumla kiafya. psychological dynamics: nguvu ya kisaikolojia: stadi ya msukumo wa saikolojia ambao ni msingi wa mwenendo, hisia na mhemko wa mtu na jinsi vinavyohusiana na uzoefu wa awali. Kimsingi, nguvu hii

186 hujishughulisha na hamasa ya kundi kwa kudhamiria au kutokudhamiria; mathalani, kundi linaweza kupagawishwa kwa kukosa haki k.v. kufanyiwa ukatili, kukandamizwa kiasi cha kuamua kuchukua hatua za pamoja au kijamii. Wakandamizaji agh. hutumia mbinu mbalimbali zikiwamo za kuficha na kutafsiri hali kiupotoshaji ili kushawishi umma. Mnyukano kati ya pande hizi mbili ndio huitwa mtukutiko wa mpagao. psychological services: huduma za kisaikolojia: usaidizi wa familia na mtoto ili kuwezesha utendaji kisaikolojia na kimwenendo (ukuaji wa uhusiano na mhudumu, mwenza, mwitiko kwenye mazingira ya kijamii, n.k.). psychological: -a kisaikolojia: -enye kuathiri akili, mwenendo, mtazamo na tabia ya mtu. psychologist: mwanasaikolojia: mtu aliyepata mafunzo na kupewa kibali cha kutafiti, kutathmini na kutoa tiba kwa watu kuhusiana na matatizo yao kijamii, kihisia, kisaikolojia, kimwenendo au kiukuaji. Hata hivyo, mwanasaikolojia hana mamlaka ya kuelekeza dawa. (taz. clinical psychologist ). psychology: saikolojia: taaluma inayohusika na michakato ya kiakili na kimwenendo. psychometrist: mwanasaikometria: mtaalamu anayefuzu kwenye uendeshaji wa vipimo vya kisaikolojia 168 akijipambanua na yule wa shule kwenye maeneo mengi kwani mwanasaikometria hasisitizi sana afua za kiushirikiano. psychometry: saikometria: utanzu mpana wa kisaikolojia inayojishughulisha na upimaji wa akili. psychopathetic personality/personality disorder: mvurugiko haiba: hali ya kuwa na matatizo ya upendo na kujipanga kisaikolojia yakishadidishwa na mivurugiko fuasi ya kiusonji. psychosis: saikosisi: dhana ya jumla yenye kuelezea mojawapo ya mivurugiko mingi ya kiakili inayobainishwa na kujitenga kijamii, kutoona uhalisia, kusawajika kwa haiba, kutofikiri sawasawa kiasi kwamba kila mojawapo ya vipengele hivi huingilia uwezo wa kumudu kukabiliana na matakwa halisi ya maisha ya kila siku. psycho-social development: ustawi wa kisaikolojia jamii na kihisia: ukuaji wa mtu kulingana na mazingira yake yakiujumuisha uanzishaji na uendelezaji wa uhusiano wa njia mbili zenye umuhimu katika maisha ya mhusika na jinsi anavyoitikia mazingira yaliyomzunguka. psycho-socio and emotional well being: ustawi wa kisikolojia, kijamii na kihisia: afua zinazolenga hali ya kisaikolojia, mazingira ya kuishi, uhusiano, usaidizi ambavyo vina athari kwenye hali ya kisaikolojia.

187 Dhana hii hujielekeza kwenye ustawi wa mhusika kisaikolojia, na jinsi ya kuchangamana na mazingira kijamii. Hata hivyo, mhusika siyo lazima awe na ufahamu wa uhusiano wake na mazingira. psychosomatic illnesses: ugonjwa wa mawazo: 1. kilema cha kisaikolojia kinachoathiri akili na mwili. 2. maradhi yenye kusababishwa na matatizo ya mawazo. psycho-therapist: tabibu saikolojia: bingwa wa afya ya akili anayetibu kwa njia ya unasihi. psychotherapy: tiba saikolojia: 1. dhana pana inayotumika kwenye mikabala mbalimbali ya tiba ya kasoro za kiakili na kimhemko. 2. tiba ya akili kupitia unasaha na isaikolojia; 3. njia mojawapo ya kutibu magonjwa kwa kunasihi. psychotic: -a saikosisi: -enye kuathiriwa na mvurugiko wa akili. ptosis: tosisi: hali ya kuinamia chini kwa kikawa au kigubiko cha juu cha jicho ambapo jicho huwa limefunikwa nusu. civ puppet: kibaraka: 1. mtu aliye kwenye nafasi ya uongozi (hususani wa nchi) ambaye uamuzi wake huwakilisha matakwa ya mataifa ya nje au makundi masilahi yanayomnufaisha yeye binafsi. 2. mtu asiye na uwezo ambaye anatumiwa na mtu mwingine. pus: usaha: kiwoevu cheupe au cha njano kilichojaa vijidudu ambacho agh., hupatikana ndani ya kidonda kilichoambukizwa. pyloric stenosis: polasisi nyembamba: ulaji kidogo kutokana na wembamba au kupungua kwa kipenyo cha ujia wa tumbo kunakotokea tangu utotoni. 169

188 Qq quadriplegia (tetraplegia): kwadriplejia: 1. kupooza au kukosekana kwa msogeo kwenye misuli ya mikono na miguu yote miwili kunakosababishwa na maradhi au kuumia sehemu ya juu (karibu na shingo) ya uti wa ubongo. 2. kupooza miguu na mikono yote. quadripresis: kwadriparesisi: hali ambapo hisia hubaki kamili ila viungo huwa dhaifu. 170

189 Rr radiotherapeutics: tibamiali: taaluma ya ujuzi wa kutumia miali yenye nishati kubwa kwa matibabu hususani yale yanayohusu saratani. radiotherapist: daktari wa tibamiale: mtaalamu wa kutibu kwa kutumia miali. radiotherapy: tibamiali: mbinu ya kutibu ugonjwa kwa kutumia mnururisho. ramp: ngazimbetuko: aina ya hanamu inayosimikwa kama nyongeza au mbadala wa ngazi za kawaida kwenye majengo na vyombo vya usafiri ili kumwezesha mtumiaji kitimwendo na yule mwenye kusukuma rukwama, kibeba moto au vifaa vingine vya kubebea vitu kufikia jengo au eneo kwa urahisi zaidi. Kiujumla, miundombinu hii, ni ya lazima kwa mtumiaji wa kitimwendo pale ambapo huduma ya vipandishi au lifti ya kuunganisha miinuko au orofa mbalimbali haipatikani. Aina hii ya miundombinu inaweza kuwa ya kudumu, ya muda au ya kuhamishika. Inapokuwa ya kudumu, husanifiwa kwa kufungiwa au kwa vyovyote kushikamanishwa na sehemu inayohusika. Inapokuwa ya muda, huegeshwa juu ya sakafu au ubamba wa zege na agh. hutumiwa kwa kipindi kifupi tu. Kwa kawaida, ngazimbetuko ya kudumu, hutengenezwa kwa metali ya aluminiamu, zege au mbao. Ile ya kuhamishika huwa ni ya aluminiamu au mbao na hukunjika ili kurasisha 171 usafirishaji wake. Kimsingi, aina hii ya miundombinu, huwa ni kwa ajili ya matumizi ya majumbani lakini pia inaweza kutumika kwenye magari kwa zamu kupakia na kushusha kitimwendo kisichokaliwa na mtumiaji. Pamoja na umuhimu wake, kwa baadhi ya ulemvu jongevu, hupata shida kwenye ngazimbetuko kiasi cha kupendelea ngazi za kawaida. Japo mwinamo unaopendelewa ni ule yenye uwiano wa vipimo vya kati ya 1:16 na 1:20, kanuni kuu ya ujenzi wake ni uwiano wa urefu wa sentimeta 12 kwa mwinuko wa sentimeta moja (1:12). Kwa kuzingatia kuwa mwinamo hutegemeana na urefu wa eneo uwiano kati ya mlalo na mwinuko, mtumia kitimwendo bado humudu kujongea na kutumia huo wa 1:12 na hata ule wa 1:16. (taz. accessibility symbol).

190 reading machines: mashine somaji: aina ya teknolojia ya kielektroniki ambapo mashine hutumika kusoma matini yaliyochapwa kwa maandishi ya kawaida ili asiyeona waweze kuyaelewa bila kuhitaji kuwa na binadamu wa kumsomea. Teknolojia hii imetumika sana katika nchi zilizoendelea kabla ya ugunduzi wa maunzilaini maalum ya kompyuta kwa minajili hii. Kwa hivi sasa aina zote mbili za teknolojia zinatumika sanjari. reason: taamuli: uwezo wa kuvuta wazo au fikira juu ya jambo fulani. reasonable accommodation: marekebisho stahili: mabadiliko na marekebisho ya lazima na yenye kufaa yanapohitajika kutokana na hali fulani ili kuhakikisha kuwa mtu mwenye ulemavu ananufaika au 172 anatumia haki zake zote za binadamu na uhuru wa msingi kwa kiwango sawa na wengine, Mabadiliko haya yanaweza kufanyika kwenye ngazi yoyote ya mfumo wa elimu, ajira, starehe na burudani, tiba, n.k. Hata hivyo, licha ya umuhimu wake, mabadiliko haya yafanyike pasipo kutaabisha isivyowiana au isiyovumilika, kwa upande ule unaoyatekeleza. rectal exam: uchunguzi puru: kuangalia sehemu ya mwisho ya utumbo mkubwa ili kubaini ukuaji au matatizo mengine. Uchunguzi huu unaweza pia kutoa taarifa za kuta za uke. regress: -enye kuendelea kusawijika: enye kuharibika zaidi polepole enye kupungua uwezo wa kusikia taratibu siku hadi siku. rehabilitate: karabati au rekebisha: weka katika hali nzuri karibia na ile ya awali. Agh. hatua hizi huchukuliwa baada ya uharibifu kutokea. Kwa muktadha wa watu wenye ulemavu, ni pale ambapo mtu ama anapata kilema cha nasibu au kile alichozaliwa nacho kinarekebishwa ili kukmwongezea mhusika kiwango cha uwezo wa kutenda. Upasuaji wa mifupa, viungo mnemba na nyenzokongojea ni sehemu ya afua hii. Ili kukamilisha utegemezaji wa mhusika, afua hii sharti iendane na mikakati ya kijamii na kiufundi pia kwa lengo la kukuza uwezo na jamii kubeba jukumu lake

191 la kumwondolea mikingamo hususani ile ya kimazingira.. rehabilitation: marekebisho: 1. afua za kumwezesha mtu kupata upya stadi, uwezo, au maarifa ambazo zinaweza kuwa zilivurugika kutokana na kupata kilema, au mabadiliko ya kiwango cha kilema au hali ya mambo na mazingira ya kuishi. Kwa maneno mengine ni kumrudishia uwezo au kumsaidia mtu mwenye kilema kumudu vizuri mazingira ya nyumbani au/na kwenye jamii baada ya kupata kasoro. Kwa mtu anayepata kilema, agh. afua hii hujumuisha masuala ya kitabibu, kijamii na ufundi stadi. Kwa hiyo, mikabala k.v. tibamaungo, tibaliwaza, upasuaji mifupa, uundaji viungo bandia, utambuzi mazingira, mafunzo ya kuandika na kusoma nuktanundu, kuelewa lugha ishara/mpapaso, n.k. ni sehemu muhimu ya marekebisho kwa mtu mwenye ulemavu. Afua za marekebisho zinaweza kufanyikia kwenye taasisi au vituo maalumu k.m. hospitali au/na katika jumuia. 2. michakato iliyopangiliwa ikiwa na malengo mahususi, muda wa utekelezaji na rasilimali ambapo mtaalamu au/na mhudumiaji hushirikiana katika kusaidia jitihada binafsi za mtu ili afanikiwe kwa kadiri inavyowezekana kwenye utendaji na kuyamudu mambo na hivyo kukuza kiwango chake chz kujitegemea na ushiriki wake kwenye jamii. related services: huduma ambatani: huduma muhimu kwa ajili ya mtoto kufaidi kutokana na elimu. Huduma hizi zinaweza kujumuisha: usafiri na huduma mwega kama vile kuongea, kusikia, saikolojia, tibamaungo na tibaliwaza, burudani, upimaji na utambuzi wa mapema, unasihi, ukalimani wa lugha ishara, huduma za tiba kwa lengo la uchunguzi na tathmini, huduma za siha shuleni, huduma za uamara shuleni na unasihi wa wazazi, na mafunzo. remedial reader: msomaji mgango: dhana ya kijana anayehitaji usaidizi mahususi katika kusoma au kuelewa maelekezo au mafundisho. (taz. itinerant teacher, peer tutor, child to child learning, resource room ). remediation approach: mkabala mgango: mafunzo rekebishi ambayo huhusika na maelekezo au mafunzo yanayolenga kufidia mapengo au upungufu kwenye hazina ya stadi za mtoto. 173

192 residential school programme: programu za shule za bweni: mfumo wa elimu maalumu iliyoidhinishwa kutolewa kwenye sehemu ambapo mtoto huhudhuria masomo na kulala hapo. residential treatment: tibamakazi: sehemu rekebishi ya kuishi ambapo tiba na matunzo hutolewa kwa mtoto mwenye mivurugiko ya kimhemko kiasi cha kuhitaji tiba mfululizo na/au kusimamiwa au kupata ahueni dhidi ya misongo. resilience: zihirejezi: 1. mwelekeo au uwezo wa ndani ya mtu wa kumwezesha kuondokana na hali au matukio ya msongo na kufanikiwa kurudia shughuli za kawaida. 2. ustahimilivu. resistance: upambanaji: uwezo wa kitu kujikinga chenyewe dhidi ya kile ambacho kwa kawaida kingeweza kudhuru au kuua. Bakteria, virusi na vimelea vinaweza kustahimili madhara ya baadhi ya dawa hususani viuajisumu na dawa dhidi ya vijigeuzi kiasi kwamba tiba hizi hazitibu tena maradhi. resource centre (RC): kituo rasilimali: programu inayogharamiwa na wadau mbalimbali ikiwamo hazina ya nchi ambazo huhusika na mafunzo na msaada wa kiteknolojia kwa mtumishi anayehudumia mtoto mwenye 174 ulemavu wa umri wa kwenda shule. resource room: chumba rasilimali: chumba kilichotengwa na vile vya madarasa ya kawaida ambamo mtoto mwenye ulemavu anaweza kupatiwa usaidizi maalumu ili kuimarisha na kujazilizia mafundisho ya darasa la kawaida. Muda ambao mtoto huutumia kila siku kwenye chumba cha maarifa hutofautiana kufuatana na mahitaji yake, na muda wa siku unaosalia hutumika kwenye darasa la kawaida.( taz. remedial reader). resource teacher: mwalimu mwelekezi: mwalimu mtaalamu ambaye hufanya kazi ya mgango na mtoto mwenye ulemavu na hutoa ushauri kwa walimu wengine (wasio wataalamu wa masuala ya ulemavu) kwa njia ya vifaa na mbinu za kumsaidia mtoto mwenye uzito wa kufuata masomo katika darasa la kawaida. Mwalimu mshauri anaweza kuhudumia kutokea kwenye chumba cha maarifa katika eneo la shule ambamo pia vifaa maalumu vya kufundishia na kujifunzia hutayarishwa au huhifadhiwa. (taz. resource centre). resources: rasilimali: kitu chochote kinachoweza kumsaidia mtu hususan mwenye ulemavu. Rasilimali za ndani ni pamoja na umadhubuti (zihi) na motisha

193 alivyonavyo mtoto na familia yake. Rasilimali za nje ni: wataalamu, mawakala, wafanya maamuzi, vikundi vya wasaidizi, watu wa kujitolea, marafiki, jamaa; (mitandao ya mtoto na familia yake). respiratory patient: mgonjwa wa mfumo wa upumuaji: mtu mwenye tatizo katika mfumo wa hewa ambaye hutumia mashine kupumua. respiratory condition disorder: kasoro ya upumuaji: aina mojawapo ya ulemavu ambapo baadhi ya watu ama huzaliwa na hitilafu kwenye mfumo wa hewa au kutokana na maradhi. Mfumo huu huathirika kiasi cha kushindwa kupumua bila msaada hasa wa mashine. respiratory disease: ugonjwa wa mfumo wa upumuaji: maradhi ya mfumo wa hewa. respiratory distress syndrome (RDS): mlimbikodalili wa mfumo wa upumuaji: kasoro ya upumuaji kwa mtoto mchanga aliyezaliwa kabla ya muda. Hali hii ni miongoni mwa visababishi vya kawaida vya vifo vya kundi la watoto waliozaliwa kabla ya muda. Halikadhalika, ni maradhi ya kawaida kwenye wodi za watoto mahututi. Dalili za kawaida ni upumuaji wa kujilazimisha na udhaifu wa uzungushaji oksijeni kwenye tishu za mwili katika chumba cha hewa. Mtoto mchanga mwenye dalili hii 175 yuko hatarini kuwa na mvurugiko sugu wa mapafu na maradhi ya kiwambo cha hialini. respiratory distress: uharibifu wa mfumo wa upumuaji: udhaifu wa ubadilishaji wa hewa kwenye mapafu unaosababisha upungufu wa upatikanaji oksijeni kwenye damu. Ni mvurugiko wa kawaida ambao huwatokea watoto waliozaliwa kabla ya muda mara wanapozaliwa. respiratory infections: maambukizo katika mfumo upumuaji: aina nyingine ya ulemavu pale ambapo maabukizo haya hudumu kwa muda mrefu au husababisha athari za kudumu. Mathalani, bronkitisi, kifua kikuuu, enfisema, kichomi, saratani ya mapafu, mivurugiko ya kuzaliwa, n.k. Katika nchi zinazotoa pensheni ya ulemavu, kundi hili huhesabiwa miongoni mwa wenye ulemavu baada ya kuthibitishwa na madaktari. respite care: matunzo mpokezano: huduma ya kupokezana anayopewa mhudumu mkuu ili apate fursa ya mapumziko na kupunguza msongo kwenye familia ya mtu mwenye ulemavu. Huduma hii, huongeza ufanisi wa jumla wa mhudumu mkuu. Na kwa kawaida hupatikana katika nchi zilizoendelea. responding: uitikiaji: jinsi mtoto anavyofuatilia mwelekeo na vitendo vya vitu na watu.

194 retard or retarded: taahira:** mtu mweye udumavu wa akili kiasi cha kukabiliwa na ugumu kwenye ujifunzaji. Kwa sasa dhana hii hutumiwa na wanajamii kukashifia wale wasio na uelewa wa kutosha kuhusu jambo fulani. Kiujumla, istilahi hii imebeba maana ashirifu hasi yenye kulenga kudhalilisha aliye na hali ya udumavu wa akili kwa kudhani kuwa hawezi kuwa na mchango wowote kwenye jumuia yake. Kiusahihi, mtu mwenye hali hii anapaswa kuitwa mwenye ulemavu wa akili au ugumu wa ujifunzaji. Rett s disorders: mvurugiko wa aina ya Rett: hali ya nadra ya vinasaba isiyorithiwa ikitokana na mivurugiko ya kinyurolojia baada ya kuzaliwa ambayo huwatokea wasichana pekee na kusababisha vilema vikali vyenye kuathiri kila sehemu ya maisha ya mhusika; ikiwamo uwezo wake wa kuongea, kutembea, kula, na kupumua kiurahisi. rheumatism: baridi yabisi au jongo: taz. arthritis. rheumatoid arthritis: baridiyabisi ya rumatoidi: ugonjwa unaoendelea kwa muda mrefu na kufanya viungo hususani vifundo kuwa na maumivu makali, kukauka na agh. kupoteza umbo lake la awali. rickets: taz. bowlegs. right against unreasonable search and seizure: haki dhidi ya kukaguliwa na kukamatwa ovyo: haki ya kikatiba ya mwananchi 176 ambayo humzuia mtu kwenda nyumbani kwa mwenzake na kuchukua kitu kinachomilikiwa na mwingine kihalali bila ya ridhaa ama ya mhusika au amri ya mahakama. right to due process of the law: haki ya kutendewa sawa kisheria: 1. haki ya kikatiba ya mwananchi kutowekwa korokoroni kwa kipindi kirefu au mali zake kuchukuliwa bila ya yeye kuwa na fursa ya kujitetea mahakamani. 2. haki ya raia kutendewa kwa haki hususani kupelekwa na kuhukumiwa mbele ya vyombo vya kisheria. right to jury trial: haki ya kusikilizwa na baraza la uchunguzi wa awali: haki ya kikatiba (katika baadhi ya nchi) ya mwananchi aliyekamatwa kusikilizwa kwanza na baraza la juu la uchunguzi wa awali kabla ya kupelekwa mbele ya vyombo vya juu vya sheria. Kila inapobidi kupelekwa kwenye mahakama, ni lazima baraza likae haraka jirani na anapoishi mtuhumiwa, ushahidi dhidi yake utolewe na yeye ajieleze akisaidiwa na mwanasheria. righting reactions: mchakatotendani: hali ya mwili wa mtu kujirekebisha moja kwa moja katika kujiweka kwenye mkao wa kawaida na kuwa wima kila unapotoka katika hali moja kwenda nyingine. rigidity: ugumu wa msimamo: hali ya kutoshawishika, kutopinda, kutonyumbulika, kukakamaa.

195 riverblindiness or onchocerciasis: usubi: ugonjwa wa macho au ngozi unaosababishwa na aina fulani ya minyoo wadogo wa aina ya firalia ambao huenezwa na nzi wadogo weusi wanaoishi kwenye maeneo owevu. role playing: maigizo: mchakato wa vikundi vikiwamo vya wanafunzi kufanya mazoezi na kuwa na desturi ya kuiga mienendo ya yale yanayotendeka agh. yakihusiana na mila za kijamii. rollator: roleta: aina ya wenzojongevu wenye magurudumu na breki. Roleta zimeundwa ili kutoa msaada kwa sehemu ya juu ya mwili. Hutumiwa na mtu mwenye shida ya kujongea na kwa kustarehesha au kuondosha mavune. Roleta huenda kimtelezo juu ya ardhi, ndani na nje ya nyumba. Wakati kijongevu cha kijadi hutakiwa kunyanyuliwa kwa kila ngazi, huhitaji msuli, nguvu na upatanisho, roleta hurahisisha matembezi zaidi na inaweza kurekebishwa na kubadilishwa kulingana na mahitaji ya mtumiaji. Kwa kawaida roleta hukunjika kuruhusu kuhifadhika na kusafirishwa ndani ya gari dogo, skuta au chombo chochote cha safiri. rood approach: mbinuasili: uthibiti wa uchangamshaji vihisishi, matumizi ya mfuatano wa kiontojeni na matakwa ya kudai mwitiko kwa njia ya vitendo. rooting response: uitikiaji chanzo: msogeo wa kutafuta chakula ambao hutokea kwa mtoto mchanga kufuatia mguso kwenye midomo au mashavu ukibainishwa na kufungua kinywa na kugeuza kichwa kuelekea upande mguso uliko. Hali hii hutokea kwa mtoto wa umri wa miezi minne hadi mitano, ambaye hajaanza kulishwa na pale anapowekwa kwenye mkao unaohusianishwa na kulishwa. rote skill: stadi ghibu: tabia ya kutenda kwa ulaghailaghai bila kudhamiria. rubella: surua (pia hujulikana kama surua ya Kijerumani au ya siku tatu): maambukizo yasiyo makali kwa mtoto, lakini yenye kuweza kusababisha masikitiko kwa mjamzito kupoteza mimba, kuzaa mtoto mfu au mwenye ulemavu k.m. upofu, uziwi, uharibifu wa moyo au ubongo na viungo vingine vya mwili. Chanjo za utotoni ndizo zinazoweza kutoa kinga dhidi ya maradhi haya. 177

196 Ss safe patterns of sexual behavior mienendo ya ngono salama: utaratibu wa kujamiiana kwa kuchukua kila tahadhari ya kuzuia kuambukizana virusi vya UKIMWI au kutofanya ngono zembe. safeguards: ulinzi: kanuni au utaratibu unaowekwa ili kulida kundi au jambo fulani. safety: usalama: suala muhimu sana katika uga wa ulemavu kutokana na kwamba hali na viwango vya uatilifu husababisha mahitaji ya ulinzi thabiti. scar: kovu: alama inayoachwa kwenye ngozi au tishu yenye mikwaruzo au iliyotuna baada ya kupona. scheduling: utayarishaji wa ratiba: mpangilio wa utaratibu wa jinsi ya kutekeleza mambo mbalimbali kwa kuainisha jambo linalotakiwa kutekelezwa, mhusika na muda wa kulikamilisha. schizo schizoid: skizoidi**: ni mvurugiko wa kutojihusisha na watu wengine, kuwa na maisha ya upweke na kutokuwa na shauku yoyote. Hali hii inalemaza japo mhusika hakabiliwi na tishio la kusambaratika kisaikosisi. Matabibu na wale wasio na ulemavu humpachika mwenye hali hii jina la sizofrenia** kama kumfedhehesha kwa kisingizio kwamba vitendo vyake havikubaliki au havitabiriki. schizoid personality disorder: msawajiko wa haiba skizoidi: hali inayodhihirishwa na mtu kuwa na 178 aibu, hisia kali; kujitenga na wengine, kuwa na ndoto za mchana, kuepuka ushindani wa karibu kiuhusiano, na kuwa na tabia za kipekee. Mchakatotendani wa mtu mwenye kasoro hizi kwa mambo yanayomsumbua agh. huwa mpweke na kutoweza kuelezea hisia kinzani zenye ushari. schizophrenia: skizofrenia:** 1. maradhi ya kiakili ya muda mrefu yanayodhihirishwa na upotoshaji mkubwa wa uhalisia, kujitenga na jamii na mvurugiko wa mawazo, lugha, maono, mwitikio wa kihisia au mvurugiko mkubwa wa akili unaodhihirishwa kwa maneno yasiyoeleweka, kuharibika vibaya kwa uhusiano baina ya mhusika na wenzake, kuvurugika kwa michakato ya kuwazia mambo, kupungukiwa na uwezo wa utambuzi, kuwa na athari dhahiri zisizofaa. 2. ugonjwa sugu wa akili ambao, agh. huanza mwanzoni mwa utu uzima; mwathirika wa sizofrenia hushindwa kuhimili misukosuko ya mazingira yake ya nje na badala yake huishi katika ulimwengu wake mwenyewe wa kusadikika. cv schizotypal personality disorder: mvurugiko wa haiba sizofrenia: hali yenye kuashiria kuwa na mawazo ya ajabu, utambuzi wa mawasiliano na mwenendo kutokuwa mbaya kiasi cha kufikia sifa za sizofrenia na ambayo hujidhihirisha kwa mtu kuwa na mawazo au fikira za woga.

197 Mara nyingi hali hii husababishwa na kuwepo na upekee kwenye mawasiliano yasiyo bayana au utumiaji wa maneno yasiyofaa wakati wa kuchangamana. school phobia: hofu ya shule: woga wa kupindukia wa kwenda shule na mambo yanayohusiana na shule. Chimbuko linaweza kuwa ni wasiwasi wa kuondoka nyumbani na kuwaacha wanafamilia. school psychologist: mwanasaikolojia wa shule: bingwa aliyefuzu katika upimaji wa afya ya akili ya mwanafunzi wa au/na utoaji huduma ya kisaikolojia katika mazingira ya shule. Hufunzwa kumpima mtoto maeneo ya kielimu, kijamii na kimwenendo. Huwa ndiye mtumishi pekee shuleni mwenye mafunzo sadifu ya kupima akili (mithili ya vipimo vya Stanford Binet au Wechsler). Mbali na tathmini, mwanasaikolojia wa shule anaweza kuandaa programu za uboreshaji mienendo, kutoa mapendekezo mahususi ya kielimu, au kunasihi mtoto mmojammoja au kikundi. sclerosis: sklerosisi: hali ya sehemu fulani ya mwili kuwa ngumu kutokana na uvimbe/mfutuko au fibrosisi; hutumika hususani kuelezea kupungua kwa tembwe nyumbufu katika kuta za ateri (ateriosklerosisi) na kuongezeka kwa tishu ya glia (gliosisi) katika mfumo wa neva. cvi 179 scoliosis: skoliosisi: hali ya kupindika, hususani mgongo kwa kubonyea upande mmoja na mwingine kutuna. screen: chunguza: 1. pima kwa kutumia eksirei na mbinu ya floresensi. 2. pima mtu ili kugundua kama ana hitilafu fulani au la. screen enlargers, or screen magnifiers: vikuzaji skrini: vitumi vinavyofanya kazi sawa na kiookuzi kwa ajili ya kompyuta kukuza sehemu ya skrini ili kuongeza usomekaji na kurahisisha mwonekano wa vitu kwenye kompyuta. Baadhi ya vikuzaji skrini huruhusu mtu kuvuta karibu au mbali sehemu fulani ya skrini. screen readers: visomaji skrini: 1. programu za maunzilaini yenye kubadilisha maandiko kuwa sauti iliyosanisiwa ili mtu asiyeona kuweza kusikiliza maudhui ya mtandaoni. 2. programu zinazomwezesha mtumiaji asiyeona kutafuta maudhui mtandaoni kwa njia mbalimbali; mathalani, kusoma kila kitu kuanzia juu hadi chini, kuvinjari kiunga kimoja na kingine, au kutoka kichwa kimoja cha habari hadi kingine, au kutoka fremu moja hadi nyingine (endapo zipo fremu), n.k. Programu za aina hii ni:

198 JAWS, Window Eye, Home Page Readers. 3. programu zinazoweza kutumiwa na kiziwi asiyeona pale visomaji skrini vya kubadilisha uamilifu wa matini kuwa ya nuktanundu na kuweza kupapasika. Kimantiki, kisomaji skrini hugeuzageuza vitumishi vya kiishara au michoro na vielelezo kuwa vya kisauti. Visomaji skrini ni muhimu kwa mtu asiyeona mwenye kutumia kompyuta. screen resolution: uundaji taswira kwenye skrini: dhana inayotumika kuelezea idadi ya vinukta vilivyotumika kuonyesha sura. Utaswirishaji wa juu zaidi humaanisha kwamba nukta zaidi zimetumika katika kuunda sura na matokeo yake ni sura angavu na safi zaidi. screening: uonyeshaji: filamu au programu za televisheni zinazoonekana kwenye skrini. scrotum: kifukokorodani: 1. kifuko kilicho katikati ya miguu ya mwanamume ambamo ndani yake hukaa kokwa mbili. 2. ngozi inayohifadhi kende katika mamalia. secondary disability: ulemavu fuasi: tatizo linalotokea baada ya kilema cha awali kutatizika zaidi kuliko kilivyokuwa mwanzoni; k.m. msinyao wa vifundo baada ya mguu au mkono kudhoofu; ugonjwa wa kisukari kusababisha uhanithi, kukatwa kiungo au kupata upofu. 180 segregated educational facility: huduma za kielimu zilizotengwa: eneo la kielimu lililo tofauti na yale ya mfumo wa kawaida kwa ajili ya mtoto asiye na ulemavu, agh. likifahamika kama shule maalumu. segregation: utenganisho: mfumo ambao umekuwa ukikiuka haki za binadamu kwa kudhani kuwa mtu mwenye ulemavu hawezi wala hustahili kujumuishwa na watu wengine wasiokuwa na hali hiyo. Kwa maana hiyo, afua za kumhudumia, daima zimekuwa ni zile zilizotengwa kwa ajili yake, kwa maana ya makazi na huduma za kijamii. Mfumo huu umechangia sana kudumaza stadi za maisha ya kundi hili. seizure disorders: mivurugiko ya mitukutiko: mashambulio yanayobainishwa na misogeo isohiari au mabadiliko ya ufahamu au mienendo. Hizi ni dalili za mivurugiko ya ndani kwa ndani kwenye ubongo. Mara nyingi, nguvu za umeme mwilini hupitia kwenye mishipa ya neva kimpangilio. Mtukutiko hutokea pale milipuko isiyo na mpangilio ya nguvu za umeme mwilini zinapoingilia kazi za ubongo. Shambulio hili linaweza kutengwa kulingana na chanzo, sehemu ya ubongo inayohusika au dalili zake. seizure: mtukutiko: shambulio la ghafla la ugonjwa; tukio la kurudiarudia kwa ugonjwa (ang. epilepsy).

199 self-advocacy: kujitetea: hali ya kujiwakilisha kwa kufanya utetezi binafsi kudai haki na masliahi au kujitafutia jawabu la tatizo linalomhusu. Aina hii ya utetezi ndilo lengo la aina nyinginezo za utetezi; stadi za kujihifadhi na kujifanyia usafi, kujilisha, kujivisha na kujitunza katika ujumla wake. self assessment: kujitathmini binafsi: hali ambapo mtu huwajibika kujipima yeye mwenyewe jinsi alivyomudu kutekeleza mambo yanayomhusu katika kipindi maalumu. Hii inaweza kuwa kimasomo, kiajira, n.k. self directed learning: ujifunzaji binafsi: mtido wa ufjiunzaji wa kujielekeza binafsi badala ya mwalimu kumlisha mwanafunzi kila kitu kwa kumkaririsha. Mtaala hutoa fursa kwa mwanafunzi kufanya udadisi baada ya maelekezo ya awali kwenye mada, halafu hutakiwa kujiongezea maarifa kwa kudadisi na kugundua mambo. self esteem: kujithamini: hisia za mtu za kujithamini. (Chukulia kujistahi kama taswira yake mwenyewe aliyonayo kichwani. Sasa fikiria jinsi taswira hiyo ingeliweza kubadilika iwapo daima hakuelewa kinachozungumzwa, kama angeshindwa mtihani kutokana na kuelewa vibaya maelekezo, nk). Nyakati nyingi istilahi hii humaanisha kujitukuza; kujiona; kiburi. 181 self evaluation: taz. self assessment. self-contained programme: programu kamilifu: mazingira maalumu ya kimasomo kwa mtoto stahilifu mwenye mahitaji maalumu ya elimu na huduma ambatani zenye kuhitaji utaratibu thabiti wa kimaelekezo au kiufundishaji. self-contained special education classroom: darasa toshelevu la elimu maalumu: chumba cha masomo kilichotengwa na ambacho mtoto mwenye mahitaji maalumu kielimu hutumia muda wake mwingi wa kutwa anapokuwa shuleni. Kwenye mfumo huu, mtoto huyu huchangamanishwa na wenzake (wasio na ulemavu) kila inapowezekana; k.m. katika mambo yasiyokuwa ya kimasomo na kwenye viwanja vya michezo. self-directed learning materials: vifaa binafsi vya kujifunzia: (ang. self directed learning ). self-fulfilling prophecy: utimizaji wa ndoto binafsi: falsafa kwamba mtu atatenda kulingana na matarajio yenye kudhihirishwa na wale waliomzunguka (au kile anachopachikwa kuwa). self-help skills: stadi binafsi za kujimudu: maarifa na utendaji wa shughuli za kawaida za kujitunza binafsi kama vile kuvaa nguo, kuoga, kujitawaza mwenyewe kwa msaada au bila msaada wa visaidizi rekebefu. (taz. activities of daily living ).

200 self-limitations: ukomo binafsi: viwango vya mipaka anayojiwekea mtu mwenyewe katika utendaji. semantic pragmatic disorder (SPD): mvurugiko wa elimumaana vitendo: ugonjwa wa lugha ambao huathiri mchakato wa uelewa na matumizi ya lugha kivitendo. Vitendo hujielekeza kwenye matumizi ya lugha katika muktadha wa kijamii (kujua kipi cha kusema na lini kisemwe kwa watu). Elimumaana hujielekeza kwenye maana ya maneno na misemo. semantics: elimumaana: kipengele cha lugha kinachojihusisha zaidi na maana au kueleweka kwa lugha. senile dementia: kupungua kwa kumbukumbu uzeeni: hali ya kuzorota kwa akili kwa muda mrefu inayoongezeka polepole ikihusishwa na msinyao wa jumla wa ubongo na uharibifu wa nyuroni. Kisababishi cha hali hii hakijulikani bado. Hakika uzee siyo sababu ya hali yenyewe ila inawezekana kuwa aina hii ya ugonjwa inazo chembechembe za Alzema kwa mbali. Uchakavu unaweza kuwa wa viwango vya chini hadi vya juu sana. Ugonjwa huu unapaswa kutofautishwa kwa makini na ule wa mlimbikodalili wa ubongo ambao hutibika. senses: milango ya fahamu: mjumuiko wa milango mitano ya fahamu inayosaidia kwenye mawasilino kati ya mtu na mazingira yake; kuona, kusikia, kugusa, kunusa na kuonja. sensitivity: kiwango cha hisia: jambo linaloweza kuchochea hisia kali kutegemeana na aina ya muonjo au mlango wa fahamu. sense of dignity and self worthy: kuthamini utu: hali ya kutambua hadhi na thamani mtu aliyonayo. sense of humour: ucheshi: hali ya kuwachangamkia watu wengine. sensorimotor: -a hisimjongeo: -enye kupokea msogeo wa neva za fahamu. sensory aphasia: afazia fahamu: hali ya kutoweza kuelewa maana ya lugha iliyoandikwa, inayoongewa au ishara za mguso kutokana na maradhi au majeraha kwenye vituo vya kusikilizia, na kuonea katika ubongo. Pia hufahamika kama afazia pokezi. sensory awareness: utambauzi wa fahamu: uwezo wa kupokea vichocheo kutoka kwenye mazingira, na hisi za kuona, kusikia, kugusa, kunusa na kuonja. sensory development: ukuaji wa milango ya fahamu: hali ambapo moja au zaidi ya milango ya fahamu inavyokuwa na kuweza kuitikia vichocheo ipasavyo. Hujielekeza kwenye ukuzaji wa stadi na utendaji katika kutambua na kupambanua vichocheo vya nje na ndani, ikiwa ni pamoja na vile vya miguso, kutambua mwendo, upokeaji wa 182

201 vichocheo vya ndani, kuona, kusikia na matundu ya milango ya fahamu. sensory impairment or disorder: kilema cha milango ya fahamu: kasoro inayoathiri mguso, uoni, mionjo, mnuso au usikivu. Uatilifu wa utendaji wa mojawapo au zaidi ya moja ya milango ya fahamu. Hali kama hiyo inaweza kuwapo tangu kuzaliwa au inaweza kujitokeza wakati wowote wa maisha kutokana na kuumia au maradhi. sensory learning: ujifunzaji hisishi: mbinu kuu ya kumfundisha mtu mwenye uziwipofu kwani umaizi wake hutegemeana sana na kuhisi mambo yaliyomzunguka. sensory nerve: mshipa wa fahamu: selineva inayomwezesha mtu kuhisi k.m. anapokanyaga kitu chenye ncha au joto kali. Agh. mshipa huenda sanjari na kitendo kisicho hiari ili kuepusha madhara. Mathalani, kitu kisichotakiwa kikiingia jiachoni, puani au kinywani, mara moja machozi, mate au kamasi hutokea kwa wingi ili kuzimua kile kisichotakiwa. Wakati mwingine mtu hujikuta anapata kichefuchefu na kutapika katika mazingira kama haya. sensory processing disorder (SPD): mvurugiko wa uchakataji fahamu: kasoro changamani ya ubongo inayomsababishia mtoto kutafsiri visivyo taarifa za kila siku za kihisia kama vile msogeo, sauti na mguso. Mtoto mwenye mvurugiko wa aina 183 hii anaweza kuwa na hisia kali au kujisikia kuelemewa na taarifa. sensory: -a fahamu: -enye kuhusiana na mifumo mingi ya fahamu: kugusa, mwendo, kunusa, kuona, kusikia, n.k. sepsis: sepsisi: maambukizo makali yanayosambaa kwenye damu. service animal (in a broader term assistant animals): mnyama mwega: mnyama yeyote aliyefunzwa au anayetenda majukumu kwa manufaa ya mtu mwenye ulemavu k.v. mbwa mwongozaji ambaye ni mfano mashuhuri wa wanyama waongozaji kwa huduma kama vile: kumwongoza mtu asiyeona (mnyama mwongozaji hususani mbwa); uashiriaji kwa viziwi kuhusu sauti au milio (mnyama msikilizaji); kumfanyia kazi mtu mwenye aina nyingine za ulemavu mbali na kutoona au uziwi k.m. kutoa ulinzi usiohusisha ukali au vitisho; shughuli za uokozi; kuvuta kitimwendo; kumsaidia mtu aliyepoteza fahamu kutokana na kifafa; kutahadharisha juu ya kuwapo kwa vichochea mizio; kutumwa kutafuta vitu mathalani dawa au simu; kuzuia mienendo ya kihalifu, kutoa faraja (ni mwega wa kihisia); n.k (taz. live assistance and intermediaries ). servitude: utumwa: hali ambapo mtu huwa chini ya miliki ya mwingine akipangiwa kazi ngumu kwa

202 malipo duni au bila malipo kabisa. Kundi la watu wenye ulemavu ni miongoni mwa waathirika wa hali hii pale wanapofanyishwa kazi za ndani zisizo na idadi wala ujira wa haki kwa kisingizio kuwa anapewa matunzo. severe and profound multiple disorders: mivurugiko mikali tofautitofauti: upungufu wa kinasaba ambao huhusisha viungo, ufahamu, akili na/au kuchangamana kijamii. Upungufu huu hauishii kwenye mfumo wowote ila hujidhihirisha kwenye mifumo yoyote ya kimazingira na agh. hujumuisha maeneo mengi ya kiutendaji. Mtu mwenye mivurugiko ya kiutendaji kwenye ngazi hii huhitaji sana mabadiliko ya mazingira kwa kuzingatia matunzo, tiba na makazi. sex linked condition: halirithi ya jinsi: hali ambazo mtoto huzipata kutoka kwa wazazi kwa njia ya chembeuzi jinsi. Wazazi wa kike ni waenezaji wa hali hii bila wao wenyewe kuwa nayo. Mifano hujumuisha distrofi ya misuli na hemofilia. sex: jinsi: tofauti za kibiolojia kati ya mwanamke na mwanaume ambazo hufafana duniani kote. sexism: ujinsia: ubaguzi wa kundi la jinsi moja dhidi ya kundi lenye jinsi tofauti. Mathalani, kubaguliwa na kutawaliwa kwa mwanamke mwenye ulemavu na mwanamume, k.v. kubakwa na mwanamume mwenye kuishi na virusi vya UKIMWI ili ajitakase kwa njia ya ngono au mtazamo wenye kusababisha hili. sexist: -enye upendeleo kijinsia: mtu ambaye humtendea tofauti au kumzungumza vibaya mwenziye wa jinsi tofauti na yake. sex-role stereotyping: kukariri majukumu kijinsia: hali ya kunasibisha visivyo mienendo, uwezo, shauku, maadili na majukumu ya mtu au kikundi kwa kuegemea jinsi. sexual abuse: unyanyasaji kingono: 1. hali ya kumlazimisha mtu kufanya ngono bila ridhaa yake. 2. kufanya tendo la kujamiiana baina na miongoni mwa mahirimu, kushambuliwa au kunyonywa kingono. sexual and reproductive health: afya ya ngono na uzazi: maarifa muhimu kwa mwanadamu hususani wa kike yanayomwezesha kumudu kuutawala mwili wake kwa kadiri ya utashi wake. Mwanamke mwenye ulemavu hupungukiwa maarifa haya kutokana na kutengwa na mifumo rasmi na ile ya kijamii. Kwa maana hiyo, ubora wa maisha yake huathiriwa. sexual embarrassment: usumbufu kijinsia: mazingira ambayo hujengwa hasa na jinsi ya kiume isiyokuwa adilifu kwa kulazimisha hisia zake kwa mtu wa jinsi ya kike k.m. mazoea ya kutamka matusi ya nguoni kwenye 184

203 kadamnasi kiasi cha kudhalilisha jinsi. sexual and gender based violence: uonevu kwa misingi ya jinsi na ujinsia: hali ya kudhulumiwa kimwili, kihisia au kingono. sexual mental fantasies: taswira za kingono: hali ambapo mtu hujenga tabia ya kuifurahisha nafsi yake kwa kujenga taswira ya kingono na mtu anayemtamani ili kuamsha ashiki. Mara nyingi hiki huwa chanzo cha tabia ya kujichua (kupiga punyeto) hasa yule mwenye ulemavu wa aina ya kuwaogopa wanawake, wapiga chabo, n.k. huathiriwa sana na hali hii. sexual orientation: mvuto wa ngono: hali ya mtu kuvutiwa kingono na kuwa na uhusiano wa kimapenzi bila kujali jinsi. sexual violence: uonevu kingono: tendo lolote la kingono, ikiwa ni pamoja na jaribio la kupata ngono, matamshi yasiyotakiwa ya kingono, kutongoza, matendo ya kusafirisha wanawake kwa lengo la kuendesha biashara ya kingono kwa shuruti, vitisho vya kudhuru au kutumia nguvu vinavyofanywa na mtu yeyote bila kujali uhusiano na mwathirika katika hali yoyote ikiwa ni pamoja na majumbani na kazini. sheltered workshop: karakana ya amali tengefu: shughuli za kiufundi za uzalishaji ambazo dhana zake zimekuwa zikibadilika 185 ili kuendana na zile dhana na utambuzi ambao umekuwa ukiibuka kila baada ya vipindi. Huko nyuma, shughuli za aina hii zilikuwa zimetengwa mahususi kwa ajili ya kundi la watu wenye ulemavu. Kufuatia wito wa mwelekeo uliopo wa suala la ulemavu na kuwajumuisha wahusika katika nyanja zote za maisha, baadhi ya nchi zimebadilisha majina ya afua zenyewe na utekelezaji wake k.v. vituo vya amali, ujasiria jamii, uzalishaji kwa watu wenye ulemavu, n.k. shock: mshtuko: hali ya hatari kwa kudhoofu vibaya au kupoteza fahamu, kuwa na mapigo ya haraka au dhaifu ya moyo. Hali hii husababishwa na kuishiwa damu mwilini, kuvuja sana damu, majeraha, kuungua au maradhi makali. shunt: kichepuzi: mpira ambao huingizwa katikati ya mishipa ya mwili kwa njia ya upasuaji. Lengo lake ni kuondosha maji ya ziada na kupunguza mgandamizo kwenye ubongo kwa mwenye hidrosifalasi. Agh. uchepushaji hulenga kupunguza mgandamizo kwenye ubongo na kwa kuhamishia kiwoevu katika ogani nyinginezo kama vile kwenye moyo au tumboni; k.m. mchoro wa pili ni aina ya kichepuzi ambayo hutumika sehemu nyingi katika kufanikisha lengo hili.

204 sickle-cell anemia (SCA): anemia selimundu: ugonjwa wa kurithi wenye athari kubwa kwenye utendaji na umbo la seli nyekundu za damu. side effects: athari tokezi: mabadiliko yanayotokea mwilini zaidi ya yale yanayohitajika katika kupambana na maradhi au ujauzito kama matokeo ya mjibizo wa homoni au matumizi ya dawa. sign language: lugha ishara: mawasiliano rasmi kwa njia ya mikono ambapo maneno na dhana huwasilishwa kwa njamna ya mikao ya mikono, ishara za maungo na/au wajihi, mifumo ya ishara za kimaumbo, tajihia za vidole, ili kuwasiliana na/au miongoni mwa viziwi au wale wenye usikivu hafifu na uziwipofu. Lugha ishara hujumuisha ishara za lugha halisi mbalimbali ikiwamo ya Kiswahili. Kila kundi la viziwi (kitaifa au kikanda) linaweza kuwa na lugha ishara zake. Halikadhalika, kuna lugha ishara za kimataifa. sign: dalili: pamoja na mambo mengine, ni ashirio la hali ya maradhi ambazo huthibitishwa kwa kifaa utaratibu wa kisayansi na mchunguzi aliyefunzwa kuliko kutolewa taarifa tu. signatories to the convention: mtiaji saini mkataba: mtu, wakala au asasi inayosaini makubaliano rasmi. Katika utaratibu wa Umoja wa Mataifa, hii huwa hatua ya mwanzo baada ya Baraza Kuu kupitisha azimio la kuukubali Mkataba unaohusika inayofuatiwa na uridhiaji kwa mwanachama mmojammoja. single parent: mzazi mmoja: mtu ambaye hajaolewa, hajaoa au aliyejitenga/tarakiwa na mzazi mwenzake kisheria na ana mtoto au watoto anaowatunza peke yake au kiushirika na mzazi mwenzie kwa mujibu wa hukumu ya mahakama. sip-and-puff system: upumuaji endeshi: teknolojia saidizi inayotumia msukumo wa hewa katika utumaji ishara kwenye kifaa cha kieletroni. Hewa hii ni ama kwa kuvutwa au kupumuliwa kupitia kwenye mrija, tyubu au kifimbo maalumu. Kimsingi, teknolojia hii hutumiwa na yule ambaye mikono yake haifanyi kazi. Ni njia inayotumika kuongozea kitimwendo kwa aliye na paraplejia au aliyeumia vibaya uti wa ubongo. 186

205 na kushabikia jambo wakati mwingine hata bila kuichambua kwa kina. slow learner: mwanafunzi mwenye uzito wa kujifunza: mwanafunzi anayetumia muda mrefu zaidi kuelewa mafunzo kutokana na sababu za kimaumbile kwenye mfumo wa ubongo. situation of risk and humanitarian social and vocational ability: uwezo emergencies: hali ya hatari na wa kumudu mambo ya kijamii na mahitaji ya dharura: mwitiko wa kiufundi: hali ambapo mtu mwenye haraka wa jamii baada ya maafa ulemavu anapoweza kumudu kutokea k.m. ukame, mafuriko, ajali kuchangamana kwenye jamii ya moto, vita, tetemeko la ardhi, (akichangia maoni na kushiriki kimbunga, n.k. ili kunusuru uhai na shughuli za kijamii) na pia kuzalisha kuwapunguzia waathirika mateso. kwa manufaa yake binafsi na ya Maafa yanapojitokeza, agh. mtu jamii anamoishi. mwenye ulemavu huwa mwathirika social integration: mtangamano wa mwanzo kutokana na: (i) jamii: mchakato unaodhihirisha kutomudu kujiokoa mwenyewe, na utaratibu ambao mtu mwenye (ii) kukosekana kwa maandalizi ya ulemavu hasa ule wa kisakitria makusudi ya mwitiko wa papo kwa hujiongezea na kukuza uwezo papo kunusuru mwathirika. wake wa kujumuika. Kwa Maandalizi kama haya ni pamoja na kuunganika inamaanisha kujenga (a) kuwapo kwa kanzidata ya na kufanikiwa kudumisha kuziwezesha mamlaka kumjua kila mjibizano wa kiuhusiano ili mtu mwenye hali hii anapoishi na kujenga urafiki, kupeleka hisia (b) sehemu fikivu anapoweza nzuri na werevu pia. kupelekwa pale hali ya dahrura social interaction: mchangamano inapotokea. jamii: hali ambayo mtu mwenye skill: stadi: ujuzi au maarifa ya kufanya ulemavu huweza kuchangamana jambo vizuri. na wanajumuia kirahisi na hivyo slogan: kaulimbiu: wito muhimu katika kushirikishana uzoefu pamoja na harakati za kushawishi mabadiliko kupata fursa za kuchangia kwani ujumbe muhimu hutolewa maendeleo ya pale anapoishi. kwa ufupi na kwa njia inayovutia social model: mtindo wa kijamii: kiasi cha mlengwa kuikariri kiurahisi namna ya kuliona tatizo la mwenye 187

206 ulemavu kwamba limejikita ndani ya jamii, na siyo ndani ya mhusika mwenyewe. Kwamba siyo kilema kinachomlemaza mhusika bali mitazamo na vizuizi vinginevyo ndani ya jamii kwa ujumla. Marekebisho yanayofanyika kwa kina katika muundo wa kijamii hujielekeza kwenye uondoshaji mikingamo ngazi ya mhusika binafsi, halikadhalika katika mazingira, mtazamo na taasisi mtawalia. Mtindo wa kijamii uliasisiwa ili kukabiliana na hali ya suala la ulemavu kuwa la kitabibu zaidi pamoja na athari zake kubwa kwenye utambuaji wa mhusika mwenye ulemavu. Halikadhalika athari hasi za kimtazamo ambazo hujikita kwenye mitindo ya kihisani na kitabibu. Mtindo wa kijamii hulenga zaidi kuweka uelewa mzuri zaidi wa haki za mtu mwenye ulemavu na matokeo ya lazima dhidi ya mikingamo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira yenye kuathiri uwezo wake wa kushiriki katika maisha ya jamii. social pressure: msukumo wa kijamii: tukio ambapo mtu hulazimika kutenda jambo kwa kuitikia mtazamo wa jamii badala ya kupima uwezo, sababu na matokeo ya kutenda jambo lenyewe. Mtu mwenye kidhibiti nafsi nje, ni mwepesi wa kuanguka kwenye mtego huu. 188 social protection: uhifadhi jamii: mfumo ambapo mamlaka za nchi huweka utaratibu wa kumtambua mapema na kumhudumia raia mhitaji katika utaratibu maalumu usio na usumbufu ambapo uwezo hujengwa polepole ama kwa kuchangia kidogo kabla ya tukio au rasilimali kutokana na hazina ya serikali kutengwa kwa minajili hiyo. Kwa utaratibu huu mhusika huhudumiwa bila usumbufu. social re-integration: mtangamano mpya wa jamii: hali inayomtokea mtu baada ya kujitenga na jamii yake kutokana na maradhi ya muda mrefu au ulemavu, kufungwa gerezani kwa muda mrefu, kushiriki kwenye vikundi vya kihalifu (mauaji, matumizi ya mihadarati), n.k. social security: hifadhi kijamii: 1. muunganiko wa afua ambazo huanzishwa na jamii ili kusaidia kustawisha na kunufaisha kila mwanajamii kwa kadiri inavyowezekana katika nyanja za utamaduni, ajira, ustawi wa jamii ambazo hutolewa ndani ya nchi. Halikadhalika, inaweza kuwa programmu ya kiserikali inayolenga kukuza ustawi wa umma na hususani makundi yenye uelekeo wa kudhurika (watoto, wazee, wagonjwa, wasiokuwa na ajira, watu wenye ulemavu) kwa njia ya misaada inayohakikisha upatikanaji wa

207 rasilimali za kutosha kwa ajili ya chakula na makazi, huduma bora za afya, na hali njema. Kwa ujumla huduma zenye kulenga kuhifadhi jamii, agh. hujulikana kama huduma za jamii. 2. ruzuku ya serikali kwa wasiojiweza na wasio na kazi. cvii social skills: stadi za jamii: 1. maarifa changamano kwa wanarika. 2. stadi za uhusiano kati ya mtu na mtu, kuwajibika kijamii, kujistahi, ujanja au mbinu, unyofu k.v. tahadhari au uangalifu, kutatua matatizo ya kijamii na uwezo wa kuheshimu kanuni au sheria na kuepuka kuonewa. social system: mifumo ya kijamii: utaratibu wa kuweka matabaka ya watu kwa malengo, majukumu na matarajio mahususi. social work services: huduma za uamarajamii: miawana inayotolewa kwa familia katika muktadha wa kijamii ambayo inaweza kumpatia mhitaji mazingira sadifu kwa ustawi. socially maladjusted: -enye mhemko katika jamii: -a matatizo makubwa ya kujihusisha na watu wengine ipasavyo kutokana na kuwa na mhemko. social welfare: masilahijamii: utaratibu wa serikali wa kutatua matatizo ya wanajamii ili kuwaboreshea maisha. Utaratibu huu hutofautiana kati ya jamii zilizoendelea na zile zinazoendelea. Kwa nchi 189 zilizoendelea, utaratibu huu huhusisha utoaji wa ruzuku na afua za matunzo kwa mtu asiyekuwa na ajira au kipato ili amudu kujikimu. Kwa nchi zinazoendelea, utaratibu huu huishia kwenye uendeshaji wa makazi kwa baadhi ya watu wasiokuwa na matunzo, usuluhishi wa migogoro ya ndoa, uadilishaji wa vijana walio kwenye mgongano na sheria, miradi ya watoto chini ya miaka saba, n.k. sociopath: mkirihisha jamii: mtu mwenye mvurugiko wa kihaiba unaojidhihirisha kwa kuwa na tabia ya kutochangamana na jamii hasa mwenye kutumia mabavu bila kujutia. sonic guide: sauti elekezi: kifaa cha kielektroni kwa ajili ya mtu wasiyeona ambacho huvaliwa kichwani na hutoa sauti na kugeuza picha kuwa kelele zenye kusikika kwa ajili ya kumwelekeza mtumiaji. spastic hemiplegia: mshtuko wa hemiplejia: hali ya kupooza kwa mkono na mguu wa upande mmoja kutokana na madhara katika ubongo wa nyuma ambako husababisha kukakamaa. Inawezekana mikono na miguu yote kuhusika na upande mmoja ukikakamaa zaidi kuliko mwingine. Hii huitwa hemiplegia ya pande mbili au mshtuko wa kwadriplejia.

208 spastic quadriplegia: mkakamao kwadriplejia: kuharibika kunakokuhusisha mikono na miguu yote. Kuharibika kwa telensefaloni hufifisha misogeo kutokana na kuongezeka kwa kukakamaa kunakolingana katika sehemu zote nne, yaani mikono na miguu yote. spastic: mwenye mkakamao misuli**: mtu mwenye mpoozo wa ubongo. Hata hivyo, istilahi mwenye mtindio wa ubongo** hutumiwa na wengi kiudhalilishaji katika kubainisha mtu yeyote anayetenda tofauti na wengine kwa vichocheo vya nje. Kiusahihi, inafaa mtu mwenye hali hii kutambuliwa kama aliye na ulemavu wa ujongeaji kutokana na kwamba uatilifu kwenye ubongo huathiri mjongeo wake pia (taz. hemiplegia, quadriplejia, paraplegia ). spasticity: mkakamao misuli: 1. a kukakamaa misuli; -enye kuhusiana na misuli inayokakamaa ghafla. 2. hali ya kukakamaa kusikodhibitika kwa kukaza au kuvuta misuli ambako hufanya ujongeaji kuwa mgumu. Agh. mkakamao hutokea sanjari na ubongo kupooza, kuumia kwa uti wa ubongo au ubongo wenyewe. spatial orientation: utambuzi maeneo: uwezo wa kupangilia eneo kwa kuzingatia mtu mwenye ulemavu na mazingira yake kwa kuwianisha umbali, ukubwa, nafasi na uelekeo. 190 special assistance: msaada mahususi: mafunzo yaliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya mwalimu ili kumsaidia kufundisha darasani au kwenye maabara, akitumia vitabu vilivyorekodiwa kwenye kanda, wasomaji kwenye maktaba, wakalimani wa lugha ishara, vifaa darasani vilivyorekebishwa, maboresho ya miundombinu au mbinu nyingine zinazofaa katika kufanya vifaa vinavyotolewa shuleni au/na mbinu zinazotumika kufundishia kumnufaisha pia mtoto mwenye kilema k.m. usikivu, upofu au hitilafu ya kiungo. special citizen: raia maalumu:** tasfida iliyobuniwa na kutumika kipindi fulani na katika baadhi ya nchi badala ya kiwete ili kukwepa ukakasi. Hata hivyo tasfida hii haikukubalika kimataifa na badala yake mtu mwenye ulemavu likawa mbadala. special education (SPED, Speced): elimu maalumu: mafunzo mahususi yaliyoandaliwa ili kukidhi mahitaji ya kipekee ya mwanafunzi mwenye ulemavu wa aina fulani tu. Hii ni pamoja na mafunzo ya darasani, mazoezi ya viungo, nyumbani, hospitalini na kwenye makazi. special education classroom: darasa la elimu maalumu: (ang. self-contained special education classroom ).

209 special education coordinator: mratibu wa elimu maalumu: msimamizi wa programu za elimu maalumu katika ngazi ya shule, wilaya au taifa. special education services: huduma maalumu za elimu: programu, huduma au mafunzo yaliyoandaliwa (yakitolewa bila kuzigharimu familia) kwa ajili ya mtoto wa umri zaidi ya miaka mitatu aliye na mahitaji na stahilifu kwa huduma kama hizo. Huduma hizi hujumuisha mbinu maalumu za kujifunzia, au vifaa kwenye darasa la kawaida au/na darasa na programu maalumu iwapo ujifunzaji au matatizo ya kimaumbile ni ya kiwango kikubwa. special education teacher or specialist teacher: mwalimu mtaalamu wa elimu maalumu: mtu aliyefuzu mafunzo ya nyongeza kwa minajili ya kumwelimishaji mwanafunzi mwenye kilema k.v. akili, uziwipofu, n.k. kwenye ngazi ya elimu ya awali, msingi au sekondari. special educational needs (SEN): mahitaji maalumu ya kielimu: mambo ya msingi kwa matatizo ya ujifunzaji au ulemavu ambayo huhitaji elimu maalumu kutolewa kwa ajili ya mhusika. Mlengwa ni mtoto mwenye umri wa lazima wa kwenda shule au kijana mwenye uzito wa ujifunzaji kutokana na ulemavu, lugha, mifadhaiko ya maisha, tabaka la kabila au hali ya 191 kiuchumi na kipawa cha kuelewa haraka. Hali hizi husababisha ama uzito au wepesi zaidi wa ujifunzaji kuliko wengine ambao humkwaza mtoto kutumia vifaa vya elimu au/na mbinu za ufundishaji au ujifunzaji ambavyo kwa kawaida hutolewa kwa jumla kwa wengine wenye umri sawa na wake katika shule za kawaida au michepuo ya baada ya elimu ya msingi kiasi cha kuhitaji mbinu mbadala za kufundishiwa na kujifunzia tofauti na wenzake. special learning needs: mahitaji maalumu ya ujifunzaji: kuwa katika hali ya kuhitaji uangalizi makini ili kusaidiwa wakati wa kujifunza. special needs child: mtoto mwenye mahitaji maalumu: 1. dhana ya jumla ya kumpambanua mtoto ambaye hafikii matarajio ya kielimu kiasi cha kuhitaji huduma na rasilimali ambazo ni tofauti na zile zinazohitajiwa na watoto wa kawaida. 2. dhana inayotumika kumwelezea mtoto mwenye ulemavu au aliyeko hatarini kupata ulemavu ambaye anahitaji huduma maalumu au kutendewa tofauti ili aendelee na masomo. 3. dhana ya dhalilishaji kwa mwenye uzito wa kujifunza ambayo ni kejeli inayoelekezwa kwa mtoto kwa kufikiriwa kwamba si mahiri darasani.

210 special olympics: olimpiki maalumu: michezo inayoshirikisha watu wenye ulemavu wa akili peke yao wa umri wa kuanzia miaka minane na kuendelea. special population: kundi maalumu: jumuiko linalobainishwa kama mojawapo ya makundi duni kwa vigezo vya kiuchumi, kitaaluma, kutomudu vizuri lugha, ulemavu, wanaume wanaofanya kazi ambazo kwa jadi hufanywa na wanawake, wanawake wanaofanya kazi ambazo kijadi hufanywa na wanaume. special schools: shule maalumu: dhana ya jumla inayotumika kwa kubainisha shule zilizotengwa kwa ajili ya watoto wenye kilema cha aina moja au mchanganyiko wa aina za vilema au wenye vilema na wasiokuwa navyo. special seat: kiti maalumu: 1. aina ya kiti kinachotengezwa mahususi kwa ajili ya mtu mwenye hali na kiwango fulani cha ulemavu wa viungo; mathalani, aliyepata kilema kutokana na kuumia uti wa ubongo kiasi cha kupooza na kupoteza hisia sehemu kubwa ya maungo yake. Kiti cha aina hii humsaidia kukidhi haja za ujongeaji, kuandika, kulia na hata kujisaidia (muktadha wa watu wenye ulemavu). 2. nafasi za uwakilishi kwenye medani za kisiasa zinazotengwa kwa ajili ya kujazwa na kundi fulani la raia; 192 k.v. wenye ulemavu, vijana, wanawake, n.k. specialised instruction: mafunzo maalumu: 1. huduma za awali zenye kujumuisha shughuli ambazo huendeleza upatikanaji wa stadi katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na michakato ya utambuzi na kuchangamana kijamii. 2. msaada wa kimafunzo kwa mtoto, familia na wote walio katika mazingira yanayomzunguka mhusika ili kuboresha maendeleo yake ya ukuaji na ustawi. specific learning disability: uatilifu mahususi wa ujifunzaji: 1. mvurugiko katika kuelewa au kutumia lugha ya kutamka au kuandika unaobainishwa na uwezo mdogo wa kusikiliza, kufikiri, kuongea, kusoma, kuandika, tahajia, au kukokotoa hesabu. Hali hii hujumuisha mwanafunzi mathalani mwenye mvurugiko wa mawazo, kuumia ubongo, hitilafu ndogo za ubongo, disleksia, na afazia ya ukuaji. Dhana hii haihusishi mwanafunzi mwenye matatizo ya ujifunzaji ambayo kimsingi yanatokana na kilema cha uoni, uziwi, ujongeaji, kupooza ubongo au changamoto za kimazingira, kiutamaduni na kiuchumi. 2. kasoro

211 moja au zaidi ya michakato msingi ya kisaikolojia inayohusika na uelewa au matumizi ya lugha iliyoandikwa au kuzungumzwa ambayo inaweza kujidhihirisha katika hali ya kushindwa kusikiliza, kufikiri, kuongea, kusoma, kuandika, kutamka au kukokotoa hesabu. Pale matatizo haya yanapochunguzwa kwa karibu zaidi hupambanua vikundi vidogovidogo zaidi k.v. disleksia na kitatiza ukokotozi. speech and language disorders: kasoro za uongeaji: hali ya kukabiliwa na ugumu wa kuwasiliana ipasavyo. Kwa maneno mengine, dosari katika usemaji ni kilema au upungufu katika kutamka sauti, au/na umahirilugha na kasorolugha ambacho ni kilema cha uelewa au/na matumizi ya mifumo ya kuongea, kuandika na ishara nyinginezo. speech and language therapy: tiba lugha na matamshi: taaluma ya matunzo kiafya, yenye jukumu la kumwezesha mtoto, kijana au mtu mzima mwenye matatizo ya uongeaji, lugha na mawasiliano aweze kufikia kiwango cha juu cha kuwasiliana na kumudu kujitegemea katika nyanja zote za maisha. speech delay: kuchelewa kuongea: hali ya kukawia kuongea sawasawa kulingana na umri. speech detection threshold: ubainishaji mwanzo wa matamshi: 193 kiwango cha chini kabisa cha ufifiaji wa sauti ambacho msikilizaji anaweza kusikia maongezi kwa 50%. speech disorder or impairment: kilema matamshi: hali ya kutopangiliwa kwa maongezi. Kutoweza kutamka baadhi ya sauti, kukosea au kuharibika kwa utendaji au uamilifu hususani kwenye sauti, herufi, maneno, ishara ambavyo viko nje ya uwezo wa mhusika kuvitoa au kubaini kwamba havikukamilika k.m. ukokotezaji wa maneno, kutotamka sawasawa, kilema cha uongeaji. speech input or speech recognition: utambuzi wa matamshi: mbinu ya kudhibiti kompyuta na kuunda maandiko kwa imla. Maunzilaini ya maongezi huunganishwa na kipazasauti. Maunzilaini ya aina hii ndiyo humwezesha asiyeona na mwenye uoni hafifu, ulemavu wa kuzungumza, n.k. kumudu kutumia kompyuta bila kusaidiwa. speech recognition: programu za utambuzi sauti: maunzilaini yanayomruhusu mtu kuamrisha na kuchakata data kwa kutumia sauti yake badala ya puku au kicharazio. Mfumo huu hutumia kipaza sauti kilichoambatanishwa kwenye kompyuta. Kwa utratibu huu, kinachoweza kutumika kuunda maandiko na nyaraka kama vile barua au ujumbe wa baruapepe, kuramabaza intaneti, kuvinjari vitumi

212 na orodha la chaguo hufanyika kwa sauti (kutoa imla). speech therapist: tabibu matamshi: mtaalamu anayefanya kazi na kwa kushirikiana na wengine katika kuboresha na kurekebisha dosari za matamshi. speech or language therapy: tiba lugha: 1. programu ya uboreshaji na usahihishaji wa dosari za matamshi au lugha au mawasiliano aliyonayo mtu asiofikiriwa kuweza kufanya vizuri bila msaada wa aina hiyo. 2. marejeo ya utambuzi na afua za mapema; msaada wa mafunzo kwa mtoto, familia na wanajumuia wenye kuhusika na mazingira ya mtoto ili kukuza stadi zake za kuzungumza na kuwasiliana. speech: matamshi: utoaji wa sauti na maneno yenye maana inayotafsirika kwa namna ileile kwa mtamkaji na msikilizaji. speech-language pathologist: bingwa matamshi: mtaalamu aliyefuzu mafunzo ya mawasiliano ya binadamu, ukuzaji wake na kasoro zake kwa kuendesha upimaji, uaguzi na tiba kwa mtu mwenye kasoro za kimawasiliano. Bingwa huyu wa matamshi anaweza kujishughulisha na aina mballimbali za matatizo ikiwa ni pamoja na: makosa ya uzungumzaji, upungufu wa lugha, sauti, na mbinu za mawasiliano mbadala kwa mtu asiyeweza kutamka. 194 speechreading: usomaji matamshi: mchakato wa kuuelewa ujumbe wa sauti kwa njia ya kuangalia uso wa msemaji. Mbinu hii inaweza kutumiwa na mtu mwenye uoni mzuri; hata hivyo, ni asilimia ya lugha ya mazungumzo inayoweza kueleweka kwa kutumia mbinu hii peke yake. Halikadhalika, usomaji matamshi huhusisha matumizi ya vidokezo kama vile ishara, maelezo kwa wajihi, na dalili za hali au mazingira. spina bifida: ugweuti mchomozo: mgongo uliopasuka. Istilahi hii hujielekeza kwenye kundi la hitilafu za kuzaliwa ambazo huingilia ukuaji wa mfumo mkuu wa mishipa ya fahamu (yaani ubongo, ugweuti na tishu). Ni dosari inayotokana na matatizo ya awali kabisa ya ukuaji wa mtoto kabla ya kuzaliwa pale mifupa ya mgongo inapokosa kufunga kwenye mrija wa kati wa mishipa ya neva (uti wa ubongo). Hali hii husababisha kubakia kwa sehemu isiyokingwa ambayo huvimba na kuchomoza kama kifuko cheusi kikifunikwa na utando mwepesi sana unaopenyeza kiwoevu kutoka kwenye ukamba na katika ubongo. Aina tatu za hali hii (kutoka kwenye kiwango cha chini hadi kikubwa) ni: i) ugweutimchomozo okuta; ii) meningosili na iii) meningomiloseli. Aina hizi zinaweza kusababisha hali nyinginezo kama vile: kushindwa

213 kudhibiti msogeo wa misuli, kutodhibiti utokaji wa takamwili, au mbinuko wa uti. Kutambulisha hali hii kwa istilahi mgongo wazi** siyo sahihi kwani maana ashirifu yake inakanganya. spinal column: uti wa mgongo: pingili laini za mfupa ambao huhifadhi ugweuti zilizopo mgongoni mwa viumbe. spina-bifida-occuta: ugweutimchomozo okuta: mpasuko fiche wa mgongo unaotokana na kasoro ya mgongo na dosari nyinginezo zinazofunikwa na ngozi. Aina hii ni ya kawaida zaidi na haina athari kubwa. Agh. mpasuko kwenye mifupa ya uti wa mgongo huwa mdogo kiasi kwamba ugweuti hauchomozi, na hivyo ni uharibifu kidogo sana hutokea au kutotokea kabisa. Ngozi kwenye eneo la jeraha inaweza kuwa ya kawaida, sehemu hiyo huota nywele, kuwapo kwa mbonyeo au alama ya kuzaliwa kwenye ngozi. Watu wengine wenye ugweutimchomozo wanaweza kutokuwa na tatizo lolote, na huenda hata wasijue kuwepo kwa hali hii labda kama watachukuliwa eksirei ya mgongo. Hata hivyo, mara kadhaa tatizo hujitokeza na ushauri wa kitabibu huhitajika. spinal cord: ugweuti au utiubongo: neva kuu na sehemu ya mfumo mzima wa neva iliyomo ndani ya uti wa mgongo ambapo ndipo mishtuko kutoka kwenye neva za fahamu za maungo mbalimbali ya mwili na taarifa hupokelewa na kupelekwa kwenye ubongo. spinal cord injury: ugweuti ulioumia: kuharibika kwa kiasi kikubwa au kukatika kwa milango ya fahamu na neva tendaji (ukamba wa kati wa neva) shingoni au mgongoni kiasi kwamba misogeo na hisia hupotea kabisa. Uharibifu wa aina hii husababishwa na ajali za aina tofautitofauti. Sehemu iliyojeruhika ndiyo huamua ni kiasi gani cha athari na eneo la mwili litakaloathirika. Kuumia kwa uti wa ubongo sehemu ya shingo, husababisha kwadriplejia na ule wa mgongoni husababisha paraplejia. (Taz. cerebrum ). 195

214 mwenzake mwenye ulemavu ambaye bila kufanya hivyo, ingebidi mtu mwingine abebe jukumu hilo. staggering gait: mjongeo myumbo: namna ya kutembea kwa kuyumbayumba au kupepesuka (Taz. ataxia ). standard rule on the equalization of spinal muscularatrophy: kudhoofu opportunities for persons with kwa misuli ya ugweuti: ugonjwa wa disabilities: kanuni za viwango vya kurithi unaoathiri sehemu ya mfumo usawazishaji wa fursa kwa watu wa neva wenye kudhibiti misuli ya wenye ulemavu: waraka wa Umoja msogeo hiari. Seli nyingi za mishipa wa Mataifa wa Mwaka wa Kimataifa ya neva yenye kudhibiti msogeo wa Watu wenye Ulemavu (1981) hupatikana kwenye uti wa ubongo. ambao ni mwongozo kwa Hali hii ni ya kimisuli kwani kimsingi yaliyotakiwa kutendwa na nchi chenye kuathirika ni misuli ambayo wanachama wa Umoja huo ili hukosa kupokea ishara kutoka kuboresha maisha ya kundi hili. Hata kwenye seli hizi za neva. Atrofi ni hivyo, waraka huu haukuwa na dhana ya kitabibu kuhusu msinyao hadhi ya kushurutisha uzingatiwaji ambao kwa ujumla ndiyo hutokea wake ila kuweka viwango elekezi pale misuli isipojishughulisha. kwa nchi iliyoamua kufanya hivyo. Ugonjwa huu huhusisha upoteaji wa Upungufu huu ndio uliochochea seli za neva zinazojulikana kama madai ya Mkataba wa Kimataifa wa nyuroni za mota kwenye uti wa Haki za Watu wenye Ulemavu. ubongo na hubainishwa kama standardised achievement test (SAT): ugonjwa wa nyuroni za mota. kipimo cha matokeo yanayokubalika: splint: banzigango au kitata: wenzo kipimo kinachotumiwa ambacho uliotengenezwa kwa mifupa, mbao, huwekewa kanuni zenye kuelekeza bati au plastiki kwa minajili ya desturi ili kuhakikisha kwamba daima kukaza, kuunga au kunyoosha mchakato hautabadilika; hivyo, sehemu ya mifupa iliyovunjika au kumbukumbu zilizoingizwa na mtu iliyojeruhika. Unaweza kuwa wa yeyote kuweza kulinganishwa. kuondolewa au kufungiwa daima state party to a convention: nchi (taz. back slab ). mwanachama iliyoridhia mkataba wa spouse advocate: mtetezi mume au kimataifa: maafikiano rasmi kati ya mke: mtu mwenye kukidhi mahitaji nchi mbili au zaidi ambayo ya utetezi wa mwanandoa utekelezaji wake hufuata utaratibu 196

215 maalumu. Mathalani, mikataba ya Umoja wa Mataifa na ile ya Kikanda, hufuata utaratibu wa: (i) kupitishwa na mamlaka ya juu k.v. Baraza Kuu; (ii) kutiwa saini na nchi wanachama walau kwa idadi ya chini kabisa iliyotamkwa na kifungu cha mkataba wenyewe ili kuruhusu mchakato wa uridhiaji kuanza; (iii) kuridhiwa na kila nchi iliyoutia saini; ili kupata idadi ya chini ya waridhiaji iliyotamkwa kwenye kifungu cha mkataba wenyewe, na hivyo kutangazwa kuanza kutumika rasmi. Nchi nyingine husika huendelea kuridhia taratibu. static: tuamo: -lio tulia tuli bila ya kusogea. statistical relativity: uwiano wa takwimu: njia ya kubainisha ufafanuzi wa tofauti za kimkengeuko kwa misingi ya mfululizo wa mwenendo au tabia. Wastani wa mifululizo hukokotolewa na hali ya mtu hulinganishwa na wastani huo. stature: kimo: umbali kutoka utosini hadi chini wayoni wakati mtu amesimama. status: hadhi/uluwa: taadhima au cheo alichonacho mtu. status offense: utukutu: mwenendo wa mtoto usiokuwa wa kijinai kama vile utoro, ukwepaji kazi, na kuvunja amri ya kutotoka nje ambako kunaweza kusababisha kuchukuliwa kwa hatua na mahakama ya watoto. stereotypes: mapokeo kaririwa: hali ya kugubikwa na mawazo ya 197 kimapokeo ambayo huwa hasi, ya kijumlajumla na kwa kiwango fulani yenye taswira za kudumu za mtu au watu katika kundi fulani maalumu. Taswira hii hujengeka kwa kutenganisha au kupamba baadhi ya sifa za kimaumbile, kiakili, kiutamaduni, kiajira, binafsi, n.k. zinazoonekana kulipambanua kundi. Hali hii huelekea kupuuzia upekee wa nafsi ya mtu kama vile kusawirisha mtu mwenye ulemavu kama tegemezi, mwenye mikasa, mlaaniwa, asiyeweza, asiye na ajira, ombaomba, asiyekuwa na siha, aliyekosa msaada, asiyekuwa na akili, kiumbe mwenye kuteseka, mwenye kuhitaji huruma, hisani na uangalizi wa watu wasiokuwa na ulemavu, asiyeweza kuwa na familia kwa vile hawezi kuwa mzazi bora; ni mkali kutokana na mustakabali wake; huuchukia ulimwengu wa wasio na ulemavu; inabidi kuwasiliana naye kwa namna ya pekee kwa kutumia viashiria kwa vile ni mpumbavu**; anahitaji programu maalumu za elimu kwa ajili yake tu, au kuwa mzigo kwa jamii. Mtu yeyote kwenye kundi hili anayeoneka tofauti, huchukuliwa kama shujaa asiyemithilika, n.k. sterilization: utasishaji: 1. mchakato wa kuangamiza vijidudu vya magonjwa katika vifaa vinavyotumika kwenye tiba. 2. mchakato wa kufanya kiumbe asiwe na uwezo wa kuzaa ikiwa ni

216 pamoja na kuhasi au kufunga kizazi kwa njia nyingine. stigma: unyanyapaa: ubaguzi anaofanyiwa mtu kutokana na hali aliyonayo. stigmatize: nyanyapaa: bagua mtu kutokana na hali aliyo nayo. stillbirth: uvoromoko: hali ya kujifungua mtoto asiye na uhai. stillborn: kivoromoko: mtoto asiye na uhai wakati wa kuzaliwa. stimulation: uchangamshaji: uchocheaji wa kasi katika utendaji. stimuli: kiamshi: kitu au mchangamano unaotumika kuhamasisha au kuchochea ustawi au ukuaji. Kiamshi Kinaweza kuwa cha kusikia, mwendo, mguso, kuona, n.k. stimulant: kichangamsho: kichocheo au kiburudisho, fahamu, mzinduo, kishawishi chenye kusababisha mwitikio (hasa kwa seli za neva k.m. mwanga, joto, umeme, baridi kali). strabismus: makengeza: 1. hali ambayo mboni za macho huelekea ndani (taz. esotropia) au huelekea nje (eksitropia) ambapo panakuwepo na kuhitilafiana kwa mchepuko kati ya macho mawili 198 kiasi kwamba uoni wa karibu na wa mbali au ustigimati hutokea. Visababishi visivyo vya kawaida vya hali hii hujumuisha: tosisi (kunyong onyea) kwa mboni ya jicho moja, maradhi ya konea (ambayo husababisha mwanga kupenya na kuingia kwenye jicho), hitilafu ya mtoto wa jicho tangu kuzaliwa, kuumia jicho utotoni. 2. hitilafu ya kuona kutokana na mihimili ya kuona ya macho kutokutana katika kitu kinachoonwa kwa vile misuli ya nje ya macho kutosogea kwa pamoja. cviii ( taz. ambliopia) strengths: umadhubuti: 1. rasilimali ya kipekee ya ndani (vitu) ya familia ambayo hujumuisha uwezo wa kumudu, motisha na hiari ya kusaidia kwenye ustawi; mathalani, ukaidi, werevu, ushupavu; stadi bora za ujongeaji na mwendo, ukamilikaji wa ufahamu, n.k. 2. nguvu ya kisheria, mantiki au uadilifu. stress: msongo: 1. hali inayotokana na jinsi mtu anavyochukulia matukio au shughuli zenye kumletea fadhaa, mkandamizo, mahangaiko au wasiwasi mwilini na akilini mwake. 2. hali za ndani au nje ambazo huingiliana na mihemko au utambuzi na uamilifu wa mtu kijumuia. 3. fadhaa inayotokana na shida, taabu, dhiki, matatizo, msongo (wa mambo), shinikizo, n.k. Dalili za mfadhaiko ni pamoja na

217 zile za kiakili, kijamii, kimwili ambazo hujumuisha kuchoka sana (mavune), kuwa au kutokuwa na hamu ya chakula, maumivu ya kichwa, kulia, kukosa usingizi au kusinzia kupita kiasi, matumizi ya vileo au tabia za ushurutishaji. Hisia za hofu, kukata tamaa au ugoigoi zinaweza kuambatana na mfadhaiko. stuttering: ugugumizaji: hali ya kukwamakwama kwa maneno au/na mwingiliano wa mfuatano wa uongeaji wenye kubainishwa na kusitasita, kurudiarudia au kurefusha neno, silabi au kirai mfano: aaaanaakwenda; sssisisitaki, n.k. Kigugumizi hutambulika kama mojawapo ya mivurugiko ya lugha. stylus: kitobozi: kifaa kama sindano kinachotumiwa na asiyeona kuandikia kwa kutumia kibao (sleiti) na karatasi maalumu. stroke: kiharusi: 1. maradhi ya kupotea kwa ghafla kwa fahamu, hisia, au uwezo wa kujongea kutokana na kuvuja au kuganda kwa damu kwenye ubongo. 2. shambulio la ghafla la kupooza kutokana na kuvuja damu au kuziba kwa mshipa wa damu katika ubongo. structural abnormalities: uatilifu maumbile: hali ya kuwepo kwa kasoro kwenye mpangilio wa ulaji kutokana na mataya kupishana, kakaa wazi, au kuvimba kwa ufizi. stump: kigutu: sehemu ya kitu kizima inayobaki baada ya kukatwa; kibubutu. subcutaneous injection: sindano ya sabukuteni: sindano inayodungwa kwenye tishu yenye mafuta mengi iliyo chini ya ngozi na siyo kwenye misuli. subcutaneous: -a sabukuteni: -a chini ya ngozi. substance abuse: matumizi mabaya ya dutu: matumizi ya kupita kiasi ya kitu chenye uraibu k.v. mihadarati, tumbaku, vileo, n.k. kinachohatarisha maisha na afya ya mtumiaji. substitute: kibadala: kitu kinachoweza kuwa tofauti lakini kikajaza nafasi na kwa kiwango fulani kikakidhi haja ileile ambayo kitu cha kawaida kingeikidhi. 199

218 successor trustee: mdhamini wa mrithi: mtu anayebeba jukumu la kusimamia amana baada ya kifo au kukosa uwezo wa kisheria wa mwasisi. sufferer: -enye kuteseka:** mtu mwenye ulemavu ambaye kwa mtazamo wa baadhi ya wanajamii humchukulia kuwa mwenye mateso. Hata hivyo, utafiti unaonyesha kwamba mateso na masumbuko ya mtu mwenye hali hii havitokani hasa na maumbile yake bali mitazamo, desturi, mila tamaduni na mifumo isiyozingatia usawa na hasa kwenye mgao wa rasilimali. Katika nchi zinazozingatia hili, kundi hili hufurahia maisha sawa na watu wasiokuwa na ulemavu. sun screen lotion: mafuta kinga: aina ya mafuta ambayo hutumiwa zaidi katika kujikinga na miale ya jua ambayo husababisha saratani ya ngozi kwa mtu mwenye ualbino pale anapojianika juani kwa muda. sun glasses: miwani jua: miwani inayovaliwa na mtu kwa ajili ya kuzuia miale ya jua. Miwani hii ni muhimu kwa mtu mwenye ualbino kutokana na macho yake kuathiriwa na mwanga. superego: dhamiri: msukumo wa ndani ya nafsi inayomwambia mtu kuwa jambo analolifanya ni zuri au baya. superiority complex: hisia za kujikweza: hali ya mtu kuwa na silika ya kujiona bora zaidi kiasi cha kuwadharau wengine. 200 supination: supinesheni: ugeuzaji wa kiganja na mkono kuelekea juu. support services: huduma za msaada/mwega: afua za pekee za kuchangia katika kuboresha au kurahisisha ushiriki wa mtu mwenye ulemavu katika shughuli mbalimbali k.m. programu za mafunzo ya ufundi stadi na elimu, huduma za utengemalishaji, mafunzo kazini kwa ajili ya walimu, kuhimiza na kuondosha unyanyasaji wa kijinsia kwenye mafunzo ya elimu na ufundi stadi. usafiri, msaada wa kifedha, vikundi vya kusaidia, huduma za uangalizi wa nyumba, upumzishaji, n.k. supported employment (SE): ajira mwega: mafunzo ya ufundi stadi na msaada endelevu kwa mtu agh. mwenye ulemavu aliyeajiriwa kwenye eneo au fani mchanganyiko ndani ya jamii. Ajira hii inaweza kutolewa kwa mtu ambaye hajawahi kuajiriwa kwenye mfumo mchanganyiko, au ambaye ajira yenye ushindani imekatishwa au ni ya vipindivipindi kutokana na ulemavu wa ukuaji na ambaye ulemavu wake huhitaji

219 huduma mwega kutolewa kwenye ajira kama hiyo. supportive educational environment: mazingira wezeshi ya elimu: mfumo ambamo hali ya usikivu, mwanga na mitindo ya ufundishaji ni rekebifu ili kukidhi mahitaji ya mwanafunzi mmojammoja kulingana na mahitaji yake. Mifano ya mazingira wezeshi kwa mwanafunzi mwenye kilema cha usikivu inaweza kuwa: chumba na ushoroba zenye mazuria, madirisha wenye mapazia, dari zenye vigae sikizi, na viwango vidogo vya kelele. Matumizi ya vielelezo saidizi onyeshi, idadi ndogo ya wanafunzi, kuwa kielelezo kizuri cha lugha kwa mwanafunzi, kuhakikisha kuwa vifaa vya kusikilizia viko katika hali nzuri na vinatumika. support: kiegemezi: wenzo, kifaa k.v. kivutio, kibanio, kinachoingiza au kufungiwa wenzo kwenye kiti au kifaa cha kutembelea ili kuziweka sehemu maalumu za mwili kwenye mkao unaotakiwa. survivor: mnusurika: mtu aliyesalimika kwenye maafa au ajali kwa kupoteza 201 au kudhoofu kwa kiungo chake au kuathirika kwa namna nyingineyo, mathalani kisaikolojia. Kwa mtu aliyepata kilema cha nasibu, hii ni hatua ya kati na hali yenye kutumainisha baada ya kushinda fadhaa, kunusurika lakini kupoteza kiungo cha mwili au uamilifu wake. Baadaye, mwathirika huikubali hali yake mpya na kuanza kujijenga tena ndani ya jamii. susceptibility: urahisi wa kuathirika: hali ya kitu au dutu kudhurika kwa wepesi. susceptibility to violence: rahisi kuonewa: mtu ambaye ni mwepesi wa kuathiriwa na kuonewa. symbol for accessibility: ishara ufikivu: alama ya kitimwendo hutumika pale inapotakiwa kuonyesha ufikivu kwa mtu mwenye ukomo wa ujongeaji kiasi cha kulazimika kutumia kitimwendo. Mathalani, alama ya kitimwendo inatumika kuashiria milango inayofikika, maliwato au simu inayofikiwa kwenye kimo cha mtumiaji wa wenzo huu kwa ujongeaji. Kumbuka kuwa milango yenye ngazimbetuko haipitiki kikamilifu endapo hakuna viondoa vizuizi vingine kama vile upana wa milango yenyewe. Kwa ujumla, anayetumia kitimwendo, njia mbadala kwake ni ya mwinuko hafifu. Taz. ramp.

220 symbol: alama: ishara ambazo hutumika kuonyesha kitu, hali au dhana fulani. Taz. disability access symbols. symptom severity: dalili mbaya: kigezo cha kubainishia kinachojielekeza kwenye kiasi cha ukengeufu dhidi ya desturi. symptom: dalili: 1. kielelezo cha hali ya mabadiliko mwilini. 2. matakwa ya nafsi. syndrome: mlimbikodalili: 202

221 Tt tactile defensiveness: kingampapaso: hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha hisia kiasi cha kutoweza kuvumilia kuguswa au kugusa vitu laini inayosababishwa na neva za fahamu. tactile graphics: mchoro mpapaso: picha, michoro, ramani, maandishi, michoro nakshi, n.k. ambavyo ni taswira zenye kutumia dutu zilizotunishwa ili mwenye upofu aweze kuzihisi kwa kupapasa na hivyo kuwasilishiwa ujumbe. Sanaa mguso zinaweza kuwa sehemu ya taswira yenye kufikika kwa kutumia njia tofautitofauti kama vile maelezo kwa maneno, sauti au mwitiko wa mpapaso. Mojawapo ya matumizi makuu ya michoro mpapaso ni kwenye maandalizi ya ramani kwa ajili ya wenye upofu.. tactile paving: utandazaji vibamba mpapaso: mfumo wa muundo wa viashiria vilivyofumiwa juu ya ardhi kwenye njia za watembea kwa miguu, ngazi, majukwaa ya kupandia garimoshi na vituoni ambayo humsaidia mwenda kwa miguu aliye na hitilafu za uoni. Vionyi mpapaso huwa na mfumo bayana wa vidutu vilivyokatwa ncha ambavyo ni vyepesi kugundulika kwa fimbo maalumu au wayo. Vidutu hivi pia hupakwa rangi ya chungwa ili 203 kurahisisha kuonekana hata kwa aliye na uoni hafifu ili kumtahadharisha kuwa anakaribia kuingia barabarani, kingo hatari za barabara k.v. kubadilika kwa usawa wa njia). tactile: -a kupapasika, -enye kuhusiana na hisia za kugusa. tactile: -a kupapasika, -enye kuhusiana na hisia za kugusa. tactile perception: utambuzimpapaso: uwezo wa kutafsiri na kufahamu maana za vichocheo vya kihisia vinavyotokea kwa njia ya mpapaso. tactile system: mfumo mpapaso: utaratibu wa kutafsiri mguso mwepesi, mkandamizo, halijoto, maumivu, mtetemo na kichocheo cha nchambili kupitia ngozi au vipokezi vya mgusano. tactile: -a kupapasika, -enye kuhusiana na hisia za kugusa. tactual sign: ishara mpapaso: aina ya lugha ishara ambayo ishara hufanywa wakati watu wakitazamana uso kwa uso na kushikana mikono ili kuhisi misogeo.

222 tadoma: tadoma: mbinu ya usomaji matamshi kwa kugusa ambapo msikilizaji huweka kidole gumba kwenye mdomo na koo la muongeaji. talipes equininovarus: talipesi: taz. club foot. talking-large-print-word: vichakata maongezi na maandishi makubwa: pogramu za maunzilaini ambazo hutumika kusanisi matamshi ili kutoa mwitiko wa sauti wa kile kinachochapwa. Kichakata maandishi makubwa humwezesha mtumiaji kuona kila kitu kwenye maandishi bila kuongeza upana wa skrini. tantrums (fits of crying, screeming and angry or destructive behaviours): hamaki: 1. athari ya kisaikolojia yenye kusababisha gadhabu, kulia kwa nguvu, kulalamika au kuwa na mienendo ya kiuharibifu. 2. mtoto kurusha mateke, kujaribu kuvunjavunja na kutupatupa vitu, kuuma, kuharibu kila kitu au mtu yeyote anayemkaribia na hata yeye mwenyewe. tease tania: dhihaki mtu hasa kwa dhamira ya kumchokoza, kumsumbua, kumdadisi au, kumsunza. telecommunication device for the deaf (TDD): kitumi cha mawasiliano kwa viziwi: kifaa cha kielektroni cha kicharazio ambacho hutuma, kupokea na kuchapa ujumbe kwenye njia za simu ili kuwawezesha 204 viziwi kuwasiliana kwa njia ya simu. Namba ya simu yenye kufuatiwa na kitumi hiki humaanisha kuwa wakala au kampuni ya simu (au mtu mwingine ambaye ni kiziwi) anacho kifaa cha kuwasiliana kielektroni na viziwi wenzake. telecommunications device for the deaf (TDD): modemu hawilishi: vitumi vinavyounganishwa kati ya kompyuta na simu ili kumwezasha mtu kuchapa ujumbe kwenye kompyuta na kuutuma kwenye simu chapa. Hata hivyo, ujio wa intaneti, facebook, simu za mkononi umechuka nafasi ya teknolijia hii ya awali. telephone amplifier: kipazasauti cha simu: kifaa kilichoambatishwa kwenye simu na ambacho hukuza sauti ili isikike vizuri zaidi. telephone loud ringer: kiongeza mlio wa simu: kifaa chenye kuongeza ukubwa wa sauti na kubadili mlio ili uweze kusikika vizuri zaidi. telephone ring signaler: kiashiria mlio wa simu: kifaa kinachodokeza kwa kumulika pale simu inapoita.

223 telephone typewriter (TTY): simu chapa (SC): mashine hii pia hujulikana kama simu yenye maandiko (SM) au kifaa cha mawasiliano kwa viziwi (KMV). SC hubainisha kifaa kinachotumiwa kimawasiliano na/kati ya viziwi, wenye usikivu hafifu, wenye ulemavu wa kimatamshi au/na watu wenye usikivu. Teknolojia za aina hii zilikuwa maarufu kabla ya kuzinduliwa kwa simu za kiganjani. tellatouch: chapampapaso: mashine ndogo ya kuandikia inayomwezesha mtu kuchapa ujumbe ulioandikwa kwa nuktanundu. Aina hii ya kifaa hurahisisha mawasiliano kati ya mwenye uziwipofu na mtu mwingine asiyekuwa na tatizo hili. Zipo aina nyingi za vifaa kama hivi vyenye kutumia mifumo ya kielektroni. tetanus: pepopunda: ugonjwa unaotokana na sumu kali ya bakteria klostridiumu tetani ambayo husababisha mikazo ya misuli. Pepopunda inaweza kusababisha ulemavu kwa mifupa kuvunjika kutokana na mkakamao, kutojongea kwa muda mrefu, matumizi ya dawa kali za usingizi na uharibifu wa ubongo. tetraplegia: tetraplajia: kupooza kwa limbu zote nne (ang. quadriplegia ). text-to-speech (TTS) or speech synthesizers: visanishi matamshi: vifaa vinavyopokea taarifa zinazotokea kwenye skrini katika umbo la herufi, tarakimu na alama za vituo na kisha kutamka kwa sauti kwenye kompyuta. Kwa kutumia visanishaji huwawezesha mtumiaji wa kompyuta asiyeona au mwenye uzito wa ujifunzaji kusikia kile anachokichapa. Halikadhalika, hutoa matamshi kwa yule asioweza kuwasiliana kimatamshi, lakini anaweza kuwasilisha mawazo yake kupitia machapisho au matini. the disabled people s movement: tapo la watu wenye ulemavu: jitihada za pamoja za vuguvugu na harakati zinazolenga kushawishi mabadiliko kwenye medani za kisiasa na kijamii kwa kuhimiza au kupinga utekelezaji wa masuala fulani ili kulinda au kuboresha mustakabali wa kundi. Katika hali ya vuguvugu dhamira hufanana na kila mwanatapo hujitoa mhanga katika kutekeleza yaliyokubaliwa kwa kadiri 205

224 anavyoweza. Tapo hujengwa na mtandao mpana, kama misingi au shina kwa vyama au wakereketwa binafsi. theatre: thieta: 1. jumba au uwanja wa maonyesho au tamthilia. 2. eneo la tukio maalumu. Kwa kuzingatia suala la ufikivu, eneo hili ni muhimu katika kuwezesha au kukwaza mchangamano baina ya mtu mwenye ulemavu na jumuia yake. 3. ukumbi wa mhadhara. 4. chumba cha upasuaji agh. hospitalini. 5. sanaa ya maonyesho.. therapist: tabibu: 1. mtu mwenye stadi mahususi inayopatikana kwa njia ya mafunzo na tajiriba katika fani moja au zaidi ya mafunzo ya afya. 2. mjuzi wa tiba. therapy: tiba: mbinu ya kisanaa au kisayansi inayotumika kutibu hisia au ugonjwa kwa kutumia dawa, miale, upasuaji, mazoezi au unasihi. thermoform: uundaji joto: mchakato wa uzalishaji ambapo karatasi za plastiki hupashwa joto la kiasi kinachohitajika na kisha kutengenezwa umbo linalotakiwa kwa kumiminwa ndani ya au kuzungushwa kwenye kalibu na kutengenezwa ili kuumba kitu kinachoweza kutumika. Mtindo huu hutumika kuzalisha michoro, ramani, n.k. kwa ajili ya asiyeona na mwenye uziwipofu (taz. tactle graphics ). thoraco-lumbar corset: banio rekebishi kifua na kiuno: kifaa kilichotengenezwa ili kutoa msukumo 206 ndani ya tumbo kwa njia ya nguvuhai. Husaidia kuimarisha kiwiliwili na kuenea hadi kwenye maeneo ya kifua na uti. Agh., mikanda ya mabegani hujumuishwa ili kusaidia mwili usiegemee mbele. threshold of discomfort: kilele cha kero: kiwango cha juu cha kelele kereheshi. Kimachini cha kiwango cha kelele agh. cha maongezi ambacho msikilizaji hukichukulia kuwa cha kukerehesha. thrombolitic therapy: tiba thromboli: matibabu yanayohusiana na ugandaji damu ndani ya mishipa. thrombosis: thrombosisi: kuganda kwa damu katika ateri za damu. tinnitus: tinitasi: 1. hali ya makelele kwenye masikio au/na kichwani yasiyo na chanzo cha nje k.v. miluzi, mivumo. 2. sauti ya mvumo masikioni. cix tip-toe: chuchumia: hali ya mtu kutembelea ncha za vidole kutokana na msinyao wa mishipa.

225 tissue: tishu: 1. malighafi za kutengeneza misuli ya ogani za mwili. 2. mkusanyiko wa seli zinazofanana na ambazo hutekeleza jukumu fulani mwilini. cx tone control: udhibiti toni: hali inayoruhusu urekebishaji wa wimbisauti ya mwitikio wa shimesikio kuwa chini au juu. Bingwa wa usikivu hutoa vidhibiti hivi kwa mteja mwenye kiwango mahususi cha upotevu wa usikivu. tone deafness: uziwi toni: hali ya kutoweza kupambanua kati ya sauti mbili zenye mawimbisauti tofauti katika mfiko wa usikivu ulio sawa. Pale ambapo hakuna ukosefu dhahiri wa uelekeo wa mawimbisauti huwa katika hali ya kutoweza kupambanua iwapo mtu anaimba ndani au nje ya mlinganisho wa sauti. tone: toni: 1. kiwango cha mkazo wa misuli. 2. sauti fulani dhahiri k.v. hasira. 3. mkazo wa kawaida wa misuli katika sehemu fulani ya mwili au mwili mzima. torso: kiwiliwili: pingiti au mwili bila ya kichwa wala miguu na mikono. torture: tesa vibaya: sababishia mtu maumivu, msononeko, ili kumfanya apate machungu kiakili au kimwili kwa kumlazimisha kufanya jambo au kutoa taarifa. totally blind: upofu kamili: hali ya kukosa kabisa uwezo wa kuona. Dhana hii hutumika kwenye muktadha wa kielimu kumwelezea mwanafunzi mwenye kilema kikubwa cha upofu ambapo hujifunza kwa kutumia nuktanundu au njia nyingine zisizotumia uoni. touch screens: skrini mpapaso: kioo cha skrini ambacho kikiguswa huruhusu michakato ya kompyuta kuendelea na hurahisisha utendaji wa moja kwa moja kuliko kutumia puku au kicharazio. Skrini za aina hii hurahisisha matumizi kwa mtu mwenye ulemavu wa mjongeo. Skrini mpapaso ama hutengenezewa ndani ya monita ya kompyuta au inaweza kuongezwa kwenye monita hiyo. Simu smati za kiganjani ni mfano mzuri wa teknolojia hii. touch tours and other tactile experiences: mpapaso ufahamu: njia kuu ya kupata taarifa au kufurahia sanaa kwa kugusa. Kwa mtu asiyeona, kupapasa hukamilisha taswira yake akilini kuhusu kitu kilivyo. Zaidi ya kupapasa kazi asilia za sanaa, uzoefu wa mpapaso hujumuisha: vibadala, vifani, nguzo, ushikiliaji wa vitu vinavyotoa ujumbe juu ya shughuli na kazi nyinginezo. Mathalani, mtu asiyeona akitaka kuchagua gari la kununua, atatembelea uga wa kuuzia magari na kupapasa aina za magari 207

226 zilizopo ili pamoja na maelezo ya ziada aamue ni lipi analolipendelea. touchpad or trackpad: pedilengeshi mpapaso: kifaa cha kuonyeshea mithili ya hisishi mpapaso ambacho hutumika kama kibadala cha puku ili kumwezesha mtu mwenye aina fulani ya ulemavu kutumia kompyuta kwa urahisi sana (taz. trackball ). toxemia: toksimia: 1. hali ya hatari wakati wa ujauzito inayoweza kusababisha mitukutiko. 2. uwepo wa sumu ya vimelea katika damu. cxi trachea: umio pumzi : 1. uwazi unaoelekea kutoka nyuma ya koo hadi kwenye mapafu ambao husafirisha hewa nje na ndani ya mwili wa mnyama. 2. neli kubwa ya gegedu na membreni ambayo huanzia chini ya larinksi na kuishia katika bronkasi. tracheostoma: trakeostoma: tundu lililotobolewa katika shingo hadi kwenye koo. tracheostomy: trakeostomi: 1. hali ya kutoboa tundu kwenye koromeo au kupitia shingo hadi koromeo ili kusaidia upumuaji pale ambapo njia za kawaida kupitia puani na kinywani zinapoziba kutokana na maumbile au maambukizo. Kwa vile hii huwa hali ya kudumu, hugeuka kuwa aina ya kilema. Bila msaada wa mashine, mhusika huwa hatarini kupoteza maisha kwa kukosa hewa ya oksijeni. 2. Upasuaji wa mlango wa uzazi. 208 trachoma: vikope: 1. ugonjwa unaotokana na maambukizo ya bakteria aina ya klamidia wanaoweza kusababisha upofu kutokana na maambukizo yanayojirudiarudia. Trakoma husambazwa kwa kushirikiana nguo, kugusana na kupitia nzi baada ya kugusana na macho au pua za mtu mwenye maambukizo. 2. ugonjwa wa vikawa vya macho ambao hupeleka makovu kwenye konjaktiva, ukungu wa konea na hatimaye upofu. cxii trackball: kitufe oneshi: kitumi chenye umbo la duara kinachot umiwa kuendes ha kasa kwenye skrini. Kwa mtu mwenye ulemavu wa mjongeo,

227 kitumi hiki humfaa sana kwa kumrahisishia matumizi ya kompyuta bila kulazimika kubofya kicharazio. tragic: -a kusikitisha: -enye hali ya kusikitisha inayomtokea mtu pale anapopata kilema cha nasibu kutokana na ajali au maradhi. Mwanzoni hali yenyewe huchukuliwa kama maafa bila kuona faraja yoyote siku zijazo. trainable: -enye kufundishika: -enye kiwango cha udumavu wa akili kulingana na matarajio ya ufundishikaji, ambacho huhusisha upimwaji wa akili wa ya ujifunzaji hasa katika maeneo ya stadi za kujimudu, ufanisi kwenye baadhi ya taaluma kulingana na jamii. Upimaji huu agh. hukomea maeneo ya nyumbani na ya karibu sana; kazi za kijamii au shughuli za uzalishaji zilizohifadhiwa kwa ajili ya mtu mwenye ulemavu. transcribe: nukuu: andika kila neno analotamka mtu mwingine. Utaratibu huu agh. hutumika kwenye muktadha wa kisheria ama mahakamani au wakati wa kuchukua maelezo sehemu nyingine kwa ajili ya kumbukumbu, Bungeni (uandaaji wa Hansard) na huduma saidizi kwa mtu asiyeona hasa mwanafunzi au mtumishi. transcriber: mnukuzi: mtu anayefanya kazi ya kunukuu. transdisciplinary: -a michepuo mbalimbali: -enye taaluma nyingi zinazofanya kazi pamoja wakati 209 wa upimaji wa awali wa mwanafunzi. transference: ambukizo: hali ambayo bila kudhamiriwa mtu huambukizwa hisia na mitazamo ambayo kabla ya hapo vilihusishwa na mtu muhimu kwa mhusika. Uhusiano na uambukizo hufuata mtido wa sampulikifani. Msakaitria hutumia shani hii kama zana ya kutibia kwa kumsaidia mgonjwa kuelewa matatizo ya kihisia na chanzo chake. Katika uhusiano wa mgonjwa na tabibu wake, uambukizo unaweza kuwa hasi au chanya. transferred competence: hawilisho la kisheria: hatua ambayo huchukuliwa na mahakama ya kutoa mamlaka kwenye muktadha mmoja kwenda muktadha mwingine. transgender: jinsifiche: 1. bainisho la mtu ambaye utambulisho wa jinsia haufanani na ule wa jinsi yake wakati wa kuzaliwa. 2. dhana inayojielekeza kwa mtu ambaye jinsi na jinsia yake daima au mara nyingi haviendani. Dhana hii ina maana pana yenye kujumuisha mabadiliko kabla au baada ya kufanyiwa upasuaji, bila kuwa na jinsia, kuwa na jinsi zaidi ya moja na utoaji wa homoni za kiume. Masuala ya ubasha, ushoga na usenge ni sehemu ya dhana hii. 3. dhana inayomuelezea mtu

228 ambaye utambulisho wake kijinsia au/na maelezo ya ujinsia hutofautiana na jinsi aliyonayo tangu kuzaliwa. transition plan: mpango mpito: programu iliyosanifiwa kutoa muhtasari wa hatua za mpito kwa mtu kutoka shule na kuingia kwenye utu uzima, kwa kutambua huduma maalumu zinazotakiwa kwake, shughuli zinazotakiwa kufanyika kipindi akiwa shuleni, ratiba na majukumu katika ukamilishaji wa shughuli hizo. transition services: huduma mpito: kivunge cha shughuli kwa ajili ya mwanafunzi zilizosanifiwa kwenye mchakato wa matokeo ambayo huchochea maendeleo kutoka shuleni kwenda kwenye ajira mchanganyiko ikiwa ni pamoja na ajira zenye misaada, elimu ya astashahada, mafunzo ya ufundi stadi, kuendelea na elimu ya watu wazima, huduma za watu wazima, kuishi kwa kujitegemea, na kushiriki kwenye jamii. Shughuli hizi (a) zitajikita kwenye mahitaji binafsi ya mwanafunzi, b) zitatilia maanani upendeleo na matakwa ya mwanafunzi, na c) zitajumuisha lakini siyo kuishia kwenye mafunzo ya desturi za jamii, kuandaa malengo ya ajira na yale ya baada ya maisha ya utu uzima baada ya masomo, na pale zitakaposadifu, kujipatia stadi za maisha ya kila siku na uamilifu wa tathmini ya stadi na huduma. transition: mpito: mchakato wa kuvusha muda na mazingira katikati ya mifumo miwili, programu au taasisi za kimaisha (mfano, kutoka nyumbani hadi shuleni, shule hadi shule, shule au nyumbani hadi kwenye ajira au maisha ya kujitegemea). trauma: kiwewe: 1. mshtuko au kuumia ghafla. 2. kisababishi cha mvurugiko wa sauti ambapo gegedu zoroto hukatika au huanikwa na jeraha hali inayoweza kuhitaji kurekebishwa kwa njia ya upasuaji. Japo kipaumbele kinaweza kuwa kutibu njia ya hewa, sauti nayo itahitaji kuangaliwa, kwa hiyo utabibu utatakiwa. Sauti itakayotoka kwenye zoroto iliyofanyiwa matibabu, kwa vyovyote itakuwa ya chini ikiwa na mpumuo wenye mvumo. treatment modality: mfumo wa tiba: mbinu inayotumika kumtibu mtoto, k.v. k.m. kurekebisha mwenendo na tiba mchezo ni baadhi ya tiba kwenye mfumo huu. Mtindo huu wa tiba ni wa mtu mmojamoja na haupo ule wa jumla uliosadifu kwa wote. treatment: tiba: afua iliyosanifiwa ili kubadili mienendo au hali nyinginezo zinazohusiana na hitilafu za mtoto kihisia au/na kumsaidia yeye na familia yake kukabiliana na kilema. 210

229 tremor: mtetemo: hali ya kujongea au kutetemeka kusiko kwa hiari; msogeo ambao hutokea kwenye miguu au mikono kila mara, bila hiari wala kudhibitika. tri-cycle: baiskeli gurudumu tatu: aina ya baiskeli inayoendeshwa kwa nguvu za misuli au umeme ambayo hurahisha ujongeaji kwa mtu mwenye kilema cha ujongevu. triplegia: triplejia: kupooza kunakohusisha miguu yote miwili na mkono mmoja. trust corpus: mfuko wa amana: dhana inayojumuisha mali zote zilizohamishiwa kwenye udhamini. Mathalani, iwapo mfuko umeanzishwa kwa kiasi cha shilingi 250,000.00, kiasi hicho ndicho mfuko kwa maana ya mali zilizo kwenye amana. trust: amana: 1. amana inayoweza kuanzishwa kwa ajili ya kumfadhili mtu au kundi fulani au kwa madhumuni ya kutoa hisani, n.k. 2. asasi ya kisheria iliyoasisiwa ama kwa maafikiano ya kimaandishi yaliyosainiwa wakati wa maisha ya mfadhili au kwa wasia. Amana husimamiwa na hadidu zilizoandikwa kwenye waraka. 3. mtu au asasi iliyoandaliwa kudhibiti au kuendesha milki za upande mwingine kama inavyoelekezwa na amana. Dhima yake ni kuhakikisha kuwa mfuko unawekezwa vizuri na kutumika kama ilivyoelekezwa na mwasisi pamoja na sheria za nchi. Mfadhili na mdhamini mwasisi anaweza kuwa mtu yuleyule. trustee: mdhamini au mkabidhi: mtu yeyote anayehifadhi mali, mamlaka au nafasi ya amana au wajibu kwa manufaa ya mtu mwingine; mathalani, i) kutekeleza majukumu kadha wa kadha yanayohusu amana bila yeye kuwa mfadhiliwa; ii) kuhifadhi mali kwa niaba ya mfadhiliwa; iii) kuhudumu kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa mfuko k.v. kwenye bodi ya wadhamini ya taasisi inayojishughulisha na masuala yanayonufaisha jamii. trusteeship: udhamini: kubeba jukumu la kutunza amana. trustor: mfadhili: mtu aliyeasisi amana. tumor: tyuma: 1. uvimbe wowote ule. cxiii 2. saratani; yaani mkusanyiko wa seli ambazo hazina faida yoyote ile mwilini na ambazo 211

230 huweza kuingilia utendaji kazi wa mwili. twin track approach: mkabala wa mikondo pacha: dhana yenye kusisitiza ukweli kuwa ulemavu ni suala mtambuko, ila mtu mwenye ulemavu ana mahitaji mahususi yanayopaswa kutimizwa kwa afua mahususi. Ujumuishaji hauwezi kufanikiwa labda kama hatua zinachukuliwa sawia ili: i) kutoa huduma za marekebisho na utengamano, kuzuia athari zaidi za vilema, kutoa visaidizi, nyenzo na vifaa muhimu, ii) kujenga uwezo wa vyama vya watu wenye ulemavu ngazi za msingi kwa kuwawezesha kukuza stadi za maisha, kujithamini, kuzielewa haki zao, kuwa na uwezo wa kupambanisha hoja na taasisi na wadau. Mathalani, mtu mzima mwenye ulemavu asiyejua kusoma na kuandika, hujihisi kuwa duni, hapati visaidizi muhimu, na hivyo, hawezi kushiriki kwenye mijadala inayohusu maslahi ya kijamii, hata kama ataalikwa, jambo ambalo ni muhali. cxiv 212

231 Uu universal declaration of human rights: azimio la haki za binadamu: waraka wa mwanzo kabisa wa kimataifa ulioelekeza kuhusu haki za binadamu na jinsi gani serikali za nchi ziwatendee raia wake. Waraka huu ulitungwa kufuatia maafa yaliyotokana na Vita Kuu ya II ya Dunia. universal design or design for all : usanifishaji kwa wote: 1. usanifujenzi wa bidhaa, mazingira, miundombinu, majengo, programu, mawasiliano na huduma ili viweze kutumiwa na kila mtu kwa kiwango cha juu kinachowezekana, bila ya kuhitaji marekebisho au usanifu maalumu. Usanifu huu haubagui vifaa saidizi mahususi kwa makundi maalumu ya watu wenye ulemavu pale vinapohitajika 2. hali ya bidhaa kuwa na ukubwa na kutoa nafasi sadifu kwa ajili ya kukaribiwa au kusogelewa, kufikiwa, kuegemezwa na kutumiwa bila kujali kimo, ukubwa na msogeo wa mtumiaji; kufaa na kuuzika kwa mtu mwenye ulemavu anuwai, ulinganifu kimatumizi. Ni vyepesi kueleweka bila kujali uzoefu, maarifa, umahirilugha, na kiwango cha umakini wa mtumiaji, n.k. universality: umajumui: jambo ambalo hupatikana kila eneo la kijiografia duniani. Mojawapo ya vitu vyenye sifa ya namna hiyo ni haki za binadamu ambazo 213 hufanana duniani kote bila kujali rangi, kimo, utamaduni, imani za kidini, maadili ya kisiasa, n.k. ureter: ureta: njia ambayo mkojo hupitia kutoka kwenye figo hadi kibofu cha mkojo. urethra: urethra: njia ambayo mkojo hupitia kutoka kwenye kibofu hadi nje ya mwili. urine and bowel management: ushughulikiaji takamwili: mbinu za kumsaidia mtu aliyeumia ugweuti na kuwa na kiwango kikubwa cha kilema cha ujongeaji na akili katika kukabiliana na matatizo ya ufukunyungu au/na kufunga choo. user-friendly: rahisi kutumika: -enye kusanifiwa kwa kuzingatia mahitaji na hali za kila mtumiaji, yaani mtoto, kijana, mzee, mjamzito, mtu mwenye ulemavu, mgonjwa, n.k. Kwa hiyo, kila mmoja kuweza kutumia bidhaa au huduma hiyo kiurahisi (taz. universal design au design for all ).

232 Vv vaccinations or vaccines: dawachanjo: 1. dawa zenye kudungwa mwilini ili kutoa kinga dhidi ya magonjwa mahususi kama vile tetenasi au pepopunda. 2. utiaji dutu mwilini ili kuanzisha kingamwili. Miili ya binadamu hukingwa dhidi ya magonjwa kama yale ya kupooza, pepopunda, kifaduro, tetekuwanga, ukosefu wa vitamini A, n.k. kwa njia ya chanjo na hivyo kupunguza matukio ya ulemavu. validity: uhalali: kiwango ambacho kipimo hupima kile kinachostahili. Uhalalli hutaarifu kile kinachoweza kuhitimishwa kimantiki na kimakini kutokana na alama za upimaji. varicose: -a mishipa neva: mishipa limfu ambayo imejikunjakunja na kutanuka. varicose stocking: soksi ndefu za miguuni: aina ya tiba ambayo hushauriwa na tabibu pale dalili za mishipa hususani ya miguu huonekana kutanuka na kujikunjakunja. Soksi hizi ndefu huwa ni za kubana na hivyo huzuia kutanuka kwa mishipa. vascular: -a kifereji vascular tissue: tishukifereji: tishu maalumu yenye kazi ya kupitisha kioevu mwilini na kwenye mishipa ya damu. verbalisms: uzungumzaji: matumizi ya maneno kupindukia ambapo watu hutumia maneno yenye maana ndogo kwao. 214 vestibule: vestibuli: kaviti ndogo mwanzoni mwa mwanya mfano wa sikio, pua, n.k. video remote interpreters: video kalimani lugha ishara: aina ya huduma ya mawasiliano kati ya kiziwi na watu wengine hasa mahali pa kazi, mikutanoni, masomoni, n.k. Huduma hii huhitaji mkalimani mmoja tu wa kuunganisha mawasiliano kati ya kiziwi na wenzake wasiokuwa na uziwi kwa kupitia video na vifaa vingine vya kimawasiliano. victim: mwathirika (ang. tragic ). violate: kiuka: kwenda kinyume cha utaratibu unaofahamika kisheria. violation of: ukiukaji wa: kitendo kinachofanyika kinyume cha maafikiano au amri; mathalani, kumwingilia mtu au kitu; kuvunja kanuni au sheria. violence: uonevu: kutenda kinyume cha sheria au kanuni dhidi ya mtu mwingine au kundi. visual acuity: kuona sawasawa: 1. uwezo wa mtu kuona na kutofautisha vitu kulingana na

233 umbali alipo. 2. ukali au usahihi wa uoni. visual aid: kielelezo onyeshi: kifaa, mashine au matendo yoyote yenye kuruhusu hadhira kupata taarifa kwa kuona k.m. ubao wa chaki, projekta, maonyesho ya filamu, michoro ya picha, michezobubu, na kompyuta. visual closure: uoni kamili: uwezo wa kung amua kitu kutokana na vielelezo onyeshi visivyokamilifu. visual discrimination: uoni tofautishi: uwezo wa kulinganisha au kubaini sifa za maumbo mahali pale umbo moja linapofanana na lingine. visual impairment: kilema uoni: 1. hali ya kuwa na uoni pungufu (kwa viwango mbalimbali) kwenye moja ya macho au yote mawili ambayo hata msaada wa kitabibu haumwezeshi mhusika kutenda shughuli za maisha ya kila siku bila msaada. Kwa hiyo hii ni dhana ya jumla katika uga wa uoni inayohusisha hatua tofautitofauti za hitilafu za uoni; yaani kuanzia hafifu hadi ile ya kutoona jumla. Hali hii husababisha ugumu kwenye masomo au katika kuishi maisha ya kujitegemea. Upotevu wa uoni unaweza kuainishwa kwa kiwango cha usahihi wa kuona, kuona pembeni, na uwezo wa kufuatilia, kubadilisha mkazo wa macho na kuangazaangaza. Misamiati ya 215 kuona kiasi, uoni hafifu, upofu kisheria, upofu wa jumla hutumiwa katika muktadha wa kielimu kuelezea kiwango cha hitilafu ya uoni wa mtoto mwenye kilema hicho. Kasoro za macho zinazoweza kusababisha vilema vya uoni zinavyoweza kujumuisha: uharibifu wa retina, ualbino, mtoto wa jicho, matatizo ya misuli yanayosababisha kuvurugika kwa uoni, mvurugiko wa konea, kisukari, kasoro za na maambukizi ya kurithi. 2. hali ya kupungukiwa au kuukosa kabisa uoni wa ama jicho moja au yote mawili kugundua na/au kuchakata picha. Hali hii husababishwa na mambo mbalimbali ya kibiolojia na kimazingira. Kupoteza uoni hasahasa hujitokeza miongoni mwa vijana kutokana na hali za kinasaba, ambazo huumiza sehemu za jicho. Uharibifu mojawapo au zaidi ya sehemu za mfumo wa uoni ambao ni pamoja na: kilema cha maumbile au usikivu; kilema cha mishipa ya fahamu ya optiki au pitio la optiki; kilema cha tabaka la uoni. visual motor coordination or visual motor integration: mota uoni patanifu: uwezo wa macho kupatana na misogeo ya mkono au/na mwili na michakato ya mawazo kwenye ubongo ili kutimiza shughuli mahususi ya mota kama vile kuandika, kuchambua na kushona.

234 visual perception: utambuzi uoni: uwezo wa kutambua, kupangilia na kutafsiri au kutoa maana ya kile kinachoonekana mathalani, sura au picha. vitreous fluid: giligili jicho: kitu kama ute ambacho hujaza sehemu kubwa ya ndani ya jicho. vocational rehabilitation: marekebisho amali au ufundi: 1. huduma za kufanya uchunguzi, kutoa ushauri, kuendesha mafunzo, kurekebisha maungo, uanagenzi kwa mtu mwenye ulemavu kwa minajili ya kumwandaa na kumuhusisha kwenye ajira ambazo humsaidia kuwa na kiwango kikubwa cha kujitegemea. Msamiati wenye kukubalika sasa ni huduma za marekebisho. 2. shughuli ambazo hutolewa kwa mtu aliyepata kilema kwa nasibu ili amudu ama kuendelea na ajira yake ya awali katika hali yake mpya au apate stadi mpya na kubadilisha kitengo, idara au ajira. vocational education: mafunzo amali au ufundi: masomo yaliyopangiliwa yakilenga kumwandaa mtu kupata stadi ili kuajiriwa katika fani maalumu au makundi ya fani zinazoshabihiana kwa karibu na ambazo ni mahususi na zinasadifu mahitaji ya wahusika waliofuzu au tarajali. Mafunzo ya ufundi stadi 216 yanaweza pia kujumuisha programu za udadisi. vocational guidance programmes: programu za ushauri: shughuli ambazo hujihusisha na huduma za unasihi wa kikazi kwa mhitimu wa masomo, aliye na ulemavu au anayebadili mfumo wa maisha. vocational training programme: programu za mafunzo amali au ufundi: mafunzo, kozi, huduma au shughuli iliyoandaliwa na kupangiliwa kimtawalia ili kukidhi malengo ya kiajira kwa mhusika kuwa na stadi za kiufundi. vocational rehabilitation specialist: bingwa marekebisho amali au ufundi: mtaalamu aliyefuzu kwenye uandaaji na utekelezaji wa programu za kumsaidia mtu mwenye kilema kupata na kudumu kwenye ajira au amali. voice disorder: mvurugiko wa sauti: aina ya kilema cha uongeaji kinachobainishwa na ama uzito wa sauti usiofaa kimazungumzo, kiusikikaji au kiubora. voice screen reader: kisomaji skrini: programu maalumu kwa ajili ya yule asiyeona inayomwezesha kupata taarifa zilizomo kwenye kompyuta, kwa njia ya sauti badala ya yeye mwenyewe kulazimika kusoma maandishi. volume control: kidhibiti sauti: chombo kinachobadilisha kiwango cha ukubwa wa sauti wa shimesikio au kifaa saidizi cha aina hiyo. Kwa kawaida kidhibiti hiki

235 kimewekwa kiasi kwamba kila sauti inayoingia isikike katika hali na kiwango kinachotakiwa. Hata hivyo, ukubwa wa sauti unaweza kurekebishwa na mhusika kulingana na mazingira anamosikilizia. voyeurism: upigaji chabo: hali ya kuamsha ashki au kujitosheleza kingono kwa ama kuangalia sehemu za siri au kwa kuchungulia watu wanaojimai. voyeur: mpigachabo: mtu ambaye utoshelezaji wa ashiki yake kingono kutokana na kuchungulia kwa siri miili iliyo uchi au watu wanaojamiiana. volunteer: valantia: mfanyakazi asiyelipwa ujira wa kisheria ila anaweza kupata posho ya kujikimu tu wakati akijitolea. vulnerable: -a kuathirika kiurahisi: -enye kuweza kudhurika au kuathirika kwa upesi. vulnerable group: kundi lenye urahisi wa kuathirika: kundi lisilokuwa na usalama kwa kukosa utaratibu wa kiulinzi. 217

236 Ww waiting period: kipindi subira: kipindi kilichopo katikati tangu ulemavu ulipoanza na tarehe ya kuanza kupokea mafao. Mfumo huu umezoeleka katika nchi ambapo mtu mwenye ulemavu hupatiwa aina fulani za msaada ikiwa ni pamoja na posho za kujikimu na kuhudumia ulemavu. Huduma hizi hujumuisha, makazi na uangalizi wake, wasaidizi, usafiri, matibabu, n.k. waive: samehe: uondolea madai au achilia haki. waiver: msamaha wa muda: 1. kusamehe madai ya haki kwa hiari k.m. abiria kusamehe madai yanayohusiana na kuumia au kupoteza maisha kwenye ajali wakati wa kuabiri chombo cha usafiri au mfanyakazi kukubali kusamehe kiasi cha malipo ya kipindi cha ulemavu, au mtu mwenye ulemavu kutochangia gharama za matibau baada ya kujieleza na kuridhisha mamlaka kuwa hawana uwezo 2. hati ya kusamehe madai: Hata hivyo, msamaha wa aina hii huwa ni kwa muda tu na agh. hutolewa kwa waraka wala si kwa sheria (taz. exemption ). walking stick or cane: fimbo kongojea: taz. bakora walker/walking frame (also known as a Zimmer frame): kiunzigemeo: aina ya wenzo madhubuti uliotengenezwa kwa mbao au metali madhubuti katika umbo la kiunzi chenye ncha miguso mitatu au zaidi. Mtumiaji wake hukitanguliza mbele yake na kukifumbata wakati wa kutembea. Ncha mguso zinaweza kuwa na mipira iliyokaziwa kama ilivyo kwa wenzo na fimbokongojea, vigurudumu au hata mchanganyiko wa vyote viwili. Kiunzigemeo cha magurudumu pia huitwa roleta. Wenzo wa aina hii huwa ni kwa ajili ya kurahisisha ujikongojaji kwa mtu mwenye kilema cha ujongeaji au matatizo ya mgongo kutokana na kuumia kwa ajali, maradhi, n.k. 218

237 walker cane hybrid: kiunzigemeo mahuluti: wenzo wa miguu miwili kwa ajili ya kutoa mwega ubavuni ambao hauwezi kutolewa na bakora ya kawaida. Aina hii ya wenzo inaweza kutumiwa kwa mikono miwili mbele ya mtumiaji kama ilivyo kwa kiuziimo na hivyo kutoa mwega wa ziada tofauti na bakora. Aidha, unaweza kurekebishwa kulingana na mahitaji, mathalani, kutumiwa na mkono mmoja au miwili kwa mbele au ubavuni au kwa kusaidia kupandia ngazi. Wenzo huu siyo mbadala wa kiuziimo cha miguu minne na cheye kutoa mwega mara nne kwa kutumia mikono. Aina hii ya wenzo ni kwa ajili ya kuziba pengo kati ya bakora na kiunzigemeo. wardship: ulinzi: hali ya kukasimiwa jukumula ulezi wa mtu hasa mtoto aliye chini ya mamlaka ya mahakama. Wechsler Intelligence Tests: vipima akili aina ya Wechsler: mfululizo wa upimaji wa maongezi na utendaji unaotumika sana kwenye uga wa elimu kuanzia ile ya awali, kipindi cha utoto na utu uzima. wedge: kabarimaungp: kifaa chenye umbo la kabari kinachotumika kusaidia kuweka mkao sawa kulingana na aina ya kilema cha mtu. wands and sticks: kirungu na fimbo mpapaso: wenzo ambao huvaliwa kichwani, hushikiliwa kwa mdomo au kufungwa kidevuni na hutumiwa na mtu asiye na mikono kuweza kubonyeza vitufe kwenye kicharazio cha kompyuta, n.k. 219 weight for length/height: uwiano uzito na kimo: rekodi yenye kuonesha vipimo vya mtu kwa kuwianisha uzito na urefu. weight-bearing: kuhimili uzito: hali ya kiungo mahususi cha mwili kumudu kubeba uzito wa mwili. Mathalani, magoti yanaweza kuhimili kubeba uzito wa mwili pale nguvu ya misuli ya paja inapokuwa mizuri na si kinyume chake.

238 well-baby care: matunzo mazuri ya mtoto: ufuatiliaji wa kinga na matunzo ili kutathmini afya ya mtoto mpaka mwaka wake wa pili. wheelchair cushion: mto kitimwendo: aina za mito midogo na laini kwa ajili ya kuboresha uimara, kuleta hisia za raha, kuweka mwili sawasawa, kupunguza mitikisiko kwenye maeneo yasiyosawazika, kinga dhidi ya vidonda mkandamizo, na husaidia wakati wa kuhamia kwenye kitimwendo kingine. Halikadhalika, unaweza kutumika kwenye sehemu nyingine za kukalia. Mto huu unaweza kuwa na maumbo, vipimo na vifaa mbalimballi (hewa, vitu tepetepe au jeli, n.k.). wheelchair: kitimwendo: 1. kiti kilichosimikwa kwenye fremu yenye magurudumu mawili au moja mbele na mengine makubwa pembeni ambacho hutumika kama njia ya kujongea kwa mtu asiyeweza kujikongoja na kumudu kufanya hivyo. Magurudumu yanaweza kuzungushwa na mhusika mwenyewe kwa mikono yake, kusukumwa na mtu mwingine kutokea nyuma au mota ndogo. 2. wenzo wa kujimudu unaotumiwa na mtu mwenye ulemavu wa maungo au mgonjwa hususani aliyeumia viungo au anayekabiliwa na ugumu wa kutembea kutokana na umri. Kwa vile matumizi mengi ya kiti hiki (katika nchi zinazoendelea) ni 220 maeneo ya hospitali, hivyo, wenzo huu kwa wengi hunasibishwa na ugonjwa. Dhana hii siyo kweli kwani watumiaji wake wengi siyo wagonjwa ila wenzo yenyewe ni kama sehemu ya maumbile inayowawezesha kujongea na hata kujitegemea kwa kiwango fulani. Pia haifai misemo kama aliyezuiliwa au kufungiwa kwenye kitimwendo kwani mpanda kiti hiki hukiona kuwa chombo wezeshi badala ya kizuizi. Kutokana na matumizi anuwai ya vitimwendo maumbo yake nayo pia hutofautiana kulingana na matumizi kusudiwa. Alama ya kitimwendo inatakiwa kutumika tu kuonyesha ufikiaji wa mtu mwenye ukomo wa kujongea ikiwa ni pamoja na mwenye kutumia vitimwendo k.m. kuonyesha mlango wa kuingilia bafuni au eneo la simu ambalo linazingatia mahitaji ya mtumia kitimwendo.

239 wheelchair lift, (platform lift, or vertical platform lift): kinyanyua kitimwendo: aina ya wenzo wenye kutumia nguvu za umeme uliosanifiwa kwa minajili ya kunyanyua kitimwendo na mtumiaji wake kwa pamoja na hivyo kukwepa viunzi vya ngazi na vinginevyo vya aina hiyo (taz. bridge plates ). Kinyanyua kitimwendo kinaweza kusimikwa nyumbani au mahali pa kazi na agh. huongezwa kwenye vyombo vya usafiri vya binafsi na vya umma kama mbadala wa kipandio cha ngazi ambacho humsafirisha abiria bila ya kuwa na nyenzo yake. Jitihada hizi ni kukidhi mahitaji ya ufikivu yanayotamkwa kisheria na kimikataba. wheeled walker: ang. walking frame wheelboard/wheelbench: chelezomjongeo: aina mojawapo ya wenzo wa kujikongojea ambao mtumiaji wake hasa ni yule asiyemudu kusimama mwenyewe kwa viungo vyake. Kwa hiyo yeye huzungukazunguka kwenye mazingira yake akiwa amelalia chelezomjongeo. 221 white blood cell: selidamu nyeupe: seli ya damu kama vile ya kwenye limfu ambayo haina ile rangi nyekundu inayowajibika hasa na kupigana na chembe za magonjwa. white cane or long cane: fimbo nyeupe: ufito ambao agh. hupakwa rangi na hutumika kumwongoza mtu asiyeona ili kutambua vikwazo vilivyo mbele yake na kujihakikishia usalama, ustadi na kujitegemea katika matembezi kwenye mazingira aliyoyazoea au mapya. Japo wenzo huu kimataifa umetambuliwa rasmi kama fimbo nyeupe, ikumbukwe kuwa siyo fimbo zote kwa minajili hii huwa na rangi nyeupe. Sehemu nyingine ambayo hali ya uchumi na teknolojia bado ni duni, fitomwitu hukidhi haja. Kutokana na kupanuka kwa teknolojia na ubunifu, wenzo huu unaendelea kuboreshwa zaidi kiasi cha kumwezesha mtumiaji kumudu mambo mengi. Fimbo hii inapotumiwa ipasavyo, mhusika hutabiri mazingira ili kugundua vizuizi, au mabadiliko ya usawa njiani, humpatia muda wa kutosha kusimama au kubadili uelekeo pale inapobidi. Nguvu zake huruhusu kutumika kama kidadisi cha kumwezesha hata mtumiaji kugundua

240 mazingira au vitu vyenye kuvutia. Aidha, rangi zake bainishi humtambulisha mtumiaji kuwa mwenye kilema cha uoni. Ni kiashirio cha uwezo kuliko ulemavu na hutumika kama ishara ya kujimudu kwa mwenye kuibeba. Halikadhalika, ufito huu huitwa ufito wa Hoover kama kumbukizi kwa yule aliyeubuni. Urefu wa ufito huu hutegemeana na matakwa ya mtumiaji mwenyewe na kwa kawaida huwa na kimo cha kutoka chini kwenye nyayo hadi kifuani mwa mtumiaji. Baadhi ya makundi hupendelea kutumia fito zenye urefu zaidi ya kipimo hiki na visawe vyake ni: - fimbo ongozaji: ufito mfupi zaidi ambao huanzia chini kwenye nyayo na kuishia kwenye nyonga ya mtumiaji ukiwa na ukomo zaidi kiujongeaji. Aina hii ya ufito hutumika kukagulia ngazi na kingo zabarabara. Halikadhalika unaweza kutumika kimshazari kwa ajili ya kuukinga mwili na kuhadharisha mtumiaji kuhusu vizuzi vilivyo mbele yake. - fimbo utambuzi au ishara: kimsingi katika baadhi ya nchi, ufito huu hutumika kuhadharisha watu wengine kuwa mbembaji ana kilema cha uoni. Aina hii ya ufito huwa ni nyepesi na fupi kuliko aina nyingine na haufai kuwa zana ya kutembelea fimbo egemeo: ufito mweupe kwa ajili ya kuimarisha mwili wa mtumiaji asiyeona. Kwa rangi yake, ufito huu pia hutumika kama wenzo wa utambuzi. Aina hii ya wenzo ina ukomo mkubwa kwa maana ya kutembelea. - fimbo ya kitoto: fimbo inayotumika sawa na ufito mrefu wa mtu mzima ila hii ni kwa ajili ya matumizi ya watoto. - fimbo kijani: katika baadhi ya nchi, aina hii ya fito hutumika kutambulisha kuwa mtumiaji ana uoni hafifu wakati ule mweupe hutambulisha upofu wa jumla. Fimbo ndefu nyeupe zinaweza ama kukunjika au kunyooka na kila aina ya hizi ina faida na hasara zake. Agh. hutengenezwa kwa aluminiamu au palstiki zilizoimarishwa ama na graffiti au utembo na huwa za aina tofauti kulingana na utashi wa mtumiaji. ufikivu kwa wasioona au wenye uoni hafifu: alama hii hutumika kuashiria ufikivu kwa mtu asiyeona au wenye uoni hafifu pale wanapotaka: kutalii kwa kuongozwa, njia kuelekea kwenye vivutio vya asili, au bustani zenye kunukia uturi na utalii mpapaso au maonyesho kwenye makumbusho yanayoweza kugusika (kwa wasioona). wholistic: -a utimilifu: enye hali ya kujihisi kuwa binadamu kamilifu, katika mlingano, wa fahamu. Dhana hii hutumika kwa mapana zaidi baki

241 ya unasihi na kuuguzwa hadi kwenye jumuia na jamii. whooping cough: kifaduro: ugonjwa wa kikohozi cha muda mrefu kinacho-sababishwa na bakteria wa spishi ya bodetela agh. kwa watoto. wide range achievement test: upimaji wa stadi za msingi: usaili mfupi wa kutathmini ujuzi wa kuandika, kuhesabu na kusoma. Mtindo huu hutumiwa sana shuleni katika kupima ufanisi wa kielimu. wide brimmed hut: kofia pana (pama): kofia yenye ukingo mpana unaozunguka pande zote inayovaliwa na mtu mwenye ualbino ili kumkinga dhidi ya miali ya jua ambayo humfanya aote mbaranga na kisha kuwa na saratani ya ngozi. will: wosia: maelezo anayoyatoa mtu kuelezea mgawanyo wa mali na madeni kwa wanufaika baada ya kifo chake. withdrawing behaviour: tabia ya kujitenga: mwenendo wenye kubainishwa na hali ya kupungukiwa shauku ya kukutana na watu wengine na unaweza kujumuisha kushindwa kuzungumza, kurudia hali ya 223 utoto, kuonyesha hofu nyingi, unyong onyevu, n.k. within normal limits: kiwango cha kawaida: dhana inayotumika pale matokeo ya upimaji yanapoonekana kuwa sawa. work experience programme: programu ya tajiriba za kazi: mpango unaosimamiwa na shule ambao kupitia ajira za muda hutoa uzoefu katika mazingira ya ajira ili kumsaidia mhitimu wa shule kupata stadi muhimu katika uhusiano wa binadamu, mielekeo, halitabia za kiajira, na maarifa ya jumla yanayohitajika kuweza kufanikiwa kiajira na kuchagua kazi au/na programu ya mafunzo ya amali. Maudhui ya mpango huu yanahusiana na lengo la kazi la mwanafunzi. workers' compensation: fidia ya mfanyakazi: 1. mpangilio wa mafao yanayolipwa kwa mfanyakazi kutokana na kuumia, ulemavu, kupoteza kiungo, au kifo pale hali inaposababishwa na mazingira hatarishi mahali pa kazi. Malipo ni jukumu la mwajiri. 2. mafao kwa mfanyakazi yanayolipwa kwa mujibu wa sheria na kwa niaba ya mwajiri. 3. fidia pale mfanyakazi anapoumia au kufia kazini. Fidia ya kuumia huanza wakati haki ya kulipwa inapofikia na ile ya kifo hutokea kutokana na ajali kazini.

Ukweli kuhusu Mchochota wa ini (au hepatitisi), aina A, B na C na jinsi ya kuepukana na ambukizo

Ukweli kuhusu Mchochota wa ini (au hepatitisi), aina A, B na C na jinsi ya kuepukana na ambukizo Ukweli kuhusu Mchochota wa ini (au hepatitisi), aina A, B na C na jinsi ya kuepukana na ambukizo Fakta om hepatitt A, B og C og om hvordan du unngår smitte Swahili/norsk Hva er hepatitt? Hepatitt betyr

Detaljer

Ordliste for TRINN 1. (utviklende matematikk-oppgavehefter 1A, 1B,2A, 2B, 3A og 3B, - refleksjonsord som kan hjelpe å forstå oppgaver).

Ordliste for TRINN 1. (utviklende matematikk-oppgavehefter 1A, 1B,2A, 2B, 3A og 3B, - refleksjonsord som kan hjelpe å forstå oppgaver). Ordliste for TRINN 1 (utviklende matematikk-oppgavehefter 1A, 1B,2A, 2B, 3A og 3B, - refleksjonsord som kan hjelpe å forstå oppgaver). Bok og side Ord på norsk I oppgavetekstene står ofte verb i imperativ

Detaljer

Je, kukosa nidhamu ni kawaida kwa Wanorwe? Typisk norsk å være uhøflig?

Je, kukosa nidhamu ni kawaida kwa Wanorwe? Typisk norsk å være uhøflig? Reidun Aambø Je, kukosa nidhamu ni kawaida kwa Wanorwe? Typisk norsk å være uhøflig? Reidun Aambø Je, kukosa nidhamu ni kawaida kwa Wanorwe? Typisk norsk å være uhøflig? 2010 Author Translator Publisher

Detaljer

Ord og begreper. Norsk Morsmål: Tegning (hvis aktuelt)

Ord og begreper. Norsk Morsmål: Tegning (hvis aktuelt) Ord og begreper Norsk Morsmål: Tegning (hvis aktuelt) Få Chache Mange Wengi\nyingi Venstre Kushoto Høyre Kulia Øverst Juu zaidi Nederst Chini zaidi Lite Ndogo Mye Kiasi Flest Færrest Oppe Zaidi Chache

Detaljer

Ukweli kuhusu VUKIBI na UKIMWI

Ukweli kuhusu VUKIBI na UKIMWI Ukweli kuhusu VUKIBI na UKIMWI Swahili/norsk Fakta om hiv og aids Aids er en alvorlig sykdom som siden begynnelsen av 1980-tallet har spredd seg over hele verden. Aids skyldes et virus, hiv, som overføres

Detaljer

MADAWA ASILI KATIKA NCHI ZA

MADAWA ASILI KATIKA NCHI ZA SHUKRANI Kutokana na Ukalimani uliofanyika kufanikisha toleo la Kitabu hiki kufikia hapa, ni kutokana na ushirikiano na mchango wake aliotoa Mch. Richard J. Hermas (wa Bad Neustadt/Saale Ujerumani), ambaye

Detaljer

Geitekillingen og Leoparden på norsk og swahili

Geitekillingen og Leoparden på norsk og swahili Geitekillingen og Leoparden på norsk og swahili Katika sehemu hiyo ya nchi, palikwapo na mama mbuzi. Alikuwa na mwanambuzi mdogo. Mwanambuzi huyo alikuwa mnyama mdogo mzuri sana. Macho yake yalikuwa yanang

Detaljer

Eksamensoppgave i SWA1111 Swahili språk II

Eksamensoppgave i SWA1111 Swahili språk II Institutt for språk- og litteratur Eksamensoppgave i SWA1111 Swahili språk II Faglig kontakt under eksamen: Assibi Amidu Tlf.: 73 59 65 22 / 73 59 65 47 Eksamensdato: 28.05.2014 Eksamenstid (fra-til):

Detaljer

EKSAMENSOPPGAVE SWA1101 Swahili språk I

EKSAMENSOPPGAVE SWA1101 Swahili språk I EKSAMENSOPPGAVE SWA1101 Swahili språk I Faglig kontakt under eksamen: Assibi Amidu Tlf faglig kontakt / instituttkontoret: 73 59 65 22 / 73 59 65 47 Eksamensdato: Torsdag 6. desember 2012 Eksamenstid:

Detaljer

EKSAMENSOPPGAVE SWA1111 Swahili språk II

EKSAMENSOPPGAVE SWA1111 Swahili språk II EKSAMENSOPPGAVE SWA1111 Swahili språk II Faglig kontakt under eksamen: Assibi Amidu Tlf faglig kontakt / instituttkontoret: 73 59 65 22 / 73 59 65 47 Eksamensdato: 01.06.2012 Eksamenstid: 6 timer Studiepoeng:

Detaljer

MAKE MAKE Arkitekter AS Maridalsveien Oslo Tlf Org.nr

MAKE MAKE Arkitekter AS Maridalsveien Oslo Tlf Org.nr en omfatter 1 Perspektiv I en omfatter 2 Perspektiv II en omfatter 3 Perspektiv III en omfatter 4 Perspektiv IV en omfatter 5 Perspektiv V en omfatter 6 Perspektiv VI en omfatter 7 Perspektiv VII en omfatter

Detaljer

Eksamensoppgave i SWA1101 Swahili språk I

Eksamensoppgave i SWA1101 Swahili språk I Institutt for språk og litteratur Eksamensoppgave i SWA1101 Swahili språk I Faglig kontakt under eksamen: Assibi Amidu Tlf.: 73 59 65 22 Eksamensdato: 18.12.2015 Eksamenstid (fra-til): 09.00 15.00 Tillatte

Detaljer

Bli bedre i norsk. se forskjellene mellom norsk og swahili

Bli bedre i norsk. se forskjellene mellom norsk og swahili Bli bedre i se forskjellene mellom og Bli bedre i se forskjellene mellom og 2010 Bli bedre i se forskjellene mellom og Hans Olaf Wiull ISBN 82 7724 146 3 Vox, Nasjonalt fagorgan for kompetansepolitikk

Detaljer

EKSAMENSOPPGAVE SWA1101 Swahili språk I

EKSAMENSOPPGAVE SWA1101 Swahili språk I EKSAMENSOPPGAVE SWA1101 Swahili språk I Faglig kontakt under eksamen: Lill Kristin Lund Kibakaya Tlf faglig kontakt / instituttkontoret: 73 59 65 44 / 73 59 65 29 Eksamensdato: Tirsdag 7. juni 2011 Eksamenstid:

Detaljer

HERRENS PROFETI AV NR. 2. EN SPESIELL KUNNGJØRING. HERREN ÅPENBARER ENDELIG TIL SIN TJENER DEN HERLIGE KIRKEN SOM VIL KOMME TIL HIMMELEN.

HERRENS PROFETI AV NR. 2. EN SPESIELL KUNNGJØRING. HERREN ÅPENBARER ENDELIG TIL SIN TJENER DEN HERLIGE KIRKEN SOM VIL KOMME TIL HIMMELEN. HERRENS PROFETI AV 15.01.17 NR. 2. EN SPESIELL KUNNGJØRING. HERREN ÅPENBARER ENDELIG TIL SIN TJENER DEN HERLIGE KIRKEN SOM VIL KOMME TIL HIMMELEN. Priset være HERREN, HERRENS MEKTIGE PROFET, HERREN velsigne

Detaljer

Internasjonal standardisering. Erlend Øverby erlend.overby@hypatia.no

Internasjonal standardisering. Erlend Øverby erlend.overby@hypatia.no Internasjonal standardisering Erlend Øverby erlend.overby@hypatia.no Internasjonal standardisering SN/K186 Standard Norge, Komite 186 Norsk skyggekomite: ISO IEC/JTC1/SC36 CEN TC353 ISO/IEC JTC1/SC36 (ITLET)

Detaljer

! Munch!på!Tøyen!eller!i!Bjørvika?!

! Munch!på!Tøyen!eller!i!Bjørvika?! MunchpåTøyenelleriBjørvika? En#diskursanalyse#av#debatten#om#det#nye#Munchmuseet#sett#i# sammenheng#med#museenes#samfunnsrolle# SeungHaeYu Instituttforkulturstudierogorientalskespråk Dethumanistiskefakultet

Detaljer

VEDLEGG B FOTODOKUMENTASJON

VEDLEGG B FOTODOKUMENTASJON I Bildeliste fra tilstandsvurdering: Bilde 1: Fylling/Landside; Utglidning og bevegelse i steinvegg... II Bilde 2:Fylling/ Landside; Utglidning og bevegelse i steinvegg, sett fra landside... II Bilde 3:

Detaljer

Kiwanis International District Norden Org. nr:

Kiwanis International District Norden Org. nr: Kiwanis International District Norden Org. nr: 983 757 189 (Distriktets norske klubber er godkjent som mottaker av skattefrie gaver etter skattelovens 6-50) DISTRIKTSLOVEN LOVPRESISERINGER/LOVPRAKSIS norsk

Detaljer

Kurskategori 2: Læring og undervisning i et IKT-miljø. vår

Kurskategori 2: Læring og undervisning i et IKT-miljø. vår Kurskategori 2: Læring og undervisning i et IKT-miljø vår Kurs i denne kategorien skal gi pedagogisk og didaktisk kompetanse for å arbeide kritisk og konstruktivt med IKT-baserte, spesielt nettbaserte,

Detaljer

Nedenfor kan brukeren se hvor bestemmelsene fra gammel avtale er plassert i ny Hovedavtale. Hovedavtalen Hovedavtalen

Nedenfor kan brukeren se hvor bestemmelsene fra gammel avtale er plassert i ny Hovedavtale. Hovedavtalen Hovedavtalen Avtalespeil Hovedavtalen 2010-2013 ctr. Hovedavtalen 2014-2017. Ved revisjon av Hovedavtalen SAMFO og LO (2014-2017) er det foretatt en omredigering, herunder er det foretatt språklige og tidsmessige oppdateringer.

Detaljer

Paletten, innføringstjenesten i Bamble kommune. Informasjon til foreldre/foresatte.

Paletten, innføringstjenesten i Bamble kommune. Informasjon til foreldre/foresatte. Paletten, innføringstjenesten i Bamble kommune. Informasjon til foreldre/foresatte. Amharisk Bamble kommune Amharisk Arabisk Chin Dari Engelsk Nepali Norsk Polsk Somali Swahili Tysk ባምብለ የራስ ገዝ አስተዳደር

Detaljer

Centre for Professional learning in Teacher education. and University of Tromsø

Centre for Professional learning in Teacher education. and University of Tromsø ProTed Centre for Professional learning in Teacher education University of Oslo and University of Tromsø Mål for ProTed senteret Senteret har som sitt langsiktige mål å drive fram fremtidsrettede og bærekraftige

Detaljer

Da!har!vi!avklart!det!

Da!har!vi!avklart!det! Daharviavklartdet En#studie#av#emneavrunding#i#møtesamtaler# SaraJ.Koppang Masteroppgaveiretorikkogkommunikasjon RETKOM4195(30stp.) Instituttforlingvistiskeognordiskestudier Dethumanistiskfakultet UNIVERSITETETIOSLO

Detaljer

verktøyskrin Grafisk profil ved Norges teknisk-naturvitenskapelige universitet

verktøyskrin Grafisk profil ved Norges teknisk-naturvitenskapelige universitet 1 Services and Systems Development Grafisk verktøyskrin Grafisk profil ved Norges teknisk-naturvitenskapelige universitet Selvhjelpspakken for informasjon og formidling ved NTNU: www.ntnu.no/info/selvhjelp

Detaljer

Bærekraftig FM til tiden/ Bærekraftig FM på tid

Bærekraftig FM til tiden/ Bærekraftig FM på tid Downloaded from orbit.dtu.dk on: Sep 28, 2019 Bærekraftig FM til tiden/ Bærekraftig FM på tid Nielsen, Susanne Balslev Publication date: 2015 Document Version Peer reviewed version Link back to DTU Orbit

Detaljer

Nasjonalt kvalifikasjonsrammeverk og læringsmål i forskerutdanningen

Nasjonalt kvalifikasjonsrammeverk og læringsmål i forskerutdanningen Nasjonalt kvalifikasjonsrammeverk og læringsmål i forskerutdanningen Roger Strand Senterleder, Senter for vitenskapsteori, UiB Medlem, Dannelsesutvalget Styreleder, Vestnorsk nettverk forskerutdanninga

Detaljer

Produktkalkyler i SAS Cost and Profitability Management hos Avinor

Produktkalkyler i SAS Cost and Profitability Management hos Avinor Insert Client / Partner logo Produktkalkyler i SAS Cost and Profitability Management hos Avinor Presentasjon på SAS Fans brukersamling - av Hild Eirin Strømme Litt om meg Bakgrunn Utdanning og annen erfaring

Detaljer

Folkeforbundet og krigens bekjempelse. Avhandling for graden doctor philosophiae

Folkeforbundet og krigens bekjempelse. Avhandling for graden doctor philosophiae Karl Erik Haug Folkeforbundet og krigens bekjempelse Norsk utenrikspolitikk mellom realisme og idealisme Avhandling for graden doctor philosophiae Trondheim, oktober 2012 Norges teknisk-naturvitenskapelige

Detaljer

THE BENDING MOMENT ENERGIZING CORPORATE BUSINESS STRATEGY. David E. Hawkins

THE BENDING MOMENT ENERGIZING CORPORATE BUSINESS STRATEGY. David E. Hawkins The Bending Moment THE BENDING MOMENT ENERGIZING CORPORATE BUSINESS STRATEGY David E. Hawkins David E. Hawkins 2005 Softcover reprint of the hardcover 1st edition 2005 978-1-4039-9838-5 All rights reserved.

Detaljer

Offshore Wind Turbine Support Structures. Erfaringer med å søke EU finansiering

Offshore Wind Turbine Support Structures. Erfaringer med å søke EU finansiering Offshore Wind Turbine Support Structures Erfaringer med å søke EU finansiering 1 Agenda 5 Steps to EU-funding Introduksjon Ø Steg 1: Big picture Ø Steg 2: Nåsituasjonen Ø Steg 3: Finansieringsalternativer

Detaljer

NY BESLUTNINGSSTØTTE FOR DE PREHOSPITALE AKUTTMEDISINSKE TJENESTENE FOR DIAGNOSTISERING VED HJELP AV SMART TEKNOLOGI

NY BESLUTNINGSSTØTTE FOR DE PREHOSPITALE AKUTTMEDISINSKE TJENESTENE FOR DIAGNOSTISERING VED HJELP AV SMART TEKNOLOGI NY BESLUTNINGSSTØTTE FOR DE PREHOSPITALE AKUTTMEDISINSKE TJENESTENE FOR DIAGNOSTISERING VED HJELP AV SMART TEKNOLOGI Jan Håvard Skjetne og Anders Liverud BRIDGE - Prehospital Monitoring HEALTH AND CARE

Detaljer

Information search for the research protocol in IIC/IID

Information search for the research protocol in IIC/IID Information search for the research protocol in IIC/IID 1 Medical Library, 2013 Library services for students working with the research protocol and thesis (hovedoppgaven) Open library courses: http://www.ntnu.no/ub/fagside/medisin/medbiblkurs

Detaljer

Klasseromseksamen i. LING2111 Språkendring og språktypologi. Våren 2012

Klasseromseksamen i. LING2111 Språkendring og språktypologi. Våren 2012 DET HUMANISTISKE FAKULTET ------------- Klasseromseksamen i LING2111 Språkendring og språktypologi Våren 2012 Tid: Onsdag 25. april 2012 kl. 12.15-14 (2 skoletimer) Sted: Foredragssalen i Veglaboratoriet

Detaljer

Delegeringsreglement for Røros kommune. Vedtatt av kommunestyret 310316, sak 12/16 280416, sak 17/16

Delegeringsreglement for Røros kommune. Vedtatt av kommunestyret 310316, sak 12/16 280416, sak 17/16 Delegeringsreglement for Røros kommune Vedtatt av kommunestyret 310316, sak 12/16 280416, sak 17/16 INNHOLDSFORTEGNELSE 1. Overordnet reglement for delegering av myndighet... 3 1.1 Formål... 3 1.2 Hjemmel...

Detaljer

KUNNSKAPSLØFTET EN PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING FOR PEDAGOGISK PERSONALE I VERDAL OG LEVANGER KUNNSKAPSLØFTET: PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING

KUNNSKAPSLØFTET EN PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING FOR PEDAGOGISK PERSONALE I VERDAL OG LEVANGER KUNNSKAPSLØFTET: PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING KUNNSKAPSLØFTET: PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING FOR PEDAGOGISK PERSONALE I GRUNNSKOLENE I LEVANGER OG VERDAL KOMMUNER HØRINGSUTKAST MAI 2005 1. Innledning Kunnskapsløftet er en ny og omfattende reform av

Detaljer

SIU Retningslinjer for VET mobilitet

SIU Retningslinjer for VET mobilitet SIU Retningslinjer for VET mobilitet Gardermoen, 16.09.2014 Oppstart- og erfaringsseminar Tore Kjærgård Carl Endre Espeland 2 Kort om Erasmus+ EUs utdanningsprogram for perioden 2014 2020 Budsjett: 14,7

Detaljer

Multimedia in Teacher Training (and Education)

Multimedia in Teacher Training (and Education) Multimedia in Teacher Training (and Education) Bodo Eckert, Stefan Altherr, Hans-Jörg Jodl Second International GIREP Seminar 1-6 September 2003 University of Udine, Italy Content Training courses for

Detaljer

verktøyskrin Grafisk profil ved Norges teknisk-naturvitenskapelige universitet

verktøyskrin Grafisk profil ved Norges teknisk-naturvitenskapelige universitet 1 Services and Systems Development Grafisk verktøyskrin Grafisk profil ved Norges teknisk-naturvitenskapelige universitet Selvhjelpspakken for informasjon og formidling ved NTNU: www.ntnu.no/info/selvhjelp

Detaljer

[ Web Accessibility Initiative ]

[ Web Accessibility Initiative ] [ Web Accessibility Initiative ] [ nett for alle ] Brendan Johan Lee Department of Informatics University of Oslo, Norway brendajl@simula.no February 2, 2011 [ Nettet er for alle ] The power of the Web

Detaljer

Internasjonalt gradssamarbeid, hva og hvordan. Internasjonaliseringskonferansen 2014, torsdag 6. mars, kl. 10:30, Rådssalen

Internasjonalt gradssamarbeid, hva og hvordan. Internasjonaliseringskonferansen 2014, torsdag 6. mars, kl. 10:30, Rådssalen Internasjonalt gradssamarbeid, hva og hvordan Internasjonaliseringskonferansen 2014, torsdag 6. mars, kl. 10:30, Rådssalen I II III IV Fire presentasjoner Rammene for og refleksjoner rundt 1) Nordic Master

Detaljer

Innledende arbeid i en EU-søknad Seminar UV-fakultet EUs Horisont 2020: Erfaringer fra søknadsskriving

Innledende arbeid i en EU-søknad Seminar UV-fakultet EUs Horisont 2020: Erfaringer fra søknadsskriving Innledende arbeid i en EU-søknad Seminar UV-fakultet EUs Horisont 2020: Erfaringer fra søknadsskriving Peter Maassen 28. januar 2016 Kontekst Forskergruppe ExCID Aktiviteter fokusert på: o Publisering

Detaljer

Halvårsrapport Tyskland 2013

Halvårsrapport Tyskland 2013 Halvårsrapport Tyskland 2013 Tyskland Tyskland er det tredje største markedet etter USA og Storbritannia innen meetingsnæringen med circa 1200 event- og incentiveagenturer, rundt 1500 corporate planners

Detaljer

Recognition of prior learning are we using the right criteria

Recognition of prior learning are we using the right criteria Recognition of prior learning are we using the right criteria Reykjavik 13.09.2012 Margrethe Steen Hernes, seniorrådgiver Nasjonal politikk Bakgrunn (1997 98) : Stortinget ber Regjeringen om å etablere

Detaljer

Vålerenga football foundation

Vålerenga football foundation Vålerenga football foundation Inkluderingsprosjektet hjelper barn, ungdom og voksne med dårlig økonomi Mål: Like muligheter gode opplevelser bedre helse Tiltak: Inkluderingsfond (støtte til treningsavgift

Detaljer

Liste omhandlet i Avtalens artikkel 3 DEL I

Liste omhandlet i Avtalens artikkel 3 DEL I VEDLEGG A Liste omhandlet i Avtalens artikkel 3 DEL I RETTSAKTER OMHANDLET I EØS-AVTALEN SOM ENDRES VED AKT OM TILTREDELSESVILKÅRENE FOR REPUBLIKKEN BULGARIA OG ROMANIA OG TILPASNINGEN AV DE TRAKTATER

Detaljer

LOVSPEIL. Aml. 1977 / Aml. 2005

LOVSPEIL. Aml. 1977 / Aml. 2005 LOVSPEIL Aml. / Aml. 2005 Dette lovspeilet er utarbeidet av Direktoratet for arbeidstilsynet og viser hvor bestemmelser i arbeidsmiljøloven av er å gjenfinne i den nye arbeidsmiljøloven som trådte i kraft

Detaljer

The Union shall contribute to the development of quality education by encouraging cooperation between Member States and, if necessary, by supporting

The Union shall contribute to the development of quality education by encouraging cooperation between Member States and, if necessary, by supporting The Union shall contribute to the development of quality education by encouraging cooperation between Member States and, if necessary, by supporting and supplementing their action, while fully respecting

Detaljer

MYNTER Frederik III, 1648-1670

MYNTER Frederik III, 1648-1670 Fredag 30. november, ca. 19.00 (rett etter Postkortene) MEDALJER 1251 Roald Amundsen 1872-1928, 80 årsjubileum 1952. Evensen. Bronse. 53 mm. 300,- 1252 Fyrst Paul Alexander Leopold og Emilie von Schwargburg.

Detaljer

Kost-nytte innen sikkerhet: Hva er prisen, hva er verdien, og hvordan prioritere blant tiltak?

Kost-nytte innen sikkerhet: Hva er prisen, hva er verdien, og hvordan prioritere blant tiltak? Kost-nytte innen sikkerhet: Hva er prisen, hva er verdien, og hvordan prioritere blant tiltak? Aida Omerovic Seminar om kost-nytte analyse i en risikoevaluering 18. Feb. 2015 SINTEF Technology for a better

Detaljer

INF2820 Datalingvistikk V Gang 6.3 Jan Tore Lønning

INF2820 Datalingvistikk V Gang 6.3 Jan Tore Lønning INF2820 Datalingvistikk V2017 8. Gang 6.3 Jan Tore Lønning I dag CKY-algoritmen fortsatt fra sist Python-implementasjon av CKY Chomsky Normal Form (CNF) Chart-parsing BU-algoritme for chart-parsing 3.

Detaljer

Software applications developed for the maritime service at the Danish Meteorological Institute

Software applications developed for the maritime service at the Danish Meteorological Institute Software applications developed for the maritime service at the Danish Meteorological Institute Anne Marie Munk Jørgensen (ammj@dmi.dk), Ove Kjær, Knud E. Christensen & Morten L. Mortensen Danish Meteorological

Detaljer

Ikke-diskriminering Article 1 (3) The Purposes of the United Nations are: Article 55 (c)

Ikke-diskriminering Article 1 (3) The Purposes of the United Nations are: Article 55 (c) Av Hadi Lile Ikke-diskriminering Article 1 (3) The Purposes of the United Nations are: [ ] promoting and encouraging respect for human rights and for fundamental freedoms for all without distinction as

Detaljer

Lehrer, Professor für histor. Hilfswiss. an der Univ. Ffm

Lehrer, Professor für histor. Hilfswiss. an der Univ. Ffm 1 Maschinenschriftliche Abschriften der Briefe Otto Schumanns an Martin Havenstein und Havensteins an Schumann aus dem Zeitraum 1930 1944. Die Originalbriefe befinden sich im Besitz der Schumann-Erben.

Detaljer

IAHV- NORGE ÅRSRAPPORT

IAHV- NORGE ÅRSRAPPORT 2012 IAHV- NORGE ÅRSRAPPORT IAHV- NORGE Org. Nr 895 115 142, Adresse: Kongensgate 3, 0153 Oslo Konto: 15031618786, http://www.iahv.no Organisasjonen IAHV : IAHV- International Association for Human Values,

Detaljer

PENSUM VÅREN 2015 SWAHILI. Institutt for språk og litteratur NTNU

PENSUM VÅREN 2015 SWAHILI. Institutt for språk og litteratur NTNU PENSUM VÅREN 2015 SWAHILI Institutt for språk og litteratur NTNU Det anbefales at pensumlistene leses på bakgrunn av de opplysninger som er gitt i fagbeskrivelsene i Studiehåndboka. Studiehåndboka 2014/2015

Detaljer

Svar 1: Minimum ett i hver kommune, samt flere svartjenester på funksjoner/enheter.

Svar 1: Minimum ett i hver kommune, samt flere svartjenester på funksjoner/enheter. Spørsmål og svar 2 Vi har mottatt følgende spørsmål i forbindelse med anbudskonkurranse «Telefonitjenester til Midt-Trøndelagskommunene» Saksnr. 2016/818» pr 13.04.2016. Oppdragsgiver har valgt å svare

Detaljer

Nordenfjeldske Filatelistforenings Stempelkatalog Trøndelag Levanger kommune. NB omfatter ikke Levanger by - se egen fil Levanger By. EKNE Innsendt??

Nordenfjeldske Filatelistforenings Stempelkatalog Trøndelag Levanger kommune. NB omfatter ikke Levanger by - se egen fil Levanger By. EKNE Innsendt?? Nordenfjeldske Filatelistforenings Stempelkatalog Trøndelag Levanger kommune NB omfatter ikke Levanger by - se egen fil Levanger By Innhold: Ekne Kastrå (Sundalen i Aasen) Markabygda (Birkelund - Skogns

Detaljer

KUNNSKAPSLØFTET EN PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING FOR PEDAGOGISK PERSONALE I VERDAL OG LEVANGER KUNNSKAPSLØFTET: PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING

KUNNSKAPSLØFTET EN PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING FOR PEDAGOGISK PERSONALE I VERDAL OG LEVANGER KUNNSKAPSLØFTET: PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING KUNNSKAPSLØFTET: PLAN FOR KOMPETANSEUTVIKLING FOR PEDAGOGISK PERSONALE I GRUNNSKOLENE I LEVANGER OG VERDAL KOMMUNER 1. Innledning Kunnskapsløftet er en ny og omfattende reform av hele grunnopplæringen.

Detaljer

Monitoring water sources.

Monitoring water sources. Monitoring water sources. Generell Informasjon Versjon 2 Url http://com.mercell.com/permalink/38336681.aspx Ekstern anbuds ID 223314-2013 Konkurranse type: Tildeling Dokument type Kontraktstildeling Prosedyre

Detaljer

Sustainability Programme

Sustainability Programme Sustainability Programme Even Wiger, 9. Februar 2012 Norway shall be a leader in environmental issues. Rally Norway is one of the best environmental pioneers in any sports- and cultural activities in

Detaljer

Internasjonalt samarbeid og nye kunnskapsmuligheter

Internasjonalt samarbeid og nye kunnskapsmuligheter Internasjonalt samarbeid og nye kunnskapsmuligheter Havdagen oktober 2011 Peter M. Haugan, Professor i oseanografi ved Geofysisk Institutt, UiB, også tilknyttet Bjerknessenteret for klimaforskning og Nansen

Detaljer

buildingsmart Norge seminar Gardermoen 2. september 2010 IFD sett i sammenheng med BIM og varedata

buildingsmart Norge seminar Gardermoen 2. september 2010 IFD sett i sammenheng med BIM og varedata buildingsmart Norge seminar Gardermoen 2. september 2010 IFD sett i sammenheng med BIM og varedata IFD International Framework for Dictionaries Hvordan bygges en BIM? Hva kan hentes ut av BIM? Hvordan

Detaljer

INSTRUKSER, STATUTTER OG RETNINGSLINJER FOR HEDRUM ORIENTERINGSLAG. GODKJENT AV STYRET 3. FEBRUAR 2014.

INSTRUKSER, STATUTTER OG RETNINGSLINJER FOR HEDRUM ORIENTERINGSLAG. GODKJENT AV STYRET 3. FEBRUAR 2014. 1 INSTRUKSER, STATUTTER OG RETNINGSLINJER FOR HEDRUM ORIENTERINGSLAG. GODKJENT AV STYRET 3. FEBRUAR 2014. INSTRUKS FOR STYRETS ARBEID LEDEREN Lederen har den daglige ledelse av idrettslaget. Lederen skal

Detaljer

Familieeide selskaper - Kjennetegn - Styrker og utfordringer - Vekst og nyskapning i harmoni med tradisjoner

Familieeide selskaper - Kjennetegn - Styrker og utfordringer - Vekst og nyskapning i harmoni med tradisjoner Familieeide selskaper - Kjennetegn - Styrker og utfordringer - Vekst og nyskapning i harmoni med tradisjoner Resultater fra omfattende internasjonal undersøkelse og betraktninger om hvordan observasjonene

Detaljer

ICF anvendt i forskning

ICF anvendt i forskning ICF anvendt i forskning Eksempler fra egen forskning Regional ICF konferanse Skien 3. november 2004 Sigrid østensjø Funksjon i dagliglivet hos barn med cerebral parese (CP) Formålet er å gi en flerdimensjonal

Detaljer

INF2820 Datalingvistikk V Gang 2.3 Jan Tore Lønning

INF2820 Datalingvistikk V Gang 2.3 Jan Tore Lønning INF2820 Datalingvistikk V2016 7. Gang 2.3 Jan Tore Lønning I dag CKY-algoritmen Python-implementasjon Chomsky Normal Form (CNF) 2. mars 2016 2 Dynamisk programmering I en beregning kan det inngå delberegninger

Detaljer

License Management Morten A. Steien EDB Business Partner Industri

License Management Morten A. Steien EDB Business Partner Industri License Management Morten A. Steien EDB Business Partner Industri 2009-02-04 EDB Business Partner organisasjon Bank & Finance Public sector Telecom Industry 1000 FTE s 1600 MNOK revenue Application Services

Detaljer

MUS Musikk, teknologi og produksjon. 22 august 2014

MUS Musikk, teknologi og produksjon. 22 august 2014 MUS4830 - Musikk, teknologi og produksjon 22 august 2014 Om emnet (Fra emnebeskrivelsen) Målet for emnet er å videreutvikle ferdigheter, innsikt og refleksjon om teknologi tilknyttet musikkfeltet og muliggjøre

Detaljer

Per Tonny Berg Partner & Business Development Manager

Per Tonny Berg Partner & Business Development Manager Per Tonny Berg Partner & Business Development Manager presentert av i samarbeid med Det praktiske Slå av lyden på mobiltelefonen Toaletter Kaffe og garderobe Lunsj kl. 12-13 Det praktiske WIFI = Oljemuseum

Detaljer

The Future of Academic Libraries the Road Ahead. Roy Gundersen

The Future of Academic Libraries the Road Ahead. Roy Gundersen The Future of Academic Libraries the Road Ahead Roy Gundersen Background Discussions on the modernization of BIBSYS Project spring 2007: Forprosjekt modernisering Process analysis Specification Market

Detaljer

Inga Bostad, direktør, Norsk senter for menneskerettigheter. Fri og avhengig! Spennet mellom hverdag og vedtatte rettigheter

Inga Bostad, direktør, Norsk senter for menneskerettigheter. Fri og avhengig! Spennet mellom hverdag og vedtatte rettigheter Inga Bostad, direktør, Norsk senter for menneskerettigheter Fri og avhengig! Spennet mellom hverdag og vedtatte rettigheter Hva og hvem passer inn? Å ha rett og få rett makt, avmakt, språk og byråkrati

Detaljer

Kan sykdom hos oppdrettslaks gi færre villaks? Åse Helen Garseth og Eirik Biering

Kan sykdom hos oppdrettslaks gi færre villaks? Åse Helen Garseth og Eirik Biering Kan sykdom hos oppdrettslaks gi færre villaks? Åse Helen Garseth og Eirik Biering La oss starte med å definere hva vi vet... Helsesituasjonen hos oppdrettslaks (2013-tall) SAV/PD 99 Smittsomme sykdommer

Detaljer

INF2820 Datalingvistikk V Gang 2.3 Jan Tore Lønning

INF2820 Datalingvistikk V Gang 2.3 Jan Tore Lønning INF2820 Datalingvistikk V2016 7. Gang 2.3 Jan Tore Lønning I dag CKY-algoritmen Python-implementasjon Chomsky Normal Form (CNF) 1. mars 2016 2 Dynamisk programmering I en beregning kan det inngå delberegninger

Detaljer

Liste omhandlet i avtalens artikkel 3 DEL I RETTSAKTER OMHANDLET I EØS-AVTALEN ENDRET VED TILTREDELSESAKTEN AV 16. APRIL 2003

Liste omhandlet i avtalens artikkel 3 DEL I RETTSAKTER OMHANDLET I EØS-AVTALEN ENDRET VED TILTREDELSESAKTEN AV 16. APRIL 2003 VEDLEGG A Liste omhandlet i avtalens artikkel 3 DEL I RETTSAKTER OMHANDLET I EØS-AVTALEN ENDRET VED TILTREDELSESAKTEN AV 16. APRIL 2003 Strekpunktet nevnt i artikkel 3 nr. 2 innsettes på følgende steder

Detaljer

NORSK LOVTIDEND Avd. I Lover og sentrale forskrifter mv. Utgitt i henhold til lov 19. juni 1969 nr. 53.

NORSK LOVTIDEND Avd. I Lover og sentrale forskrifter mv. Utgitt i henhold til lov 19. juni 1969 nr. 53. NORSK LOVTIDEND Avd. I Lover og sentrale forskrifter mv. Utgitt i henhold til lov 19. juni 1969 nr. 53. Kunngjort 22. juni 2018 kl. 15.10 PDF-versjon 22. juni 2018 22.06.2018 nr. 76 Lov om endringer i

Detaljer

ДЪРЖАВА [BG] SECTION. Нигерия Рибни продукти. [bg] Validity date from 14/08/2018 [bg] Date of publication 01/08/2018. [bg] List in force

ДЪРЖАВА [BG] SECTION. Нигерия Рибни продукти. [bg] Validity date from 14/08/2018 [bg] Date of publication 01/08/2018. [bg] List in force ДЪРЖАВА [BG] SECTION Нигерия Рибни продукти [bg] Validity date from 14/08/2018 [bg] Date of publication 01/08/2018 00040 FDF/C/02 Atlantic Shrimpers Ltd. Lagos Lagos FDF/C/03 ORC FISHING AND FOOD PROCESSING

Detaljer

E-Learning Design. Speaker Duy Hai Nguyen, HUE Online Lecture

E-Learning Design. Speaker Duy Hai Nguyen, HUE Online Lecture E-Learning Design Speaker Duy Hai Nguyen, HUE Online Lecture Design Educational Design Navigation Design Educational Design Some Important Considerations: 1. Authentic learning environment: For effective

Detaljer

Nordenfjeldske Filatelistforenings Stempelkatalog Trøndelag Flatanger kommune

Nordenfjeldske Filatelistforenings Stempelkatalog Trøndelag Flatanger kommune Nordenfjeldske Filatelistforenings Stempelkatalog Trøndelag Flatanger kommune INNHOLD: Bjørøya Bjørøen - Bjørø Bosviken Einvika Einviken Flatanger Lauvsnes - Lausnes - Løvsnes Hasvåg Hasvåg i Flatanger

Detaljer

Prosjektplanlegging i IT. Atle Spilde Lars Gunnar Lundestad

Prosjektplanlegging i IT. Atle Spilde Lars Gunnar Lundestad Prosjektplanlegging i IT Atle Spilde Lars Gunnar Lundestad 2 Capgemini 3 Agenda Best practise IT bransjen Verden sett med IT Googles Forventingsstyring Ansvarliggjøring i verdikjeder 4 Metodeverk som dekker

Detaljer

Note 38 - Investments in owner interests

Note 38 - Investments in owner interests Note 38 - Investments in owner interests Subsidiaries, affiliates, joint ventures and companies held for sale Company Registered office Stake in per cent Investment in significant subsidiaries Shares owned

Detaljer

PROTOKOLL. Titstede: Fra Hovedorganisasjonen Virke: Bente J. Kraugerud Marianne Pedersen. Fra NITO: Tom H. Christoffersen øyvind Kyrkjebø

PROTOKOLL. Titstede: Fra Hovedorganisasjonen Virke: Bente J. Kraugerud Marianne Pedersen. Fra NITO: Tom H. Christoffersen øyvind Kyrkjebø - Partsforhotd, måneders PROTOKOLL År 2018, den 19. juni ble det gjennomført forhandlinger metlom Hovedorganisasjonen Virke og NITO om revisjon av Hovedavtalen Titstede: Fra Hovedorganisasjonen Virke:

Detaljer

INTPART. INTPART-Conference Survey 2018, Key Results. Torill Iversen Wanvik

INTPART. INTPART-Conference Survey 2018, Key Results. Torill Iversen Wanvik INTPART INTPART-Conference 2019 Survey 2018, Key Results Torill Iversen Wanvik INTPART Scope of the survey 65 projects, 2015-2017 Different outset, different countries Different needs Different activities

Detaljer

Global Geoparks Network og UNESCO Global Geoparks

Global Geoparks Network og UNESCO Global Geoparks Global Geoparks Network og UNESCO Global Geoparks Hva er det og hva skal til? Kristin Rangnes EGN vice coordinator, kasserer i GGN, medlem i UGG Council Fristende å starte med hva geopark IKKE er! Ikke

Detaljer

Liste omhandlet i Avtalens artikkel 3 DEL I

Liste omhandlet i Avtalens artikkel 3 DEL I 443 der Beilagen XXIII. GP - Staatsvertrag - 42 norwegische Anhänge (Normativer Teil) 1 von 15 VEDLEGG A Liste omhandlet i Avtalens artikkel 3 DEL I RETTSAKTER OMHANDLET I EØS-AVTALEN SOM ENDRES VED AKT

Detaljer

Nasjonalt fakultetsmøte Bergen april Prosjektleder Heidi Dybesland

Nasjonalt fakultetsmøte Bergen april Prosjektleder Heidi Dybesland Nasjonalt fakultetsmøte Bergen 27.-28. april 2017 Prosjektleder Heidi Dybesland Hvem deltar? Alle institusjoner med samfunnsvitenskapelig forskning ble invitert med. Hvor publiserer forskerne? Institusjonene

Detaljer

SOROPTIMIST INTERNATIONAL NORGESUNIONEN

SOROPTIMIST INTERNATIONAL NORGESUNIONEN SOROPTIMIST INTERNATIONAL NORGESUNIONEN LOVER og retningslinjer Pr. 1. oktober 2014 Ajourført utgave pr 1.10.2015 1 INNHOLD UNIONSLOVER OG -VEDTEKTER Artikkel I Generelle bestemmelser... 4 Artikkel II

Detaljer

Hvordan kvalitetssikre åpne tidsskrift?

Hvordan kvalitetssikre åpne tidsskrift? Hvordan kvalitetssikre åpne tidsskrift? Innlegg ved Halvdagsseminar om åpen tilgang til vitenskapelige artikler I forbindelse med den internasjonale Open Access-uken, Universitetsbiblioteket i Bergen 26.

Detaljer

COMMISSION REGULATION (EU) No 1171/2014 of 31 October 2014 amending and correcting Annexes I, III, VI, IX, XI and XVII to Directive 2007/46/EC of the

COMMISSION REGULATION (EU) No 1171/2014 of 31 October 2014 amending and correcting Annexes I, III, VI, IX, XI and XVII to Directive 2007/46/EC of the COMMISSION REGULATION (EU) No 1171/2014 of 31 October 2014 amending and correcting Annexes I, III, VI, IX, XI and XVII to Directive 2007/46/EC of the European Parliament and of the Council establishing

Detaljer

Integrating Evidence into Nursing Practice Using a Standard Nursing Terminology

Integrating Evidence into Nursing Practice Using a Standard Nursing Terminology Integrating Evidence into Nursing Practice Using a Standard Nursing Terminology Kathryn Mølstad, RN, Norwegian Nurses Organisation Kay Jansen, MSN, PMHCNS-BC, DNPc, University of Wisconsin- Milwaukee,

Detaljer

Liste omhandlet i avtalens artikkel 3 DEL I RETTSAKTER OMHANDLET I EØS-AVTALEN ENDRET VED TILTREDELSESAKTEN AV 16. APRIL 2003

Liste omhandlet i avtalens artikkel 3 DEL I RETTSAKTER OMHANDLET I EØS-AVTALEN ENDRET VED TILTREDELSESAKTEN AV 16. APRIL 2003 404 der Beilagen XXII. GP - Staatsvertrag - Anhänge Norwegisch (Normativer Teil) 1 von 89 VEDLEGG A Liste omhandlet i avtalens artikkel 3 DEL I RETTSAKTER OMHANDLET I EØS-AVTALEN ENDRET VED TILTREDELSESAKTEN

Detaljer

Norway. Museum Statistics for 2011. Statistical data from 134 museums that were open to the public and had at least one man year regular staff.

Norway. Museum Statistics for 2011. Statistical data from 134 museums that were open to the public and had at least one man year regular staff. Norway Museum Statistics for 2011. Statistical data from 134 museums that were open to the public and had at least one man year regular staff. Arts Council Norway Tel: +47 21 04 58 00 post@kulturrad.no

Detaljer

Lisbeth M Brevik Hva kjennetegner kvalitet i engelskundervisningen? Koding av video-observerte engelsktimer ved norske ungdomsskoler (9.

Lisbeth M Brevik Hva kjennetegner kvalitet i engelskundervisningen? Koding av video-observerte engelsktimer ved norske ungdomsskoler (9. Lisbeth M Brevik Hva kjennetegner kvalitet i engelskundervisningen? Koding av video-observerte engelsktimer ved norske ungdomsskoler (9. trinn) LISA: Linking Instruction and Student Achievement Trinn 1:

Detaljer

INF109 - Uke 1a

INF109 - Uke 1a INF109 - Uke 1a 19.01.16 NOTE: Download the latest version of python: 3.5.1. 1 Introduksjon 1.1 Goodbye world! For å komme i gang, start IDLE fra Start Programs Python3.5.1 IDLE. (Varierer litt fra datamaskin

Detaljer

O v e r o r d n e t m a k r o p e r s p e k t i v p å d i g i t a l e m u l i g h e t e r

O v e r o r d n e t m a k r o p e r s p e k t i v p å d i g i t a l e m u l i g h e t e r O v e r o r d n e t m a k r o p e r s p e k t i v p å d i g i t a l e m u l i g h e t e r S t r a t e g i s k s t y r i n g a v v i r k s o m h e t e r Brit Tone Bergman 19/09/2018 2 En v e r d e n i e

Detaljer

Dokumentasjon av systematisk litteratursøk

Dokumentasjon av systematisk litteratursøk Kategori Pasientbehandling atikk Gyldig fra 05.12.2011 Organisatorisk plassering Helse Bergen HF - Medisinsk servicedivisjon - Ergoterapiavdelingen - Revmatologisk avd. Versjon 1.00 Skjema Dok. eier Solveig

Detaljer

Brukermedvirkning i forskning: kun i festtaler eller også i praksis?

Brukermedvirkning i forskning: kun i festtaler eller også i praksis? Brukermedvirkning i forskning: kun i festtaler eller også i praksis? Lillehammer Oktober 2017 Anne-Mette Bredahl, Psykologspesialist, Phd. TRS kompetansesenter for sjeldne diagnoser Leder av tematisk forskningsgruppe

Detaljer

Referat styremøte Nmf Trondheim 20. april 2016

Referat styremøte Nmf Trondheim 20. april 2016 Referat styremøte Nmf Trondheim 20. april 2016 Tilstede: Augusta Horn Welle-Strand, Kristina Albertsen, Knut Lien, Rannei Hosar, Anna Christiansen, Martin Campo, Johanne Johnsen Rakner, Inga Skogvold Rygg,

Detaljer